Simulizi Zetu

Simulizi Zetu creativity
(1)

16/12/2023

❤️🌹 THE TWINS🌹 ❤️

💖✅EPISODE 02✅💖

Phone kuring nikareceive📲. Joyliz akauliza mbona siz yake amedelay kuishia home🙄. Na mimi huku nadai kumpiga chain kwa pu*ssy😂. Bytha huyu Amanda alikua interested sio ati useme ako cheap😂. Mse k**a dem ako form zako hata mostly u don't need to struggle with a lot of words. We ni kucheza tu kibazenga na uko ndani😂.

Girls like di*ck mse usidanganywe😂. So Amanda akakua confused aende ama abaki. But Joyliz persisted ati Amanda aishie home. Na mimi chuma 🍆 ilikua boiling point 😋.

Amanda=: Pole Abisa I'll have to go maybe next time will spend some day together okay staki kugombana na siz
Me=: It's ok

Nikamdrive hadi kwa gate yao. Tukashuka then Amanda grabbed me slowly and started kis°sing me hapo nje. Actually the girl was in love 😂. Nikamhold poa ungedhani narepare kitu😂. Gate ikafunguliwa Joyliz akatupata 😢💔. Mse sema kuwacha Amanda k**a sufuria moto🔥. Joyliz akatuangalia na vile nikaona amechange sura once akaboil akajam nikajua nimechoma😂. Joyliz alikua na dem flani hivi ameiva sasa huyo kisubmarine lazima nitajua ni nani.

Me=: Ooh joy how's u
Joyliz=: The way i am... Amanda kwani ilikua uishi huko?
Amanda=: Noo was going round the town with Abisa

Joyliz alikua amejam sijui mbona😂. Akanichapa macho zingine kali k**a za mse amefinywa balls😂🙄.

✅ONE WEEK LATER✅

A week passed. One morning Amanda akanicall.

Amanda=: Hey Abisa
Me=: Hello uko poa
Amanda=: Yeah..can we meet today?
Me=: No maybe weekend ju leo naishia Job

The following weekend nikafika place alisema tumeet. Kufika hapo napata ni Joyliz 😂. Joyliz alikua na scratch kando ya maskio so it was easy identifying her ju walikua wanafanana sana. So nikashindwa huyu ako na ajenda gani😂ama anataka tu discuss BBI😂.
Nikapata amebuy juice hapo 🍷.

Me=: Ooh where is she?.. Amanda
Joyliz=: Zii nilitumia phone yake kukucall..i want to talk to you
Me=: Huh Ok go on
Joyliz=: Are u dating my siz Abisa?
Me=: Noo why?
Joyliz=: Naona the way you two are behaving
Me=: Huh but we are not dating... unajua mi hukua friendly so na kila mtu thaz why
Joyliz=: Wow so she's your friend
Me=: Kind of
Joyliz=: Well..but i just wanted to hang around with you today.. Abisa ur a hot dude
Me=: Huh santii

Mambo ndio hiyo😂. Hot dude ataboil hio pu*ssy yako kisubmarine itoke vapour utashangaa😂. So huyu naye alikua on another level. Tukapiga picha kibao na maselfie📸💏. So ye anajua Amanda ni friend wangu💔. Tukatoka hapo tukaishia club. Ye ndio alikua ananishow place anadai tuende ju ye ndio aliniita😁. Tukaingia club hadi first floor 🔥. Ngoma ilikua imeshika so mi ni kufuata haga zake na nyuma k**a bodyguard from Beijing 😁. Kufika tu hivi dem akaniuliza nakunywa nini nikamshow sidai kitu. Akaitisha mzinga moja🍾. Tukastone kiasi zikamshika😁. Dem akaanza kutwerk, nilirombosewa hizo mahaga hadi mzuka ikapanda😋. Dem akakam akanikalia akaanza kunichum akitake pics. So sikutaka azime akiwa na mimi😂.
Akalewa kiasi akaanza kuropokwa

Joyliz=: Abisa... know what..ur handsome....i love you..i loveeee yoooo i love you Abisa..show me your di*ck you small kid

Huyo zikashika😂
Nikambeba k**a gunia hadi kwa dinga nikamdrive hadi kwao soldier akafungua gate nikamueka ndani nikapotea😂. Nikaishi tao kufanya 123 then nikaishia kwa hao. Jioni after supper 🥞 nikatulia nikistream movies. Kiasi text ikadunda pale WhatsApp. Kuangalia ni Amanda amenitext. Kuopen chat nagongana na zile pics Joyliz alikua akinikiss😱😲...

Kuona hizo pics nikajua bazenga nimechoma😱. Kwanza imagine tulipiga na Joyliz then Amanda ndio anazituma🙄. Nikakua confused coz recently Amanda alinicall tumeet kuenda napata ni Joyliz 😲. Kisubmarine nikakosa otherwise. Nikacall Amanda hashiki call. Kucall Joyliz pia hashiki📲😰.
So Amanda amejua nataka siz yake pia na how comes akaona hizo pics 🙄.
Amanda akaanza kunitext

Amanda=: Fu*ck boy unataka kufu*ck mimi ama siz?...i knew...so u wanted to play games and break my heart?
Me=: Amanda i don't know what ur talking about..tunaweza meet tuongee hii mambo?
Amanda=: Kuongea nini na wewe?..am sure uv fu*cked my siz.. delete my number and never call me again

😰Sasa hapo mkuu nimeharibu kabisa. Sijui Amanda alipata aje hizo pics kwa phone ya Joyliz. Nikajaribu kumcall akaniblock. Joyliz pia akaniblock 😕. I was confused kwani ilikua trick ama😂. So nikawachana na story zao hivo.

❤️TWO MONTHS LATER ❤️

Ilikua Sunday nilikua nataka nitoke niishie mahali kuona beshte flani. Kufungua hivi mlango Amanda na Joyliz wakaingia na ule dem walikua naye ile siku🙄. Nikashindwa sasa hawa wamekujia nini.

