20/10/2022
CHOMBEZO.
......Model (14)........
.......by fadhili elias......
.......Fb page:fadhili Elias stories.
........ fatilia page hii upate simulizi za kusisimua
LIKE KWA WINGI,BILA KUSAHAU KU KOMENTI&SHARE.
ILIPOISHIA......
"Ninakupenda sana fadhili....wewe ni wangu peke yangu".
Hayo yalikuwa ni mambo aliyokuwa akiyawaza latifah.hakika alikuwa katika mateso makali,latifah alikuwa akitumikia adhabu bila kulijua kosa lake.....
"Ntakutafuta fadhili......."latifah alijiapiza .
Kweli bhana asubuhi ya siku iliofuata latifah alikuwa ndani ya daladala akielekea kule kwenye kampuni anayofanyia kazi fadhili.huko ndiko alikokuwa akipenda sana kuanzia.alipofika akaruhusiwa moja kwa moja kuonana na mr.denis kwa sababu walikuwa wakifahamiana tangu siku ile ya kwanza latifah alipokuja kwenye hii kampuni... .
"Waoo shem karibu,karibu ukae.karibu sana"m.denis alimchangamkia latifah .
"Asante shemu....nimeshakaribia"latifah alijibu.kikapita kimya cha muda kadhaa ndipo mr.denis alipouvunja ukimya huo...
"Mmmnh!!shemu za nyumbani!!??"
"Nzuri tu shemu japo sio sana"latifah aliongea kwa upole ulioashiria kulikuwa na kitu kilichokuwa kinamsumbua.
"Kivipi shemu wangu"aliuliza mr.denis .
"Shemu....rafiki yako ananitesa sana"latifah akatumbua jipu.
"Anakutesa??anakutesaje tesaje yani sijakuelewa hapo".
"Ki ukweli shemu,mpaka muda huu naonana na wewe.....nina k**a mwezi na kidogo sijaonana na fadhili......rafiki yako aliniambia hanitaki wakati sijawahi kumkwaza kwa chochote,tangu niwe nae katika mahusiano.alinitumia meseji yenye maneno makali saana...yaa...nii ku...kuuanzia siii...iiku hiyo aaakaawa...aaa hapatiiikani kwenye simu yake.shemu nisaidie kunirudishia fadhili wangu ninampeeenda.....shemu ninampendaa sana rafiki yakoo....."latifah aliongea hivyo kwa uchungu hali iliopelekea badae ashindwe kuzuia machozi yasimtoke...akajikuta akianza kulia kwa kwikwi.
"Shemu latifah,nyamaza wala usilie.nitamuita fadhili...ntamuuliza juu ya hili kisha tutaju kitakacho endelea"mr.denis aliongea maneno ya kumtia moyo latifah.mr.denis yeye k**a yeye hakufurahishwa na tabia ambayo fadhili alimfanyia mpenzi wake latifah...... .
"Yani shemu,k**a kuna uwezekano naomba uniitie asaivi ninahitaji kuzungumza nae...nina hamu sana ya kumuona mwanaume wangu..please nisaidie"latifah alisema huku uso wake ukionesha masikitiko makubwa sana.wazo hilo mr.denis akaliona kuwa ni jema,akachukua simu yake ya mkononi kisha akabonyeza bonyeza halafu akaweka simu sikioni............
********
Siku hii nilichelewa sana kuamka ndiyo maana mpaka muda huu nilikuwa sijafika kazini.lakini wakati nipo ndani ya gari,mara simu yangu ikaita nilipoangalia aliyenipigia alikuwa ni mr.denis mkurugenzi wangu...nilishangaa sana kwa sababu haikuwahi kutokea kitu k**a hicho.yani mr.denis alikuwa na mida yake maalumu ya kunipigia simu..nikaiacha ikaita kidogo kisha nikapokeaa..... .
"Haloo boss...niko njiani ninakuja"niliongea bila kumuacha mr.denis ajibu
"Uko sehemu gani??"aliuliza hivyo mr.denis.
