05/11/2023
UJUMBE: KUZALIWA MARA YA PILI.
(Kuna Siri kubwa na nzito, soma hadi mwisho)
Na, Eliudy ML. YoLoGood.
YOHANA 3:1-7
1.Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. 2.Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, Umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye. 3.Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 4.Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5.Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia Ufalme wa Mungu. 6.Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7.Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
UTANGULIZI:
-Kitabu hiki cha Injili ya Yohana, kiliandikwa na Yohana mwenyewe, mmoja wa wanafunzi wa Yesu katika Thenashara, (ndiye aliyependwa sana na Yesu), Yn 13:23; 21:20.
-Huyo ndiye ayashuhudiaye na kutueleza haya yamhusuyo Yesu na Nikodemo, nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli. Yn 21:24.
-Yohana alikiandika kitabu hiki kwa mataifa ya Asia ndogo akiwajuza kuwa "Yesu ni mwana wa Mungu". Anamuelezea Yesu k**a MUNGU, na Uungu wa Kristo Yesu. Yn1:1; 20:28.
____
Ujumbe: Kuzaliwa mara ya Pili.
-Ni muhimu sana tujifunze juu ya hili somo ili tujue maana ya 'Kuzaliwa mara ya pili', na tunawezaje basi kuzaliwa mara ya pili.
-Katika mistari hii michache tutaangazia vifungu vifuatavyo vitatu k**a sio vinne:-
1. UTAMBULISHO WA NIKODEMO-(1)
2. YESU AKIJIBU SWALI (LISILO WAZI) LA NIKODEMO-(2-4)
3. KUZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO-(5), na
4. MBEGU ILIYOPANDWA HULETA MATOKEO YA KILE KILICHOPANDWA-(6-7).
1. UTAMBULISHO WA NIKODEMO-(1)
Mst. 1.Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi".
Ni utambulisho wa Nikodemo, kuonyesha wasifu wake. Alikuwa mtu mwenye cheo kikubwa. Tunafahamu kwamba viongozi wengi katika Uyahudi walikuwa kinyume na Yesu, lakini sivyo kwa Nikodemo k**a tutakavyoona hapa.
2. YESU AKIJIBU SWALI (LISILO WAZI) LA NIKODEMO-(2-4)
Mst. 2.Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, Umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.
-"alimjia usiku"-- Kwa nini usiku??,. alifanya hivyo kwa kificho ili asigundulike na wengine (viongozi wa kiyahudi) walio kinyume na Yesu. Kumbuka alikuwa ni kiongozi mkuu, na harakati za viongozi wakuu ilikuwa ni kumpinga Yesu na hata kujaribu kuwazuia watu wasiende katika mikutano yake wala kumsikiliza na kuongea habari zake.
-"Rabi"-- Alionyesha kujinyenyekesha, kwamba hata yeye ni mwanafunzi wa Yesu (ingawa kwa siri ya moyo wake, kuwa alikuwa akimkubali Yesu...tutaona hapo chini). Rabi maana yake ni Mwalimu.
-"twajua ya kuwa u mwalimu,"-- Licha ya kwamba Yesu ni Rabi kwake, pia alimuona kuwa ni mwalimu, ambaye anaweza kumfundisha, akaelewa vyema juu ya maswali kadha wa kadha aliyokuwa nayo moyoni.(Maswali yasio wazi kwa mwingine yeyote isipokuwa kwake na kwa Mungu pekee).
-"Umetoka kwa MUNGU";-- Kwa hiyo moyo wake ni tofauti na wengine, yeye anamwamini Yesu kuwa ndiye Masihi, ametoka kwa Mungu, hata amethibitisha kwa ishara anazoziona. (Yn 14:11).
_____
Mst. 3.Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
"-Yesu akajibu"-- Akajibu nini? kwani kuna swali limeulizwa?, hebu tazama mst wa pili, hakuna swali lililoulizwa, sasa Yesu anajibu nini??.
--Hapa tunaona kwamba YESU aliujua moyo wa Nikodema na kujua maswali aliokuwa nayo moyoni, kitendo tu cha Nikodemo kufungua kinywa kumueleza anachofahamu juu yake, basi Yesu akajibu moja kwa moja maswali yake.