Amanda=: Hey Abisa leo tumekuja kukutembelea
Me=: Ooh welcome tho natoka
Joyliz=: Just a minute mr handsome

Kusema tu Mr handsome Amanda akanitupia macho😂. Tukarudi tukakaa niskie moshene zao.

Amanda=: Actually Abisa am sorry for sending you the pics...siz alinishow alilewa hadi hakumbuki if she kissed u
Me=: Haina noma am ok
Joyliz=: Am sorry Abisa for making you two disagree...ooh na huyu hapa is our cousin Chloe.
Me=: Hi Chloe...am Abisa
Chloe== Hi..nice to meet you

Nikajua kumbe this ladies wanashare password ya phone 😂, this twins were dramatic 😂.
Nikaleta Juice tukakunywa 🍷. Sijui mbona temptations hunitafuta k**a magnet 😰. Chloe was tempting my eyes with her yummy b***s 😍..i was just staring at her. Akanotice kisubmarine nikawacha hio ufala nisijulikane tena😂. Joyliz sasa amejua mimi na Amanda we have feelings for each other na hio kitu inamuuma sana😂. Then tukatoka. Amanda akanivuta kwa hao nyuma akanipea hug 😍..then we kissed hadi tukasahau tunangojwa😂.

🚆DRIVING DAY🚆

The following day tulielewana nawafunza kudrive. So nikawafunza kudrive kiasi waka master basic skills. Nikawabeba hadi kwao. My love chemistry na Amanda ilikua imeanza kugrow. Nikawafikisha home sikuingia kwa hao juu staki maswali mingi na maparo wao. So Amanda hugged me, then akanikiss kiasi, Joyliz was staring at us🌚. Wakaingia kwa hao so nikiwa natoka kuangalia upstairs huko nje nikaona Chloe...she waved at me😍...

TO BE CONTINUED 🔥

13/12/2023

♥️🌹THE TWINS🌹❤️
✅✅EPISODE 01✅✅
💖SEASON PREMIERE 💖

FOLLOW PAGE Simulizi Zetu
I was taking rounds in my new Mercedes Benz sprinter 🚗 on the outskirts of the town in the evening . Bazenga dinga ilikua mpya so ni full tank kurock tu😂😂. Then nikapita place flani mbele kiasi kulikua na madem wawili nikacheki haga tu kwanza na nyuma zilikua zimeshona k**a number plate ya subaru🍑😋. Nikapause dinga kando yao. Nikawagotea "Hey cuties.. ready for a ride?". Wakaangaliana wakasmile then wakapuase😂😂, wacha wasmile sahii hawajui next maybe I'll be giving them a ride on my bed with flat tires 😂😂. Kisubmarine nikashuka nikafungua wakaingia moja akakaa mbele then ule akaa nyuma. Huyu tumekaa naye haga zimejiseti fity kwa gari hadi karibu nisahau direction niingie kwa kibanda😂😂.

Me=: Oups am Abisa 😊

"Am Joyliz and my siz back there is Amanda"😊

Me=: Wow.. Joyliz and Amanda..u two are amazing 😍... btn wewe na yeye nani mkubwa?😊
Joyliz=: Huh we are twins🥰
Me=: Wow wow... can't wait to have this breed of hottys😋....ur too cute to walk on foot🥰
Joyliz=: Well...our driver isn't available this week.🥰
Me=: Ooh well it's ok😊

Walikua wanaishia tao. So pale kwa ile mirror hukua hapo mbele nilikua naangalia hapo then macho inapatana na Amanda akiwa huko nyuma😂😂. Was just winking at her, then she kept on smiling 😹. Joyliz hakujua bazenga napea siz yake smile huko nyuma😹. Dem ata ni smilia two seconds the next minute anamoan kwa bed yangu k**a ambulance 🚨😹. Kuangalia hapo kwa kio tena nifinyie Amanda macho macho zikapatana sita k**a vidole za pedi🙄, yangu, ya Joyliz na Amanda 😹. Nikajifanya niko serious nikapiga about turn hadi tao😹. Wote wameiva hadi nashindwa nitavuka na mgani. Lakini kiundercover nikatulia unajua pia tamaa iliua fisi lakini nowadays fisi zili evolve hazikufi 😹.

Me=: Do u know how to drive🥰
Amanda=: We don't🥰
Me=: Ok so give me your numbers..nitawacall nikiwa free niwafunze kudrive🥰

Mkuu niwafunze kudrive kwani mi nafanya driving school 😂😂. Nikapewa number 😂😂. Hio ni penalty sasa ni kufunga tu bao😂😅. I'll call them niwafunze kuride gari manual ya two flat tires k**a tuk tuk😂🍆. Nikawafikisha tao wakashuka.

Joyliz=: Thanks Abisa for the ride... please next time utufunze kudrive.🥰
Amanda=: (laughing) yea Abisa come let me give you a hug.🥰

Nikapewa hug sema b***s kugonga chest 😍. Wakaishia wakishake haga 😋🍑 bazenga nilikua nimejishika kwa dinga k**a hawker wa cabbage 😂. Nikadrive hadi kwa hao 🚗. Kuangalia kwa sit ya nyuma napata Amanda alisahau phone yake📱....

Kuona hio phone hapo nyuma nikajua bazenga nitacheza submarine 😅😂. Ilikua almost 7pm na giza ilikua imeshika kiasi 🌌. So nikapack dinga nikaingia kwa hao.

Hio phone ikaanza kuring, kuangalia sikureceive ju nataka hii plan i work kiundercover vile mi nataka😂😂.
The next morning nikaamka then midmorning hapo nikacall Joyliz.

Me=: Hey joy ur siz alisahau phone kwa dinga hapa😊
Joyliz=: Ooh shiet thanks Abisa she thought it has been stolen🥰
Me=: No worries..nitampata aje nimpee🥰

Joyliz akapea Amanda phone tukabonga nikamshow nimpate tao place flani nimpee phone😂. Amanda was a howty manze 🥰😋. Joyliz the twiny, was sexy as well but naona Amanda ako ithaa ile mbaya anajua kucheza na rada😂😂. But i suspected hio phone iliwachwa hapo na mambo flani😂😂..tutajua.

