Mtawala Radio

Mtawala Radio Mtawala Radio "duniani k**a mbinguni"
Online Radio

SERIKALI YAZINDUA NYUMBA 109 ZA WAATHIRIKA HANANG .•  ✍️ Na, Veronica Martine •Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tan...
20/12/2024

SERIKALI YAZINDUA NYUMBA 109 ZA WAATHIRIKA HANANG .

✍️ Na, Veronica Martine

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Desemba 20, 2024 amezindua na kukabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba 03, 2023 Hanang, Mkoani Manyara.

Nyumba hizo ambazo zimejengwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) zipo katika kijiji cha Wareti, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.

Ujenzi wa nyumba hizo ulitokana na maamuzi ya Rais Dkt. Samia baada ya kutembelea eneo lililoathiriwa na maporomoko ya tope. Uamuzi huo ni muendelezo wa dhamira ya dhati ya Serikali ya kuwalinda wananchi wake na kurejesha hali ili waendelee na mfumo wa maisha baada ya maafa.


tanzaniaackson





Endelea Kusikiliza Mtawala Radio, Mtawala Radio tunasikika Duniani kote.

Call | WhatsApp | SMS 0758 555 000.

Instagram | Facebook | X

✍🏿Na | Mhariri wa

📍TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU 0758 555 000.





MAZUNGUMZO KATI YA KONGO NA RWANDA YAKWAMA KUFANYIKA.•  ✍️ Na, Veronica Martine •Mazungumzo yaliyopangwa kufanyika Jumap...
16/12/2024

MAZUNGUMZO KATI YA KONGO NA RWANDA YAKWAMA KUFANYIKA.

✍️ Na, Veronica Martine

Mazungumzo yaliyopangwa kufanyika Jumapili kati ya viongozi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kumaliza mzozo wa mashariki mwa Kongo yamefutwa baada ya majadiliano kukwama.

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa ofisi ya Rais wa Angola, Joao Lourenço, mpatanishi wa Umoja wa Afrika kwa ajili ya kumaliza mzozo huo.

Serikali ya Kongo imesema kwenye taarifa yake kwamba hatua hiyo inatokana na ujumbe wa Rwanda kukataa kushiriki.

Imesema Rwanda inaitaka Kongo ifanye mazungumzo ya moja kwa moja na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Kigali na waliodhibiti eneo kubwa la mashariki mwa Kongo, tangu mwaka 2021.

Kulikuwa na matarajio makubwa kwamba mkutano huo ulioandaliwa ungemalizika kwa makubaliano ya kumaliza mgogoro.

Kagame na Tshisekedi walikutana mara ya mwisho Oktoba jijini Paris lakini hawakuzungumza moja kwa moja, huku mazungumzo yao yakiendelea kupitia upatanishi wa Luanda.




Endelea Kusikiliza Mtawala Radio, Mtawala Radio tunasikika Duniani kote.

Call | WhatsApp | SMS 0758 555 000.

Instagram | Facebook | X

✍🏿Na | Mhariri wa

📍TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU 0758 555 000.





WAZIRI KABUDI AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA KALI WALIONG'OA VITI UWANJA WA TAIFA.•  ✍️ Na, Veronica Martine •Waziri wa Habari...
16/12/2024

WAZIRI KABUDI AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA KALI WALIONG'OA VITI UWANJA WA TAIFA.

✍️ Na, Veronica Martine

Waziri wa Habari Prof Palamagamba Kabudi amesikitishwa na vitendo vya mashabiki kung’oa viti katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dec 15,2024.

Waziri Kabudi amemuagiza Katibu mkuu wa Wizara hiyo kuchukua hatua Mara moja kuwaandikia Barua Simba SC naj Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Ili gharama za uharibifu zilizosababishwa wakati wa wa mechi hiyo hiyo zilipwe

Simba SC wametakiwa kutoa Ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili wote waliong’oa viti wak**atwe na wachukuliwe hatua za kisheria ili kukomesha tabia hiyo” Waziri Kabudi

Kwa upande wake K**anda Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Jumanne Muliro amesema fujo hizo zimesababishwa na Mashabiki wa Timu ya CS SFAXIEN kutoridhika na maamuzi ya Refa wa mchezo huo kuchezesha mechi hiyo kwa zaidi ya dakika saba ambazo aliziongeza k**a dakika za nyongeza jambo lililopelekea timu ya Simba kupata goli la pili na la ushindi.


tanzaniakabudipjam



Endelea Kusikiliza Mtawala Radio, Mtawala Radio tunasikika Duniani kote.