"Nakaribia mkuu..samahani leo nimechelewa".
"Ok.wahi haraka huku ofisini,ukifika njoo moja kwa moja kwenye ofisi yangu".
"Sawa nimekuelewa mkuu".nilijibu huku moyoni nikijiuliza ni nini kilichoko ofisini mpaka mr.denis anipigie simu?lakini nilishindwa kuelewa.bhasi ndani ya dakika kadhaa tayari nilikuwa ndani ya kampuni yetu..muda huu nilikuwa nimeukaribia mlango wa kuingilia ndani ya ofisi ya mr.denis.nilipo ingia nilipigwa na butwaa baada ya kumkuta latifah amekaa huku akiwa ameshika tama,lakini punde aliponiona aliamka kwa kasi na kuja kunikumbatia.wakati huo mr.denis alikuwa akitazama kile kilichokuwa kikiendelea pale mbele ya macho yake.nilikasirika sana pindi latifah aliponikumbatia kwani kwa sasa nilikuwa sina hisia nae za kimapenzi..... . Ndani ya dakika mbili nzima latifah alikuwa bado amening 'ang'ania,ilionekana alikuwa amenimisi sana.baada ya mr.denis kuona bado latifah alikuwa amenikumbatia akasema...... .
"Shemu hebu kaeni hapo".
Ndipo latifah akaniachia na kurudi kukaa kwenye sehemu niliomkuta amekaa mwanzo....nami nikakaa kwenye kiti kingine ambacho kilikuwa kinatazamana na kiti alichokikalia latifah... .
"Fadhili huyu ni nani wako?"lilikuwa ni swali kutoka kwa mr.denis,akiniuliza mimi.
"Huyu ni ex girlfriend wangu"nilijibu
"Tangu lini.....na kwa nini hukuniambia?".
"Tangu mwezi mmoja uliopita,na ilikuwa ni personal issue ndio maana sikutaka kukuambia".
"Alikufanyia nini huyu mwanamke mpaka ukafikia hatua ya kumwambia kuwa humtaki"mr.denis aliniuliza tena.
"Ni maamuzi tu.mwanamke huyu hajanifanyia chochote kibaya kilichopelekea nimuache...ilaaa kuna sababu zangu binafsi zilizonifanya nisitishe mahusiano nae".
"Huoni k**a unamtesa?.hujiulizi mwenzio alijisikiaje pindi ulipomwambia kuwa humtaki??hebu kuwa na huruma na mwenzio bhana....shemeji yangu anakupenda sana,tena sana.please k**a kuna tofauti zenu zozote naomba mkazungumze,leo nakupa ofa ya kupumzika nenda mkayajenge na mwenzio then utanijulisha.sitaki discussion na wewe....over.ukumbuke niliokwambia siku za nyuma kuwa mimi ni k**a kaka pia ni mshauri.kwa muda huu nimesimama k**a kaka wala sio boss au mshauri.hivyo ninakuamuru nendeni mkayazungumze"mr.denis ak**aliza kuzungumza kisha akatutaka tutoke.bhasi tukaongozana mimi na latifah mpaka nje.
JINSI ILIVYOKUWA KWA JINI SURYATH.
jini suryath baada kutoweka kule kwenye chumba cha fadhili baada ya kupigwa na radi,alitokezea kwenye makaburi ya buguruni.huko alilia sana...... .
"Hiiiii hiiiiiii hiiiiii........hizi kazi zingine hazifai,watu wana mungu wao wananiagiza mimi niende nikafe...hihiii
iii,yule mtu hawezekani ulinzi alionao ni hatari...aaiiiyaaa ebu ona mwili wangu unavyoniuma...ngoja kwanza niende kwa mkuu"jini suryath alijiongelesha mwenye huku akilia k**a mtoto,alipomaliza kusema hivyo akatoweka kuelekea kule kwa mganga adobe,gongola mboto.
ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua jini suryath alikuwa ndani ya kijichumba cha mganga adobe.mganga adobe kwa sababu aliujua ujio wa jini huyo moja kwa moja kwa moja akaanza kuzungumza nae...... .