Nikajiandaa nikatoka na dinga hadi tao. Sikumpata hio place, nikangoja for like thirty minutes nikaona anakam solo. I thought watafuatana na Joyliz 😂. Dem alikua amevaa stretcher 🤯. Haga ziko mtaa in full force😋 b***s zimeshona😋. Akafika Akanihug🥰

Me=: Cutie u forgot ur phone🥰
Amanda=: huh never mind was confused🥰
Me=: Fity so can i take u around🥰
Amanda=: Is okay Abisa 🥰

Tukaingia kwa dinga tukachapa rounds nikimpea machocha😂. Then tukaingia kwa restaurant tukadish🥞. After hapo tukarudi kwa dinga.

Me=: So Amanda si leo ujue kwangu ull be coming to visit me na ur siz🥰
Amanda=: Maybe another day....🥰
Me=: Today is another day🙄🥰

Nikadrive hadi home. Tukaingia kwa hao. Chuma kwa boxer uzito imeongezeka hadi boxer line imeraruka😂😂. Tukatulia kwa hao nikaleta champagne 🍷.

Amanda=: Wow Abisa...ur house is classic..unastay na nani hapa🥰
Me=: Huh thanks😊..nakaa solo so why don't you keep me company?😊
Amanda=: Huh time will tell don't worry🥰

Nikatembeza dem kwa hao tukapanda hadi floor ya juu. Di*ck ikakosa adabu tukipanda stares akaona vile pale central kumejaa🍆😂. Akanyamaza tukapanda hadi juu. Nikampeleka bedroom kumshow but ajue next time atakua anaingia huko k**a kitchen 😅😂. Tukarudi ground tukatulia.

Amanda =: Abisa u look like a fu*ck boy😂
Me=: 😂Why...how😂
Amanda=: Jana kwa gari the way u were winking at me🥰😅

Sasa nikaona conversation inakua tamu😂😂. Hapo ameingia kwa mtego sasa. Nikamsongea nikamshika mkono dem akaanza kuchemka😋

Me=: Come on Amanda😊...mi ni boy mpoa tu but u know ur a hot cake😋..ur just cool😊..too hot to assume😋..i like ur as°s😋

Nikamshika haga nikaspank😂😋. Dem akacheka nikajua huyu atajua chuma ikitoka nje hua hairudi ndani na baridi😅😂. Matime zilikua zimesonga ilikua almost afternoon. Nikajua huyu atadoz hapa. Nikataka kukill time asiboeke tukaingia kucheza video game hadi 6pm. Nikaweka pad kando 🎮ju tulikua tumechoka. Nikamsongea nikamhold mkono.

Me=: Amanda look at me😋😊

Eye contact akaniangalia k**a CID😂. Akaanza kusmile zake hapo nikamhold kichwa poa tukiwa hapo kwa sofa 🛋️. Suddenly tukaanza 😘 kis°sing. Phone ikaring 📲. Kuangalia ni call ya Joyliz....

TO BE CONTINUED 🔥🇰🇪

13/12/2023

CHEMSHA BONGO😅😅

-What comes once a year
-Twice in a month
-4times in a week
-6times in a day😅😅

NB/ HATA MIMI SIJUI JIBU😂😂😂😂

11/12/2023

NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA

🔥 SEHEMU YA 60🔥

Tukamuona kijana akikatisha mbele yetu, tukamuita na kusalimiana nae kisha kuanza kumuuliza. Ila kabla hatujamuuliza vizuri, tulishangaa kumuona yule dada wa kwanza aliyekimbia akija na kundi la watu huku wakiwa wamebeba silaha mbali mbali, wengine magongo, mawe, fimbo nakadhalika, halafu wote walikuja tuliposimama mimi na Sam. Hofu ikatutawala na hatukujua cha kufanya.

Wale watu walizidi kuja tuliposimama sisi, yule mkaka tuliyesimama nae akatuuliza kuwa kuna tatizo gani kwani
"Kwakweli hatujui kaka yangu"

Kisha akatuambia,
"Kwa jinsi nijuavyo kijiji hiki, hapa lazima kuna hatari. Ni bora mkimbie tu maana mnaweza kuuwawa bila ya kutarajia"

Tukashindwa kuelewa pa kukimbilia na wale watu walizidi kuja upande wetu. Sam akaona k**avile tunapoteza muda, akanishika mkono na kuanza kukimbia na mimi.

Wale watu wakaanza kutukimbiza sasa, na sisi tukazidi kukimbia huku tukigeuka nyuma na kuangalia walipofikia. Walipofika kwa yule mkaka tuliyekuwa tukiongea nae wakasimama kidogo nadhani walikuwa wanachukua maelezo au kumpa maelezo kidogo ila na sisi tuliendelea kukimbia.

Nikafika mahali na kuchoka sana nikasimama, kugeuka nyuma nikawaona wale watu wote na yule mkaka wameungana kutukimbiza.
Sam akanivuta tena,
"Twende Sabrina hapa si salama"

Tukaendelea tena kukimbia, kwakweli nilichoka na kuhemea juu juu kwani sikujua tatizo ni nini na usalama wangu uko wapi. Kwa bahati nzuri tukaona gari ikikatisha pale njiani, Sam akaisimamisha nayo ikasimama kisha tukapanda na kuondoka huku tukihemea juu juu bila ya kujielewa.

Dereva wa lile gari hakutuuliza chochote ila alitupeleka hadi mjini.
Alipofika mahali pale mjini akasimamisha gari ili tushuke, nasi tukashuka.

Nikafungua mkoba ili nimlipe, wakati nainama kumlipa akaniangalia na kutabasamu bila ya kupokea ile pesa kisha akaondoa gari.
Nilishtuka sana, nikamsogelea haraka Sam na kumkumbatia kwani sikuamini nilichokiona. Yule dereva alikuwa ni yule kijana wa ndotoni, kwakweli niliogopa sana. Sam akaniuliza,
"Kwani kuna nini Sabrina?"