Call | WhatsApp | SMS 0758 555 000.

Instagram | Facebook | X

✍🏿Na | Mhariri wa

📍TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU 0758 555 000.





UZINDUZI WA YOO MAWE ALBUM KUFANYIKA ECO BEACH BUKOBA DEC 23,2024.•  ✍️ Na, Veronica Martine •Mwanamuziki wa Nyimbo za A...
15/12/2024

UZINDUZI WA YOO MAWE ALBUM KUFANYIKA ECO BEACH BUKOBA DEC 23,2024.

✍️ Na, Veronica Martine

Mwanamuziki wa Nyimbo za Asili kutokea Bukoba Mkoani Kagera Dr Mtawala anatarajia kuzindua Album yake ya Kwanza yenye Nyimbo 16 zenye vionjo mbalimbali zikiwemo Asili ya Kihaya,Kiganda na Kinyarwanda.

Uzinduzi huo utafanyika Bukoba Tarehe 23,2024 Mkoani Kagera huku Wadau Mbalimbali wa Muziki wa Asili wakitarajiwa kuhudhuria.

Habari njema ni kwamba hakutakuwa na kiingilio, na Uzinduzi utaanza Saa Kumi Jioni mpaka Saa sita usiku Watu wote mnakaribishwa.





Endelea Kusikiliza Mtawala Radio, Mtawala Radio tunasikika Duniani kote.

Call | WhatsApp | SMS 0758 555 000.

Instagram | Facebook | X

✍🏿Na | Mhariri wa

📍TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU 0758 555 000.





TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU 0758 555 000. •Mtawala Radio Tunasikika Duniani kote Bila Mipaka. •...
13/12/2024

TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU 0758 555 000.

Mtawala Radio Tunasikika Duniani kote Bila Mipaka.

Follow us on Instagram | Facebook | X

UWEPO WA KIMBUNGA CHIDO KATIKA BAHARI YA HINDI.•  ✍️ Na, Veronica Martine •Ofisi ya Waziri Mkuu inatoa taarifa kwa umma ...
13/12/2024

UWEPO WA KIMBUNGA CHIDO KATIKA BAHARI YA HINDI.

✍️ Na, Veronica Martine

Ofisi ya Waziri Mkuu inatoa taarifa kwa umma kufuatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu uwepo wa kimbunga “CHIDO” katika Bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.

Kimbunga hicho kinatarajiwa kuelekea maeneo ya kaskazini mwa Msumbiji katika kipindi cha siku nne zijazo (tarehe 13 hadi 16 ya mwezi Disemba, 2024).

Aidha, kwa sasa, kimbunga hicho hakiashirii uwezekano wa kusababisha athari za moja kwa moja hapa nchini.

Hata hivyo, kutokana na ukaribu wa maeneo ambayo kimbunga “CHIDO” kinatarajiwa kupita (Kaskazini mwa Msumbiji) na maeneo ya kusini mwa Nchi ya Tanzania upo uwezekano mdogo wa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa itakayoambatana na upepo mkali na mawimbi makubwa ya Bahari kwa maeneo ya Mtwara na maeneo jirani hususani kati ya tarehe 14 na 16 ya Disemba 2024.

USHAURI: Wananchi wanaoishi kando kando ya Bahari, Watumiaji wa Bahari na wananchi wengine waliopo katika Mikoa ya kusini wanashauriwa kuchukua tahadhari na kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Vile vile, Mamlaka za Serikali za Mitaa zikiongozwa na K**ati za Usimamizi wa Maafa katika ngazi za mikoa, wilaya, kata na kijiji/mtaa zinatakiwa kuchukua hatua za tahadhari na kusimamia utekelezaji wake kwa wananchi waliopo katika maeneo yao.

Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kufuatilia kwa ukaribu mwenendo wa kimbunga hicho.


tanzaniaackson




Endelea Kusikiliza Mtawala Radio, Mtawala Radio tunasikika Duniani kote.

Call | WhatsApp | SMS 0758 555 000.

Instagram | Facebook | X

✍🏿Na | Mhariri wa

📍TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU 0758 555 000.