"Suryath umekamilisha kile alichokuagiza salimuuu???"aliuliza mganga adobe,jini suryath akainamisha kichwa chake chini kisha akasema... .
"Mkuu...nimeshindwa"jini suryath alisema,kauli ile ilimkela sana mganga adobe.alimuona jini huyo kuwa ni mzembe .
"Suryath......suryath....suryath unaleta utani na kazi si ndio??yule ana nguvu gani za kukushinda wewe ee suryath kuna binadamu yeyote anayekushinda nguvu??....ebu niambie ilikueje mpaka ukashindwa na mtoto mdogo k**a yule"alifoka mganga adobe .
"Mkuu,yule kijana ana lindwa mnoo,siwezi kumdhuru wala hata wewe pia hutoweza ana nguvu za ajabu sana kijana yule"alisema suryath huku bado akiwa ameuinamisha uso wake chini .
"Hahaaahaaaaaa....suryath umefikia hatua ya kunidharau si ndio.ninani anayeweza kushindana na mimi.......ni naniiii nakuulizaaaa???"hakika mganga adobe akacharuka akaanza kuimba nyimbo za kuwaita mashetani wake.....
"Ooohhh haiiiiiyaaaaa nane soje nsikuona nomyagwe yakigamba mgambile mbuliiii,sonho nali wamanya wa ukayaaaaa.....haiiiiiyaaa tyaaaa tyaaaa ooooopsuuuuuu"aliimba hivyo mganga adobe akirudia rudia maneno yake ya mwanzo karibu mara nne.mara moshi ukafuka katika kile chumba yakatokeza majitu matatu ukimchanganya na jini suryath jumla wakawa wanne .
"Ziiindaaa....,nombiii,naweliyaah.....nimewaita hapa kuna tatizooooo,huyu mwenzenuuu nilimuagiza kazi leo ya kwenda kumfanya kijana mmoja anaitwa fadhili ili awe kichaa,lakini ameshiindwaaa hahaahaaaaa,sasa ninawaagiza ninyi mulishughulikie hilooo....huyu suryath hawezi kitu....ameumia sana.nawapa siku tatu muwe mmeshafanya hiyo kazi haya potea"mganga adobe aliwatuma mashetani wake kwenda kuifanya kazi ambayo suryath aliishindwa.suryath yeye aliambiwa abaki ili apatiwe matibabu kutokana na kuwa mwili wake ulikuwa na vidonda vya kuunguzwa na radi.
Wale mashetani watatu wakatokea makaburi ya kinondoni huko walienda kufukua maiti ya mtoto wa miezi sita aliyekufa kwa kuunguzwa na moto.ili wamtafune k**a kitoeo,na kwa ajili ya kuongeza nguvu zao za kishetani.baada ya kumaliza wakaweka kikao ili kupanga namna ambayo wataweza kufanya ili kukamilisha kazi waliopewa na mkubwa wao.bhasi walipanga kuifanya hiyo kazi usiku wa siku iliokuwa inafuata.kwa sababu siku hiyo usiku wake tayari ulishaanza kuisha kwani mida hiyo ilikuwa k**a saa tisa na nusu kuelekea saa kumi za asubuhi.zinda ambaye alikuwa ndiye kiongozi akawaamuru waende kupiga kambi kwenye makaburi ya buguruni ili kuingoja siku iliokuwa ikifuata.
*****
Upande wa salimu alipoamka asubuhi bado alikuwa na furaha sana kwani aliamini asubuhi hiyo ni lazima atasikia habari juu ya fadhili kuugua ugonjwa wa ukichaa.lakini alishangaa mpaka inafika saa nane mchana bado alikuwa hajasikia ata fununu za habari alizokuwa amezitarajia kuzipata...furaha yake ikaanza kufifia kadri dakika zilipozidi kusonga mbele....mwisho huzuni ikaugubika moyo wake hasa baada masaa kufikia kumi na moja tangu palipopambazuka.salimu alishindwa kuelewa tatizo lililofanya mpaka muda huo kusiwepo na taarifa zozote kuhusu fadhili.lakini kuna muda alijipa matumaini kwani mganga adobe hakuwahi kumuangusha.salimu akazidi kusubiri mpaka saa tatu za usiku hakukuwa na chochote alichokisikia....
