Shirkomedia

Shirkomedia Best studio in Eastern and Central Africa from Mombasa. Book sessions with Prod. Shirko 0702470243

Pumzika kwa amani brother   hii taarifa imetufikia ghafla mno. Hatuna maneno mengi ya kusema maana mioyo yetu baridi kia...
07/06/2024

Pumzika kwa amani brother hii taarifa imetufikia ghafla mno. Hatuna maneno mengi ya kusema maana mioyo yetu baridi kiasi huzuni imetanda muda huu. Sanaa ya zanzibar imefunga ukurasa wa harakati kwa msanii mpambanaji, jasiri, kiongozi na mwenye upeo na moyo wa kuibeba zenji flavour juu zaidi. Allaah ampe hifadhi ya salama kwenye mapumziko mema ya pepo baada ya msamaha wake. You will be always remembered in our hearts. Reat easy champ.

Supporting young generation 🔥   tukutane baadae kwenye listening album session ya kijana wetu.
24/05/2024

Supporting young generation 🔥 tukutane baadae kwenye listening album session ya kijana wetu.

Ukiishi kwa msukumo wa amri ya nafsi yako na moyo wako au akili yako mwenyewe (mawazo yako mwenyewe) ukifanikiwa ni rahi...
23/03/2024

Ukiishi kwa msukumo wa amri ya nafsi yako na moyo wako au akili yako mwenyewe (mawazo yako mwenyewe) ukifanikiwa ni rahisi sana kupongezwa na watu hata wale ambao walikudharau ila haiwezi kuwa sawa na pale unapokosea au kufanya maamuzi mabaya kwa kutumia njia hiyo. Kwanini? Watakusema watu vibaya na kutumia kila mifano mibaya kuwa wewe ndio chanzo ya hasara hii na hii na ubaya ule, hata k**a wao walifanya mengi ya kukosea lakini nani aliyewaona? Nani anaejua hilo? Walifanyia kuwa siri yao, wewe uliwaamini ukawahusisha je wao walikuamini wakakuhusishia yao? Usipende kuhusisha wengi (waliomo na wasiomo) kwenye mambo yako ya heri au yenye muelekeo wa manufaa ili wakuamulie au kukupa msukumo wa maamuzi. Wapo watakao kushauri vyema na huenda ni wachache ila wewe unatazama wengi watakushauri vipi je hao wakiwa ndio wenye muongozo mbaya si ndio umepotea? Fanya siri na jitahidi iwe na wachache unaowaamini kwenye hili usimkose mwalimu wako, mzazi wako pengine, rafiki wa kweli maana huwezi kumkosa japo mmoja na mshauri mzuri aliyekupita maarifa au utulivu wa akili k**a sio elimu. Kukosea mwenyewe ni rahisi kujipoza maumivu na kufanya maamuzi ya kujirekebisha sababu huna mtu wa kumlaumu zaidi ya nafsi yako. Ila muongozo wa mtu ukija kukuharibia maisha yako utaishi kulaumu mtu huyo mpaka unakufa huku umesahau kuwa muamuzi wa misho ni wewe hata k**a alikushauri mtu. Watu wa aina hiyo ni rahisi sana kukukimbia unapoharibikiwa baada ya kukuaminisha kitu ambacho kina asilimia kubwa ya kufeli au kukufelisha. Kuwa makini tuliza akili maamuzi yako ni makubwa kuliko ya kuamuliwa na mtu yoyote na mitandao hii ya kijamii ndio chanzo. Inaweza ikakupa watu wa kukuamulia mazuri kwa idadi ukafuata na ukaangukia kushoto na kuharibikiwa huku bado ukayafuata.

Happy birthday to you my brother Adha Yooh aka VICTOR MO. SAV CLAN haijawahi kuwa kamili bila uwepo wako. You were a rea...
11/03/2024

Happy birthday to you my brother Adha Yooh aka VICTOR MO. SAV CLAN haijawahi kuwa kamili bila uwepo wako. You were a real G. God bless you, ishi miaka ya kutosha kubema mafanikio na maisha yako kwenye ukurasa mwingine. Lets wish this brother of mine a happy birthday 🔥🔥🔥

My bit bite highlights performance at the   redcarpet event is available on youtube. Support share like and give your hu...
10/03/2024

My bit bite highlights performance at the redcarpet event is available on youtube. Support share like and give your humble comments. The link is 👇🏼

DISCLAIMER: I hereby declare that I do not own the rights to this music/song. All rights belong to the owner. No Copyright Infringement Intended.

28/01/2024

Shirkomedia yawaletea Dude jipya kutoka kwa Msanii Dazlah wimbo wa taifa akimshirikisha Benzema. Ngoma hio imeandaliwa Na Maestro mfalme wa Manandananda Vidole mia nane elfu 😅😅 Shirko Awadh Salim akishirikiana na producer Kalavu 👑
Kimbia pale Youtube upate kuona Kipindi moja safi 🎥🎞🎬

https://youtu.be/0DmMw1O_-cI

Conversation between those pros who built eachother’s profiles back then and now here comes the biggest change of the aw...
04/01/2024

Conversation between those pros who built eachother’s profiles back then and now here comes the biggest change of the awaited time. 2024 is the revolutional year.