MALALAMIKO YA WANANCHI KUFANYIWA KAZI NA MFUMO WA UTOAJI TAARIFA KUBORESHWA.•  ✍🏿Na Dr. Mtawala. •Waziri wa Mambo ya Nda...
12/12/2024

MALALAMIKO YA WANANCHI KUFANYIWA KAZI NA MFUMO WA UTOAJI TAARIFA KUBORESHWA.

✍🏿Na Dr. Mtawala.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa (Mb) ameiagiza Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Ndani kusimamia Kitengo kinachoshughulikia Malalamiko yanayotolewa kwa Wizara, Taasisi na Vyombo vya Usalama kuhakikisha wanayafanyia kazi na kutoa mrejesho wa utatuzi wa malalamiko kwa Wananchi.

Aidha, Bashungwa amevitaka Vitengo vya Mawasiliano na Habari vya Wizara, Vyombo vya Usalama na Taasisi zote kuboresha mfumo wa Mawasiliano na Habari kwa umma.

Ameeleza hayo 12 Disemba, 2024 wakati akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo mara baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara yaliyopo Mji wa Serikali Mtumba - Dodoma na kusisitiza kuwa ni haki ya Watanzania kupata Taarifa sahihi kwa wakati.

“Kuna Malalamiko mengine yanakuwepo kwa sababu hamna Taarifa sahihi au Taarifa imechelewa, kwahiyo lazima mhakikishe mnashughulikia Malalamiko na kutoa mrejesho” Bashungwa.

Vilevile, Bashungwa ametoa wito kwa Watumishi wa Wizara kutoa ushirikiano kwake na viongozi wengine wote ili kwa pamoja kutimiza adhima ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwahudumia Wananchi.

Kwa Upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo amemkaribisha Waziri Bashungwa na kumhakikishia ushirikiano wa karibu katika utekelezaji wa majukumu katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Endelea Kusikiliza Mtawala Radio, Mtawala Radio tunasikika Duniani kote.

Call | WhatsApp | SMS +255 758 555 000.

Instagram | Facebook | X

✍🏿Na Dr Mtawala | Mhariri Vera wa

**ambinguni

Msimu Wetu Mpya Wa Januari Mwaka 2025 Tunakuletea Vyuma Vipya kuwa Tayari Msikilizaji wetu wa Mtawala Radio. •Mwaka 2025...
12/12/2024

Msimu Wetu Mpya Wa Januari Mwaka 2025 Tunakuletea Vyuma Vipya kuwa Tayari Msikilizaji wetu wa Mtawala Radio.

Mwaka 2025 Tunasema Ishi Kidijitali na Mtawala Radio zima Redio Mbao kaa kwa Kitulia na Mtawala Radio.

Tusikilize kupitia www.mtawalaradio.online au kupitia App's za Online Radio Search Mtawala Radio Popote ulipo Duniani.

"duniani k**a mbinguni"

Hujambo......!!!•Endelea Kusikiliza Mtawala Radio Kupitia www.mtawalaradio.online au kupitia App's Zote za Online Radio ...
12/12/2024

Hujambo......!!!

Endelea Kusikiliza Mtawala Radio Kupitia www.mtawalaradio.online au kupitia App's Zote za Online Radio Search Mtawala Radio Popote ulipo Duniani.

Follow us on Instagram

"Duniani K**a Mbinguni"

**ambinguni

RAIS MWINYI AFUNGUA RASIMU YA DIRA YA MWAKA 2050.•  ✍️ Na, Veronica Martine •Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la...
11/12/2024

RAIS MWINYI AFUNGUA RASIMU YA DIRA YA MWAKA 2050.

✍️ Na, Veronica Martine

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amezindua Rasimu ya Dira ya Maendeleo ambapo amesema malengo makuu ya Rasimu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ni kugusa moja kwa moja katika kuboresha maisha ya Watu, Elimu, Afya, Ustawi wa Amani na haki pamoja na kuwa na Dira Jumuishi ambayo itamshirikisha kila Mwananchi kutoa mchango wake kwa maendeleo ya Taifa.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipozindua Rasimu ya kwanza ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Mkoa wa Mjini Magharibi, hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali za SMT na SMZ akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.

Aidha , Rais Dk.Mwinyi ameiagiza timu kuu ya wataalamu ya Dira ya Maendeleo ya 2050 kukutana na wadau mbalimbali kuhakikisha kazi ya kupokea maoni inakamilika kikamilifu ili kuwa na Dira yenye kubeba maono ya wananchi wote.

