WILD ROCKY TV

WILD ROCKY TV UCHANGANUZI WA MASUALA NYETI YANAYO FUNGAMANA NA MAISHA YA NDOA

20/10/2022

💞MHESHIMU HUYU BINTI SIKU AKIKUACHA UTACHANGANYIKIWA!💞

👉Kuna baadhi ya wanaume, binti akishamkubali kimapenzi na kukolea, akaonyesha kuwa anampenda sana basi anaanza kumnyanyasa, kumpiga na kumdharau, anaanza kuona k**a yeye ndiye kampa huyo binti maisha. Kana kwamba kabla ya kukutana nayeye binti alikua hana maisha, alikua takataka hajielewi🤔.

K**a vile hana familia na k**a vile akimuacha hawezi kuishi. Yaani unakutana na mwanaume anavyomnyanyasa binti wawatu basi unaweza kudhani huyu ndiye yule jamaa ambaye anashikilia koki ya bomba la pumzi hivyo siku akiamua kulizima basi ndo binti anaishia hapo🤣.

Nikukumbushe tu ndugu yangu, huyo binti alikua na maisha kabla yako. Yaani mpaka unamuona amependeza, ukavutiwa naye alikua anakula, analala, anavaa ndo hata ukamtamani. Yaani hiyo miaka mitano ya kukaa naye ni kidogo ukilinganisha na miaka 20 ambayo alikua bila wewe.

Hivyo k**a aliweza kuishi miaka ishirini bila wewe kwanini ashindwe sasa🤔. Anaweza kutoishi bila wewe na kukunyenyekea na kukupenda si sababu eti kuwa maisha yake yatakoma kwakua kaachana na wewe. Ubaya nikuwa, mwanamke unayemnyanyasa hivi siku akikuacha utachanganyikiwa, narudia, ukijiona unamnyanyasa mwanake siku akikuacha utachanganyikiwa!🤣🤣🤣

20/10/2022

K**a huna mpango wa kumuoa muambie binti wa watu, huna haja ya kwenda kujitambulisha kwao wakati una maisha mengine, haikufanyi kuwa mjanja wala mwanaume Zaidi kutoa kishika uchumba ili tu akukubali kimwili.

Hata k**a unaona kwamba huwezi kupata mwanamke bila kumdanganya ila si kwa kiwango cha kwenda mpaka kwao. Unatakiwa kujua kuwa, unapoenda kwa mwanamke ukajitambulisha bila kumuoa, aibu unayompa ka wazazi wake, marafiki na ukoo wake ni kubwa.

Najua unaona sifa kwakua ukishaondoka basi kila kitu kwako kinakua sawa ila ulishawaza kuhusu yeye. Vipi maisha yake baada ya hapo yatakuaje, ni wanaume wangapi wanamtaka lakini anawakataa kwakua anajiona k**a yeye ni mchumba wa mtu? Acha hizo mambo usifike huko sio ujanja!

07/09/2022

KUNA MUDA TUNAJITAHIDI SANA KUYALINDA na KUYATETEA MAHUSIANO YADUMU.

Tuko tayari kupoteza ili wao wapate, tuko tayari kutengwa na kusemwa vibaya na jamaa zetu ili KUWALINDA na KUWATETEA wawe salama na wasidharaulike tunaamua kuwalinda na kila mtu atakayeonekana adui wa MWILI na ROHO kwake.

Kwa ufupi tunafanya mengi ya HATARI na yanye GHARAMA kwa ajili yao. Wakati mwingine tunaaminika tumeshikwa AKILI au hatuna PAKWENDA, hatujitambui nk (fasili za watu).

Unayempenda yeye hakupendi, unayemtetea yeye hajali, unayemhitaji yeye hakuhitaji nk. Mara nyingi tunateswa na kunyanyaswa na wale tunaowathamini na tunaowapenda kwa dhati.

Kuna wakati tunawaasamehe, tunajishusha na kubeba makosa yao ili wao wabaki salama na maisha yaendelee lakini wanafanya makosa yaleyale yanayotuumiza.

Ifike wakati tukubali kuachia vitu hata k**a tulivitesekea sana kuvipata maana si kila kitu kinahitaji uvumilivu vingine vinahitaji kuviachilia ili ubaki salama.

07/09/2022

HII NI KWA WALE MABINTI WA NIACHIE MWANAUME WANGU!

K**a uko kwenye mahusiano ya kawaida tu, halafu kila siku kazi yako nikuwapigia wanawake wengine kuwaambia achaneni na mume wangu wakati huyo mwanaume hajakuoa! Narudia hajakuoa, ni mpenzi tu labda hata mnaishi naye bila ndoa au kajitambulisha tu kwenu lakini hakuna ndoa basi jua kuwa huyo si mwanaume wako.

Huyo mwanaume bado anatafuta mwanamke wa kuwa naye, hana ndoa bado anaweza kuolewa yoyote kati ya hao unaowapigia simu! Najua unajiambia mimi kwao nafahamika! Unajuaje k**a hao wengine nao hawafahamiki! Ananihudumia kwa kila kitu, kwani hao wengine vipi hawahudumii!

Katoa mahari kwani huko kwingine anashindwa kutoa! Muda mwingi niko naye si ni kwakua wewe ni king’ang’anizi! Ninachotaka kusema hapa ni hivi, huyo mwanaume si mume wako, hata k**a humuachi badala ya kujipa kazi ya kupigia wanawake wenzako simu yhembu amka, waza hivi asiponichagua mimi nimejiandaaje na maisha yangu!

Wengi wakishaanza kufumania badala ya kuamka kujifikiria wao ndiyo kwanza wanabeba mimba ili kimshukilia mwanaume! Dada nani kakuambia wewe pekee ndiyo mwenye kizazi, ndiyo kwanza utasikia kmapa mwanaume mtaji, anahangaika na mawifi kwa waganga, mara kujipendekeza kwa Mama mkwe ili apendwe yeye!

