Uzalendo wa Kitanzania

Uzalendo  wa Kitanzania UKURASA HURU WA KUCHAMBUA & KUJADILI MADA MBALIMBALI ZA SIASA, UCHUMI & JAMII. Hapa Kazi Tu
(6)

Ukurasa Maalumu Wa kutoa, Kuchambua Na Kujadili Habari Mbalimbali za Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.

SHEHE KIPOZEO: PEPONI HAKUNA KUJISAIDIA eponi hamna kujisaidia, kujisaidia kwake ni kutokwa na jasho. Na jasho la mtu wa...
11/07/2024

SHEHE KIPOZEO: PEPONI HAKUNA KUJISAIDIA

eponi hamna kujisaidia, kujisaidia kwake ni kutokwa na jasho. Na jasho la mtu wa peponi tone moja likidondoka katika ardhi hii dunia nzima itanukia manukato ya ajabu kabisa, yaani Mungu kafanya ufundi kutengeneza pepo'' - Sheikh Kipozeo

Mwamba wa Lusaka ndani ya jezi ya yanga kwa mara ya kwanza
09/07/2024

Mwamba wa Lusaka ndani ya jezi ya yanga kwa mara ya kwanza

TANZIA: MFANYABIASHARA MAARUFU YUSUPH MANJI AFARIKI DUNIA AKIPATIWA MATIBABU NCHINI MAREKANI Mfanyabiashara ambaye ni Of...
30/06/2024

TANZIA: MFANYABIASHARA MAARUFU YUSUPH MANJI AFARIKI DUNIA AKIPATIWA MATIBABU NCHINI MAREKANI

Mfanyabiashara ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Quality Group Limited, Yusuf Manji amefariki dunia leo Juni 30, 2024 akiwa nchini Marekani.

Manji aliwahi kuwa mwanasiasa akitumikia nafasi ya Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM kati ya mwaka 2015-2017.

Aidha Manji amewahi kuwa Mfadhili na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC

YUSUPH MANJI IS NO MORE

Prominent businessman and former Yanga Club sponsor, Yusuf Manji, passed away yesterday, Saturday, June 29, 2024, at midnight in Florida, USA, where he was receiving treatment. The news of his death was confirmed by his son, Mehbub Manji.

BREAKING NEWS:  MCHUNGAJI  PETER MSIGWA AHAMIA CCMAliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, kupitia Chama cha Demo...
30/06/2024

BREAKING NEWS: MCHUNGAJI PETER MSIGWA AHAMIA CCM

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo ametambulishwa rasmi leo Jumapili, Juni 30, 2024 katika kikao cha k**ati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

29/06/2024

VITUKO VYA WAJAWAZITO NJOMBE: MTOTO MMOJA ANA BABA WANNE NA KILA MMOJA ANATOA HUDUMA AKIAMINI MTOTO NI WAKE

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Godfrey Kiowi, amesema moja ya changamoto wanazokutana nazo Wajawazito ni kuwa na zaidi ya Kadi Moja za Kliniki hali ambayo inachangia migogoro katika Jamii, hivyo ameshauri Serikali ibadilishe Mfumo huo

Amesema "Hizi kesi tunakutana nazo huko Mtaani, mtoto mmoja ana Baba wanne na ukifuatilia kila mmoja amepewa kadi yake na kila Baba anatoa Huduma kwa muda wake halafu kesho kila baba anasema Mtoto ni wa kwake."

MWANAHARAKATI  EDGAR MWAKALEBELA ALMAARUFU SATIVA ADAI ALITEKWA, KUPIGWA RISASI KICHWANI   NA  KUTUPWA MSITUNI KATAVI!ZI...
28/06/2024

MWANAHARAKATI EDGAR MWAKALEBELA ALMAARUFU SATIVA ADAI ALITEKWA, KUPIGWA RISASI KICHWANI NA KUTUPWA MSITUNI KATAVI!

ZITO KABWE AMTAKA IGP NA WAZIRI MAMBO YA NDANI KUWAJIBIKA!

