Radio5tz

Radio5tz Radio 5 is one of Tanzania's most popular Swahili speaking radio station, broadcasting news and entertainment

News segment comprises of accurate; soft and hard local, international and national news. Entertainment segment encompasses Blues, Afro vibes and R&B, of both local (African) and international flavors that provide a rare source of relaxation in the hectic world we live in.

Jisajili Sasa.
12/02/2025

Jisajili Sasa.

07/02/2025
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry William Silaa amesema utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi nchi...
07/02/2025

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry William Silaa amesema utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi nchini umelenga kurahisisha utoaji na upokeaji wa huduma mbalimbali, ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Waziri Silaa ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya kwanza ya Wiki ya Anwani za Makazi 2025.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dkt. Festival Dugange amesema wizara hiyo ni mdau mkuu katika utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi hususan kupitia kwa watendaji wa kata, vijiji na mitaa ambao wana wajibu wa kuwezesha uwekaji wa miundombinu; kuhuisha taarifa; na kukusanya taarifa mpya.

Maadhimisho ya Wiki ya Anwani za Makazi kwa mwaka 2025 yanaadhimishwa kwa mara ya kwanza tangu kukamilika kwa Operesheni Anwani ya Makazi iliyofanyika mwaka 2022, huku kauli mbiu ikisema “Tambua na Tumia anwani za Makazi Kurahisisha Utoaji na Upokeaji wa Huduma”.

Cc.

Mawaziri wa SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC wanakutana leo jijini Dar es Salaam kujadili mzozo wa DRC kabla ya k...
07/02/2025

Mawaziri wa SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC wanakutana leo jijini Dar es Salaam kujadili mzozo wa DRC kabla ya kikao cha Marais wa jumuiya hizo kitakachofanyika Jumamosi.

Kongamano hilo linatarajiwa kutafuta suluhu ya mzozo wa mjini Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na serikali ya Rwanda, ambao wameuteka mji wa mashariki wa Goma, wamekuwa wakikabiliana vikali na majeshi ya serikali ya DRC.

Kulingana na Umoja wa Mataifa zaidi ya miili 2,000, ilipatikana imetapakaa mjini Goma wiki jana kufuatia makabiliano baina ya M23 na wanajeshi wa serikali.

Kongamano la viongozi wa SADC na EAC linafanyika huku kukiwa na changamoto ya kuwaleta wadau wote wa mzozo wa DRC.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi, akiapa kutozungumza na waasi wa M23, huku EAC ikipendekeza majadiliano kati ya wote wanaohusika kwenye mzozo huo.

Cc.

Rais Donald Trump amesaini amri ya utendaji inayoiwekea vikwazo Mahak**a ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), akiituhumu kwa v...
07/02/2025

Rais Donald Trump amesaini amri ya utendaji inayoiwekea vikwazo Mahak**a ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), akiituhumu kwa vitendo vinavyokiuka sheria na visivyo na msingi vinavyoilenga Marekani na mshirika wake wa karibu Israel.

Trump amesaini hatua hiyo wakati Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alipokuwa akizuru Washington.

Novemba mwaka 2024 Mahak**a ya ICC ilitoa hati ya kuk**atwa kwa Netanyahu kwa tuhuma za uhalifu wa kivita huko Gaza, jambo ambalo Israel inakanusha, ICC pia ilitoa kibali cha kuk**atwa kwa k**anda wa Hamas.

Amri ya utendaji ya Trump imesema hatua za hivi majuzi za ICC ziliweka historia ya hatari, ambayo inahatarisha Wamarekani kwa kuwaweka kwenye unyanyasaji na uwezekano wa kuk**atwa.

Marekani si mwanachama wa ICC na mara kwa mara imekataa Mamlaka yoyote ya chombo hicho juu ya Maafisa wa Marekani au raia.

Cc.

Nahodha wa zamani wa Real Madrid Marcelo da Silva ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 36Mbrazili huyo anayet...
06/02/2025

Nahodha wa zamani wa Real Madrid Marcelo da Silva ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 36

Mbrazili huyo anayetajwa kuwa beki bora wa kushoto wa muda wote amethibitisha kustaafu kwake dakika chache zilizopita kupitia ukurasa wake wa instagram

Marcelo anastaafu soka akiwa na kumbukumbu nzuri ya kubeba mataji 6 ya Laliga na mataji 5 ya UCL akiwa na Real Madrid

Kitu gani unakumbuka zaidi katika miaka 20 ya uchezaji wa Marcelo?

Cc.

Sababu moja kwa nini sichukulii Grammy kwa uzito ni kwa sababu kabla ya kutangaza jina lako k**a mshindi, watakupigia si...
06/02/2025

Sababu moja kwa nini sichukulii Grammy kwa uzito ni kwa sababu kabla ya kutangaza jina lako k**a mshindi, watakupigia simu na kukuuliza useme “All Hail Lucif€r” mara tatu. Ikiwa hutatii au hutatoa jibu hilo, basi ndivyo itakavyokuwa. Tuzo yako itatolewa kwa mtu mwingine.

Mimi niko poa sana na mauzo yangu ya rekodi huko Jamaika na katika nchi za Karibea. Mimi si k**a baadhi ya wasanii wa Nigeria ambao watataka kufanya chochote kwa ajili ya utukufu wa kupata tuzo. Huu ni mtazamo wa Shatta Wale, msanii maarufu kutoka Ghana.

Cc.

 :  1 - 1
06/02/2025

: 1 - 1

Address

Njiro Block J
Arusha
P.O.BOX15883

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Radio5tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Radio5tz:

Share

Category