Sikuwa na maelezo kwakweli ila nikamuomba Sam kuwa tutafute hoteli ya karibu ili tuweze kupumzika maana nilihisi akili yangu kuanza kupoteza muelekeo kabisa. Sam hakupingana na mimi bali alikubali na tukafanya k**a tulivyokubaliana, tukatafuta hoteli na kwenda kukaa na kupumzisha mawazo kwanza.

Tukiwa pale hotelini, Sam akaendelea kunidadisi kwani hakuelewa chochote.
"Unajua Sabrina haya mambo ni ya ajabu sana! Inatakiwa kuwa makini sana. Tusishangae tupo hoteli sasa Kigoma ila kufumba na kufumbua tupo baharini tena Dar, inatakiwa uniambie mambo yalivyo usifanye k**a wale wasemao kwenye msafara wa mamba kenge nao wapo, nahitaji tuwe msafara mmoja Sabrina k**a mamba basi wote mamba na k**a kenge basi wote kenge"
"Nakuelewa Sam"
"K**a unanielewa niambie ukweli, lengo la kuja Kigoma ni nini na lengo la kwenda kwenye kile kijiji ni nini?"

Nikapumua kwanza kwani maelezo yangu yalikuwa yakigongana gongana. Sam alitulia kabisa ili nimwambie kinachotakiwa kufanya.
Nikaamua kumwambia kwa kifupi kuwa lengo langu la kuwa Kigoma ni kufatilia familia ya wakina Carlos kwakuwa siwajui, Sam akanishangaa sana na kuniuliza,

"Ulikubali vipi kuolewa na mtu ambaye huifahamu familia yake?"
"Ni historia ndefu Sam, kwa kifupi niliolewa nae bila ya kutarajia."
"Sasa familia yake unaitafutia nini kwasasa?"
"Nahitaji kuijua"
"Unadhani utaipata? Si nilikwambia mimi kuwa Carlos sio mtu wa kawaida ila hukutaka kunisikia. Ungenielewa toka mwanzo basi haya yote yasingekuwepo kwasasa"

Ikabidi nimsimulie Sam kuhusu wazazi wa bandia wa Carlos, naye akashangaa sana. Nikamweleza nilipoambiwa nikawatafute wazazi wa ukweli wa Carlos kwa nia ya kumjua ni nani na pia kuweza kudai talaka.

Sam aliposikia neno la taraka akafurahi zaidi na kuendelea kusema kuwa atakuwa bega kwa bega na mimi katika hili.
"Ila kwavile muda umekwenda sana acha tupumzike halafu kesho tufanye hiyo kazi kwa uangalifu zaidi."

Muda ulikuwa umeenda kidogo, tukaenda dukani na kununua baadhi ya nguo za kubadilisha kisha tukarudi pale hotelini kupumzika.
Sikutaka kushirikiana chochote na Sam, ilibidi tuwe kaka na dada ili kuepuka matatizo yasiyo na lazima.

Wakati wa kulala kila mmoja alilala upande wake ingawa chumba kimoja, namshukuru sana Sam ni mwanaume muelewa na asiyekuwa na papara za makusudi.

Usingizi ukanipitia, ikaja ndoto ya ile siku niliyok**atwa uchawi na kufanya mambo ya ajabu na kushangaza watu kisha nikaliona lile kundi la jana yake likitaka kunipiga.

Nikashtuka sana toka usingizini huku jasho likinitoka kwa wingi, nikamuangalia Sam pembeni ila hakuwepo hapo ndipo uoga ukanishika kuwa ni kitu gani kimempata mtoto wa watu tayari kwani najijua kuwa mimi nina majanga ndiomana nilikuwa nakataa kuja nae huku, sikujua nimuulize nani maana ulikuwa ni usiku. Nikainuka pale kitandani na kutoka nje ili nijaribu kumuangalia alipoelekea.

Nilipotoka nje kabisa ya ile hotel, nikamuona Sam akielekea k**a maeneo ya barabara kuu. Nikaanza kumkimbilia, nilipofika nikamshika mkono wake kwa nguvu huku nikimvuta kuwa turudi ila ikawa k**a kuna mtu ninayevutana nae yani mimi namvuta na huyo mtu anamvuta pia hadi nikaanguka chini. Sam alizidi kuondoka, nikapata wazo la kumuita kwa nguvu
"Wee Sam"

Akashtuka na kugeuka nyuma, akaniona pale chini ila Sam alikuwa k**a mtu aliyepigwa na bumbuwazi kwani alinikodolea macho tu bila ya kusema chochote. Nikainuka pale chini na kumfata tena alipo, nikamtingisha kwa mkono na kumuita tena
"Wewe Sam wewe"

Sasa akashtuka k**avile mtu aliyetoka kuamka, akaanza kunishangaa mimi badala ya mimi kumshangaa yeye, kisha akaniuliza
"Kwani imekuwaje?"
"Imekuwaje nini? Hebu turudi ndani"

Nikamshika mkono na kurudi nae, kwenye mlango wa ile hoteli tukakutana na muhudumu mmoja wapo wa pale ambapo alituuliza kulikoni.

Nikamjibu kwa kifupi kuwa mwenzangu aliondoka gafla tena akiwa usingizini, yule muhudumu akatuambia
"Hii ndio Kigoma jamani kuweni makini"

Kisha akaondoka na kutuacha pale tukitazamana. Nikamshika tena Sam mkono na kurudi kwenye chumba chetu kisha nikamuuliza kuwa anatatizo gani
"Hata mimi sielewi Sabrina"
"Mmh haupo makini Sam"
"Makini gani wakati nilikuwa nimelala jamani, ila gafla nikasikia k**a naitwa hapo ndio nikaitika ila sikujua ni nani aliyeniita ila ndio sijajielewa hadi uliponishtua"
"Usipende kuitika unapoitwa usiku, huwa ni wachawi hao wanaofanya hayo mambo"
"Ila yote ni sababu ya kusahau kumuomba Mungu atulinde Sabrina yani tunalala tu k**a kuku ndiomana tunapatwa na makubwa"

Tukaamua kuomba kisha kulala maana ni kweli tulisahau kufanya hivyo kwakweli. Tukalala vizuri sasa hadi kunakucha.
Mipango ya leo ilikuwa ni Sam kwenda peke yake kwanza kuchunguza kile kijiji hadi apapate kwakina Carlos kisha mimi na yeye tukiondoka twende moja kwa moja kwa wakina Carlos.