"Nilitekwa Jumapili mida ya saa moja usiku na kupelekewa kituo cha Oysterbay ninajua kituo cha Oysterbay hawana taarifa zangu lakini walinipeleka kwenye karakana ya kituo cha Oysterbay ambapo nililala pale tangu saa mbili mpaka saa 11:20 asubuhi kisha wakaja kunichukua washikaji ambao nimekuwa nao kwa siku zote hizo mpaka jana (Juni 26, 2024) mpaka leo hii asubuhi (Juni 27, 2024) ambao walinipiga risasi ya kichwa, lakini Mungu ni mwema nimepigwa kichwani lakini Mungu amenipitisha kwenye taa, hivi tunavyoongea meno yangu upande wa kushoto yanahitaji kufanyiwa marekebisho” Amesimulia Sativa akizungumza na kituo cha habari cha Nipashe.

TANZIA:  DKT SHOGO MLOZI MBUNGE BUNGE AFRIKA MASHARIKI AFARIKI DUNIA Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ...
13/06/2024

TANZIA: DKT SHOGO MLOZI MBUNGE BUNGE AFRIKA MASHARIKI AFARIKI DUNIA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ametangaza kifo cha Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Dk Shogo Mlozi leo Alhamisi June 13, 2024 kabla ya kuanza kwa kikao cha 46 cha mkutano wa 15 wa Bunge la 12 Bungen

Dkt. Tulia amesema ““Leo asubuhi tumepokea taarifa kwamba Mh. Dkt. Shogo Richard Mloz ambaye tulimchagua kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki hatunae tena, hii ni taarifa ya awali tutakapopata taarifa za ziada tutawataarifu tusimame kaa dakika moja tumpe heshima zake za mwisho”

Tembelea Rwanda
11/06/2024

Tembelea Rwanda

09/06/2024

MHESHIMIWA KIGWANGALA:
MWEKEZAJI WA SIMBA ANADAIWA SHS BILIONI 43 NA WANACHAMA
SIMBA HAIJAUZWA, HAIDAIWI NA
MWEKEZAJI HANA MAMLAKA YA KUMILIKI KLABU YA SIMBA

"K**a ni kudaiana tu, tena bila mikataba, basi na sisi wana Simba tunamdai mwekezaji pesa nyingi sana!

Tulimtaka aweke bilioni 20 kwenye account yetu ili tununue bonds, kumbe hakuweka! K**a angeweka tungenunua bonds za miaka 25, at a coupon rate of 15.95% tungepata faida ya bilioni 3.19 kila mwaka. Kwa miaka 7 aliyotuzubaisha bila mafanikio yoyote yale, tungevuna bilioni 22.33!

Deni la pili: ni pesa alizotukosesha kutokana na ufadhili wa Azam - bilioni ngapi? Kwa mwaka ni bilioni 3. Kwa miaka 7 ni bilioni 21!

Na yeye matangazo yake alikuwa analipia ufadhili kiasi gani?

Tayari kwa haya mawili tu, tunamdai mwekezaji Glezabhai zaidi ya bilioni 43.33! Taja na wewe madeni mengine tunayomdai Glezabhai ili twende sawa!

Halafu, Wajumbe wa Bodi waliokurupuka leo kutoka usingizini tuna jambo nao: watuambie walimpa Glezabhai mamlaka ya kumiliki timu yetu kwa msingi upi? Maana hakufuata prospectus ya mchakato wa transformation wa kampuni inavyotaka.

Nimemuona Ndugu Issa akitumia Memorandum ya kampuni…how? K**a mchakato wa kulipia hisa haujakamilika hiyo document haina nguvu yoyote ile, ile bodi yao waliyokuwa wanakaa haina maana yoyote ile. Na wala Simba Sports Club haijauzwa na wala haidaiwi na mtu - kimsingi tumerudi GROUND ZERO!

Ile bodi ilikuwa genge la watu walioiteka tu timu yetu kinyemela. Kwa taarifa za Ndg. Issa, maana yake Glezabhai hana haki wala mamlaka yoyote yale kisheria kwenye Simba. Simba SC ni club ya wanachama kwa asilimia 100.

