NURU Digital Media

NURU Digital Media GET BREAKING NEWS, ENTERTAINMENT, PRODUCTION AND ADVERTISEMENT, COVERAGE AND INTERVIEWS . FOLLOW US.
(1)

11/12/2024

Serikali ya uongo na hongo-Shirika la AFRICOG lashtumu serikali

11/12/2024

Polisi watupa vitoa machozi kwa waandamaji dhidi ya mauaji ya kikatili ya wanawake.

11/12/2024

Uchaguzi wa ODM mashinani watiwa doa baada ya wanasiasa kudai hakua wa halali

10/12/2024

*Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh*

_Hadithi na ayah zinatusisitizia kipaumbele cha kuhudumia familia kwanza._

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) kuwa Rasuli wa Allaah (ﷺ) amesema:
" *Dinari unayotumia katika Njia ya Allaah (jihaad), na Dinari unayotumia kumwacha huru mtumwa, na Dinari unayoitoa sadaka kwa maskini, na Dinari unayotumia kwa familia yako, yenye ujira mkubwa zaidi ni ile unayotumia kwa familia yako."*
[Muslim]

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِیمِ
Wanakuuliza watoe nini? Sema: Kheri mnayo itoa ni kwa ajili ya wazazi na jamaa na mayatima na masikini na wasafiri. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua.
[Qur'an 2:215]

Allah kwa Rehma zake atujaalie tuisome Quran na sunnah na kufuata maamrisho yake.

*Aamyn*

10/12/2024

Rais Ruto akutana kwa mara ya kwanza na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, handisheki ikinukia

10/12/2024

Mwekezaji wa kigeni aanza kilimo cha karakara katika maelfu ya ekari Shakahola.

10/12/2024

Rais awaahadi Wakenya milioni 4 kulipa mikopo ya Hustler Fund wanayodaiwa ili waweze kuongezewa kiwango mara dufu

04/12/2024

'Wataalamu' wa ODM walioingia serikalini sasa waabudu Ruto

04/12/2024

Gavana Aanza Msako dhidi ya Wamiliki wa Nyumba wa Jiji

04/12/2024

Idadi ya wale ambao wameaga dunia baada ya ukuta kuanguka eneo la Miritini imefikia watu 8

04/12/2024

Gavana Abdulswamad aagiza Mmiliki wa mradi wa ukuta uliosababisha maafa, Mombasa kutiwa nguvuni

04/12/2024

Watu 2 Wafariki, 46 Wakilazwa Hospitalini Baada ya Kula Mchele na Maharage huko Vihiga

SIKU YA UTAMADUNI YAFANA Rongo university Chuo Kikuu cha Rongo kimeadhimisha Siku ya Utamaduni leo kwa sherehe za kufana...
29/11/2024

SIKU YA UTAMADUNI YAFANA Rongo university

Chuo Kikuu cha Rongo kimeadhimisha Siku ya Utamaduni leo kwa sherehe za kufana zilizoleta pamoja wanajumuiya ya chuo hicho na wageni waalikwa kutoka maeneo mbalimbali.

Hafla hiyo ambayo huandaliwa kila mwaka, imelenga kusherehekea utofauti wa tamaduni za Kenya na mataifa mengine kupitia maonesho ya mavazi, vyakula, muziki, na michezo ya jadi. Washiriki walionyesha utajiri wa tamaduni zao kwa mavazi ya kienyeji, nyimbo za kiasili na Ngoma.

Mkuu wa chuo, Profesa Samuel Gudu , aliongoza shughuli hizo kwa hotuba iliyosisitiza umuhimu wa kuhifadhi na kukuza tamaduni za Kiafrika k**a sehemu ya urithi wa kizazi kijacho.

Moja ya vivutio vya siku hiyo kilikuwa ni maonesho ya vyakula vya jadi kutoka jamii mbalimbali za Kenya, ambavyo vilivutia umati mkubwa. Pia, vikundi vya burudani k**a vile wasanii wa ngoma na kikundi cha taarab cha Pwani viligharamia burudani na kuzua shangwe miongoni mwa waliohudhuria.

Siku ya Utamaduni imetajwa kuwa ya mafanikio makubwa na imeongeza mshik**ano wa kijamii na fahari ya kitaifa miongoni mwa wanajumuiya wa chuo Cha Rongo

Tukio hili limehitimishwa na gwaride la kitamaduni lililoshirikisha wanafunzi kutoka idara mbalimbali za chuo, huku viongozi wa chuo wakiahidi kuendeleza sherehe hizi kwa kiwango kikubwa zaidi miaka ijayo.

MOHAMMED ISMAIL

CHAMA CHA KISWAHILI CHA RONGO ALMAARUFU (CHAWAKIRO) CHA ADHIMISHA MIAKA KUMI TANGU KUASISIWA, KISWAHILI HOYEE, KISWAHILI...
27/11/2024

CHAMA CHA KISWAHILI CHA RONGO ALMAARUFU (CHAWAKIRO) CHA ADHIMISHA MIAKA KUMI TANGU KUASISIWA, KISWAHILI HOYEE, KISWAHILI AJIRA HUTOA, KISWAHILI CHEMCHEMI YA MAARIFA.

MAADHIMISHO YA CHAWAKIRO
27/11/2024

MAADHIMISHO YA CHAWAKIRO

26/11/2024

Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh*

_Aya na Hadithi zinahimiza waumini kuwa na mazungumzo mazuri, kuepuka ugomvi, na kuwa waangalifu dhidi ya fitna za Shetani zinazoweza kudhoofisha uhusiano wa kijamii._

Mtume (ﷺ) alisema:
"Yeyote anayeamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho basi na aseme jambo jema au anyamaze."
(Bukhari na Muslim)

Riwaya nyingine

Mtume (ﷺ) alisema:
"Hakika mja anaweza kusema neno bila kulifikiria, ambalo linampeleka katika moto wa Jahanamu umbali wa mashariki na magharibi."
(Sahih Bukhari)

Riwaya nyingine

Mtume (ﷺ) alisema:
"Shetani ameathirika, amekata tamaa ya waumini kumuabudu, lakini bado hatakubali, ataeneza fitna kati yao."
(Sahih Muslim)

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِیمِ
Waambie waja wangu waseme maneno mazuri, maana Shet'ani huchochea ugomvi baina yao. Hakika Shet'ani ni adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu.
[Qur'an 17:53]

Allah kwa Rehma zake atujaalie tuisome Quran na sunnah na kufuata maamrisho yake.

*Aamyn*

Address

Mombasa
Mombasa

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NURU Digital Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share