Picha ya siku Ally Mahaba Mbossokhan Chikuzee kenya
18/12/2023

Picha ya siku Ally Mahaba Mbossokhan Chikuzee kenya

Tangazo Maalum kwa wasanii wote MombasaPanapo majaaliwa asubuhi ya leo siku ya ijumamosi tarehe 9 Disemba 2023 majira ya...
09/12/2023

Tangazo Maalum kwa wasanii wote Mombasa
Panapo majaaliwa asubuhi ya leo siku ya ijumamosi tarehe 9 Disemba 2023 majira ya saa nne asubuhi. Mstahiki Govenor wetu wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ameomba kukutana na wasanii wote wa pale Swahilipot Hub ameomba atakaeipata taarifa hii ampe na mwingine insha Allaah tukutane sote pamoja pale.

Alhamdulillaah jambo la ndoa ya president wa sanaa yetu ya pwani AMOURY tumemaliza awamu ya kwanza (nikah) awamu ya pili...
08/12/2023

Alhamdulillaah jambo la ndoa ya president wa sanaa yetu ya pwani AMOURY tumemaliza awamu ya kwanza (nikah) awamu ya pili ni pale Noble Hall kwa ajili ya familia na marafiki wa bwana harusi kwa waalikwa rasmi.
Taarifa nyingine ni hii hapa kwa wasanii wote panapo majaaliwa tukiamka asubuhi kesho siku ya Ijumamosi saa nne asubuhi. Mstahiki Govenor wetu Abdulswamad Shariff Nassir ameomba kukutana na wasanii wote wa Mombasa pale Swahilipot Hub ameomba atakaeipata taarifa ampe na mwingine insha Allaah tukutane sote pamoja pale.

Rashidabdallah_supercup finals tarehe 17 kitanuka kwenye jukwaa la waswahili mji wa waswahili burudani za kiswahili watu...
06/12/2023

Rashidabdallah_supercup finals tarehe 17 kitanuka kwenye jukwaa la waswahili mji wa waswahili burudani za kiswahili watumbuizaji waswahili🤣haya njoo sasa anga hizi 🔥🔥 Tsofa Mael's uje ku dj Amoury Ally tunampa udhuru akiwa kwenye asali ya mwezi. Hii disemba nyie na misso misondo mmeamua ni matukio tu!!!

17/11/2023

Pole producer Producer Totti dah hii imetugusa sote wadau wa muziki kiundani maana suala hili ya studio kupata athari k**a hii ni jambo la kuhuzunisha. Elnino imeingia kwa fujo sana. Be strong bro this will pass too.

Burudani limewasha gari na taa ya kijani inaashiria safari ndo hii ya tarehe   FIRST EDITION. Tarehe 2 Disemba mwezi wa ...
16/11/2023

Burudani limewasha gari na taa ya kijani inaashiria safari ndo hii ya tarehe FIRST EDITION. Tarehe 2 Disemba mwezi wa kifunga mwaka na hii ni kubwa sana kwa tasnia ya pwani. Tunahitaji ubunifu k**a huu wa hali ya juu. List ya wasanii ni ndefu tuelewane hii show sio ya wasanii wa eneo moja tu venue zinachaguliwa kutokana na nguvu ya wadhamini.
Nimependa hii sana na nimetoa support na k**a una maswali nifuate lakini ifahamike matasha huru k**a haya yafanyike na sio kusubiri county iandae matamasha wakati tunaamini Mombasa ndio lilikuwa chimbuko la burudani miaka ya nyuma maana kulikua hakupoi huko tamasha huko tamasha ila sasa hivi tunasubiri tamasha moja mwaka mzima 😳 na manyimbo yote haya tunayorigishiana mitandaoni huyu katoa album huyu katoa ep na hamna hata birthday ya kwenda kuperform.
Tuache kulaumu laumu kila mtu aandae tamasha na hiyo ndio itatoa nafasi kwa wasanii wanaostahili tukitegemea moja tu tutalaumiana kwanini sipo kwanini huyu na sio mimi.
Naamini wahusika waliwatafuta watu kwa uwezo wa kuwafikia na k**a hukufikiwa ulitakiwa uwatafute wahusika na hukufanya hivyo. Wengi wameona kulalamika huku mitandaoni ni rahisi kuliko kuwatafuta wahusika its too sad. Tuache maisha ya kusubiri kutafutwa na kukausha tupo kwenye dunia tofauti ya kutegemeana. Mfwate mtu mpaka akwambie sitaki ushirikiano na wewe ndio uangalie pa kwenda na sio kufwata wanayokwambia watu fulani hafai na wewe uyabebe hivyo kwa dhana zako. Lets support activities k**a hizi na wenye ubunifu mwingine walete tuonyeshe support.