Vilevile Rais Dk. Mwinyi ameziagiza Tume za Mipango ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Serikali ya Mapiduzi ya Zanzibar kuhakikisha wanaratibu zoezi la uhakiki kwamba linafanyika kwa ufanisi wa hali ya juu pamoja na kuisambaza rasimu hiyo kwa vyombo mbalimbali na kuweka mfumo halisi wa kupokea maoni.


tanzaniaackson
hmwinyi

Endelea Kusikiliza Mtawala Radio, Mtawala Radio tunasikika Duniani kote.

Call | WhatsApp | SMS 0758 555 000.

Instagram | Facebook | X

✍🏿Na | Mhariri wa

📍TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU 0758 555 000.





RAIS SAMIA AWAAPISHA MAWAZIRI.•  ✍️ Na, Veronica Martine •Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluh...
10/12/2024

RAIS SAMIA AWAAPISHA MAWAZIRI.

✍️ Na, Veronica Martine

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaapisha;

Mhe. Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mhe. Abdallah Hamis Ulega kuwa Waziri wa Ujenzi.

Mhe. Jerry William Silaa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hafla hiyo imefanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024.


tanzaniaackson





Endelea Kusikiliza Mtawala Radio, Mtawala Radio tunasikika Duniani kote.

Call | WhatsApp | SMS 0758 555 000.

Instagram | Facebook | X

✍🏿Na | Mhariri wa

📍TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU 0758 555 000.





TCRA YARATIBU KIKAO CHA CRASA.•  ✍🏿Na Dr Mtawala. •Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano ya Kielektroniki, Shirika la Wasimami...
10/12/2024

TCRA YARATIBU KIKAO CHA CRASA.

✍🏿Na Dr Mtawala.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano ya Kielektroniki, Shirika la Wasimamizi wa Huduma za Mawasiliano wa nchi zilizopo kusini mwa Afrika (CRASA), Bw. Shukya Kiroga akitoa utangulizi wa wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha k**ati ya Mawasiliano ya Kielektroniki (ECC) cha CRASA kilichoratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), 10 Desemba, 2024.



Endelea Kusikiliza Mtawala Radio, Mtawala Radio tunasikika Duniani kote.

Call | WhatsApp | SMS +255 758 555 000.

Instagram | Facebook | X

✍🏿Na drmtawala | Mhariri Vera wa

📍TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU +255 758 555 000.




RAIS SAMIA ASAMEHE WAFUNGWA 1548.•  ✍️ Na, Veronica Martine •Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza msama...
09/12/2024

RAIS SAMIA ASAMEHE WAFUNGWA 1548.

✍️ Na, Veronica Martine

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza msamaha kwa Wafungwa 1548 ambapo Wafungwa 22 kati yao wameachiliwa huru December 09, 2024, na Wafungwa 1526 wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu.

Taarifa iliyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema msamaha huo wa Rais Samia ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

“Ni matarajio ya Serikali kuwa Wafungwa walioachiliwa huru watarejea tena katika Jamii kushirikiana na Wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani” RAIS SAMIA


tanzaniaackson


Endelea Kusikiliza Mtawala Radio, Mtawala Radio tunasikika Duniani kote.

Call | WhatsApp | SMS 0758 555 000.

Instagram | Facebook | X

✍🏿Na | Mhariri wa

📍TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU 0758 555 000.





MAMIA YA WAKAZI WASHIRIKI MATEMBEZI KUIOMBEA ARUSHA-TANZANIA.•  ✍🏿Na Dr. Mtawala. •Mamia ya wakazi wa Mkoa wa Arusha wak...
09/12/2024

MAMIA YA WAKAZI WASHIRIKI MATEMBEZI KUIOMBEA ARUSHA-TANZANIA.

✍🏿Na Dr. Mtawala.

Mamia ya wakazi wa Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Paul Makonda pamoja na Viongozi wa Madhehebu Mabalimbali kwenye matembezi ya pamoja ya kuuombea Mkoa wa Arusha na kuliombea Taifa la Tanzania Disemba 09, 2024, pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Arusha.

Shughuli ya Maombi imefanyika kwenye Viwanja vya pembezoni mwa mzunguko wa Barabara kwenye mnara wa Mwenge hapo Jijini Arusha.




Endelea Kusikiliza Mtawala Radio, Mtawala Radio tunasikika Duniani kote.

Call | Whatsap | SMS +255 758 555 000.

