05/09/2024
MALIPO MBALIMBALI
1. Arbuni/Rubuni/Advansi/Chambele/Kishanzu - malipo ya kwanza ya kuzuia kitu kisiuzwe.
2. Risimu - bei ya kwanza ya kukinunua kitu mnadani.
4. Fidia - malipo yalipwayo na shirika la bima kwa ajili ya hasara au maumivu yaliyompata mtu.
5. Zawadi/Tuzo/Takrima/Hidaya - atunukiwacho mtu k**a ni ishara ya mapenzi, wema, ushindi au kwa utendaji mzuri wa shughuli.
6. Karo - malipo ya masomo shuleni.
7. Ushuru - malipo yanayotozwa bidhaa forodhani.
8. Mshahara - malipo ya mfanyakazi mwishoni mwa kila mwezi.
9. Mahari - malipo ya kuoa ua kuolewa.
10. Dhamana - malipo kwa niaba ya mtu ili ahudumiwe au aachiliwe huru kwa muda maalumu kesi au daawa inpoendelea mahak**ani.
11. Kivusho - malipo ya kuvuka daraja, mto au kivuko chochote.
12. Nauli - malipo ya kusafiria.
13. Faini - malipo anayotozwa mhalifu mahak**ani.
14. Kibarua - malipo ya kufanya kazi kutwa au malipo ya usiku.
15. Mtaji - pesa za kuanzishia biashara.
16. Riba - faida inayotozwwa na mkopeshaji au ziada ya benkini.
17. Arshi / Dia - malipo kwa ajili ya kumtoa mtu damu.
18. Rushwa/Kadhongo/Chirimiri/Chauchau/Kilemba/19. Mvugulio - malipo au zawadi anayotoa mtu ili kupata haki asiyostahili.
20. Kilemba - ada ya harusi wanayopewa wajomba wa bibiharusi; pia malipo anayotoa mwanagenzi kwa mhunzi wake baada ya kuhitimu mafunzo yake.
21. Kiingilio - malipo ya kuingia mahali kwa mfano mchezoni au densi.
22. Kombozi - malipo ya kukombolea kitu au mtu.
23. Koto/Ufito - ada anayotoa mzazi kwa mwalimu anapomwingiza mtoto wake chuoni.
24. Ridhaa - malipo apewayo mtu aliyevunjiwa hadhi au heshima yake.
25. Fichuo - malipo anayopewa kijana anapotoka jandoni.
26. Kiinuamgongo/Pensheni/Bonasi - malipo baada ya kustaafu.
27. Kodi - mapato au malipo kwa serikali kutokana na mishahara ya wafanyakazi au mapato mengine.
28. Karadha - mkopo bila riba au malipo ambayo ni sehemu ya mshahara apewayo mtu katikati ya mwezi.
29. Bahashishi - malipo ya kuonesha shukrani.