04/06/2024

WATOTO SITA WAMUUA MAMA YAO MZAZI KWA KUMTUHUMU KUWA MCHAWI

Watu sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za mauaji ya mama yao mzazi, Shija Mageranya (77) mkazi wa Kijiji cha Ndua, Kata ya Kasororo wilayani Misungwi.

Watuhumiwa hao ambao ni Kashinja Dotto (55), Joseph Dotto (20), Magerani Dotto (44), Nyanzala Dotto (34), Masaga Dotto (46) na Milapa Dotto (30) wanadaiwa kufanya mauaji hayo wakimtuhumu mama yao kuwa mshirikina. K**anda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo la mauaji limetokea Juni mosi mwaka huu katika kijiji hicho ambapo watoto hao walikuwa wakimtuhumu mama yao ana waloga wajukuu zake.

"Majira ya saa 2:30 usiku bibi huyo alikuwa anapata chakula cha usiku pamoja na wajukuu wake, ghafla waliingiliwa na mtu mmoja jinsia ya kiume ambaye aliwasalimia kisha akachomoa panga lenye ncha kali na kuanza kumshambulia bibi huyo kwa kumkata sehemu za kichwani na mabegani," amesema.

"Kufuatia tukio hilo, bibi huyo alivuja damu nyingi hadi kupelekea kupoteza maisha na baada ya tukio hilo mwanaume huyo ambaye hakuweza kutambulika kwa wakati huo, alikimbia na kuwaacha watoto wale wakiwa wamesambaa huku wakimshuhudia bibi yao akikata roho mbele yao," amesema.

K**anda Mutafungwa ameseama chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni imani potofu za kishirikina ambapo watoto wa marehemu wamekuwa wakimtuhumu mama yao kuwa amekuwa akiwaloga wajukuu zake na kusababisha wapate wendawazimu na hata vifo visivyoeleweka. “Hivyo, wamepanga njama pamoja na watu wengine ambao tunawatafuta na kuamua kumuua mama yao mzazi," amesema K**anda Mutafungwa.

Imeandikwa na Anania Kajuni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima (Honoris Cau...
03/06/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima (Honoris Causa) kwenye Sekta ya Anga na Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga (Korean Aerospace University) Hee Young Hurr wa kwanza kulia, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea tarehe 03 June, 2024. Wa kwanza kushoto ni Amidi wa Shule Kuu Soo Chang Hwang

KATIBU MKUU CHADEMA JOHN MNYIKA AFUNGA NDOA
29/05/2024

KATIBU MKUU CHADEMA JOHN MNYIKA AFUNGA NDOA

MAKONDA AMSIMAMISHA KAZI MGANGA MKUU ARUSHA KWA UFISADI WA SHS MILLIONI 600Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemsima...
28/05/2024

MAKONDA AMSIMAMISHA KAZI MGANGA MKUU ARUSHA KWA UFISADI WA SHS MILLIONI 600

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemsimamisha kazi Mganga mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Dkt. Petro Mboya pamoja na watumishi wengine wa idara ya Afya wilayani humo ili kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya milioni 600 zilizokuwa zitumike kwenye sekta ya afya.

Makonda ametoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa watumishi hao bado wanaendelea na kazi wakati uchunguzi ukiendelea dhidi yao.

26/05/2024

MOSHI: MKE AMUUA MUMEWE BAADA YA KUMKUTA NYUMBANI KWA MWANAMKE ALYEZAA NAYE

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia Beatrice Elias (36), mkazi wa Mtaa wa Katanini Wilaya ya Moshi kwa tuhuma za kumuua mumewe, Ephagro Msele (43) kwa madai ya kumkuta kwa mzazi mwenzake.

Kwa mujibu wa watu wa karibu na Msele, Mei 25, 2024, Beatrice baada ya kutoka msibani alikokuwa na mumewe, alimfuatilia kila anapokwenda kwa kutumia usafiri wa bodaboda na baada ya mumewe kuegesha gari lake mahali, alidaiwa kwenda nyumbani kwa mwanamke aliyezaa naye.

