29/01/2024
Hayo yamesemwa leo Jumapili Januari 28, 2024 na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho wakati akitoa ufafanuzi kuhusu madai ya uwepo wa msongamano bandarini kutokana na kutofanya kazi kwa baadhi ya gati.
Mrisho amethibitisha kuwa, gati zote zinafanya kazi na kwa sasa meli zinaendelea kuhudumiwa katika gati zote.
Ameendelea kwa kusema kuwa, kwa leo pekee (Januari 28, 2024) kuna meli 13 kwenye gati zote kuanzia gati namba 0 hadi gati 11 zikiendelea kuhudumiwa na meli 31 zikiwa zinasubiri kuhudumiwa.
Bw. Mrisho ameongeza kuwa, kwa upande wa gati za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), terminal l kuna meli zipatazo 10 zikiendelea kuhudumiwa ambazo zimebeba shehena mbalimbali
“Pale gati namba 0 kuna meli ya MV Yangze 32 inapakua, gati namba 1 kuna meli ya MV Loa Fortune inahudumiwa, gati namba 2
kuna MV African Macaw, huku gati namba 3 kukiwa kuna meli ya MV Tong Da na meli zote hizi zinapakua mizigo mchanganyiko” alisema Bw. Mrisho na kuongeza
“Gati namba 4 hivi sasa kuna meli ya MV Fearless, gati namba 5 kuna MV Anassa, gati namba 6 na 7 kuna MV MSC Nora III, pale KOJ I kuna meli ya MT NCC Abha, KOJ II kuna meli ya MT Lubersac na mwisho pale SPM kuna meli ya MT Torm Hannah ikiendelea kupakua”