K**a ukishaanza kumfumania na unaona kuwa humuachi, badala ya kuhangaika na simu kupigia hao wengine kutaka wakuachie mwanaume wako kana kwamba ni maparachichi hayo basi hangaika kutafuta maisha yako binafsi. K**a huna kazi tafuta, k**a mlipanga kuzaa acha, kuwa makini na siku zako, fanya Biashara hata ukiachwa unakua umepoteza muda tu ila hujapoteza maisha!

07/09/2022

UFANYACHO LEO KINAWEZA KUAMUA KESHO YAKO NA HATIMA YA FAMILIA YAKO

Kila jambo unalotenda kwa mtu au katika jamii yako kwasababu ya mamlaka, cheo, nguvu ulizonazo zinaweza kuathiri uzao wako au wewe mwenyewe (kwa uzuri au ubaya)

Unamkumbuka Hamani, makosa yake kutaka kuwaua wayahudi yaligharimu jamii yake yote pamoja na yeye waliuawa. (Mchuma janga hula na wakwao)

Unamkumbuka Yeroboamu aliyekuwa mfalme wa Israel alivyomuasi Mungu na Mungu akajilipiza juu ya mwanae wa kiume akamuua. (Makosa ya baba yaligharimu maisha ya mtoto)

Unamkumbuka Mfalme Ahabu na Jezbel mkewe, makosa yao ya utalawa mbaya yaligharimu uzao wao wote na wao kuuwawa. (Mungu alijilipiza kwa mabaya yao)

Unamkumbuka mfalme Daud alivyoyakumbuka mema ya Jonathan yakawa neema kwa mtoto wa Jonathan ingawa Jonathan hakuwa hai alirejeshewa mali za babu na baba ake (Wema ni akiba utamfaa hata mwanao hata k**a wewe usipokuwepo).

Unatenda nini sasa kwa mtu au watu unaoishi nao. Je hawatajilipiza kwa mabaya yako? Maisha yako yasije kuacha kisasi juu ya wanao au makosa yako yakakugharimu wewe na uzao wako au familia yako.

Usiwaimize watu ukikumbuka wewe ni mwanadamu na una familia inaahitaji kuishi.

07/09/2022

SOME WARNING SIGNALS YOU MUST PAY ATTENTION TO IN YOUR RELATIONSHIP!

ANGER: If he/she easily gets angry when you have a little misunderstanding, he/she doesn't tolerate jokes, be conscious before you committed to him/her.

THREATENING YOU: If he/she threatening to leave you when you have a little argument, he/she will threatening and may leave you in marriage, be wise.

BEATING YOU: If he beat you up every time, if he slaps you during an argument, he will do the worst in marriage. Be wise.

LACK OF COMMUNICATION: If you are the only one that does all the calling, caring, messaging, texting... It depicts that you are forcing yourself on him/her. A man/woman that truly loves you will show it through his/her actions, he/she will not make excuses, they will find time to connect with you no matter how busy their schedule is. He/she will see you as their priority...Be sensitive.

WOMANIZER: If he womanizes, if you always see him with different girls, if he cheats on you on countless occasions, he may not change if you marry him. Look well before you leap.

HIDING YOU: If he/she hides you if he/she is not proud of you, if he/she fails to introduce you to his friends and family, it possible you are not his/her only option... Be wise.

MUMMY'S BOY/MUMMY'S GIRL: If he/she is a Mummy's boy/girl, if he/she can't make decisions by himself/herself, if he/she must consult his/her mum at all times before he/she can talk to you, his/her mum will influence him/her in marriage. Be wise.

LACK OF MATURITY: If he/she still behaves like a child, if he/she is not mature Spiritually, Emotionally, Mentally, Financially, etc. Marriage is not for kids, marriage is for mature. Be wise.

LACK OF VISION: If he/she doesn't have visions, goals, and dreams, such a man/woman can not be responsible, you will be the one taking all the responsibility if you marry him/her. A woman without vision will be a liability to a man, and a man with no vision will be a burden to a woman.

07/09/2022

K**A UKO HIVI UNAMLAZIMISHA MPENZI WAKO KUCHEPUKA!

Hujawahi kumfumania au ulishamfumania ukasamehe, lakini kila siku akichelewa kurudi utasikia ulikua na wanawake/wanaume zako! Akoongea na simu utasikia ni wanawake/wanaume zako, akisalimiana na mtu basi utasikia ni wanawake/wanaume zako, akifanya chochote kile basia kili yako inakuambia ni wanawake/wanaume zake nma unanuna.

Hata huna ushahidi au ushahidi wenyewe ni wakuuungaunga lakini unalazimishia ana wanawake/wanaume zake! Dada yangu, huyo mwanaume ni suala la muda tu, atakuchoka, yaani hizio kelele zitamlazimisha kuchepuka. Hata k**a mtu alikua malaya kaamua kuacha basi anaona hivi naachia nini k**a mtu kila sikua ananishutumu.

Kwake ataona ni bora tu kwenda kutafuta amani nnje na k**a mnavyojua wanawake/wanaume hawatafuti amani kwa wanawake/wanaume wenzao.

Siku akiipata basi hutakua na haja ya kukisiakisia labda alikua na wanawake/wanaume wake kwani utamuona huyo wanawake/wanaume wake! K**a una tabia hii jua shida si wanawake/wanaume bali ni wewe hujiamini na una kisirani, badilika kabla huyo mwanaume hajakuacha.

07/09/2022

AMKA NA HII; Ujinga ni pale ambapo unatembea na mwanaume, anakushirikisha katika mambo yake yote, wakati mwingine anakupa mpaka kusimamia vitu vyake, wakati ana mke wake au kuna mwanamke wanaishi naye hata k**a hawajafunga ndoa.

Anamdharau huyo mwanamke, anamuongelea vibaya kuwa hamtaki anakupenda wewe, lakini jioni anaenda kulala kwa huyo huyo mwanamke. Hamuachi kila siku anamuambia ni kwasababu ya watoto na wewe unakubali. Unajiona spesho kwakua muda mwingi anatumia kwako na si kwa huyo mwanamke au vitu vingi unajua wewe.