Inadaiwa kuwa, Beatrice alipofika nyumbani kwa mwanamke huyo, Kitongoji cha Pumuani A, alijificha getini na baadaye aligonga geti na mumewe ndiye aliyetoka kumfungulia.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa baada ya kukutana getini, yaliibuka mabishano kati yao, ndipo Beatrice alipofanikiwa kutekeleza tukio hilo.

K**anda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amedai leo Jumapili Mei 26 kuwa, Beatrice alimvizia mumewe akitoka nyumbani kwa mzazi mwenzake na kumchoma na kitu chenye ncha kali.

“Ni kweli kumetokea hili tukio, usiku wa Mei 25, 2024 saa 3:50 usiku katika Kitongoji cha Pumuani A, Kata ya Kirua Vunjo, mtu aliyejulikana kwa jina la Ephagro Msele, mfanyabiashara na mkazi wa Mtaa wa Katanini, Kata ya Karanga, aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya mgongoni,” amesema K**anda Maigwa.

TANZIA: RAIS WA IRAN AFARIKI KWENYE AJALI YA HELIKOPTA   —— Rais wa Iran Ebrahim Rais amefariki Dunia pamoja na Waziri w...
20/05/2024

TANZIA: RAIS WA IRAN AFARIKI KWENYE AJALI YA HELIKOPTA

——
Rais wa Iran Ebrahim Rais amefariki Dunia pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amirabdollahian na Viongozi wengine ambao walikuwa wakisafiri pamoja kwenye Helikopta ambayo imeanguka Kaskazini Magharibi mwa Iran wakati Rais huyo na Timu yake wakitokea kwenye shughuli ya kikazi mpakani mwa Nchi hiyo na Azerbaijan ambapo hakuna aliyenusurika kwenye ajali hiyo.

Chombo cha Habari cha Serikali ya Iran kiitwacho IRNA kimethibitisha vifo hivyo na kusema tayari Baraza la Mawaziri la Serikali ya Nchi hiyo limekutana kwa dharura, AFP na Reuters wamethibitisha pia vifo hivyo.

Taarifa za vifo hivyo zimethibitishwa baada ya zoezi la kuisaka ilipoangukia Helikopta hiyo kufanyika kwa saa kadhaa hadi usiku wa kuamkia leo na baadaye mabaki ya Helikopta yamepatikana katika mazingira ambayo yameashiria hakuna aliyepona katika ajali.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin alituma Ndege mbili za uokoaji pamoja na Waokoaji 50 kusaidia uokoaji ilipoangukia Helikopta hiyo usiku wa kuamkia leo huku akiahidi pia kuisaidia Iran kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha ajali hiyo ambayo inajiri huku kukiwa na mzozo mkali kati ya Iran na Israel na kupelekea baadhi ya Watu kuhusisha ajali hiyo na mzozo huo ingawa taarifa za awali kutoka Iran zinadai chanzo cha ajali ni mabadiliko ya hali ya hewa angani.

DEREVA AFARIKI BAADA YA KUMGONGA BUNDINTANGA Dereva wa pikipiki ya Afisa mifugo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, Abel Ada...
17/05/2024