Note: Kuna kitu Roho wa MUNGU ananifundisha hapa mara hii ninapotafakari, kwamba hicho kitendo cha nikodemo kusema/kutamka yale maneno katika Mst. wa pili ni kitendo cha Kuabudu kwa maneno ya sifa zitokazo moyoni mwake kuelezea ukuu wa MUNGU na uweza wake. Kwa hiyo katika kusifu na kumwabudu MUNGU kwa maneno ya sifa zitokazo katika uhalisia wa moyo, MUNGU hujibu haja ya mioyo yetu hata kabla hatujaeleza kwake, kwa kuwa anatujua mioyo yetu.(Hakuna kinachojificha mbele za MUNGU). Ok, tuendelee,..
Kwa hiyo Yesu akanyooka kulijibu swali lillilo moyoni mwa Nikodemo linalohitaji majibu ya kiualimu zaidi ili apate kuelewa(ndio maana akasema "twajua ya kuwa u mwalimu"). Hilo swali hakuna alijuaye isipokuwa yeye tu na Yesu mwenyewe(kwa kuwa ni MUNGU), hata viongozi wenzake hawajui, badala yake wanajua Nikodemo yupo upande wao....[Moyo wa mtu umebeba siri kubwa sana, MUNGU mwenyewe ndiye afunuaye siri hiyo, tabasamu la mtu na maneno ya kwamba tupo pamoja yasikuaminishe jumla,..... mtake BWANA siku zote, ndiye mwenye siri zote].
-Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.-- Lakini, majibu nayo yakawa fumbo tena, yakaibua tena maswali juu ya swali moyoni mwake. Jibu la Yesu lililenga kumfikisha panapo haja ya moyo wake.
--Hawezi kuuona Ufalme wa Mungu licha hata ya kuuingia??... Kuzaliwa mara ya pili ndio kufanyaje??.
_____
Mst. 4.Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
-Nikodemo akachanganyikiwa zaidi kwa jibu hilo la Yesu ambalo kimsingi linalenga kujibu swali lililoko moyoni mwake, ila halimnyookei kuwa jibu analolitaka lijibiwe, limejibiwa kimafumbo.
-[Kuna wakati Mungu hakujibu direct/sawasawa na ulivyotegemea, anakujibu kwa fumbo la njozi au hata la sauti ya maneno usiyoyafumbua kirahisi]... Kuna wakati MUNGU alinijibu wakati nikiwa mbele zake kwa kinywa cha mtumishi wake, lakini hilo jibu lilibaki kuwa swali kubwa tena moyoni mwangu kwa kipindi cha muda mrefu. Hichi ndicho kilichompata Nikodemo, na ninawaza tu, yumkini aliondoka bado na maswali moyoni kwa jinsi jibu baada ya jibu lilivyokuwa swali juu ya swali.
-Swali lililofuatia la nikodemo, lilionyesha dhahiri kuwa yeye na YESU ni watu wawili, kila mtu yupo ng'ambo yake. Nikodemo alikuwa katika mwili na YESU alikuwa katika roho,... Kwa hiyo ilibidi Yesu amjibu hivyo ili kumvuta toka ng'ambo alioko kuja ng'ambo hii...[Kumtoa katika mwili, kumleta katika roho]. YESU alitutoa toka ng'ambo ile ya Agano la mwili katuleta ng'ambo hii ya Agano la roho, kwa Nafsi yake katika damu, akifanya upatanisho, kutupatanisha na MUNGU, ambao hapo kwanza tulitengwa na kiambaza.
3. KUZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO-(5),
Mst. 5.Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia Ufalme wa Mungu.
-Si tu kuuona sasa, bali hata kuuingia hautaingia kabisa.
-Ni sharti uzaliwe kwa maji na kwa Roho, (Na huku ndiko kuzaliwa mara ya pili).
-Kwa hiyo, ili kuingia katika Ufalme wa MUNGU, ni LAZIMA kuzaliwa kwa maji na kwa Roho.
-Lakini, bado linaweza kubaki tena kuwa swali moyoni, ( na yumkini hata nikodemo alibaki na swali ingawa hajarudia tena kuuliza) Kuzaliwa kwa Maji ndio kufanyaje??... Je, kuzaliwa kwa Roho ndio kufanyaje pia??... Hebu tuone hapa chini.