Lakini kuna shida moja, katika hivyo vitu vyote anavyokushirikisha, hakuna hata kimoja, narudia, hakuna hata kimoja ambacho kina jina lako. Kila kitu kuna majina yake au majina ya watoto, wewe ndiyo unasimamia, labda ni mshauri mkubwa lakini hakuna hata kimoja kina majina yako. Halafu anajishaua anakupenda, mwenyewe unamuona mume kabisa kila siku kutuma status kumchamba mke wake.

Dada wewe ni tambara la daki, kazi yake ni kufutia miguu lakini haliingii ndani na k**a likiingia basi litafuta ndani kisha litarudishwa nnje, halivuki ndani. Umuhimu wako ni anapokuomba ushauri, anapokutumia kusimamia biashara zake lakini si kukuweka ndani. K**a akishaamlizana na wewe anarudi kwa mwanamke wake kulala naye basi jua kuwa unatumika tu!

25/08/2022

Don't envy!

• Someone graduated at the age of 22, but waited 5 years before securing a good job.

• Someone became a CEO at 25, and died at 50.

• While another became a CEO at 50, and lived to 90 years.

• Someone is still single, while someone from his school group has become grandfather.

• Obama retired at 55 & Trump started at 70.

• Everyone in this world works based on their time zone.

• People around you might seem ahead of you & some might seem to be behind you.

• But everyone is running their own race, in their own time.

• Do not envy them.

• They are in their time zone, and you are in yours.

So, relax.

You're not late.
You're not early.
You are very much on time.

20/08/2022

AINA ZA HASIRA ZA WANAWAKE

1. Kuna mwanamke ambaye akikasirika, huishia kulia tuu!

2. Lakini mwingine akichukia, anaongea saanaa muda wote hadi ikukere!

3. Mwanamke mwingine akikasirika, ananuna, haongei! Mtapishana tu kimya kimya. Mawasiliano kibubu-bubu. Shavu limejaa k**a Kobra!

4. Mwingine akishikwa na hasira, period ya ghafla ghafla inafuata!

5. Wako wanawake ambao, ole achukie! Atakachokishika usipokimbie anakutandika nacho, majuto baadaye! Baba mmoja alipigwa 'Pedi' ilotumika, kufuatia kung'ang'ania tendo, huku mwenzi wake yuko katika hali hiyo!

6. Mwanamke mwingine akikasirika, hasira zake zinaishia kwenye kuvunja-vunja vyombo. Au saa nyingine kugombeza-gombeza wafanyakazi na watoto! Dizaini hii, huwa ni wale waliokosa kukidhiwa haja za kihisia na waume zao!

7. Mwanamke mwingine ole akasirike. Mtajuana kitandani panapo majaaliwa! Nakwambia utaungama yote!

8. Kuna ambao wakitibuliwa, hukimbilia kufunga mabegi na kuondoka!

9. Wapo ambao wakikasirika, wanagoma kupika!

10. Wengine wakichukia, wanaamua kwenda kulala kimyaaa!!

11. Wanawake wengine wakikasirika, tumbo linakata, na pengine mpaka kuharisha!

13. Wako ambao wakishikwa na hasira, huingia maombi na kuugua kusikoweza kutamkwa. Uchungu ukiisha, wananawa uso na kwenda sokoni.

14. Yuko ambaye akishikwa na hasira, hucheka saaanaaa.... Hutajua k**a amekasirika! Dizaini hii ni hatari sana, maana anaweza kukudhuru kiurahisi.

WEE UKO KUNDI GANI?

20/08/2022

HATUA ANAZOPITIA MTU ANAYEMWACHA MWENZIE.

Baada ya kuachana, aliyeachwa hudhani yeye pekee ndiye mwenye maumivu. Hujiona ameshindwa na aliyemwacha ni mshindi. Ukweli ni kuwa maumivu hujiri pande zote mbili k**a kweli nyote mlipendana na kuzoeana.

Zifuatazo ni hatua ambazo mtu anayemwacha mwenzie huzipitia;

KIPINDI CHA AHUENI AU NAFUU

Wazo la kuachana na mtu haliji ndani ya dakika moja. Ukiona mwenzio anafanya uamuzi wa kuachana na wewe leo, ujue pengine alishawaza hivyo muda mrefu uliopita. Inawezekana alishafanya tathmini yake ya kina na kujiridhisha kuwa hapaswi kuendelea nawe.

Wakati mwingine mtu anakosa ujasiri wa kutamka kwamba mfike mwisho, lakini ukitazama matendo yake unagundua anataka nini.

Inapotokea uhusiano umefika mwisho na mtu akatamka au nia yake ikaeleweka, huwa nafuu kubwa. Angalau, kile ambacho kilikuwa kinamtesa, akifikiria jinsi gani atakifanya sasa kimekuwa. Anakuwa ameshusha mzigo mkubwa sana na kupata ahueni ya kutosha.

Hatua ya ahueni huchukua muda mchache. Mara nyingi hudumu kuanzia siku 3-7 lakini pia inaweza kudumu kwa kipindi kirefu zaidi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Mazingira ya mtu na mtu huamua kipindi cha ahueni kidumu kwa muda gani.

2. UHURU
Katika kipindi hiki, sasa anao uhakika kuwa uhusiano umefika mwisho. Anafurahia maisha yake mapya bila uwepo wa aliyetamani kuachana naye. Anaishi huru bila migogoro ambayo ilitawala uhusiano wake uliopita. Ni kipindi ambacho anaweza kujenga ujamaa na watu ambao mwenzi wake wa zamani alikuwa hapatani nao, pengine mwanzoni aliwakwepa kwa sababu ya kulinda hisia za aliyekuwa mwandani wake. Zaidi, atakuwa huru kufanya kila alichotamani kabla lakini alishindwa kwa sababu ya uwepo wa mpenzi wake

3. TATHMINI
Katika kipindi hiki anaanza kumkumbuka mpenzi wake aliyepita. Anakumbuka mazuri yake na huenda akaanza kupuuza mabaya yake. Anajiuliza yuko wapi, anafanya nini, na nani, anaendeleaje, je, ameshapata mpenzi mwingine? Anakuwa na shauku ya kujua kitu gani kinaendelea katika maisha ya

01/05/2022

👉Wadogo zangu mliopo chuo, anakupenda sawa, lakini kumbuka kuwa upendo haununui Pampas!

