TBCArusha

TBCArusha TBC Arusha 92.1MHz FM owned by

OUR LIVE STREAM LINKS

tbcarusha921.radiostream321.com

tbcarusha921.radiostream12345.com

tbcarusha921.radiostream123.com

Leo katika Hatua Yetu, tutazungumzia mchango wa jamii katika kuzuia upotevu wa maji kwa njia ya kibiashara.Tutakuwa na w...
27/02/2025

Leo katika Hatua Yetu, tutazungumzia mchango wa jamii katika kuzuia upotevu wa maji kwa njia ya kibiashara.

Tutakuwa na wageni maalum:
βœ… Anne Mshana – Afisa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma kutoka AUWSA
βœ… Mhandisi Bahati Munyeti – Msimamizi wa Kitengo cha Kuzuia Upotevu wa Maji kutoka AUWSA

Karibu msikilizaji wa TBC Arusha 92.1 FM!
Ungana na Rehema Lebayo pamoja na Deogratius Lyimo kuanzia saa 9:00 Alasiri hadi saa 10:00 Jioni kwa mjadala mzito na wa kina.

Usikose!

Leo katika Hatua Yetu, tutazungumzia kuhusu kampeni muhimu ya usalama mitandaoni  . Tutakuwa na mgeni wetu maalum, Mhand...
24/02/2025

Leo katika Hatua Yetu, tutazungumzia kuhusu kampeni muhimu ya usalama mitandaoni .

Tutakuwa na mgeni wetu maalum, Mhandisi Fransis Mihayo, Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kaskazini, ambaye atatufafanulia zaidi kuhusu hatua zinazochukuliwa kuhakikisha usalama wa watumiaji wa mitandao.

Ungana nasi kupitia TBC Arusha 92.1 FM pamoja na watangazaji wako Rehema Lebayo na Deogratius Lyimo, kuanzia saa 9:00 Alasiri hadi saa 10:00 Jioni.

Usikose! πŸ”Š

21/02/2025
Leo kwenye Hatua Yetu πŸ“šβœ¨Tunajifunza maarifa yaliyofichika ndani ya Maktaba Huria!Tutakuwa na Anande Pallangyo, Mkurugenz...
19/02/2025

Leo kwenye Hatua Yetu πŸ“šβœ¨
Tunajifunza maarifa yaliyofichika ndani ya Maktaba Huria!

Tutakuwa na Anande Pallangyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jifundishe Organization, akitufunza zaidi kuhusu nafasi ya maktaba katika kukuza elimu na ujuzi.

πŸ“ Sikiliza TBC Arusha 92.1 FM
πŸŽ™οΈ Ungana na Rehema Lebayo na Deogratius Lyimo
πŸ•˜ Saa 9:00 - 10:00 jioni

USIKOSE! β³πŸ“–

Crazy Tuesday on THE STORM madini na burudani unavipata hapa Tune in  92.1 FM Join the Gang:  &
18/02/2025

Crazy Tuesday on THE STORM madini na burudani unavipata hapa Tune in 92.1 FM

Join the Gang: &

LEO, Hatua Yetu inalenga katika kujifunza kuhusu kuwajengea uwezo wafanyakazi na kuimarisha umoja sehemu za kazi.Tutakuw...
12/02/2025

LEO, Hatua Yetu inalenga katika kujifunza kuhusu kuwajengea uwezo wafanyakazi na kuimarisha umoja sehemu za kazi.

Tutakuwa na Komba Muhili, Mkufunzi wa Mafunzo ya Uelewa Sehemu za Kazi, ambaye atashiriki nasi maarifa muhimu katika eneo hili.

Jiunge na Deogratius Lyimo na Rehema Lebayo leo kuanzia saa 9:00 alasiri hadi saa 10:00 jioni hapa 92.1 TBC Arusha.

Usikose!

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene  amesema uamuzi wa Ma...
11/02/2025

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene amesema uamuzi wa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango wa kutoendelea kuwepo katika nafasi hiyo umemshangaza, huku akisema ni uamuzi wa kizalendo na unatoa funzo kwa wanasiasa.

Akizungumza katika kikao kazi cha tano cha Serikali Mtandao kinachofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Simbachawene amesema hatua hiyo ni nadra miongoni mwa viongozi wengi wa kisiasa na inapaswa kuzingatiwa k**a mfano wa uadilifu.

β€œNi uamuzi wa kizalendo, ni uamuzi unaofundisha Tanzania na unafundisha dunia. Maana hata mimi mwenyewe sipo tayari kuuachia ubunge, bado naona ndiyo nakalia vizuri, lakini kwako umeridhika,” amesema Simbachawene

It’s a TBT Vibes 🎡 Catch  on THE STORM Tune in  92.1 FM kuhusu vibe tuachie sisi!
06/02/2025

It’s a TBT Vibes 🎡 Catch on THE STORM Tune in 92.1 FM kuhusu vibe tuachie sisi!

Leo katika Hatua Yetu, tutajadili wajibu wa kiongozi katika kuhimiza na kusimamia maendeleo.Utamsikia Christopher Rutagw...
06/02/2025

Leo katika Hatua Yetu, tutajadili wajibu wa kiongozi katika kuhimiza na kusimamia maendeleo.

Utamsikia Christopher Rutagwelela, Diwani wa Kata ya Osunyai JR, akitoa mtazamo wake.