DEREVA AFARIKI BAADA YA KUMGONGA BUNDINTANGA

Dereva wa pikipiki ya Afisa mifugo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, Abel Adamson Mwaipopo (25) amefariki Dunia baada kumgonga ndege aina ya bundi na kisha pikipiki yake kupoteza mwelekeo na kuanguka na hatimaye kupoteza maisha yake. Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando amesema tukio hilo limetokea mapema leo katika eneo la Sindeni jirani na kona ya PRS ambapo Dereva huyo alikuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili STM 0232 . Msando amesema “Kwanza naomba nitolee ufafanuzi jambo hili kwani aliyefariki sio Afisa mifugo k**a wengi walivyosema kwani Afisa mifugo wetu wa Wilaya ni Mwanamke na aliyefariki ni Mwanaume Dereva ambaye anamwendesha Afisa mifugo” “Ajali ni k**a ajali nyingime lakini akishahusishwa bundi mara zote tayari kunakuwa na hizo imani za kishirikina na hofu kwa Watu kwamba amegonga bundi kafa na yeye mwenye amekufa lakini vilevile inawezekana kwa kiasi kikubwa labda alivyomuona bundi katika kujaribu kumkwepa hakuchukua tahadhari akapata ajali ni uwezekano vilevile hakuwa amevaa kofia ngumu hivyo katika kuanguka akajigonga akapata madhara akafariki hivyo inawezekana ikawa ni ajali ya kawaida lakini kwasababu imemuhusisha bundi lazima italeta taharuki kuwa inahusiana na mambo ya kishirikina” Msando amesema k**a Serikali ngazi ya Wilaya wana amini ni ajali k**a ajali nyingine zinazotokea barabarani na hivyo ametoa wito kwa wale wote wanaotumia vyombo vya moto hususani pikipiki kuvaa kofia ngumu na kuchukua tahadhari pindi wanapokuwa barabarani na kutokwenda kwa spidi ili kuweza kuepuka kupata ajali.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupamba na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola imefanikisha kuk**...
17/05/2024

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupamba na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola imefanikisha kuk**ata jumla ya kilogramu milioni 1.96 za dawa za kulevya zikihusisha watuhumiwa 10,522 (wanaume 9,701 na wanawake 821) mwaka 2023.

Katika taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema dawa za kulevya zilizok**atwa ni he**in kilogramu 1,314.28, co***ne kilogramu 3.04, methamphetamine kilogramu 2,410.82, bangi kilogramu 1,758,453.58, mirungi kilogramu 202,737.51, skanka kilogramu 423.54 na dawa tiba zenye asili ya kulevya gramu 1,956.9 na mililita 61,672.

Mshauri huyo mdau!
16/05/2024

Mshauri huyo mdau!

Yanga Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania
13/05/2024

Yanga Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania

RAIS Kagame akiwa na mjukuu wake
11/05/2024

RAIS Kagame akiwa na mjukuu wake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya mojawapo ya Gari lililounganishwa katika...
11/05/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya mojawapo ya Gari lililounganishwa katika Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.

WAZIRI WA MAJI JUMA AWESO ASEMA ANAPOWATAZAMA WAKE ZAKE HUWA ANAPATA FURAHA YA KIPEKEE!Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameli...
10/05/2024

WAZIRI WA MAJI JUMA AWESO ASEMA ANAPOWATAZAMA WAKE ZAKE HUWA ANAPATA FURAHA YA KIPEKEE!

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amelieleza Bunge kuwa anapowatazama wake zake roho yake inapata furaha ya kipekee jambo linalosababisha kufanya kazi zake kwa kujituma na kujitoa.

Kauli hiyo ameitoa bungeni leo Ijumaa Mei 10, 2024 wakati akianza kujibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2024 / 25.

Aweso amesema: “Mimi nimeona nijipe wawili ndio maana unaniona ninakiwalaza kwa namna ya kipekee, nishukuru sana familia yangu, wake zangu wapendwa kabisa namuona pale mke wangu mpendwa Kauthar Francis Tarimo lakini pia Zainab Abdallah Issa.”

“Mimi Mheshimiwa Spika (Dk Tulia Ackson) nikiwaona hawa roho yangu baridiii," amesema Aweso.