Ukibeba mimba ya huyo mwanaume mwisho wa siku unarudi nayo kwenu, wakati yeye anaenda kutafuta na kuhangaika na kazi ili ale maisha wewe unahangaika na kulea mtoto.

Mtoto ni Baraka, lakini aje ukiwa unataka wewe. Aisee, visa vimekua vingi vya watoto kudanganyana mpaka imekuwa balaa bin beluwa...jamani, "ndiyo naakupenda ila sio na kubeba mimba ukibeba ni yako!"💔💔

07/04/2022

🔥WANAWAKE WANGEIJUA SIRI HII WENGI WANGEKUA BADO HAWAJAACHIKA!🔥
Iko hivi, sijui nani kakudanganya ila unatakiwa kujua kitu hiki. Katika TV kunakua na ratiba ya vipindi, kuanzia asubuhi mpaka jioni unajua kabisa kila alhamisi kuna kipindi flani na flani!
Siku ikibadilika unashangaa na unauliza “Kuna nini leo, mbona hawaonyeshi tamthilia flani?”
Sasa Dada zangu, wanaume sio k**a TV. Mwanaume wako kakuzoesha, kila siku asubuhi anakupigia simu kukusalimia, mchana anakutumia meseji, jioni lazima muongee kabla ya kulalaa!
Hayo ni mazoea, sio lazima afanye hivi kila siku. Shida yako nikua, siku akiacha kukupigia simu kutwa nzima, nawe unakaa kimya, unasubiria, kesho yake uanaanza kulalamika.
“Mbona jana hujanipigia!” Tena heri hata ungeishia kulalamika tu, hapana, na mnuno juu! Haiishii hapo unaanza kuchunguza k**a ana mwanamke mwingine!
Moja haikai mbili haisimami, unaanza kushika simu yake, kuangalia alikua anaongea na nani? Kumuuliza mbona umebaidlika, na mambo kibao. Mwanaume kabadilika wiki mbili tu ushaanza “K**a vipi bora tuachane!”
Labda nikupe siri moja ambayo ulikua hujiui “Mwanaume ni binadamu!” kuna wakati ana mambo yake mwenyewe, ana vitu vinamsumbua! Anataka kuwaza bila kusumbuliwa!
Najua uansema “K**a ana kitu si aniambie, mimi si ni mpenzi wake?” Dada wanaume sio k**a wanawake!
Wewe ukiwa na kitu utataka kumuambia kila mtu, akusaidie au akushauri, wakati mwingine hata akusikilize tu! Sisi wanaume tunapenda kutatua changamoto zetu wenyewe.
K**a nina tatizo, nilimalize ndiyo nimuambie mke wangu “Kulikua na moja mbili tatu!” Najua ndiyo maana tunakufa mapema, ila ndiyo tulivyo.
Kwahiyo Dada, mwanaume akibadilika wiki mbili tatu acha kukimbilia kuachana na kuhisi ana mtu mwingine, wengine wana mambo yao tu amabayo wana dili nayo!

NB: Nirahisi kutengeneza Mahusiano uliyonayo kuliko kuanzisha mengine mapya.

06/04/2022

🔥Ukisikiliza wanawakwe wengi, wale wanaosema “Sijui kwanini ameniacha, nimeona k**a kabadilika tu mawasiliano yamepungu….” Wengi unakuta hawana matatizo yoyote zaidi ya mchecheto.
(1) Aina ya kwanza ya Mchecheto uko hivi, umekutana na mwanaume, mmeanza mahusiano, unaona yanaenda vizuri, mwanaume anakujali, kakupa mipango mingi tu, miezi miwili tu unaona huyu si mume.
Sasa hapa ndiyo mchecheto unaingia, ukimuona online ushatuma meseji, asubuhi meseji, mchana simu, jioni meseji, usiku hata hamna stori unataka muongee mpaka mpitiwe na usingizi!
Mwanaume anakuchoka mapema kwakua anaona k**a huna kazi nyingine, kuna wanaopenda, ila wakwako akikuambia yuko bize kwakua una mchecheto unahisi unaachwa unapaniki!
(2) Aina ya pili mchecheto ni pale ambapo mwanaume alikua anakupigia simu asubuhi, mchana na jioni. Mnaongea, miezi miwili ya kwanza mwanaume baadaye anabaidilika, simu anapiga mara moja, anakua hakutafuti k**a mwanzo.
Basi wewe unapaniki, unajihisi kuachwa, hupumui, unaanza kulalamika, “Mbona umebadilika, mbona hivi mbona vile” Kumbe hata hajabadilika ndiyo alivyo mchecheto unakufanya uachwe!

31/03/2022

Ukimpata mwenye dini,bora ukatulie naye hata k**a hana senti.Rizki inatoka kwa Allaah.*

*🌹Utulivu wa moyo katika ndoa,hautokani na wingi wa mali anazozimiliki mmoja wa wana ndoa.*

*🌹Bali utulivu wa moyo katika ndoa unatokana na haya yafuatayo:*

*🌹Kuafikiana nyoyo na kuheshimiana*

*🌹kujaliana,kuhurumiana na kuvumiliana*

*🌹 ZINGATIA HAYA*

*🌹Kuna wengi wanaishi kwa udhalili kutokana na tamaa ya mali,walidhani wamepata kumbe ndio wamepatikana. Ni wangapi wanaishi kwa kudharauliwa na wenzi wao na sababu kuu ikiwa mmoja wao ni mwenye mali na mwenzie anatoka familia maskini?. Wangapi wana dhiki kutokana na mali anayoimiliki mmoja wao?*
*🌹Usikimbilie mali kwa yule dini yake ni hafifu utaangamizwa na mali hio. Yazingatie kwamba, mali haitibu maumivu ya hisia za mapenzi. Utaviona vingi na hunatakua na hamu navyo.*

*🌹Kimbilia kumchagua mwenye dini usalimike k**a ulivyousiwa.*

JARIBU LEO NJOO UNISHUKURU MWAKANI!>Anahisi una mwanamke mwingine kwakua kila saa uko kwenye simu yako na hutaki aguse s...
02/02/2022

JARIBU LEO NJOO UNISHUKURU MWAKANI!