Instagram | Facebook | X

✍🏿Na | Mhariri Vera wa

📍TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU +255 758 555 000.





TANZANIA INAADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU.•  ✍️ Na, Veronica Martine •Mtawala Radio inawatakia Watanzania wote Maadhimisho...
09/12/2024

TANZANIA INAADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU.

✍️ Na, Veronica Martine

Mtawala Radio inawatakia Watanzania wote Maadhimisho Mema ya Miaka 63 ya Uhuru.

Maadhimisho haya huadhimishwa Kila ifikapo Disemba 9 na Mwaka 2024 hakutakuwa na sherehe zake.

Ikumbukwe kuwa mnamo Disemba 04,2024 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa alisema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa Mwaka 2024 yafanyike katika ngazi ya mikoa na Fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya Maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii.

Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni "Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi NI Msingi wa Maendeleo Yetu"


tanzaniaackson



Endelea Kusikiliza Mtawala Radio, Mtawala Radio tunasikika Duniani kote.

Call | WhatsApp | SMS 0758 555 000.

Instagram | Facebook | X

✍🏿Na | Mhariri wa

📍TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU 0758 555 000.





CONGRATULATIONS MTAWALA RADIO.•  ✍️ Na, Veronica Martine •Mtawala Radio imetunukiwa Cheti kutoka Katika Taasisi isiyo ya...
08/12/2024

CONGRATULATIONS MTAWALA RADIO.

✍️ Na, Veronica Martine

Mtawala Radio imetunukiwa Cheti kutoka Katika Taasisi isiyo ya Kiserikali inayoitwa chini ya Mkurugenzi inayojishughulisha na Watu Wenye Usonji, ambapo ilifanya Harambee ya Chakula cha Usiku "Autism Awareness Fundraising Gala Dinner" iliyofanyika Dec 7,2024 Serena Hotel Dar Es Salaam Tanzania.

Mtawala Radio tumepokea Cheti hiki kwa Unyenyekevu wa Hali ya Juu sana. Tunaahidi kuendelea kufungua milango kwa kazi zote za Kijamii, Sambamba na hilo Menejimenti inatoa Pongezi kwa Timu nzima ya kwa kazi yao njema ya kujali Jamii haswa kundi hili ambalo lilisahaulika kwa muda mrefu. Tunatoa Pongezi kwa Wizara ya Afya Nchini Tanzania na Wadau wote waliyotoa Sapoti na Wale Wote wanaoendelea kutoa Sapoti.

Endelea Kusikiliza Mtawala Radio, Mtawala Radio tunasikika Duniani kote.

Call | WhatsApp | SMS 0758 555 000.

Instagram | Facebook | X

✍🏿Na | Mhariri wa

📍TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU 0758 555 000.





BASHUNGWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI.•  ✍️ Na, Veronica Martine •Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua In...
08/12/2024

BASHUNGWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

✍️ Na, Veronica Martine

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Innocent Bashungwa, kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, awali alikuwa Waziri wa Ujenzi.

Uapisho wake na viongozi wengine walioteuliwa Jumapili, Desemba 8,2024 utafanyika Ikulu Ndogo, Tunguu Zanzibar Desemba 10, 2024 kuanzia saa 5.00 asubuhi.


tanzaniaackson


Endelea Kusikiliza Mtawala Radio, Mtawala Radio tunasikika Duniani kote.

Call | WhatsApp | SMS 0758 555 000.

Instagram | Facebook | X

✍🏿Na | Mhariri wa

📍TANGAZA BIASHARA YAKO NA MTAWALA RADIO KWA BEI NAFUU 0758 555 000.





KATIKA ROHO Ndani ya Mtawala Radio. With Pastor Robert Mwaisaka From Grace and Truth Int. Every Saturday.•From 10:00 - 1...
07/12/2024

KATIKA ROHO Ndani ya Mtawala Radio. With Pastor Robert Mwaisaka From Grace and Truth Int. Every Saturday.

From 10:00 - 12:00EAT Tune on www.mtawalaradio.online Au kupitia App's Zote za Online Radio Search Mtawala Radio.

Follow us on Instagram | Facebook | Twitter

Call 📞WhatsApp 📲 SMS
+255 758 555 000

Mtawala Radio "Duniani K**a Mbinguni"




**ambinguni



Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255758555000

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mtawala Radio posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Mtawala Radio:

Videos

Share