Tanganzo tangazo, jumuiya ya sanaa ya pwani inatoa taarifa ya tamko rasmi kutoka kwa mheshimiwa rais wa wasanii pwani al...
27/10/2023

Tanganzo tangazo, jumuiya ya sanaa ya pwani inatoa taarifa ya tamko rasmi kutoka kwa mheshimiwa rais wa wasanii pwani aliyetawazwa ushujaa rasmi na mheshimiwa rais wa jamhuri ya Kenya William Samoei Ruto mnamo tarehe 20 mwezi oktoba siku ya maadhimisho ya mashujaa day. Rais wa wasanii wa pwani mheshimiwa AMOURY atakuwa na mengi ya kusema kwenye kituo cha taifa KBC Channel 1 TV PWANI FM akiongelea mengi kwa hiyo tunaomba macho yote na masikio yawe sambamba na kusikia yatakayo semwa siku ya leo ijumaa ya tarehe 27 mwezi oktoba majira ya saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana. Yoyote atakaepata taarifa hii amsambazie mzalendo mwingine.

Kupitia CEO wa Shirkomedia Shirko Awadh Salim Ni jambo la maana sana kuutenga muda wako baada ya kutengeneza au kuandaa ...
24/10/2023

Kupitia CEO wa Shirkomedia Shirko Awadh Salim

Ni jambo la maana sana kuutenga muda wako baada ya kutengeneza au kuandaa muziki na kujishughulisha na kitu kingine. Kiafya inapendeza sana kuihamisha akili inayotumika kwa jambo moja tu siku nzima na ikaenda kwa mfumo wa kujirudia hivyo hivyo wiki, mwezi hadi miezi ya kufuatana. Hii inatuathiri k**a watayarishaji muziki kukaa tu studio na kuumaliza muda wote hadi usiku mkubwa kuelekea alfajiri kutokea asubuhi unaweza kufanikisha kazi kadhaa tu kuwa nzuri ila sio kwa mfululizo. Tenga muda pia kuenjoy au kukaa namarafiki au kujishughulisha na kipaji chako kingine au hata kukaa na watu waliokuzidi umri au wale uliowazidi ili akili ipate kuhama kutoka kwenye mgando wa kitu kimoja. Binafsi napenda kutazama vipaji vya wacheza mpira wa miguu na hii imenipa wazo kwanini wanamuziki wasipate muda wa kuandaa nyimbo za kuhamasisha mashabiki nimeona ni muda sahihi wa kufanya jambo hili ili kutanua mabaya ya sanaa zote mbili kuwa kitu kimoja na kutegemeana. 📸 mashujaa cup final (wananyuki vs mombasa all stars)

Via Shirko Awadh SalimThis Sunday insha Allaah pin your Location at Waterfront banquet for the second edition of   i wil...
04/10/2023

Via Shirko Awadh Salim

This Sunday insha Allaah pin your Location at Waterfront banquet for the second edition of i will be with my band SAS Angham this is going to be unique and special. Mark the date 8th Oct 2023. Lets support our own Qassedah Nasheed industry by participating and attending events like this. Cc Saad F***j Ahmed M.Tarek Hashim Zein

26/08/2023

https://youtube.com/watch?v=hxKx_l-tBRY&si=IjAdZhyPLo59p3yx

Tutumie fursa hii kulinda ladha za tamaduni zetu kwa kuongeza ubunifu mzuri unaobeba maudhuo na ladha halisi.
Twende na hii hapa ya kwake iliyo bebwa na viasali asali mdalazini mziki na iliki ya vinanda kutoka Shirkomedia let’s support our own baada ya hapo tunahamia kwenye na 🎻🎻🎻🙏🏼

A birthday is just the first day of another 365-days journey around the sun. Enjoy the trip,Age is a number and yours ar...
23/08/2023

A birthday is just the first day of another 365-days journey around the sun. Enjoy the trip,Age is a number and yours are unlisted..... Happy BIRTHDAY to Our Shebby Le Grand let's Celebrate more wins and success together fam

New generation hip hop mi napenda kuiita maana ina ubunifu zaidi ya kule tulipotoka kuelekea kimataifa. Yes Mombasani th...
18/08/2023

New generation hip hop mi napenda kuiita maana ina ubunifu zaidi ya kule tulipotoka kuelekea kimataifa. Yes Mombasani the future is bright with Magongo’s finest Risto Bsb asubuhi hii ataskika pale RADIO KAYA kwenye meza moja na Caroline Mkamburi Kimegho pamoja na CaptainLui1 litaachiwa dude la kimataifa rasmi tutoe suppot kwenye mawe ya kwenda mbele🔥🔥🔥

Address

Mombasa

Opening Hours

Monday 14:00 - 20:30
Tuesday 14:00 - 20:30
Wednesday 14:00 - 20:30
Thursday 14:00 - 20:30
Friday 14:00 - 18:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Shirkomedia posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Shirkomedia:

Videos

Share