>Anahisi una mwanamke mwingine kwakua kila saa uko kwenye simu yako na hutaki aguse simu yako, wakati mwingine hata akiingia anakuta hakuna kitu na yeye huamini kuwa umefuta kila kitu kwenye simu yako.

Kitu ambacho hajui nikuwa, wakati mwingine hutaki aguse simu yako kwakua unabet, unaangalia P**n (X) kwenye simu yako, au kuna mambo yako ya kipuuzi unachart na washikaji na hutaki ayajue kwakua hayamhusu!

Ujsipoangalia naye ataanza kuchepuka akiamini kuwa nawe unachepuka! Ushauri wangu, kua na kipimo cha kutumia simu ukiwa naye, anza taratibu, unaweza kusema, nikiwa nakula naizima kabisa au weka airplane’

Ukishazoea sema, nikiwa naongea na mke angu sishiki simu kabisa. Baadaye jisemee nikipanda kitandani sishiki simu. Baada ya muda utakua umezoea, atakuelewa, shaka haitaisha ila itapungua kidogo na ndoa itakua na amaani!

UCHANGANUZI WA MASUALA NYETI YANAYO FUNGAMANA NA MAISHA YA NDOA

💞KAA NA DHAMBI ZAKO SI SIFA KUJITANGAZA!💞👉Si vibaya kutamani mtu mwingine, ni ubinadamu kuwa hapa na pale utakutana na m...
22/12/2021

💞KAA NA DHAMBI ZAKO SI SIFA KUJITANGAZA!💞

👉Si vibaya kutamani mtu mwingine, ni ubinadamu kuwa hapa na pale utakutana na mtu ambaye utamtamani, hata k**a una mtu wako tayari lakini huwezi kuzuia macho kuona na kutamani, wakati mwingine unaweza kupenda pia na kwa kiasi kikubwa ukakajikuta hata unaingia kwenye mtego. Lakini kumbuka hayo ni mambo yako binafsi, haya ni mambo ambayo yanakuhusu wewe na moyo wako, namna unavyojisikia wewe.

Kuna haja gani ya kumuonyeshe mpenzi wako kuwa umetamani au hata uko na mtu mwingine? Inakuongezea nini yeye akijua kuwa humfikirii tena k**a ulivyokua unamfikiria mwanzoni, sikuambii uigize lakini k**a hauko tayari kumuacha, k**a akitaka kuondoka unajiliza liza kuomba misamaha kwanini nusikae na dhambi zako ukambana na Mungu wako.

Katika mahusiano watu hawaumii kwakua wenza wao wanawasaliti hapana, watu huumia kwakua wenza wao hufanya upumbavu wao dhahiri. Unachepuka mpaka unarekodi video unafanya mapenzi, ili nini inamaana hujiamini kuwa kile kitendo ulikua unakifanya wewe mpaka unahitaji ushahidi? Katika kila unachokifanya kumbuka kuwa kuna leo na kesho na kumbuka kuwa mwenza wako anaweza kukusamehe kwakua anakupenda lakini kamwe hawezi kusahau ulivyomuumiza.✍.

UCHANGANUZI WA MASUALA NYETI YANAYO FUNGAMANA NA MAISHA YA NDOA

22/12/2021

🎀UKIONA NDUGU WA MUME WANAKUHANGAIKIA HIVI BASI KIMBIA!🎀

👉Achana na Dada zake, achana na Mama yake, achana na kila mtu mwingine yoyote, mtu pekee anayepaswa kukupenda ni Mwanaume mwenyewe. Ukiona ndugu wa mume wamekuganda, wanajifanya wanataka uolewe na kijana wao, wanakupa ahadi nyingi lakini mwanaume hata hajali.

Wakati mwingine unasikia kabisa kuwa, ana mtu wake, kuna mwanamke anampenda, kuna mwanamke anaishi naye, kuna mwanamke kazaa naye na anataka kumuoa, ila ndugu hawamtaki, kwasababu zao tu, labda dini, kabila au kwakua tu ana akili kuliko ukoo wao mzima!

Dada, achana na hiyo familia. Tena wakikuchukua na kukupeleka kwao, kijana yuko zake Nairobi ndugu zake wanakuchukua kukupeleka kwao huko Madongo Poromoka , unaishi ukweni kana kwamba ushaolewa, unafuta, mtoni unaenda na kwenda kukatia majani Ng’ombe kwakua Mama yake kakuambia “Mimi ndiyo Mama yake atakuoa wewe labda k**a hakukaa humu miezi 9!”

Dada acha kupoteza muda wako kwani huyo mwanaume hata akikuoa utaenda kuteseka tu! Hao ndugu wa mume si k**a wanakupenda, hapana wanakutumia kwakua wana ajenda zao, acha kutumika. Najua una hamu sana na ndoa lakini hakuna mwanamke alishawahi kuolewa na Mama mkwe, kutafutiwa kupo ila uelewane na mwanaume wako!✍