MASAA SABA NYUMA(UPANDE WA FADHILI).
tulipotoka ndani ya jengo,nikambadilikia latifah.
"Haya wee....kilichokufanya ukanyanyua miguu yako na kunifuata ni nini?? Si nilishakuambia kuwa usinitafute,kilichokufanya unitafute!!"niliongea kwa hasira .
"Fadhili subiri bhasi tutafute sehemu tukae tuongee,please sio vizuri kupayuka payuka ovyo tukiwa hapa njiani....umenielewa mpenzi"latifah alisema kwa sauti ya kubembeleza .
"Latifah,hilo jina la mpenzi ukome kuniita...mimi si mpenzi wako....hebu chukua time yako.usijisumbue kunipenda latifah ....coz mi na wewe mapenzi yetu yalishakwisha kitambo so niache niendelee na maisha yangu ok??"bado niliongea kwa paniki .
"Sio kirahisi kukuacha fadhili....yani hata ukisemaje mimi kukuacha never.sahau kabisaaa....,faadhili ebu nionee huruma mtoto wa mwenzio.unanitesa pasipo sababu...ebu angalia nilivyodhoofika sababu ya kukuwaza wewe...faaadhili amini ninakupendaaa.au niambie unataka nifanye kitu gani ili utambue thamani ya mapenzi yangu kwakooo ee nielewe bhasiii".
"Latifah yani unachokiongea kinaingilia sikio langu la kushoto yanatokea sikio la kulia...kiufupi unapigia mbuzi gitaa siwezi kukuelewa,penda sehemu nyingine kwangu the space is full".
"Usiseme hivyo......faadhili unaniumiza sana please nikubalie,fadhili naomba unipe nafasi tena...siwezi kuishi bila wewe mimi jamaniii.....please.....pleeee eeeaaaase nakuombaaa...nakuomba saana sanaa unielewe"latifah aliendelea kunibembeleza.lakini ki ukweli moyo wangu ulikuwa hautaki kusikia chochote.nilichoamua kwa wakati huu ni kuondoka na kumuacha latifah akiendelea kunilalamikia.....
"Nooo....fadhili usiondokeee....please come back to meeee"latifah aliongea huku akilia pindi alipoona nimeanza kupiga hatua ili kuondoka.....si
kumsikiliza mi niliendelea kuichapa miguu kuisogerea daladala moja iliokuwa imesimama karibu yetu nikapanda kisha daladala ikaondoka kwa kasi.sikujua latifah alikuwa na hali gani huko nilikomuacha.
USIKU WAKE.
usiku wa leo k**a ilivyokuwa jana niliwahi kulala,lakini sikukumbuka kuomba k**a siku iliopita.muda mchache baada ya kupitiwa na usingizi nilianza kuota ndoto mbaya sana...niliota nikikimbizwa na mtu aliekuwa na sura ya kutisha sana huku mkononi akiwa ameshika panga.mtu yule alikuwa akikimbia kwa spidi kuliko mimi hali iliopelekea mtu yule kunikaribia kisha akanikata mtama ulionipelekea kuanguka chini huku nikiwa nimetazama juu,yaani nilikuwa nimelala kichali chali.mtu yule bila kuchelewa akachukua panga lake na kulididimiza tumboni kwangu...nikajikuta nikiamka huku nikipiga kelele... .
"Mama nakufaaaaaaa"nilisema pindi nilipokuwa nashtuka usingizi,muda huo nilikuwa nalipapasa tumbo langu..k**a kulihakikisha k**a zima..lakini ukweli ulibaki kuwa sikuwa nimechomwa panga wala nini bali ilikuwa ni ndoto.ndipo nilipokumbuka kuwa usiku huo sikuwa nimeomba...labda ndio maana ilinitokea hali ile.nikapiga magoti nikiwa juu ya kitanda kisha nikasali kwa muda wa dakika kumi ndipo nikalala.
