Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope inaendelea na shughuli kubwa inayofanyika kwa sasa ni kufungua mitaa yote ya mji wa Katesh na kurejesha mji katika hali yake ya awali kwa kuwezesha shughuli za uzalishaji kuendelea.
Ameyasema hayo mapema asubuhi hii wakati wakikagua kazi zilizofanyika ambapo aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista J. Mhagama, Waziri wa Madini, Antony Mavunde na Viongozi wengine , leo tarehe 6 Disemba 2023.
“Maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha leo kufikia usiku, mji wa Katesh na mitaa yake iwe imesafishwa ili kushughuli za uzalishaji ziendelee kama mnavyoona Wafanyabiasha wameanza kufungua Maduka” amesema Bashungwa
Bashungwa amesema TANROADS kwa kushirikiana na TARURA tayari ameweka mpango kazi wa pamoja ambao utahakikisha kazi hiyo inaendelea kufanyika usiku na mchana mpaka shughuli hiyo itakapokamilika.
Aidha, Waziri Bashungwa amevipongeza Vyombo vya ulinzi na Usalama, kwa kazi kubwa wanayofanya ambapo wamehakikisha wanaleta vijana wa JKT wanaoshiriki katika zoezi la uokozi ikiwa ni pamoja na kusaidia kazi za kurejesha hali nzuri katika mji wa Katesh.
Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama amesema kuwa wanaendelelea kutekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais ambayo jambo la kwanza lilikuwa ni kukabiliana na mafuriko na kuhakikisha matibabu kwa wahanga yanatolewa bure.
Amesema jambo jingine ni kuhakikisha wanaendelea kutafuta miili, kazi ambayo inaendelea na inafanywa na vikosi vya ulinzi na usalama na kuhakikisha wale ambao wanaokolewa wanatayarishiwa maeneo ya kuishi na kupatiwa huduma nyingine za kijamii.
Vilevile , Waziri Jenista ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kupokea michango kutoka sehemu tofauti tofauti kwa ajili ya waanga wa maafa ili kuweza kuwarudisha katika hali yao ya awali.
Kazi hiyo ya kuondoa tope katika Mji wa Katesh Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara na kureje
RC. Makongoro aipongeza Halmashauri ya Kiteto kusimamia kwa ufanisi miradi iliyoletwa na Mh. Rais Mama Samia Wilayani Kiteto ya zaidi ya sh. Bilioni 1.2.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mh. Makongoro Nyerere amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha miradi mikubwa ya maendeleo katika Halmshauri ya wilaya ya Kiteto wakati alipotembelea na kukagua mojawapo ya mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Wilayani hapo.
Mkuu wa Mkoa huyo ameyasema hayo wakati akikagua madarasa mapya kwa shule za sekondari ambazo zimejengwa kupitia fedha za Uviko na ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ikiongozwa na Mkurugenzi wake, John Nchimbi, kwa utekelezaji wa miradi kwa kiwango kikubwa hali ambayo haikuwahi kuwa na mashaka juu ya utekelezaji wa miradi hiyo katika Mkoa wa Manyara.
“Sasa, leo nimekuja kuangalia hawa Watoto walioingia kidato cha kwanza kama wamepata madarasa na viti kama alivyoagiza Mama Samia. Katika hali ya Kawaida tunapopata miradi ya serikali, Siku zote katika Wilaya 7, nyinyi Wilaya hii ya kiteto ni namba moja.” Alisema Mkuu wa Mkoa.
Sambamba na hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, John Nchimbi amesema kuwa mambo yaliyoangaliwa Wilayani Kiteto ni kukamilika kwa wakati Miradi wa ujenzi wa Shule yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Bilioni 1.1 na kumpongeza Rais Samia kwa fedha za miradi zilizosaidia Wilaya ya Kiteto.
“Halmashauri ya Kiteto ina ukubwa wa Kilometa za mraba takribani 16,700, hivyo kuwafanya wanafunzi na wananchi kutembea umbali mrefu kufata huduma mbalimbali. Kwa ukubwa huo unamfanya kila mwanafunzi kutembea Kilometa 15 kuelekea shule, Hivyo serikali yetu imafanya mambo makubwa kuhimiza na kuwekeza katika maswala ya kijamii wilayani Kiteto.“ Aliongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Kwa sasa adha ya wanafunzi waliokua wakisoma chini na kwenye miti imepungua kutoka na takribani Shule 16 ziliwefanikiwa kupata madarasa 4 kila moja yaliyojengwa kwa msaada wa Wananc
Rais Samia aweka Historia Mpya / Sasa Maridhiano Hali Shwari, aunganisha Vyama vyote vya Siasa
Katika kuhakikisha Amani na utulivu nchini Tanzania inazidi kutawala, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anajitoa kindaki ndaki na kuwa mfano bora katika kufanikisha hilo. Wakati Tanzania inatimiza Miaka 30 ya vyama vingi vya siasa, Rasmi anatambulisha mfumo wa 4R yaani Maneno manne yakiwa nguzo katika Kuiongoza nchi. Reconciliation (Maridhiano), Resiliency (Ustahimilivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga upya) ni misingi aliyoiweka kuwa ni Muongozo katika kuiunganisha vyema Tanzania.
