20/12/2024
#ππ¨π―ππ§πππ«ππ²ππ«
ππππππ πππ πππππ ππ πππππππππππ ππ πππππ
SIKU YA TANO (20.12.2024)
KWA KUZALIWA KWAKE KRISTO KATI YETU KUMETULETEA UHAI NA KUTUFUNDISHA JINSI ITUPASAVYO KUISHI
Hebu tazameni jinsi wazazi wanavyoshughulika ili kujipatia riziki na kuwapa watoto wao hali njema ya maisha. Yesu Kristo angeweza kuwaokoa watu bila ya mateso na kufa msalabani.
Yeye alichagua njia hii ya mateso na kukubali kufa msalabani kutuhakikishia jinsi anavyotupenda alinuia mwenyewe maisha yenye shida. Nabii Isaya alimwita Bwana wa uzima βMtu wa huzuni nyingiβ maisha yake yote yalijaa mateso mengi na tena makali.
Mavutio ya mapendo yake kwetu yalioanza sio tu chache kabla ya kifo chake, lakini tangu kuzaliwa kwake hapa duniani. Alizaliwa katika mazingira ambapo kila kitu kilitumikia kumtesa muda mfupi baada ya kuzaliwa kwake, alilazimika kukimbilia Misri ambako alitumia miaka kadhaa ya utoto wake katika umaskini na taabu. Ujana wake na ubinadamu wa mwanzo ulitumika huko Nazareti kwa kufanya kazi ngumu katika uangalizi wa baba yake mlishi Yosefu. βMtoto akakua, akazidi kupata nguvu akajawa hekima na neema ya Mungu ilikuwa nayeβ¦ Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo, akazidi kupendwa na Mungu na watuβ (Lk 2; 40, 52).
Dhambi zetu zilimtesa Bwana wa uzima. Tumwombe sasa wakati huu kwa namna ya pekee azitawale nyoyo zetu ili tupate kuishi kwa uaminifu na uadilifu mbele zake. Nia yake ni kutuona sisi tulio kundi na fungu Lake tunaishi vyema na kuteseka tu kwa ajili yakeβ msiwalipe watu ovu kwa ovu au tusi kwa tusi; bali watakieni Baraka, maana nyinyi mliitwa na Mungu mpate kupokea Baraka ... lakini hata k**a itawapasa kuteseka kwa sababu ya kutenda mema, basi mna heri. Msimwogope mtu yeyote wala msikubali kutiwa katika wasiwaziβ (1 Pet 3; 9, 14). Yesu Kristo anatuambia hivi: βHeri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme wa Mbinguni ni waoβ(Mat 5:10).
1) Ee Yesu Kristo Bwana na mchungaji wetu mwema, tunayatubu makosa yetu kwako na kwa mateso yako tunajitoa kwako k**a dhabihu iliyo hai yenye kukupendeza. Tuwezeshe kukupenda kuliko chochote. Ee Bwanaβ¦
Wote: Twakuomba utusikie.
2) Ee Bwana, tunakuomba utufundishe kupitia Roho Mtakatifu kuukumbatia upendo wako maishani mwetu na kueneza popote pale ili wote wapate kukujua wewe uliye pekee Bwana na mkombozi wetu. Ee Bwanaβ¦
Wote; Twakuomba, utusikie.
3) Ee Bwana tunakuomba utufanye tuwe vyombo vyako, ili siku zote tuishi katika heshima ya watoto wa Mungu na wafuasi kweli wa mafundisho yako. Tufarijiwe katika pendo lako la milele. Ee Bwana...
Wote; Twakuomba, utusikie.
Tuombe
Ee Bwana Mungu wetu, wewe umezidi kutupenda mno ajabu twakuomba sisi viumbe na watu wako mapendo yako yawake daima, ndani ya mioyo yetu na kujibidiisha kufanana na mwanao katika yote. Roho wako daima atuongoze katika hali na kwa moyo wa kusameheana, tuwe watu na taifa linalokupendeza na linalozidi kubarikiwa nawe siku zote kwa nguvu yako tumshinde Yule muovu ibilisi na kuishi katika kweli yako daima. Ewe Maria Mtakatifu tusaidie kumpenda Mungu aliye nguvu na yote ya maisha yetu.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu, Bwana wetu.
Wote: Amina.