USIKU WA MANANE.
wale mashetani walitia timu kwenye nyumba ya fadhili.....lakini kila walipokuwa wakiingia katika chumba walichokizania kuwa fadhili alikuwemo walikuta patupu.walizunguka karibu mara tano katika kila chumba kwa kurudia rudia lakini holaa hawakufanikiwa kumuona..... .
"Huyu mtu kaenda wapi??"aliuliza nombii.
Swali hili alilouliza nombi lilikuwa halina sababu ya kuulizwa mahali hapo,kwa sababu wote watatu hawakuwa wakijua ni wapi aliko fadhili,hivyo kipindi nombi anauliza kuwa fadhili yuko wapi ni k**a alijiongelesha mwenyewe.... .
"Jamani eeh,huyu mtu yuko wapi?"nombi tena alirudia kuuliza swali lake lile lile la mwanzo,swali hilo liliwakera wenzake...ndipo zindaa akasema.... .
"Hivi nombi una kichaa?,wote tunatembea pamoja alafu unauliza utumbo.sasa unayemuuliza ni nani ilhali kati yetu hakuna anayejua huyo mtu aliko......"zindaa aliongea kwa ukali. .
"Samahani mkuu"nombi aliomba radhi kwa mkuu wake ambaye ni zindaa. . Bhasi zinda k**a mkuu wa msafara akawaamuru wenzake kuwa wajaribu tena kuzunguka pengine wanaweza kumuona.wakaanza kuingia chumba kimoja baada ya kingine,lakini hali ilikuwa ni ile ile,kuwa vyumba vilikuwa ni vitupu. .
"Jamani....mimi ninahisi tumeingia sehemu ambayo ni ya hatari,huyu mtu tuliyetumwa tumuangamize pengine ana nguvu nyingi kutushinda sisi,hivi hamuoni kuwa tumeanza zamani kuzunguka ndani ya vyumba lakini tunaambulia patupu....hii hali inaashiria hatari kwa ninavyoona"alisema naweliyah,wazo au jambo hilo aliloliongea naweliyah kwa upande mwingine lilionekana na ukweli.kwani zindaa k**a kiongozi wa msafara huo alitikisa kichwa k**a ishara ya kukubaliana na kile alichokiongea naweliyah... .
"Naweliyah......kitu ulichokiongea ni sahihi kabisa.inavyoonekana huyu mtu ametuzidi ujanja kwa leo kwa sababu haiwezekani eti tuzunguke nyumba nzima tumkose haiwezekanii.....kabisaa"aliongeza kusema hivyo zindaa.
"Sasa mkuu,tunafanyeje??"aliuliza naweliyah.
"Tuondokeni....tutakuja kesho.twendeni tukaongeze nguvu"aliamuru hivyo zindaa kisha kwa pamoja wakatoweka.
*****
chumbani fadhili alikuwa katika usingizi mtamu sana.,kipindi wale mashetani wanahangaika yeye alikuwa katikati ya ndoto nzuri na ya kuvutia.wale mashetani kwa akili yao walijua kuwa fadhili hakuwemo humo ndani kumbe fadhili alikuwemo sema wenyewe hawakumuona.yani katika zunguka yao katika vyumba,walikuwa wakiingia mpaka kwenye chumba alichokuwamo fadhili lakini kwa sababu chumba hicho kilitawaliwa na ulinzi wa malaika mashetani wale walipigwa upofu wa kutokumuona fadhili.kijana huyu alikuwa maili nyingi sana katika ndoto ambayo ilimshawishi aendelee kunogewa kulala.katika ndoto yake aliota kuwa,alibahatika kuokota sarafu mpya,alifurahi sana kwa sababu aliipata sarafu ambayo haikuwahi kuguswa na mtu wala kutumiwa na yeyote....bhasi kuwa na ile sarafu akajikuta akiitumia,yeye ndiye akawa wakwanza kuigusa na kuitumia.baadae zikaanza kujitokeza bahati za kuokota sarafu mara kwa mara,lakini sarafu hizi hazikuwa mpya k**a ile ya mwanzo,yani zilionekana tayari zimeshatumika.kijana huyu alitokea kuzichukia sarafu hizi ambazo zimetumika,kuna muda akajikuta akiikumbuka ile sarafu yake ya kwanza aliobahatika kuiokota.hakika aliiona kuwa ile sarafu ilikuwa nzuri na yenye thamani maishani mwake.akajaribu kuanza kutembea tembea mtaani pengine angebahatika kuipata kwa mara nyingine lakini hakufanikiwa.