Ila nilienda kununua simu kwanza ili niweze kuwasiliana na Sam akiwa huko maana ile simu yangu ya majanga niliiacha nyumbani, kisha Sam akanipa laini yake moja tuweze kuwasiliana.

Nikamsindikiza hadi kwenye mabasi ya kuelekea kwenye hicho kijiji, njiani akanunua kapelo ( mask ) ili aonekane tofauti na wajana kisha mimi nikarudi pale hotelini.

Nilipokuwa pale hotelini, wazo likanijia kuwa huenda wale wanakijiji ndio wale wale walioniona nilipopelekwa kimaajabu. Ingawa mimi mwenyewe sikikumbuki kile kijiji kwasababu ilikuwa kimiujiza lakini huenda wao wakawa wananikumbuka vizuri.

Wazo likanijia kuwa nikanunue nywele za bandia na miwani ili nitakapoenda tena nionekane tofauti. Sikupoteza muda zaidi, nikaenda dukani na kununua nywele za bandia na miwani na mkoba mwingine.

Kununua hivi vitu halikuwa tatizo kwangu kwavile pesa nilikuwa nayo kwa kipindi hicho, ni ile pesa niliyopewa na yule kijana wa ndotoni kwenye bahasha.

Wakati natoka kwenye lile duka la vipodozi njiani nikakutana na kijana ambaye nilikuwa simfahamu kabisa, akanisimamisha na kuanza kuongea na mimi k**avile mtu anayenifahamu
"Za siku nyingi shemeji? Khee umepotea sana"

Nilikuwa kimya nikimtazama kwavile nilikuwa simjui na wala sijawahi kumuona mahali popote pale, sasa huo ushemeji wa mimi na yeye umeanzia wapi? Nikamshangaa tu ila yeye aliendelea kuniongelesha bila ya kujali k**a simjibu wala nini.

Nikaachana nae na kuondoka ila akanifatilia nyuma huku akitaka nimjibu, nilimuangalia kwa hasira sana na kumuuliza
"Kwani unatatizo gani wewe mkaka jamani?"

Akatabasamu na kusema,
"Nilitaka unijibu tu Sabrina"

Nikashtuka na kumuuliza kuwa jina langu amelijulia wapi
"Nakujua Sabrina, wewe ni shemeji yangu"
"Shemeji yako kwa nani?"
"Mwangalie yule"

Akaonyesha kidole kwenye mti mmoja ambapo kulikuwa na mtu kasimama chini yake lakini sikumtambua na kumuuliza tena
"Yule nani?"

Kabla hajanijibu nikashtukia nipo pale chini ya ule mti huku nikitazamana na yule mtu, nikataka kukimbia kwa uogo ila akanidaka mkono na kucheka sana.

Alikuwa ni yule kijana wa ndotoni, aliniangalia usoni ila sikuweza kumtazama mara mbili kwani niliogopa sana na kujiziba sura yangu, akaniuliza tena
"Utaniogopa mpaka lini Sabrina?"

Nilikuwa natetemeka tu, akaendelea kusema
"Ingawa nimekuachia kuwa karibu na umpendae ila bado unaniogopa, naweza kufanya chochote Sabrina hutakiwi kuniogopa sana"

Bado niliendelea kujiziba usoni. Ukapita muda kidogo nikahisi k**a nipo peke yangu, nikajitoa mkono usoni ili kuangalia k**a kweli nipo mwenyewe.

Nikajikuta nipo kwenye chumba cha hoteli, nikashtuka sana na kushangaa kwakweli mambo haya yamekuwa ya ajabu sana kwangu nikatamani hata kukimbia ila nitaelekea wapi? Nilijiangalia mara mbili na kuogopa, nikatoka kwenye chumba kile.

Nikaangalia pale nje palivyo, kwakweli huyu mtu ananitishia sana na kuitoa amani ya moyo wangu kabisa. Nikatazama miti inavyopepea huku nikiwaza mambo mengi hata nikiwaza kuwa kwanini nimekuwa binadamu ambaye nateseka bila sababu za msingi wala nini.
Muda mfupi ukapita pale nje, nikashtuliwa na mtu alikuwa ni mdada ambaye pia sikumfahamu, akaniambia
"Pole kwa usiku wa jana dada"

Nikamtazama na kumuuliza
"Pole ya nini?"
"Nilijua na nyie ni wepesi kumbe wazito eeh! Pole sana kwa usumbufu"
"Mbona sikuelewi dada?"
"Yote ya usiku wa jana ni mimi niliyeyafanya, nilimuhitaji mwenza wako kwa usiku mmoja tu wa jana"

Kisha akaondoka, nilimuangalia bila ya kupata majibu juu yake.
Huyu msichana alinishangaza sana, nikaamua kwenda kukaa kwenye mgahawa ili ninywe angalau juisi huku nikimngoja Sam kwani nilikuwa natamani sana kujua yaliyojili mahali alipoenda.

Nilikaa sana pale ila Sam hakurejea na wala simu yake haikupatikana. Mawazo mabaya yakanitawala ila mwisho wa siku nikaamua kurudi kwenye chumba hotelini.