(Picha, habari na Edwin Mjwahuzi)

LISSU ATUHUMIWA  NA WANACHAMA WENZAKE  KUICHAFUA CHADEMANimeitwa kila aina ya jina baya. Kuna ushirika wa ajabu unaonish...
08/05/2024

LISSU ATUHUMIWA NA WANACHAMA WENZAKE KUICHAFUA CHADEMA

Nimeitwa kila aina ya jina baya. Kuna ushirika wa ajabu unaonishambulia, wapo wanaojiita wanachama wenzangu wanasema haya mambo yanazungumziwa ndani usiyaseme hadharani, ukisema hadharani unachafua chama, hapana ukizungumza hadharani kukemea rushwa unasafisha chama.” – Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA

... 🖐️ 𝗞𝗪𝗔 𝗛𝗘𝗥𝗜 𝗕𝗘𝗡𝗖𝗛𝗜𝗞𝗛𝗔Kocha Abdelhak Benchikha ameachana na klabu ya Simba baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa takriba...
29/04/2024

... 🖐️ 𝗞𝗪𝗔 𝗛𝗘𝗥𝗜 𝗕𝗘𝗡𝗖𝗛𝗜𝗞𝗛𝗔

Kocha Abdelhak Benchikha ameachana na klabu ya Simba baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa takribani siku (156).

Mpaka sasa klabu ya Simba imeachwa na kuacha makocha (8) tangu 2021.

◉ Benchikha — Dec » Apr 23/24 (156d)
◉ Cadena — Nov » Dec 23/23 (28d)
◉ Robertinho — Jan » Nov 23/23 (310d)
◉ Mgunda — Sep » Nov 22/23
◉ Zoran Maki — July » Sep 22/22 (67d)
◉ Franco — Nov » May 21/22 (204d)
◉ Gomes — Jan » Oct 21/21 (280d)
◉ Sven — Dec » Jan 19/21 (392d)

Benchikha aliajiriwa rasmi December 2023. Ameiongoza Simba SC katika michezo (26). Ligi kuu Tanzania bara (13), FA (3), CAF champions league (8) na Muungano (2).

◉ 26 — Mechi
◉ 14 — Kushinda
◉ 06 — Kupoteza
◉ 06 — Sare

𝗕𝗶𝗼𝗴𝗿𝗮𝗽𝗵𝘆 :

Abdelhak Benchikha alizaliwa mwaka (1963) Nchini Algeria 🇩🇿 ana umri wa miaka (61).

𝗧𝗶𝗺𝘂 𝗮𝗹𝗶𝘇𝗼𝗽𝗶𝘁𝗮 :

◉ 2023-24 — Simba SC ›› 26 Mechi.
◉ 2022-23 — USM Alger ›› 34 mechi.
◉ 2022-23 — RS Berkane ›› 11 mechi.
◉ 2020-21 — Difaa El Jadida ›› 44 mechi.
◉ 2019-20 — Mouloudia ›› 29 mechi.

◉ 2018-19 — Al-Ittihad
◉ 2017-18 — ES Setif
◉ 2017-18 — Moghreb Tetouan
◉ 2016-17 — Raja Casablanca
◉ 2015-16 — Ittihad Tanger
◉ 2014-15 — Ittihad Kalba
◉ 2013-14 — Raja Casablanca
◉ 2013-14 — Difaa El Jadida
◉ 2011-12 — Club Africain
◉ 2011-12 — MC Alger
◉ 2010-11 — Algeria Uth (17)
◉ 2009-10 — Algeria Uth
◉ 2007-08 — Club Africain
◉ 2006-07 — ES Zarzis
◉ 2005-06 — Umm Salal SC
◉ 2004-05 — CR Belouizdad
◉ 2002-03 — CABB Arreridj
◉ 2001-02 — Algeria Uth 23
◉ 1999-00 — CR Belouizdad (Assistant)

𝗠𝗮𝗳𝗮𝗻𝗶𝗸𝗶𝗼 𝘆𝗮𝗸𝗲 𝗺𝗮𝗸𝘂𝗯𝘄𝗮 :

🥉 2024 - Robo fainali CAF-CL
🏆 2023 - 🌍 CAF Confederations cup
🏆 2023 - 🌍 CAF Super cup
🏆 2014 - 🇲🇦 Morocco cup
🏆 2007 - 🇹🇳 Ligi kuu

Karibu tena Tanzania Benchikha 🙌

Imeandikwa na Tom Cruz

UMEMSIKIA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM!Mimi sio mwanasiasa wa siasa chafu chafu, nikisema ondoka kwenye mabonde ondoka ...
25/04/2024

UMEMSIKIA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM!

