#Repost
///@ariseandshinetanzania: Operation Washa Taa Kila Mkoa ,
Sasa Ni Mkoa Wa Mara Musoma Kongamano Kubwa La Ukombozi wa Ardhi Na Ukombozi Wa Nyayo Kwa Kuchovyamiguu Kwenye Mafuta Ya Upako Katika Uwanja Wa Shule ya Msingi Mkendo Kuanzia Alhamisi Ya Tarehe 24 /11 / 2022 Hadi Jumamosi Ya Terehe 26 / 11 / 2022 Muda saa 08 ; 00 Mchana .
Watu Wa Dini Zote Mnakaribishwa.
#MUSOMA#ariseandshinetanzania #2022mwakawakibalimarambili #mwamposalive
Timu ya Taifa ya Wanawake U17 @serengetigirlstz , imewasili kwenye mji wa Mumbai, India ikitokea Goa tayari kwa mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Canada utakaochezwa Oktoba 18, 2022.
@serengetigirlstz @fifawomensworldcup
Kikosi cha @yangasc kikielekea uwanjani muda huu tayari kuwavaa Al Hilal.
Mechi ni saa 3:00 usiku
#CAFChampionsLeague #LigiYamabingwaAfrika
#Repost
///@msemajimkuuwaserikali: “...ninawapongeza sana kwa
UZALENDO, UADILIFU na UMAKINI mkubwa...” @samia_suluhu_hassan
Rais Samia Amepokea Mwenge wa Uhuru Katika Kilele cha Mbio za Mwenge Huo Mkoani Kagera katika Uwanja wa Kaitaba.
Watoto wa Halaiki toka Bukoba wakiimba Wimbo wa kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere na Wiki ya Vijana kitaifa.
Kutoka Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba katika Mkoa wa Kagera.
:
Mhe. Rais @samia_suluhu_hassan akiingia uwanjani ambapo ni Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana.
#Repost
///@msemajimkuuwaserikali: “Miaka 23 Bila Mwl. Nyerere...Bado Tunaendelea Kupiga Vita...”
#Repost
///@msemajimkuuwaserikali: “Vijana 20 Nitawalipia Mimi...Serikali Itatumia Bilioni Moja Nukta Moja Kwa Mwezi Kuendesha Chuo Hiki...”
#Repost
///@msemajimkuuwaserikali: “Kwa Nini Tunajenga Vyuo Hivi…”
Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua chuo hiki cha VETA Kagera.
#Repost
///@maelezonews: 📌Serikali yaunda kamati kuchunguza wanafunzi kufeli Law School
Taarifa kuhusu uzinduzi wa Chuo cha VETA Kagera 13. Octoba. 2022
#Repost
///@gwajimad: Leo ni siku ya kimataifa ya mtoto wa kike, mojawapo ya hoja ni sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ibadilishwe umri wa kuolewa au kuoa ubadilishwe. Kifupi, serikali ikiongozwa na Rais SSH🇹🇿 Iko kwenye kufanyia kazi hoja hii.
@maendeleoyajamii @smaujata_tz @lynpink_sillem @zuhuramwinyizuu, @tuungane_dev_foundation @ishamashauzioriginal @shyrosebhanji @zamaradimketema @zamaraditv @victoriafoundationtz @tunguip @amalinyaungo @malisa_gj , @salmamsangi, @mrishompotonews @mrishompoto, @joycekiriaofficial
#Repost
///@bunge.tanzania: Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akichangia katika kikao cha Mabunge ya Ukanda wa SADC kwenye Mkutano wa 145 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kigali (KCC) Nchini Rwanda.
Dhima kuu ya Mkutano huo ni kujadili “Usawa wa Kijinsia na Mabunge yanayozingatia masuala ya kijinsia kama vichocheo vya ustahimilivu na amani Duniani” ulioanza leo tarehe 10 Oktoba, 2022.
#Repost
///@missenyidc: Kyaka Shule ya Msingi
#Repost
///@missenyidc: Mwenge wa Uhuru umepokelewa Wilaya ya Missenyi ukitokea Wilaya ya Kyerwa leo tarehe 10/10/2022.
Mkuu wa wa Wilaya ya Kyerwa Mheshimiwa Rashidi Mohamed Mwaimu alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Wilson Sakulo Mwenge wa Uhuru katika Shule ya Msingi Kyaka iliopo Kata ya Kyaka ambapo makabidhiano yalifanyika mapema leo asubuhi.
Mwenge wa uhuru ukiwa Wilaya ya Kyerwa ulikimbizwa kilomita 55.5 na miradi iliotembelewa, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi ni jumla ya miradi 04 yenye thamani ya shilingi milioni 428.82.
Mwenge wa uhuru ukiwa katika Wilaya ya Missenyi utakimbizwa kwa umbali wa kilomita 91.3 kwa ajili ya kukagua, kutembelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi ya Miradi 04 yenye thamani ya shilingi Milioni 932.1
Mwenge wa uhuru siku ya leo utaanzia katika Mradi wa Maji wa Byamtemba - Byeju, pili Mradi wa Vyumba viwili vya madarasa shule ya Sekondari Bunazi, kisha kuelekea Mradi wa barabara ya Mabuye - Itara yenye urefu wa km 2.4 na kuelekea Mradi wa usafi na Mazingira katika Kituo cha afya Bunazi na Mwisho kuelekea katika eneo la Mkesha katika uwanja wa Mashujaa.
Katika Mkoa wa Kagera tayari halmashauri za Ngara DC, Karagwe DC, Kyerwa DC, wamekamilisha kukimbiza mwenge wa uhuru na leo ni zamu ya Wilaya ya Missenyi na baada ya hapo mwenge utaelekea Wilaya ya Bukoba DC, Muleba DC na mwisho kabisa Bukoba MC ambapo kilele cha kuhitimisha Mbio za mwenge kitafanyika tarehe 14/10/2022.
Octoba ni Mwezi wa uhamasishaji kuhusu usalama wa mtandao
Kauli mbiu "USALAMA MTANDAO UNAANZA NA MTU BINAFSI"
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga amempandisha cheo Danis Minja wa jeshi hilo kwa ujasiri wake wa kuingia kwenye shimo la choo na kufanikiwa kumuokoa mtoto mwenye umri wa mwaka moja na nusu katika Kata ya Murgwanza wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
.
.
....
Askari huyo wa kikosi cha Zimamoto na uokoaji amepandishwa cheo kutoka Constable na kuwa Koplo.