4. MBEGU ILIYOPANDWA HULETA MATOKEO YA KILE KILICHOPANDWA-(6-7).
Mst. 6.Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7.Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
-Aina ya tunda au ya mazao, hutegemea aina ya mbegu iliyopandwa/kuoteshwa.
-Ipo mbegu katika mwili na mbegu katika Roho iwatofautishayo/itofautishayo.
-MUNGU ni Roho..... Yn4:24; 1Yn 3:9-10; 5:9
1Yohana 5:9-- "Kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho, na maji, na Damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja......."
-Roho, maji na Damu kwa mujibu wa andiko hili, ni hai, ni nafsi hai..... Na dio maana anasema, "watatu hawa", la sivyo angeandika "vitatu hivi".
-Kwa hiyo maji yaliyozungumzwa na YESU kwa Nikodemo sio maji haya ya kawaida tunayoyanya na kuoga. Ingawa wengi katika andiko hili husema amemaanisha kubatizwa katika maji, k**a tunavyozamishwa na kuibuliwa mule katika maji mengi. Sikatai, LAKINI muktadha huu ni wa Kiroho zaidi kuliko Kimwili, kwa kuwa hata ubatizo katika maji (kwa jinsi tufanyavyo katika mwili), hauna maana yoyote k**a ubatizo wa maji katika roho haujafanyika,(ndio kuzaliwa kwa maji). KUNA SIRI NZITO NA KUBWA HAPA... Ngoja nieleze ngaa kidogo...
-Katika kitabu cha 1Yn 5:9, tunaona maji yanazungumzwa kwamba ni nafsi iliyo hai na sio kimiminika. ndio maana akasema "watatu hawa". Ok, hebu tuone hapa tena...
-Efeso 5:26-- "....ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika Neno;"
-Yn 17:17-- "Uwatakase kwa ile kweli; Neno lako ndiyo kweli".
Yn 15:3; 1Pet1:22; Rum 8:9-11;
-Kwa jinsi ya kawaida, tunafahamu kinachosafisha au kwamba tunatumia maji kusafisha vitu kadha wa kadha, hata miili.
-Kwa hiyo katika roho, maji ni NENO la Kristo(NENO la MUNGU). Kwa hiyo anposema kuzaliwa kwa maji anamaanisha kuzaliwa kwa NENO.... Hata hivyo,..
- Tunapozungumzia ubatizo wa maji k**a kuzamishwa katika maji, ni kivuli cha mambo katika roho. Tunapaswa kubatizwa (kuuzika utu wa kale) katika NENO kabla ya ishara katika mwili. Na ndio maana nilisema haina maana mtu kubatizwa katika mwili kwa jinsi ya kawaida halafu katika uhalisia wa roho utu wa kale ungaliko. [SISEMI WATU WASIBATIZWE, ELEWA KWA JICHO LA ROHO]... Petro akasema...
1Petro 3:21-- "Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (sio kuwekea mbali uchafu wa mwili, BALI JIBU LA DHAMIRI SAFI mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo."
SWALI:- Ulishawahi kujiuliza kwa nini Biblia inasema "....askari alipomchoma mkuki ubavuni, mara ikatoka damu na maji"..??..... Kwa nini maji na damu??, kwani hayo maji yaliyotoka yalionekana kwa macho?.
Kwa hiyo KUZALIWA katika Roho, ni kwamba kilichozaliwa kwa Roho ni roho, na kwa kuwa MUNGU no Roho(Yn4:24), basi kitakachozaliwa na Mungu ni roho.
Kwa kuhitimisha, kumbuka kwamba somo letu linazungumzia KUZALIWA MARA YA PILI, tumeona maana yake kwa mapana kiasi chake, kwa mtiririko huo wa vifungu vinne katika mistari hiyo 7.
SWALI:- 1. Je, umeelewa maana ya kuzaliwa mara ya pili??..
2- Je, baada ya kuelewa, unaonaje, umezaliwa mara ya pili??... k**a bado, unachukua hatua gani sasa?.
-Amua leo hii na saa hii, kwa kuwa wokovu ni sasa na sio baadaye; tunapaswa kuzaliwa mara ya pili ili tuweze kuuona na kuingia Ufalme wa Mungu.
MUNGU WANGU WA MBINGUNI AKUBARIKI SANA.
+255763060641; +255625789040.(whatsapp, call, sms)