Radio Mbiu

Radio Mbiu Karibu tushirikiane

Ni Ukurasa wa Kituo cha Radio Mbiu inayopatikana Mkoani Kagera katika masafa ya 104.9 Fm, na ukurasa huu unakupatia habari mbali mbali ya kile kinachojiri ndani na nje ya mkoa wa Kagera katika matukio ya Dini na Kijamii..

16/02/2025

Maandalizi ya Jubilei ya miaka 25 ya Uaskofu Mhashamu Method Kilaini.

www.radiombiu.co.tz

Katika picha ni baadhi ya wanautume wa Radio Maria Jimbo Katoliki la Bukoba pamoja na wana familia ya Marehemu Justinian...
16/02/2025

Katika picha ni baadhi ya wanautume wa Radio Maria Jimbo Katoliki la Bukoba pamoja na wana familia ya Marehemu Justinian Mbegu wakisali sala ya Rozari Takatifu ya Fatima kwa nia ya kumuombea Marehemu mzee Justinian Mbegu Baba mzazi wa Magreth Rugambwa ambaye ni mwana utume Radio Maria Jimbo la Bukoba.

www.radiombiu.co.tz

SALA  YA JIONI + Sasa siku imekwisha, kwako Mungu  napandisha,  Moyo wangu wa shukrani, Nipumzike  kwa Amani,Mema mengi ...
15/02/2025

SALA YA JIONI

+ Sasa siku imekwisha, kwako Mungu napandisha,
Moyo wangu wa shukrani, Nipumzike kwa Amani,
Mema mengi umenipa, Nashindwa kukulipa,
Baba mwema ondolea, Yote niliyokukosea,
Yesu mpenzi nijie , Ombi langu usikie.
Unifiche mtoto wako, Ndani ya jeraha Zako,
Ee Mama unipe neema, Raha na usiku mwema,
Roho mlinzi kakeshe , pepo wasinikoseshe,
Naiweka Roho yangu, Mikononi mwa Baba yangu,
Bila hofu napumzika, Mwisho kwako nitafika.
AMINA. +
Uwe na jioni njema.
www.radiombiu.co.tz

15/02/2025

|| ROZARI YA FATIMA - BUKOBA

Karibu tusali pamoja Sala ya Rozari Takatifu ya Fatima kutoka Jimbo Katoliki Bukoba.

Tunaongozwa na familia ya marehemu Justinian Rugambwa, Baba mzazi wa Valantia wa Radio Maria Tanzania, Jimbo Katoliki Bukoba, Ma Magreth Rugambwa.

Nia ya Rozari ni kumwombea marehemu mzee Justinian Rugambwa apumzike kwa amani.
www.radiombiu.co.tz

Karibu tusali Sala ya Malaika wa Bwana pamoja na Masifu ya Mchana.www.radiombiu.co.tz104.9fm
15/02/2025

Karibu tusali Sala ya Malaika wa Bwana pamoja na Masifu ya Mchana.
www.radiombiu.co.tz
104.9fm

Karibu usikilize Marudio ya kipindi cha Roho Mtakatifu na Kanisa.www.radiombiu.co.tz
15/02/2025

Karibu usikilize Marudio ya kipindi cha Roho Mtakatifu na Kanisa.
www.radiombiu.co.tz

15/02/2025
Karibu tusali sala ya Rozari Takatifu ya Fatima pamoja na sala za jioni.www.radiombiu.co.tz
14/02/2025

Karibu tusali sala ya Rozari Takatifu ya Fatima pamoja na sala za jioni.

www.radiombiu.co.tz

SALA KWA BIKIRA MARIA WA MATESOEwe Mama mwenye huzuni, ninaelekea kwako kwa uaminifu kabisa. Ulipata maumivu makali mais...
14/02/2025

SALA KWA BIKIRA MARIA WA MATESO

Ewe Mama mwenye huzuni, ninaelekea kwako kwa uaminifu kabisa. Ulipata maumivu makali maishani, ukimwangalia Mwanao akifa Msalabani, na bado ulibaki karibu naye hadi mwisho. Nitazame kwa neema, mimi mwenye dhambi maskini, na unipatie kutoka kwa Mwana wako neema zote ninazohitaji kuvumilia mateso ambayo Mungu ananiruhusu kuyakabili. Amina.
www.radiombiu.co.tz

Ee Yesu mwenye huruma kabisa ambaye asili yako ni huruma na msamaha, usizitazame dhambi zetu, bali tumaini tulilo nalo k...
14/02/2025