kuna siku alikuwa katika matembezi yake ya kawaida,katika hali asiyoitegemea akajikuta akiiona ile sarafu tena.cha ajabu sarafu ikamwambia kuwa...kwa sababu yeye(fadhili)alikuwa wa kwanza kumpata na kumtumia alijikuta akitamani kuendelea kutumiwa na yeye tu,hakutaka tena kuguswa wala kutumiwa na mwingine isipokuwa yeye fadhili,hakika fadhili alifurahi sana...bhasi akataka kuinama ili aiokote...ghafla akatokea mtoto na kuikwapua ile sarafu kisha akakimbia nayo.....,ndoto ilipofika hapo fadhili akashtuka kutoka usingizini.....
****
nilishtuka usingizini nikiwa na maswali mengi juu ya ile ndoto ya sarafu nilioiota muda mchache.nikajaribu kuitafutia maana ile ndoto nikakosa.bhasi nikaamua kuipuuza kwa kuona kuwa labda ilikuwa ni ndoto ya kawaida tu,isiyokuwa na maana yeyote.mida hii ilikuwa tayari ndo kwanza mapambazuko,yaani asubuhi ya saa kumi na mbili.nikajikokota taratibu nikashuka kwenye kitanda.nikasali kisha baada ya hapo nikaingia bafuni kuoga.nilipotoka huko nikawasha jiko langu la umeme kwa ajili ya kujiandalia kifungua kinywa kabla ya kwenda kazini.nilichukua unga wa ngano kidogo nikaweka kwenye sufuria kisha nikachota chumvi kidogo nikatia ndani yake ili vichanganyike na ngano.baada ya hapo nikachukua maji ya uvuguvugu ambayo tayari nilikuwa nimeshayaanda.nikatia kwenye sufuria yenye ngano.nikakoroga ili kupata kimiminika kizito.baada ya kukoroga vizuri nikapasulia mayai manne ndani yake kisha nikakoroga tena.hapo nilikuwa naanda kwa ajili ya kutengeneza chapati za kumimina.bhasi niliendelea na hatua baada ya hatua mpaka nikakamilisha kupika chapati za kumimina.ilipokuwa inafika saa mbili kasoro,tayari nilikuwa mezani nikipata staftahi saaafi kabisa ambayo niliiandaa mimi mwenyewe.saa nne ilinikuta nikiwa kazini k**a kawaida nikiendelea na majukumu yangu.
SALIMU baada ya kuamka alitegemea atakuta taarifa zozote zinazomuhusu fadhili,lakini alishangaa kutokusikia angalau vijimaneno neno vyovyote vinavyomuongelea adui yake huyu.kichwani akabaki anajiuliza labda mganga adobe amemdanganya kwa awamu hii.kwa sababu siku za nyuma alikuwa akiyapata matokeo kwa haraka sana.k**a kuna siku alikwenda kuchukua dawa ya mapenzi..pindi alipoitumia akajikuta akitongozwa na rebecka yule demu ambaye fadhili alimkuta salimu yupo nae chumbani wakifanya mapenzi(k**a unakumbuka sehemu kwanza ya chombezo hili).bhasi ndo maana sasa akawa anategemea matokeo ya haraka k**a yale ya mwanzo......