Ili kukuza Demokrasia na haki katika nyanja ya kisiasa, Tarehe 23 Disemba 2021, Mhe. Rais aliunda kikosi kazi kikiwa na Wajumbe 24 kutoka Tanzania bara na Visiwani ili kukusanya na kuchakata maoni na mapendekezo ya wadau wa demokrasia wa vyama vya siasa nchini na kuwasilishwa serikalini kufanyiwa kazi na hatimaye kutolewa majibu rasmi Tarehe 3 Januari 2023 huku akivikutanisha vyama vyote vya siasa.
Mhe. Samia alitoa ruhusa ya kuendelea kufanyika kwa mikutano ya hadhara akisisitiza uwepo wa amani huku akiahidi kufanyika kwa mabadiliko ya mifumo ya kisiasa na kisheria na kufanyika mchakato wa katiba mpya huku akiahidi kuendela kufanyika kwa maridhiano na kuwataka Watanzania kuwa wastahimilivu na kuijenga Tanzania mpya.
RIPOTI MAALUM: Rais Samia apongeza Utekelezaji wa Miradi ya maji, Atoa maagizo mazito kwa Wizara
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aelezea mikakati ya utekelezaji wa Miradi ya maji nchini ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wake Mijini na Vijijini inayosababishwa na Mabadiliko ya tabia, Miundombinu chakavu, usambazaji hafifu na ucheleweshwaji kukamilika kwa Miradi ya maji.
Katika Kutekeleza Mikakati hiyo ya upatikanaji wa Maji, Rais Samia afanya mabadiliko ya kimfumo kama vile kuongeza fedha za miradi na Kuanzishwa kwa Wakala wa maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) huku akiongeza Uwekezaji wa Kifedha ili kuiwezesha Wizara kutoa huduma sahihi ambapo Shilingi Bilioni 139 zilitolewa kwenye kukamilisha Miradi ya maji nchini. Vile vile Rais Samia ashauri kufanyika kwa ugunduzi na kuongeza vyanzo vipya vya maji. Aidha Mheshimiwa Rais aliweza kutoa mikopo kwa Mamlaka za maji ikiwemo DAWASA kiasi cha Shilingi Milioni 500 ili kufikisha huduma ya maji kwa wananchi huku akizitaka Mamlaka zingine kujitokeza ili kuwezeshwa.
Mpaka sasa, Miradi ya Maji 218 imeshakamilika, 172 Vijijin na 46 Mijini iemanza kufanya kazi huku Miradi 128 pia imeshatekelezwa. Katika Kutatua changamoto ya maji, Rais Samia aidhinisha ununuzi wa Mitambo 4 kwa ajili ya kufanya utafiti wa vyanzo vya maji, Ununuzi wa Seti 25 za mitambo ya kuchimba Visima, huku akielezea utekelezaji wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda Mkoani Morogoro linalotarajiwa kukamilika mwaka 2025 lenye gharama ya Shilingi Bilioni 329.5 na pia kuitaka Wizara kufanya utafiti wa kutumia maji kutoka Mto Rufiji. Rais Samia pia amezitaka Mamlaka za maji kutokulimbikiza bili kwa wananchi na kuwataka wananchi kulinda vyanzo vya maji na kutoa wito kuvuna maji ya mvua kwa kujenga mabwawa.
RIPOTI MAALUMU: Rais Samia Suluhu Hassan anaeleza chanzo na jinsi ya kukabiliana na mgao wa maji jijini Dar es Salaam. Katika makala hii, Rais anaeleza chanzo cha upungufu wa maji Dar ni kupungua kwa kina cha maji katika Mto Ruvu kilichosababishwa na athari za tabia nchi. Mheshimiwa Rais pia ameeleza hatua zilizochukuliwa na serikali kukabiliana na hali hiyo. Serikali iliingiza maji lita milioni Sabini (70) jijini Dar es Salaam kutoka Kigamboni. Pia serikali imeanza ujenzi wa Bwawa la Kidunda ambalo ndio suluhisho la kudumu la tatizo la maji jijini Dar es Salaam.