Ee Yesu mwenye huruma kabisa ambaye asili yako ni huruma na msamaha, usizitazame dhambi zetu, bali tumaini tulilo nalo katika wema wako usio na mwisho utupokee sisi sote chini ya ulinzi wa moyo wako wenye huruma. Baba wa milele uwatazame kwa macho ya huruma watu wote na hasa wakosefu walioingizwa ndani ya moyo wa Mwanao mpenzi Bwana wetu Yesu Kristu ulio na huruma tele. Amina.
www.radiombiu.co.tz

Watakatifu Cyril Mtawa na Methodius Askofu.Watakatifu Cyril na Methodius walikuwa kati ya watoto 7 wa kiume wa familia m...
14/02/2025

Watakatifu Cyril Mtawa na Methodius Askofu.
Watakatifu Cyril na Methodius walikuwa kati ya watoto 7 wa kiume wa familia moja, huko Thessalonica (Ugiriki sasa).Mtakatifu Cyril akiwa mdogo kabisa.Alizaliwa mwaka 827, wakati mtakatifu Methodius alizaliwa mwaka 815.

Walipobatizwa Methodius aliitwa Michael na Cyril aliitwa Constantine. Baba yao aliitwa Teo na mama yao Maria.

Ndugu hawa walipata elimu nzuri, hata baada ya kufa kwa Baba yao. Na mtakatifu Cyril alipata daraja la upadre mara tu alipomaliza masomo yake . Mtakatifu Methodius, alibaki kuwa shemasi ,mpaka mwaka 867.

Mwaka 860, mfalme Michael wa Byzantine (himaya ya warumi) na askofu wa Constantinople Photius(Uturuki), walimtuma mtakatifu Cyril kwenda khazars
( Azerbaijan ) kufanya umisionari.

Huko aliambatana na kaka yake Methodius. Huko walifanya kazi kwa mafanikio makubwa.Mwaka 862, ndugu hao walitumwa kwenda kufanya umisionari katika nchi ya Moravia ( Czech ) kwa ombi la Mwana mfalme Rastislav.Lakini huko walikuta pia mgogoro, ambao ulianzishwa ili kudai Uhuru kutoka kwa watawala wa Kijerumani. Mgogoro huo, uliingia katika Kanisa, na kuwaletea shida kubwa.

Kutokana na matatizo hayo, ndugu hao wawili waliamua kwenda Roma, kumuona Papa, ili kuruhusu lugha ya Slovanic itumike katika ibada, na pia waseminari wa kutoka Moravia wapewe daraja la upadre baada ya kumaliza masomo yao.Papa aliwakubalia.

Lakini mtakatifu Cyril hakurudi Moravia, aliamua kubaki Roma, akiwa mtawa, na hapo ndipo alipochukua jina la Cyril. Alikufa huko Roma ,mwaka 869 Februari 14.

Ndugu yake , Methodius naye hakupenda kurudi Moravia kutokana na mgogoro huo wa siasa kuingia kanisani, lakini aliitwa na Mwana mfalme aliyeitwa Kocel. Methodius aliruhusiwa kufanya ibada, kubatiza, kwa lugha ya Slovanic. Papa Adrian II alimpa pia Methodius daraja la Uaskofu

Wakati mgogoro huo wa kisiasa ukiendelea, mfalme wa kijerumani aliyeitwa Louis, alimfunga jela askofu Methodius kwa madai ya kufanya mafundisho potofu. Lakini miaka 2 baadae Papa John VIII alifanikisha kuachiwa kwake.Lakini alimkataza pia kutumia lugha ya Slavonic katika Liturjia.

Mwaka 878, Askofu Methodius aliitwa Roma, akituhumiwa kuendelea kutumia lugha ya Slavonic na kufanya mafundisho potofu. Alimudu kujitetea, na akaamriwa kurudi katika jimbo lake, na pia kuendelea na matumizi ya lugha ya Slovanic na mafundisho yake.

Mtakatifu Methodius aliendelea pia kutafsiri maandiko mtakatifu. Alikufa mwaka 884 April 6.

Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Valentine
Mt. Abraham wa Carrhae
Mt. Antoninus wa Sorrento
Mt. Auxentius wa Bithynia
Mt. Conran
Mt. Dionysius
Mt. Eleuchadius
Mt. Maro
Mt. Nostrianus
Mt. Theodosius
M/h. Vicente Vilar David
Watakatifu Cyril na Methodius, Wenye heri na Watakatifu wengine wote wa leo, Mtuombee.
www.radiombiu.co.tz

Karibu Msikilizaji wetu tuungane pamoja tusali Rozari Takatifu ya Fatima na sala za jioni.www.radiombiu.co.tz104.9fm
13/02/2025

Karibu Msikilizaji wetu tuungane pamoja tusali Rozari Takatifu ya Fatima na sala za jioni.
www.radiombiu.co.tz
104.9fm

Karibu Msikilizaji tuungane pamoja kushiriki Ibada ya kuabudu Ekaristi Takatifu.www.radiombiu.co.tz104.9fm
13/02/2025

Karibu Msikilizaji tuungane pamoja kushiriki Ibada ya kuabudu Ekaristi Takatifu.
www.radiombiu.co.tz
104.9fm

Mtakatifu Catherine wa RicciMtakatifu Catherine alizaliwa mwaka 1522 April 23, huko Florence,  Italia .Alibatizwa , akai...
13/02/2025

Mtakatifu Catherine wa Ricci
Mtakatifu Catherine alizaliwa mwaka 1522 April 23, huko Florence, Italia .Alibatizwa , akaitwa Alexandrina.

Alipata elimu yake ya awali katika Convent ya masista ya Monticelli, hapo hapo Florence, ambako shangazi yake aliyeitwa Louisa de Ricci, ambaye alikuwa mtawa hapo.

Akiwa na miaka 14, alijiunga na convent ya Masista wa Dominican, huko Prat, Tuscany. Hapo akachukua jina la Catherine. Akapanda ngazi mbalimbali za uongozi.

Mtakatifu Catherine, alitumia muda wake wa ziada kusali, na kuomba. Alikuwa pia akipata maono katika nyakati mbalimbali.

Mtakatifu Catherine alikufa mwaka 1589, Februari 2, huko Prato, Tuscany Italia, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Alitangazwa mwenye heri mwaka 1732 Novemba 23 na Papa Clement XII, na akatangazwa mtakatifu mwaka 1746 June 29 na Papa Benedict XIV

Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Agabus
M/h. Archangela Girlani
Mt. Benignus
Mt. Dyfnog
Mt. Ermengild
M/h. Eustochium
Mt. Gosbert
Mt. Huno
M/h. John Lantrua wa Triora
Mt. Julian wa Lyons
Mt. Lezin
Mt. Martinian
Mt. Modomnoc
Mt. Polyeuctus
Mtakatifu Catherine, Wenye heri na Watakatifu wengine wote wa leo, Mtuombee
www.radiombiu.co.tz

Mwenyeheri Thomas Hemerford, na wenzake Mashahidi.Mwenyeheri Thomas Hemerford alizaliwa mwaka 1553, huko Dorsetshire Uin...
12/02/2025

Mwenyeheri Thomas Hemerford, na wenzake Mashahidi.

Mwenyeheri Thomas Hemerford alizaliwa mwaka 1553, huko Dorsetshire Uingereza. Akasoma katika chuo cha Mt John huko Oxford. Alipata shahada ya sheria mwaka 1575.Mwaka 1580 alijiunga na seminari ya kiingereza huko Roma , Italia.
Mwaka 1583 mwezi March alipata daraja la upadre huko Rheims .Mwezi wa Juni mwaka huo, alienda Hampshire. Huko alifanya kazi zake k**a Padre, na baadae akak**atwa, akafungwa, na mwisho akashtakiwa kwa kosa la kuwa Padre , na makosa mengine ya uongo.
Mtakatifu Thomas na wenzake wanne walinyongwa tarehe 7 Februari 1584.
Mtakatifu Thomas na wenzake, walitangazwa wenye heri mwaka 1929.

Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Buonfiglio Monaldo
Mt. Anthony Kauleas
Mt. Anthony wa Saxony
Mt. Benedict Revelli
Mt. Damian
Mt. Ethelwald
Mt. Febronia
Mt. Humbeline
M/h. James Feun
Mt. John wa Nicomedia
Mt. Julian
Mt. Juventius wa Pavia
Mt. Ludan
Mt. Meletius wa Antioch
Mt. Modestus
Wt. Modestus na Ammonius
Wt. Modestus na Julian
Mwenye heri Thomas na wenzake, Wenye heri na Watakatifu wengine wote wa leo, Mtuombee.
www.radiombiu.co.tz

Address

Bunena
Bukoba
35101

Opening Hours

Monday 08:00 - 18:00
Tuesday 08:00 - 18:00
Wednesday 08:00 - 18:00
Thursday 08:00 - 18:00
Friday 08:00 - 18:00
Saturday 08:00 - 16:00
Sunday 09:00 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Radio Mbiu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Radio Mbiu:

Videos

Share

Category