"Daaa!!huyu witch doctor amekuwa mzinguaji siku hizi...mbona mpaka asaivi sijasikia chochote kuhusu mshikaji??aaah ngoja nimuibukie aka ni tell k**a ishu iko guda mi nijue.siyo mi nimechili nadhani mshikaji teyari ameshakuwa mento kumbe mchizi mzima"salimu aliwaza huku akijinyanyua kuanza kwenda kituo cha daladala.moja kwa moja safari ikaiva mpaka kwa mganga wake adobe.alipofika akakaribishwa ndani....
"Nadhani kijana wangu..ujio wako ni kutaka kujua hatima ya kazi uliyonipa si ndioooo.......hahahaaaahaaaa"aliongea mganga adobe."Ndiyo mtaalamu.."salimu alijibu .
"Hahahaaaaaahaaa...sawa sawa.eeeeh kijana wangu kwa usiku wa jana imeshindikanaaaa.iiiihahaaaah aaaaa.....lakini,lakini,narudia tena lakini!! Kwa leo haiwezi kushindikanaaaa".
"Imeshindikana!!??imeshindikanaje tena mtaalamu???"salimu alihoji.
"Salimu....kijana unayetaka kumdhuru anaonekana yupo vizuri...si mtu wa kumchezea...aha aahaaaaa,ndiyo maana jini suryath amekimbia"mganga alisema kauli ambayo ilimshtua sana salimu.
"Suryath nae kakimbia...kwa nini sasa???"
"Fadhili anaonekana yuko fiti...sio wa kumuingilia haraka haraka k**a unavyodhani.ukiona jini suryath ana kimbia ujue huko sio kwa kitoto.....ila naona fadhili ameuwasha moto...ametangaza vita na mimi.hawezi akaniumizia kijana wanguu!!" .
"Heee kumbe suryath ameumia??"salimu aliuliza kwa mshangao . "Hahahaaahaaaa..ndiyo ameumia sana...lakini tayari nimewatuma vijana wangu ninaowaamini sana,kwenda kumkarabati huyo mpumbavu"mganga alijitapa.
"Kwa hiyo matokeo lini mtaalamu wangu".
"Tegemea kuanzia usiku wa leo utayapata matokeo....ikishindikana hivyo bhasi kesho kutwa mambo yatakuwa yameshakuwa mswanuu.........hahaahaaaa mi ndo adobeeee....uganga wangu nimeuchukua nigeria.hapa tanzania hakuna wakunichezea mimi,na huyu fadhili nataka awe piki piki yangu ntakuwa nampanda k**a farasi"
"Itakuwa vizuri sana mtaalamu".
bhasi baada ya salimu kuhakikishiwa kuwa kazi yake inashughulikiwa alifurahi sana,akaaga kisha akaondoka.
*****
Upande wa pili, Latifah bado hakukubali kirahisi kumpoteza fadhili.akili na moyo wake vilikuwa havijafikia hatua ya kukata tamaa ya kutokuendelea kulipigania penzi lake.asubuhi ya siku hii alijiapiza tena kuenda katika kampuni ya EH MODOLES ili akamuangalie kipenzi cha moyo wake,japo siku iliopita aliachwa katika hali ya sintofahamu na mwanaume huyo.mida ya saa sita na nusu mchana ndipo latifah alikuwa akifika katika kampuni aliokuwa akifanyia kazi fadhili.
~~~~~~~
Mida ya saa sita na madakika kadhaa niliona ndio muda sahihi wa mimi kwenda kupata chakula.nikajiweka sawa kisha nikaanza kushuka kwa kutumia ngazi kwenda chini.sio kwamba hakukuwa na lifti,zilikuwepo lakini nilijisikia tu kushuka ghorofani kwa miguu.wakati nafungua mlango ili nitoke nje nikajikuta nikigongana na mwanamke ambaye kwa muda huo sikumtambua kutokana na kwamba alikuwa ameinama akiokota vitu vyake ambayo niliviangusha baada ya kugongana,kwa haraka niligundua kuwa mwanamke huyu alikuwa na haraka ya kuingia ndani,bhasi nikainama nami kumsaidia kuokota baadhi ya vitu vilivyokuwa vimebakia......