28/09/2021

PUNGUZA MCHECHETO WA NDOA, TAFUTA KAZI KWANZA MNAKIMBILIA WAPI?
K**a umemaliza chuo mwaka huu na una mpenzi wako nayeye ndiyo k**aliza chuo k**a wewe, kabla ya kuanza kujiuliza atanioa lini hembu anza kuuliza nitapata wapi kazi au ni kwa namna gani ninaweza kujiajiri.
Kwa maisha ya sasa hivi hakuna mwanaume ambaye anaweza kukuhudumia kwa mahitaji yako yote au hata yale ya muhimu tu! Nikuambie kitu mdogo wangu kuingia kwenye ndoa bila kipato chochote ukitegemea upate kila kitu ni uongo!
Sikukatishi tamaa kwakua unamuona huyo k**a Malaika anakupenda sana na hajawahi kukunyanyasa lakini ukweli nikuwa wanabadilika na k**a umesoma Kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” utajua ni kwanini huyo mwanaume wako atabadilika pamoja na kukupenda kiasi hicho.
Najua una mchecheto wa kuolewa, una miaka 27 au 29 ushaanza kujiona mzee au mtu mzima, nirudie k**a huna kazi wewe bado mdogo sana tafuta kazi kwanza ndiyo uwaze kuolewa! K**a ukiapta amabye tayari anafanya kazi na unaona anaweza kukuhudumia basi ingia kwenye ndoa lakini tafuta kazi au kitu cha kufanya!
K**a ukikutana na mwaume akakuambia hataki ufanye kazi, labda ukapata kazi sehemu flani akakuambia usikubali kwakua tu mtakua mbali basi muambie hapana ngoja nianze kazi tukifikia kuoana nitahama! Ongea naye vizuri muelewane hasa k**a wote mnakua hamna kazi!

17/09/2021

💕💕K**A NDOA YAKO INA RAHA EPUKA KABISA KITU HIKI ITAKUFA!💕💕
Dada zangu, k**a una raha na mume wako, hembu kalisha Makalio chini, furahia ndoa yako na mume wako acha kujitangaza tangaza kwa marafiki zako! Narudisha, weka hayomakalio chini, funga mdomo wako na acha kujitangaza kwa marafiki zako.
(1) Mume wako anahudumia familia inamhusu nini shoga yako?
(2) Mume wako anapenda kucheza na watoto na akirudi nyumbani anafanya homework na watoto inamhusu nini shoga yako k**a si uzandiki na sifa za kijinga?
(3) Mume wako anawapenda wazazi wako, anatuma matumizi wkenue na kawajengea mpaka anasomesha ndugu zako inwahusu nini mashoga zako?
(4) Mume wako anajua mapenzi, anajua kukuandaa na anakufikisha kileleni unawamabia mashoga zako wa nini kuhusu maumbile ya mume wako ka a si ushamba na utoto!
(5) Mume wako anakupa hela na kila unachoomba anakupa, shoga yako inawahusu nini?
Shoga yako kila sikua anakuambia matatizo ya mume wako, anakuambia umalaya wake, anakuambia stress zake, halafu unajishaua kujisifia kuhusu huyo mwanaume wako. tena vingine vingi ni vya uongo tu unaopngea ili kuwachoma mashoga zako!
Dada ni suala la muda hao mashaoga zako watamchukua mwnauame wako, narudia, huyo ni mwanaume atachukuliwa ukiwa unashangaa! Acha kujishaua na mume wako, k**a ni raha kula kivyako, huko kujishaua kutakutokea puani na niamini nikikuambi.
Kwa mwanamke ambaye unajishaua namna hiyo, shoga yako akimtaka mume wako anampata dakika mbili tu! Kiama ni raha kula kivyako, acha kujishaua, unawafanya wamtamani, mtu hajawahi kununuliwa hata Gagulo la mtumba na mume wako kutwa kucha ni kusimulia unavyopendwa na vizawadi kwanini wasimchukue sasa!
Mwisho k**a unajiona huwezi kwua na raha bila kujitangaza basi wewe ni mgonjwa,

26/08/2021

💔💔💔💔💔💔💔💔💔💔💔💔💔💔💔💔💔
I pity those men who claim they cant date or marry those ladies with kids ...a lady having a kid but still at her matrimonial home doesn't mean she was loose...it means she gave her life to someone who later wasted it ...men how do you feel dating a p2 resistant and abortion graduate???? if you are a serious man who really need a serious relationship and you are dating a lady with a kid ...then love the kid the way you love the mother ...assume during birth the kid killed the mother ,would you have gotten the mother???
Single ladies with kids???
1.a man claiming to love you should love you with your kid out of that mentality it becomes a blind man.
2.having a kid while still at home doesn't mean your life has ended...you still have coutless chances of marriage in your lyf ... okay🚶🚶🚶🚶

23/08/2021

SIO VIBAYA KUKATALIWA.
______________________________________
Unampenda,haijalishi kwa kiasi gani,sio lazima akubaliane na wewe.
Hisia zake na zako uenda haziendani.
Haijalishi unamkubali kiasi gani kwa unavyomuona,tabia na nyendo zake hata kwa muonekano.
Mapenzi Ni kitu Fulani kikiamuliwa kizaliwe kitazaliwa tu,kwa namna na kwa njia yoyote,mahali popote,yamepangwa kuwepo yatakuwepo na endapo hayajapangwa hayawezi kuwepo,ukiyalazimisha yatakutoa machozi anytime na hayadumu.
Jambo muhimu na yakujifunza,tuangalie tunapopeleka hisia zetu K**a tunaowakabidhi mapenzi yetu nao wanatupokeaje.
Tusiishi kwenye mahusiano kwa kujipendekeza.
Kukataliwa sio lazima tuambiwe hatutakiwi,tuso
me nyakati kwa matendo.
Usikate tamaa kwa sababu uliyempenda Sana haonyeshi kukuhitaji na ni vyema kuangalia mahusiano yako ya kesho.
USIANGALIE furaha ya muda mfupi,Leo na kesho ufurahi kumbe ni furaha ya mpito,siku zijazo ni mateso na kusaga meno.
Tujifunze kuacha waende hata kwa namna gani mihoyo yetu imewaganda,tuamue kwa ukatili mkubwa.
Kupenda ni sawa lakini tusipojipenda wenyewe na kujijali wenyewe kwanza ni matumizi mabaya ya hisia,tunazipeleka pasipo kuangalia matokeo ya kesho.
Watu wa kuwaogopa Sana kuwa nao kwenye mahusiano.
Wabinafsi,hata ukimjali vipi anajiangalia yeye.
Waongo,wanatumia uongo kufanya mahovu yao.
Watawala,hawana mapenzi,kwao ni ubabe wanapendwa kutukuzwa.
Tusijipotezee muda,ukipendwa na huoni matokeo,ichukue K**a elimu ya kujifunza kwa Nini na ufanye Nini.
Sio lazima unaempenda atakupenda,tafuta mtu atakaeendana na hisia zako.
Unapojaribu kuforce itakucost inaweza isiwe Leo lakini ikawa kesho.