Nilipoingia nikamkuta Sam ameshafika ndani, inaonyesha kuwa amefika muda mrefu tu. Nikamsalimia na kumuuliza kuwa kwanini simu yake haipatikani
"Hilo swali nikuulize wewe maana muda wote nimekutafuta sijakupata"
"Sawa basi tuachane na hizo habari, nieleze mambo ya uko"
"Huko ni salama sana ila nimechoka kupita maelezo, nadhani itakuwa ni vyema k**a ningepumzika kwanza"
"Ila ungeniambia kwanza ingekuwa vizuri zaidi"

Akacheka na wala hakutaka kuniambia na kusisitiza kuwa anatakiwa apumzike kwanza kabla ya kunieleza. Sikutaka kumlazimisha sana kwahiyo nikamuacha apumzike ila akaniomba nikaagize chakula na kukileta ila atakapoamka apate kula.

Nikainuka kwa lengo la kwenda kutafuta hicho chakula. Wakati nanunua chakula nikapata ujumbe kwenye ile simu niliyobeba.
Nikafungua na kuusoma,
"Usidhani kazi niliyokupa ni rahisi kiasi hicho, wewe ni mwanadamu na lazima upambane ili mwisho wa siku mshindi ajulikane kati ya mimi na wewe"

Nikashtuka sana, nikaangalia namba iliyotuma ule ujumbe sikuona namba yoyote yani hapakuwa na namba kabisa. Nikaacha maagizo pale kwenye mgahawa na kurudi chumbani kwa lengo la kumuonyesha Sam ujumbe huo.

Nilipokaribia kwenye chumba nikashangaa kumuona mtu nisiyemfahamu akitoka kwenye chumba chetu. Nikakimbilia mlango na kufungua ili nione kuna nini. Nikashtuka sana na kuhisi kuchanganyikiwa nilipomuona Sam kitandani akiwa amechomwa na kisu halafu damu zimetapakaa kwenye kitanda kile

Itaendelea…

10/12/2023

NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA

🔥 SEHEMU YA 59🔥

Ile gari ikaja nami nikapanda na kuondoka, moja kwa moja hadi kituo cha mabasi ya mikoani. Nikashuka, wakati namlipa yule dereva nikashangaa kumuona Sam nae akishuka kutoka kwenye lile lile
gari.

Nikamuangalia Sam kwa makini na kumshangaa ila yeye alitabasamu tu na kunisogelea. Nikashindwa hata kuhoji maswali kwa yule dereva kuwa Sam amepanda vipi.

Yule dereva akapanda gari yake na kuondoka, nikamuangalia Sam mara mbili mbili bila ya kumuuliza chochote kisha nikaendelea na safari yangu ambapo Sam akaja mbele.

Niliogopa kuongea nae kwani sikuwa na uhakika k**a kweli ni Sam ninayemjua mimi, na hata k**a ndio yeye kweli amepanda vipi kwenye ile tax? Na mbona sikumuona muda wote hadi nashuka ndio nae anatokea?

Nikakaa kimya nikimtazama mbele yangu huku nikihofia kuwa huenda mauzauza yanaendelea. Akanisogelea na kuanza kuniongelesha.
"Mbona hutaki hata kuniuliza chochote Sabrina?"

Nikawaza moyoni kuwa huenda akawa ni Sam kweli halafu mie nimemchunia, ikabidi nimuulize.
"Kwani umepanda vipi kwenye ile tax maana unanitisha hadi naogopa kuwa wewe si Sam ninayemjua mimi"
"Mimi ni Sam wa ukweli kabisa Sabrina, najua unapoelekea ndiomana nimekuja kukupa kampani"
"Umejuaje ninapoelekea k**a kweli wewe ni Sam wa kawaida?"
"Nimeoteshwa Sabrina, huwezi amini. Afya yangu si njema kwasasa ila baada ya ile ndoto moyo wangu haukukubali kabisa kuona uende peke yako ndiomana niko hapa"
"Hapana Sam haiwezekani kwenda pamoja na wewe, tafadhali rudi"
"Siwezi kurudi Sabrina, nitaenda popote uendapo ilimradi nifanye kitu kukulinda."

Nikajaribu kumshawishi arudi lakini akagoma, nikaona mlolongo utakuwa ni mrefu sana, inaweza kusababisha tukakosa usafiri kabisa. Nikaona ni vyema k**a tukienda kukata tiketi kabisa, nikaongozana na Sam hadi kwenye mabasi na hatukuweza kupata basi la moja kwa moja hadi Kigoma kwa siku hiyo ikabidi tupande mabasi ya Mwanza kisha tuunganishe tukifika Mwanza. Tukapata siti za pamoja na kukaa kungoja safari.

Safari ilipoanza, nikatumia muda huo kumuhoji Sam maswali yangu ambayo yananipa mawazo sana kwa muda huo.
"Eeh niambie uliingiaje kwenye ile tax?"
"Nimeondoka kwetu mapema sana, leo nililala pale stendi kwenu. Dereva wa tax uliyempigia simu nilikuwa nae pale, aliponieleza kuwa anaenda kumchukua mteja na aliponitajia mteja mwenyewe moja kwa moja nikajua ni wewe na kumuomba kupanda. Wewe ulipopanda hukuangalia siti ya nyuma ndio niliyokuwepo Sabrina"
"Ila hii safari ni ya khatari sana Sam"
"Naelewa Sabrina ndiomana nimekuja kukupa kampani, tafadhali usiniondoe Sabrina. Mimi nakujali ndiomana nafanya yote haya"
"Ila unakumbuka mara ya mwisho mimi na wewe kuonana ilikuwa wapi?"
"Nakumbuka, ilikuwa ni guest tukipanga kutoroka"

Hapa ndio nilipokuwa napataka, nikamuuliza kwa makini sasa kuwa ni kitu gani kilitokea mpaka leo ambapo namuona kiukweli,
"Kwakweli hakuna siku ya maajabu k**a ile katika maisha yangu yote. Nilishtuka toka usingizini huku nikiona k**a mawingu mawingu hivi, wewe ukatoka na kuondoka. Alikuja jamaa mwenye misuli mingi na kunikaba, baada ya muda kidogo nikasingiziwa eti nimekaa pale guest siku tatu bila ya malipo. Nikapelekwa polisi, nikakaa huko k**a siku mbili nikatoka. Nikajipanga kuja kwenu ila njiani nikapata ajali, niligongwa na pikipiki"