"Dada samahani....sikuta......
"nilishindwa kumalizia kutamka nilichokusudia kukitamka baada ya mwanamke niliegongana nae kunitazama.LAA HAULAAAAH!!! mwanamke huyu alikuwa ni latifah.mwanamke ambaye nilikuwa nae katika mahusiano kipindi cha nyuma...
"Usijali fadhilii....haina haja ya kuniomba mimi msamaha.bali wote tunatakiwa kuombana misamaha.kwa sababu tumegongana na sio wewe ndiye ulienigonga"latifah aliongea kwa sauti laini yenye utulivu ndani yake...... .
"Umefuata kitu gani humu ndani"nami nilimuuliza huku nikiwa nimemkazia macho
"Nimemfuata nimpendaye....lakini kwa bahati nzuri nimekutana nae mlangoni...imekuwa k**a bahati kwangu"latifah alisema huku uso wake akiupamba kwa tabasamu tamu .
"Daaaa....hebu twende huku"nilisema hivyo huku nikimshika mkono latifah na kuongozana nae mpaka kwenye mgahawa.nikamwambia aagize anachotaka,latifah akakataa akadai hajisikii kula..... .
"Hivi latifah we ni mwanamke wa aina gani ambaye husikii,si nilishakuambia usinitafuteee...sasa kwa nini unanifuata fuata.latifah nilishasemaga naomba uishi k**a hujawahi kuonana na mii........."
"STOOOOP!!!fadhili usiongee mambo mengi....unavyoniona jinsi nilivyo ndivyo na wewe ulivyo......we ni mwanaume wa aina gani usiyethamini penzi la dhati unalopewa???eeeh fadhili unataka nikupendeje we mwanaume ili ujue ni kweli ninakupenda....kwanini una kuwa mkatili kwangu??kosa gani lililofanya ukanihukumu......sawa ulisema ulinisaliti ndio,na mimi nakubali lakini.......mi sikuhitaji nikuhukumu,kwa sababu najua binadamu hatujakamilika,na ndio maana ukafanya vile....fadhili mi sijali ushatembea na wangapi au utatembea na wangapi ninachotaka ni mimi kuwa na wewe....ninakupenda jamani why hutaki kunielewaaa??"latifah alisema muda huu kilio kikiwa kimemtawala.ki ukweli maneno aliyoyaongea latifah yalinichoma kwa namna moja au nyingine.hakika niliona mi ni mkosaji ambaye natesa kiumbe ambacho hakina hatia..... .
"Latifah.....ni kwa nini moyo wako hautaki kuniacha??mimi sio chaguo lakooo,nimekusaliti lakini bado unahitaji kuwa nami huoni k**a ukiwa na mimi utazidi kuumizwa na usaliti wangu??"nilisema kwa upole.
"Fadhili hayo ni madhaifu tu,yanarekebishika......mimi nipo tayari kuvumilia yote ili mradi niwe na wewe...nakupenda wewe pekee kwenye ulimwengu huu.sitamani kuwa na mwanaume mwingine zaidi yako.....fadhili I LOVE YOU,I LOVE YOU SO MUCH....please rudisha moyo wako.unipokee na unipende k**a ulivyonipenda mwanzo please naombaaa"latifah alilalamika.
Niliona ni hakika kuwa kweli nilikuwa na sababu ya kumrudia mwanamke huyu,kwani mpaka sasa sikuwa nimeona kosa kubwa alilonifanyia mpaka kufikia hatua ya kumpa adhabu ya kuachana na mimi.nilikaa kimya kwa dakika mbili nzima nikitafakari ni maamuzi gani nichukue juu ya jambo lililokuwa mbele yangu....baadae kichwa kilitoa maamuzi.kwanza nilipumua kwa nguvu sana kabla sijasema...... .
"Latifah.....nikwambie kitu..."nilisema
ITAENDELEA.