🔴#Live: YANGA SC (0) vs (0) MADEMA(LIVE MATCH)
🔴#Live: YANGA SC (0) vs (0) MADEMA(LIVE MATCH)
🔴#Live: MADEAMA (1) vs (1) YANGA SC(LIVE MATCH)
🔴#Live: MADEAMA (1) vs (1) YANGA SC(LIVE MATCH)
ETI ''MVUA HII SIO YA KAWAIDA, IMELETWA NA MTU''
Na Juliana Laizer, Sunrise Radio Arusha 94.9
Mvua kubwa isiyokuwa inatarajiwa imenyesha katika vitongoji viwili vilivyopo kata ya MFEREJINI wilayani Monduli mkoani Arusha huku wengi wakihusisha na imani nyingine, kwani sio kawaida mvua kunyesha katika majira ya mwezi wa tisa
-
Akizungumza na Sunrise Radio diwani wa kata hiyo SITATO SAKITA amesema mvua hiyo imewashangaza wakazi wengi wa vitongoji hivyo kwani katika miaka ya hivi karibuni hawajawahi kushuhudia mvua ikinyesha tena kwa ukumbwa huo.
-
Kuhusu maoni mseto yaliyokuwa yanasambaa katika mitandao ya kijamii ya wanamonduli kuwa mvua hiyo imeletwa na nguvu zingine, diwani huyo amecheka na kusema kuwa hakuna mwenyeuhakika kuwa mvua hiyo ni ya kawaida au lah, huku akiwasihi wananchi watulie na waache mawazo potofu kwani ni kawaida kutokea.
-
Kulingana na wenyeji, majira ya kawaida ya mwaka wilaya za Monduli na Longido huwa hazipati mvua kubwa katika miezi ya Agoust na Septemba hali iliyowashangaza wengi.
Lori linalosafirisha Mafuta limepinduka na kusababisha Moto mkubwa katika maeneo ya Ubungo jirani na Kituo cha Mabasi Yaendayo Kasi cha Kibo jijini Dar es Salaam
-
Jeshi la Zimamoto limefika eneo la tukio lakini kutokana na ukubwa wa Moto unaowaka eneo hilo, kazi ya uzimaji imekuwa na changamoto
-
Hadi sasa bado haijafahamika madhara kamili yaliyopatikana kutokana na Ajali hiyo ingawa taarifa za awali zinaeleza baadhi ya Nyumba za jirani na Pikipiki 2 zimeteketea kwa Moto huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan Akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT katika Uwanja wa Jamhuri — Dodoma leo terehe 10 Julai, 2023.
Rais Dkt. @Samia_Suluhu_Hassan akikagua gwaride katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo terehe 10 Julai, 2023.
"Nimeenda Bondeni nataka niwahakikishie na nimemwambia ndugu yangu Kadeti 2025 wananchi wa Mto wa Mbu , kuanzia Engaruka -Selela- Majengo hizi kata tatu hamtamuuliza kadeti kuhusu Hilo bonde Tena , tumekubaliana na watu wangu kabla ya tarehe 8 watatangaza tenda mbili , ya kwanza ni kutengeneza Mifereji mikubwa mawili kazi ya pili tutajenga fensi kuzunguka kwenye skimu" HUSSEIN BASHE WAZIRI WA KILIMO
Abiria waliokuwa wanasafiri kuelekea mikoa ya kanda ya Ziwa kwa kutumia Bus la Kampuni ya AN Classic wamenusurika kifo baada ya gari hilo walilokuwa wakisafiria kuanza kuwaka moto katika eneo la Injini.
Imeelezwa kuwa moto huo ulianza kuwaka katika eneo la Kisasa Sheli dakika chache baada ya kuanza safari kutoka kituo kikuu cha Mabasi cha mkoani Dodoma.
Wabunge wakitoka kwa kasi ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya Spika kuwataka kufanya hivyo kufuatia kengele ya tahadhari kulia wakati kikao cha bunge kikiendelea.
Shughuli za bunge zimesitishwa kwa muda hadi dharura hiyo itakapopatiwa ufumbuzi.
Asilimia 95 ya wabunge, wameipigia kura ya ndiyo Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2023/2204 ambayo ni sawa na kura 354.
Akisoma matokeo hayo Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson leo Jumatatu Juni 26, 2023 amesema "Hii ni sawa na asilimia 95 ya kura zote zilizopigwa na wabunge,”
Weeeeh Hii ni kwelly au.?
Serikali imewataka Wabunge kutoa maoni endapo kuna haja ya kurekebisha Kanuni za Utumishi wa Umma kuhusu likizo kwa wanawake wanaojifungua watoto njiti ili wapate muda wa kutosha wa kulea watoto hao wanaohitaji uangalizi wa karibu.
MSIPOKEE NAMBA ZASerikali imewataka wananchi kutotoa ushirkiano kwa watu wanaowapigia simu kwa namba za kawaida wakisema kuwa ni watoa huduma kutoka mitandao ya simu.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew amesema kuwa namba ya watoa huduma ni 100, na hivyo amezitaka mamlaka husika zinapopewa taarifa za uhalifu kutoka kwa wananchi zihakikishe wanawapa mrejesho baada ya kufanyia kazi.
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara amewataka wabunge wote wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaopinga hoja ya Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan wahame chama hicho wakatafute chama kingine.
UPDATES FEISAL
Feisal Salum ameweka wazi kuwa pesa alizochangiwa ili afungue kesi CAS atazitoa kwa Watoto Yatima , Misikitini , Kanisani na kwa wahitaji.
Video credit @azamtvsports
Mwanaume mmoja (30) amekamatwa baada ya kufungua mlango wa dharura wa ndege ya shirika la Asiana ilipokuwa ikitua nchini Korea Kusini, ikiwa bado umbali wa mita 250.
Baadhi ya abiria walikimbizwa hospitalini baada ya kupoteza fahamu na wengine kupata matatizo ya kupumua.