Akaanza kunionyesha makovu yake inaonyesha aliumia sana, nikasikitika na kukumbuka ile ajali ya Sam wa uongo kumbe ilikuwa ni kweli kwa Sam wangu wa ukweli. Akaendelea kunieleza ilivyokuwa,

"Niliumia sana, na kulazwa kwenye hospitali ya ajabu hata ndugu zangu hawakuweza kufika kwenye hospitali ile. Nilikaa pale hospitali sijui kwa siku ngapi. Siku hiyo bila ya kuelewa wala kutambua, nikarudishwa nyumbani na mtu wa ajabu kisha akaondoka. Mtu yule simjui kabisa, ndugu zangu walinihurumia sana nakumbuka hata Suzy alikuja kuniona ila wewe hukufika. Sikujua sababu ila niliumia sana moyoni, nikiwa pale kitandani na maumivu yangu nikaletewa taarifa kuwa umeolewa na Carlos. Nimejiuliza maswali mengi sana bila majibu ila natumaini leo utanijibu. Tatizo ni nini Sabrina? Je kwavile mimi sina gari na nyumba? Kwavile sina pesa k**a wengine? Ila kumbuka nina mapenzi ya dhati na wewe, nakupenda kupita ninavyojipenda mwenyewe"

Sam akainama, kwajinsi nimjuavyo nikatambua moja kwa moja kuwa Sam analia tu. Nikamuangalia Sam wangu kwa maumivu aliyonayo juu yangu, nikajiweka kwenye kundi la watu wabaya duniani yani watu wanaosababisha maumivu kwa wengine ila kiukweli mimi sikutarajia kumsababishia Sam maumivu kiasi hiki, sikutarajia kuolewa na Carlos ila imetokea kwa bahati mbaya tu kwakweli.

Nikamsihi Sam anisamehe kwanza maana hata kumueleza sikujua nianzie wapi na kuishia wapi, pia mlolongo wake ni mrefu inatakiwa nimueleze wakati ambao mambo yote yametulia. Nikamtazama kwa ukaribu Sam na kumuegamia kwenye mabega yake ambapo akaendelea kunieleza yaliyomsibu kwa siku hizo,

"Nimekuwa kitandani kwa muda mrefu sana huku nikitamani nipone ili niweze kuja kukuona Sabrina. Nilipopata unafuu, nilikuja kwenu majuzi nikamkuta Carlos akiwa nje ya nyumba yenu. Nikamshangaa, kisha akaniambia kuwa k**a nayapenda maisha yangu basi niache kukufatilia. Akanitishia vingi sana, nikapata uoga na kuondoka ila bado nikasema kuwa nitaendelea kufatilia tu hadi nipate jibu la kuuridhisha moyo wangu"

Siku ambayo Sam alikuja nyumbani ni ile siku tuliyoamua kwenda kwa ndugu wa Carlos ili kupata ukweli. Na ndiyo siku ambayo tulimkuta Carlos njiani na pia tukamkuta nyumbani, nikaanza kuoanisha matukio kwenye akili yangu na moja kwa moja ikanijibu kuwa Carlos sio binadamu wa kawaida. Nikampooza Sam kuwa asiwe na wasiwasi tena, naye akanieleza alichoota,

"Usiku wa jana nililetewa ndoto kuwa wewe unataka kusafiri leo ila katika kusafiri kwako huna nia ya kuaga, nia yako ni kutoroka. Nikaumizwa sana na ile ndoto kwani najua unaweza pata matatizo ukiwa mwenyewe ndiomana nikaamua kuja usiku kwa usiku, nimejitolea kwakweli yani liwalo na liwe ila nahitaji kuwa pamoja na wewe katika mapito haya"

Maneno ya Sam yalinipa faraja kubwa moyoni hata moyo wangu ulijipongeza kwa kumpenda Sam, mwanaume anayejua thamani ya mapenzi, mwanaume anayejua raha, furaha na maumizi ya penzi kwakweli nampenda sana Sam mpenzi wangu haya mengine yamenipata tu wala sikutarajia kupata misukosuko ya kimapenzi k**a ambayo nimeipata. Kila muda nitalalamika na kusema sikutarajia ila natakiwa kufanya kitu kwaajili ya kuokoa maisha yangu na familia yangu pamoja na mpenzi wangu Sam.

Sam alionekana kunitazama muda wote wala hakuishiwa hamu kuniangalia k**a ambavyo mimi sikuishiwa hamu kumuangalia yeye.
Tukapitiwa na usingizi ndani ya basi.

Tuliposhtuka tulikuwa Morogoro ambapo kuna baadhi ya abiria walishuka na wengine kupata ili kuendelea na safari.
Nikawaona wafanya biashara wakizunguka kwenye madirisha na biashara zao, nikatamani kununua matunda ili nichangamshe mdomo hata hivyo njaa nayo ilinipata.

Nikafungua mkoba kutoa pesa, ila nikakutana na ujumbe kwenye karatasi ambapo nikalitoa na kulisoma,

"Kwakweli binadamu mnaubahili wa ajabu, pesa nimekupa mimi ila bado umeona ubahili kuchukua ndege ili ufike mapema. Mnapenda mizunguko wakati njia ya mkato ipo. Na ndivyo ilivyo mpaka kwenye maisha yenu ambayo nayo mnayaonea ubahili pia. Unaonyeshwa njia ya mkato ili unufaike nayo ila kwa ujinga wenu mnataka mzunguko haswa wewe Sabrina sijui unamatatizo gani, wenzio wote wanapenda njia za mikato ila wewe unapenda mzunguko. Nadhani utapenda nikikufanyia muujiza mpya kwa sasa"

Nikakisoma mara mbili mbili kile kikaratasi kisha nikamuamsha Sam ili nae apate kukisoma. Alipokisoma akaniangalia na kuniuliza,
"Nani kakupa huu ujumbe?"
"Nimeukuta kwenye pochi"
"Nani kauandika?"
"Hata sijui umeandikwa na nani"

Sam akasema tutulie na tuwe makini sana kwani ule ujumbe ulimpa mashaka haswa lile swala la kusema kuwa atafanya muujiza mpya kwa sasa.