21/08/2021

Shida moja ya wanawake wanaamini kuwa hawana thamani na wanajidharau bila kuwa na wanaume. Wanachosahau ni kuwa, k**a wewe mwenyewe unajidharau, k**a wewe hujipendi basi ni ngumu kupata mtu ambaye anakupenda. Kwa mfano, kuna watu ni wanyonge, wamenyong’onyea kwakua hawana matako makubwa, kwakua labda si weupe.

Wengine wanajiona kua wamefanana sana na Baba zoa hivyo wanakua hawana mani? Wanajdharaum, ni wapwke na hata ukiwaambia kuwa unawapenda hawaamini na wanaona k**a wanatakiwa kwakua tu wao wanajichukia. Lakini wanasahau kuna wanawake wengi hawnaa matako wameolewa wanakula raha ila kuna wengine wana matako makubwa lakini hawajawahi hata kutongozwa.

Kwa maana hiyo, anza kujipenda, jifuirahia ulivyo, jiamini na utakuta wengine wanakupenda. Unajua kuna wakati mtu anakupigia simu anakuambia kuwa anajichukia ila ukimuangalie unawaza hivi huyu anachukia nini hapa!? Narudia, jipende ulivyo hata kaka kila mtu hakupendi basi utapata mmoja wa kukupenda na kiuhalishai inahitaji mtu mmoja tu wa kukupenda.

18/06/2021

💔KUBALI UHALISIA💔
💘Kamwe Hutoweza Kusonga Mbele K**a Utaendelea Kuishikilia Historia Ya Maumivu Kwa Majuto Na Kujilaumu...Kubali..,Jifunze..,Na Usonge Mbele✍️

15/06/2021

Angalia maajabu ya mwanadamu, ukaoa msichana akapata uja uzito mwezi wa kwanza kwenye ndoa, atasema 'huyu aliolewa na uja Uzito wake, ndio maana waliharakisha. ' Haya chelewa, utaambiwa hauzalishi🤣 Haya pia oa msichana mwenye mtoto, utaambiwa sasa uliona wapi mechi ikaanza 1:0. Haya usioe kabsa, utaambiwa pesa zako zaisha kwenye anasa na starehe za dunia ama pia waseme wacheza sisi kwa sisi. Cha msingi najaribu kusema, huwezi ridhisha kila mtu, mwanadamu yuyu huyu unanunua gari kabla ya kujenga atasema 'yaani ameshindwa kujenga akanunua gari' tembea kwa mguu atasema 'ni mgumu, ana pesa lakini hajijali, hicho kigari Cha laki tano pia hawezi nunua. Haya nunua hicho kigari Cha laki tano, utaambiwa 'hii ni gari Gani, wenye magari wanaendesha magari ya mamilioni. Kiufupi nenda kwa spidi yako, maisha hayana ramani, kila mmoja kwa staili yake. Kuna waliopata neema ya ndoa, kabla ya kupata mtoto, Kuna waliopata neema ya Kazi kabla ya ndoa, na Kuna waliopata neema ya mtoto kabla ndoa na Kazi, yote ni majaliwa, mwanadamu asikupangie jinsi ya kuishi, ishi leo achana na mwanadamu, na huyo mwanadamu ni MWANA WA ADAMU

02/05/2021

MAMBO MATATU AMBAYO WANAWAKE HUFANYA KUHARIBU NDOA ZAO BILA KUJIJUA!

Kuna mambo mengi ambayo wanawake huona k**a ni mambo ya kawaida, huyafanya kwa nia nzuri tu bila kujua kua yanawakwaza waume zao na inawezekana ikawa ni kigezo kikubwa cha ugomvi na kuvunjika kwa ndoa. Wanawake wengi huona kua ukishakua muaminifu, ukamjali mume wako na kumsikiliza inatosha.

Wanaona kuwa kosa kubwa la kukufanya kuachika labda ni uzinifu na dharau kwa mume. Ndiyo haya ni makosa ya kuonekana, lakini kuna makosa ambayo hayaonekani k**a makosa ila ukichunguza ni k**a mdudu ambaye hutafuna ndoa nyingi. Huleta matatizo makubwa katika ndoa, haya unaweza usiyaite makosa ukasema ni tabia ambazo k**a unazo basi badilika.

(1) KWENDA NYUMBANI KWENU MARA KWA MARA; Umeshaolewa, inawezekana unakaa karibu na kwenu au na ndugu zako, kwakua umeingia kwenye familia mpya una kaupweke flani, hujawazoea au kwakua mume anafanya kazi na wewe upo tu nyumbani unaboreka unaona bora uende kusalimia kwenu, si ni karibu wakati mwingine huna hata haja ya kuomba ruhusa.

Kila wiki uko kwenu, kila ukitoka kazini upitie kumsalimia Mama na Mama naye ukikaa siku mbili tatu utasikia kuwa mbona huji kuniona. Huwezi amini Dada yangu wanaume wengi wanachukia hii tabia, hata k**a hakuambii au haonyeshi kuchukia basi jua kuwa ni mbaya. Unapokua unaenda kwenu mara kwa mara inakua ni k**a hujaolewa flani hivi.

Unaweza kuona k**a kitu cha kawaida lakini unamfanya mume wako ajihisi k**a vile anashindana na ndugu zako, kwamba kila wakati unataka kwenda, unaenda peke yako na wala hajui huko unakoenda unaenda kufanya nini? Hata k**a ni kusalimia tu lakini mumeo hajui, kuna mambo mengi ambayo mwanaume atawaza na yote yanamfanya ahisi wewe ni mbinafsi.