Karibu ungana na Deogratius Lyimo na Rehema Lebayo kuanzia saa 8:00 hadi 9:00 alasiri hapa TBC Arusha 92.1 FM.

Usikose!

Leo katika hatua yetu, tutajadili kuhusu Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.Tutakuwa na mazungumzo maalum na Mwalimu...
04/02/2025

Leo katika hatua yetu, tutajadili kuhusu Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.

Tutakuwa na mazungumzo maalum na Mwalimu Joseph Pole kutoka Elerai Sekondari, akitupa mtazamo wake kuhusu sera hii na utekelezaji wake kwa vitendo.

Jiunge nasi pamoja na Rehema Lebayo na Deogratius Lyimo kuanzia saa nane hadi saa tisa alasiri, hapa TBC Arusha 92.1 FM.

Usikose!

Leo kwenye kipindi chetu, tunajadili umuhimu wa mafunzo ya Amali katika kukuza uchumi wa Tanzania!Tutazungumza na Ester ...
03/02/2025

Leo kwenye kipindi chetu, tunajadili umuhimu wa mafunzo ya Amali katika kukuza uchumi wa Tanzania!

Tutazungumza na Ester Mwasape, Mkuu wa Chuo cha Help to Self Help, pamoja na Emanuel Mafie, Msajili wa Chuo, ili kufahamu kwa kina mchango wa mafunzo haya kwa vijana na maendeleo ya taifa letu.

Ungana na Deogratius na Rehema Lebayo kuanzia saa nane hadi saa tisa alasiri hapa 92.1 TBC Arusha. Usikose!

Usikose mjadala wa leo kuhusu NIDHAMU YA FEDHA – fursa yako k**a Mwanamke wa Nguvu kujifunza jinsi ya kusimamia fedha kw...
01/02/2025

Usikose mjadala wa leo kuhusu NIDHAMU YA FEDHA – fursa yako k**a Mwanamke wa Nguvu kujifunza jinsi ya kusimamia fedha kwa ufanisi.

Tukio hili litamshirikisha Mgeni Maalum, mjasiriamali na mhamasishaji wa maendeleo ya wanawake, ambaye atatoa maarifa muhimu kwa mafanikio yako ya kifedha.

Jiunge na Rehema Lebayo na Martha Paul kuanzia saa 4:00 Asubuhi hadi 6:00 Mchana kupitia TBC Arusha 92.1 FM kwa elimu hii muhimu.

Usikose!

Karibu kwenye kipindi chetu leo kupitia TBC Arusha 92.1 FM!Leo tunajadili Saratani ya Shingo ya Kizazi, tukiangazia afya...
30/01/2025

Karibu kwenye kipindi chetu leo kupitia TBC Arusha 92.1 FM!

Leo tunajadili Saratani ya Shingo ya Kizazi, tukiangazia afya na njia za kuzuia ugonjwa huu.

Tutakuwa na wageni maalum:
β€’ Muuguzi Mkunga Vaileth Chahe
β€’ Afisa Afya na Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Jamii kutoka Halmashauri ya Arusha, Nancy Njovu

Jiunge na Deogratius Lyimo na Rehema Lebayo kuanzia saa 8 hadi saa 9 alasiri kupitia TBC Arusha 92.1 FM kwa mazungumzo ya kina kuhusu afya yako.

Usikose!

Karibu katika Hatua Yetu leo na TBC Arusha 92.1, ambapo tutajifunza kuhusu magonjwa yasiyopewa kipaumbele.Tutakuwa na Af...
29/01/2025

Karibu katika Hatua Yetu leo na TBC Arusha 92.1, ambapo tutajifunza kuhusu magonjwa yasiyopewa kipaumbele.

Tutakuwa na Afisa Afya na Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Jamii kutoka Halmashauri ya Arusha, Nancy Njovu.

Pia, utamsikia Shaban Mkota, Mratibu wa Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele, akitoa ufafanuzi zaidi.

Ungana na Deogratius Lyimo pamoja na Rehema Lebayo kuanzia saa nane hadi saa tisa alasiri kupitia TBC Arusha 92.1.

Usikose!

Ataelezea jinsi alivyoelimisha jamii yake kuhusu umuhimu wa watoto wa k**e na wale wenye ulemavu kupata haki ya elimu. P...
27/01/2025

Ataelezea jinsi alivyoelimisha jamii yake kuhusu umuhimu wa watoto wa k**e na wale wenye ulemavu kupata haki ya elimu. Pia, atajadili changamoto zinazowakwamisha wasichana kupata na kuhitimu elimu, pamoja na namna mafunzo aliyopatiwa na shirika la Okoa New Generation yanavyomsaidia kufanikisha juhudi za kuelimisha jamii yake.

Karibu mdau wetu, tujifunze pamoja katika kipindi chetu kuhusu Huduma ya Viungo Tiba na Viungo Tiba Saidizi.Kupitia mawi...
27/01/2025

Karibu mdau wetu, tujifunze pamoja katika kipindi chetu kuhusu Huduma ya Viungo Tiba na Viungo Tiba Saidizi.
Kupitia mawimbi ya 92.1 FM, tutajifunza mengi, ikiwemo aina ya wagonjwa wanaostahili huduma hizi.
Usikose kutusikiliza na kufuatilia mazungumzo ya kina na Deogratius Lyimo na Rehema Lebayo!

Address

Arusha Chini

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TBCArusha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to TBCArusha:

Videos

Share