Sam aliniangalia kwa makini sana kisha akaishika mikono yangu kwa nguvu kwa kutumia mikono yake na hata sikumuelewa kuwa anamaana gani kufanya vile ila nikatulia. Muda kidogo usingizi mzito ukatupitia wote wawili.

Kuja kushtuka, hatukuwa tena kwenye lile basi kubwa la mikoani bali tulikuwa kwenye daladala. Moja kwa moja nikatazama pochi yangu k**a ipo pamoja nami maana huu mchezo sikuuelewa kabisa yani, ila pochi ilikuwa palepale miguuni pangu.

Nikamuangalia Sam ambaye alikuwa bado amelala, nikamshtua
"Sam, Sam amka"

Akashtuka k**a mtu aliyeona kitu cha ajabu vile ila muda huo huo tukamuona konda wa lile daladala akisema kuwa tushuke
"Mwisho wa gari jamani shukeni"

Abiria wote walishuka ila mimi na Sam tulikuwa k**a watu waliopigwa na bumbuwazi na kuuliza
"Kwani hapa wapi?"

Yule konda hakutujibu zaidi ya kutusisitiza kuwa tushuke, na tuliposhuka ile gari ikaondoka. Tukabaki tukitazamana tu na Sam, kisha Sam akaniuliza
"Kwani tupo wapi hapa Sabrina?"
"Sijui"
"Tumefikaje fikaje?"
"Sijui"

Sam akaonyesha kuchukizwa na majibu yangu ya sijui wakati ni kweli kwamba sijui chochote wala lolote yani mimi nipo k**a yeye tu alivyo. Kuna mdada alikatisha mbele yetu, nikaamua kumuita na kumuuliza.
"Samahani dada, eti huu ni mkoa gani?"

Yule dada akatabasamu kidogo na kutujibu
"Hapa ni Kigoma mwisho wa reli"

Akacheka tena na kuondoka. Nikamuangalia Sam naye akaniangalia na kujikuta tukisema pamoja kwa mshangao
"Kigoma!!"
"Tumefikaje fikaje Sabrina?"
"Kwakweli sijui hata unavyoniuliza ni kazi bure tu maana hata mimi mwenyewe nashangaa kuwa hii Kigoma tumefikaje, lile daladala tumepandaje na tumepandia wapi hata sielewi naona miujiza tu"

Tukaona mgahawa eneo lile, tukasema ni bora tukapumzike kidogo kwenye mgahawa ule ili kutuliza akili zetu zilizojaa mawazo yasiyoeleweka kwa sasa.

Tukaagiza na chakula ila hatukuwa na hamu ya kula kwani kila mmoja alikuwa na mawazo kuwa tumefika pale kwa namna ipi na kwa mtindo upi.

Nikajua yote haya ni mipango ya yule jamaa wa ndotoni kwani anauwezo wa kufanya chochote atakacho ukizingatia ameshanipa ujumbe kuwa atafanya miujiza yake. Hofu ikanijaa juu ya Sam na uoga kunishika, nikahisi k**a kwenda na Sam hadi kijiji nilichoelekezwa kuwa ni cha kina Carlos ni kumuweka Sam mashakani.

Ikabidi nimwambie Sam kuwa aningoje hapo mjini ili mimi niende ninakotakiwa kwenda, ila Sam akanikatalia kabisa na kusema
"Ilimradi nimeamua kufanya hili basi niachie nifanye. Chochote kitakachotokea kwangu ni juu yangu mimi mwenyewe"

Sikutaka kupoteza muda zaidi, nikawafata wenyeji wa pale na kuwauliza kijiji nitakacho kwenda. Wakanipa maelekezo yote yanayotakiwa, baada ya hapo mimi na Sam tukaianza safari ya kwenda mahali ambako tumepewa maelekezo. Tukapanda gari, Sam akaniuliza
"Una uhakika kuwa hii safari ni ya muhimu Sabrina?"

Nikamuitikia kwa kichwa, Sam hakuelewa umuhimu wa hii safari kwavile hakujua kuwa naenda kufanya nini ila mimi mwenyewe ndio nilijua umuhimu wake.

Natakiwa kufanya hivi ili niinusuru familia yangu pamoja na huyu Sam asiyejua umuhimu wa hii safari kwangu.

Sikupenda kusumbuliwa zaidi na lile jini, napenda kuwa huru ndiomana nimeamua kufanya jambo hili ingawa najua linaweza kuwa na madhara kwangu.

Tulifika kwenye kijiji ambacho nimeelekezwa na kushuka, nikaangaza macho ili angalau nimpate mtu wa kumuuliza. Tukamuona mdada kwa mbali na kuamua kumuita, yule mdada akasogea karibu ila kabla sijamuuliza chochote alianza kukimbia huku akipiga kelele
"Mchawi, mchawi, mchawiiii"

Tukamshangaa sana na kujiuliza kuwa anamaana gani kutuita mchawi wakati hatujamuuliza kitu chochote bado?
Hatukuwa na sababu ya kuendelea kusimama pale badala yake tulitembea tembea ili kuangalia uwezekano wa kumpata mtu mwingine wa kumuuliza.

Tukamuona kijana akikatisha mbele yetu, tukamuita na kusalimiana nae kisha kuanza kumuuliza.

Ila kabla hatujamuuliza vizuri, tulishangaa kumuona yule dada wa kwanza aliyekimbia akija na kundi la watu huku wakiwa wamebeba silaha mbali mbali, wengine magongo, mawe, fimbo nakadhalika, halafu wote walikuja tuliposimama mimi na Sam. Hofu ikatutawala na hatukujua cha kufanya.

Itaendelea…

Address

Siaya

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Simulizi Zetu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share