Mimi sio mwanasiasa wa siasa chafu chafu, nikisema ondoka kwenye mabonde ondoka kwenye mabonde. Wapo watu watakaoniuliza sasa mkuu wa mkoa tukiondoka kwenye mabonde leo tutalala wapi? Jibu ni dogo tu, k**a kwenye maji unadhani unaweza kulala, lala, lakini nikikukuta unatandikwa bakora na utaondoka kwa sababu siwezi kukuacha ufe na sisi viongozi tupo.” – Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Waziri Mkuu Mstaafu John Samweli Malecela atimiza miaka 90 LeoAfanya Misa ya shukrani
21/04/2024

Waziri Mkuu Mstaafu John Samweli Malecela atimiza miaka 90 Leo

Afanya Misa ya shukrani

TANZIA: MTANGAZAJI MAARUFU WA CLOUDS GARDNER HABASH AFARIKI DUNIA
20/04/2024

TANZIA: MTANGAZAJI MAARUFU WA CLOUDS GARDNER HABASH AFARIKI DUNIA

RAIS SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA UDAKTARI WA HESHIMA  WA KATIKA UCHUMI NA CHUO KIKUU CHA ANKARA UTURUKI
20/04/2024

RAIS SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA UDAKTARI WA HESHIMA WA KATIKA UCHUMI NA CHUO KIKUU CHA ANKARA UTURUKI

TANZIA: MKUU WA MAJESHI YA KENYA FRANCIS OGOLLA  AFARIKI KWENYE AJALI YA HELIKOPTAMkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jene...
18/04/2024

TANZIA: MKUU WA MAJESHI YA KENYA FRANCIS OGOLLA AFARIKI KWENYE AJALI YA HELIKOPTA

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali Francis Ogolla amefariki katika ajali ya Helikopta ya Jeshi iliyotokea leo Aprili 18, 2024 baada ya kupaa kutoka eneo la Kaben, Marakwet.

Rais William Ruto ametangaza kifo hicho na kueleza, mbali na CDF Ogolla aliyechukua nafasi hiyo Aprili 28, 2023, wengine waliokuwa kwenye Helikopta hiyo ni Maafisa kadhaa wa Jeshi ambao nao wamepoteza maisha.

Rais Ruto alimpandisha cheo Luteni Jenerali Francis Omondi Ogolla kuwa Jenerali na kumteua kuwa CDF akichukua nafasi ya Jenerali Robert Kariuki Kibochi aliyemaliza muda wake.

General Francis Ogolla is dead after KDF Chopper crash

General Francis Ogolla has been confirmed dead after being involved in a Chopper crash at Kaben Cheptulel on the West Pokot - Elgeyo Marakwet border.

At the same time, several senior military officials are said to be among eight officers who are feared dead after a Kenya Defence Forces chopper crashed.

Ogolla took over as CDF on April 28, 2023.

The chopper is said to have been carrying 12 people including officers of the rank of General when it went down.

Witnesses said it burst into flames on crashing.

There was only one survivor believed to be a photographer, other officers said.

The area was cordoned off soon after the accident.

The officers were surveying the area ahead of the planned deployment of more troops to battle cattle rustlers in the area.

Police initially said five officers had died and three survived.

Also on board were other beuratic officers at the Ministry of Defence.

The Kenya Air Force Huey Helicopter had taken off from a local primary school when it went down and burst into flames.

Ogolla was named the new Chief of Defence Forces in changes in the military, taking over from his predecessor General Robert Kibochi.

Kibochi handed over to Ogolla as CDF after attaining the mandatory exit age of 62.

15/04/2024

Thanks for being a top engager and making it on to my weekly engagement list! Yusuphu Mkono, Baraka Yared

Address

Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Uzalendo wa Kitanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Uzalendo wa Kitanzania:

Share

Nearby media companies


Other News & Media Websites in Arusha

Show All