Kwanza atawaza kua labda unaenda kuwaambia siri za nyumbani kwenu, anawaza kuwa labda hufurahii ndoa ndiyo maana unaenda kwenu kupumzika, atawaza kuwa wewe ni mbinafsi unawapenda watu wa kwenu kuliko watu wakwako, mwanaume hatakuamini kwani atahisi kuwa hata siri za kwake unapeleka kwa ndugu zako.

Lakini mwanaume atawaza kuwa labda unataka mumkalie, ataona k**a unataka kumdharau kwani si kila wakati utaomba ruhusa na hata ukiomba akikuruhusu basi ni kwa shingo upande kwakua hataki maneno. Ndiyo ni ndugu zako unawapenda lakini kumbuka sasa umeolewa, unahitaji muda na familia yako mpya, kuna kitu gani umekisahau huko, miaka yote hiyo uko nao mbona ulitaka kuolewa.

Kwa wazazi wa zamani wanajua kua mwanamke haendi endi kwao mpaka apelekwe na mume wake, wanajua kua ile kuendaenda inamfanya ajali ndugu zake kuliko ndoa yake. Unapaswa kubaki na mume wako kutumia muda mwingi nayeye, sasa wewe unafanya kazi, mume naye anafanya kazi lakini mwisho wa wiki watoto mgongoni unaenda kwa Mama.

Hata k**a hufanyi kazi ila mume anafanya mwisho wawiki badala upumzike na mumeo umeenda kwenu, ndugu yangu unavunja ndoa yako na ni wanaume wachache sana ambao huamini wanawake wenye tabia hii kwani huwaona k**a hawajali ndoa. Sasa najua unajiuliza unatakiwa kutembelea kwenu angalau mara ngapi?

Binafsi naamini k**a mko karibu sana sana mara moja kwa mwezi au mara moja kila baada ya miezi miwili. Kwanza kuna simu hivyo unajua hali zao, labda k**a kuna ugonjwa ila k**a ni wazima basi ikizidi sana mara moja kwa mwezi ila wastani ni mara moja kila baada ya miezi miwili. Narudia mume wako hakuambii tu lakini haipendi hiyo tabia kila siku kwenu!

Unaweza kujiuliza hivi ni kwanini mume wangu hanishirikishi katika mambo yake, hivi ni kwanini anafanya mambo yake kimya kimya, lakini jibu likawa nikwakua tu hakuamini. Unatumia muda mwingi kwenu na unamuonyesha kuwa unawajali ndugu zako kuliko unavyomjali yeye, anaogopa kukushirikisha kwasababu ile kila siku kwenu anahisi labda mnapanga kumfilisi hata k**a hana kitu cha kufilisi.

(2) KUSHIKIWA AKILI NA NDUGU ZAKO; Rafiki yangu mmoja alikua anafanya kazi katika mkoa flani, ni Kijijini anaishi na mume wake huko na wako vizuri tu. Lakini ndugu zake kwakua wana uwezo wakaona kuwa ndugu yao hawezi kufanya kazi Kijijini hivyo wakamtafutia kazi Dar, wakamuambia ahamie huko na kumuacha mumewe huko huko Kijijini.

Rafiki yangu yule aliniomba ushauri kuwa afanyeje, amuache mume aende Dar au abaki na mumewe kwani huko anakoishi mumewe kashawekeza na hawezi kuhama, maisha yao ni mazuri tu ila yeye hapapendi na ndugu zake kwakua wana uwezo wamemtafutia nafasi Dar. Nilimuambia k**a mume wako ana akili siku ambayo utahamia Dar kuwafuata ndugu zako angepaswa kukukabidhi na talaka yako.

Alishangaa lakini nilimuambia kwangu ishu si wewe kukaa Dar, ishu si wewe kutaka kuishi mjini, lakini pale tu ambapo ndugu zako walipoamua kuingilia ndoa yenu, walipoanza kukupangia namna ya kuishi na mume wako ndiyo ambapo umeanza kuiharibu ndoa yako. Ndoa ni ya watu wawili, haina uhusiano wa ndugu wa mume au ndugu wa mke.

Kuna wanawake ambao hawawezi kufanya kitu bila kumuambia Mama yake, Baba yake au Kaka yake, mwanaume hawezi kuamua kitu na mke we utasikia “Ngoja nikaongee na Mama kwanza, Baba alisema nisifanye hiki na kile, sijui nasubiria mpaka Kaka afanye hiki…” Hapana, unapokuabali kuolewa unatakiwa kukubali pia kuwa ndugu zako si sehemu ya ndoa yako.

Labda k**a unaonewa unanyanyaswa na kupigwa ndiyo hapo ndugu wanapaswa kuingilia lakini si katika maamuzi ya kawaida ya kifamilia. K**a mwanamke una hii tabia ya kila kitu kuwashirikisha ndugu zako kabla ya kufanya maamuzi acha kwani mumeo anaona k**a hana nguvu kwako, anaona k**a vile kaoa famila nzima.

Ndoa za mabinti wengi ambao wazazi wao wana uwezo wa kifedha kidogo huvunjika kwasababu hii, wazazi wanakuamulia kila kitu na k**a mumeo akisema utasikia “K**a hataki nnjoo utakaa hapa kwani yeye ndiyo anatoa pesa… kwani umekosa nini mpaka kuhangaika na huyo mwanaume!” Wazazi wanakuona bado mtoto na wanataka kuingilia ndoa yako.

Achana na hii tabia kwani k**a ukirudi hapo nyumbani ni mwaka tu watakua washakuchoka na kukuona mzigo. Unapaswa kufahamu kua ukiolewa ndugu zako si sehemu ya ndoa yenu hivyo hata k**a utaomba ushauri jifunze kufanya maamuzi yako, inakera ndugu wakiingilia ndoa iwe ni ndugu wa upande wa mwanamke au mwanaume.

(3) KURUHUSU MARAFIKI WAIZOWEE NDOA YAKO; Kuna yule shoga yako ambaye kabla ya ndoa mlikua mnafamya kila kitu kwa pamoja, mlikua mnadanga pamoja, mnaongea kila kitu, kwako kwake na kwake kwako, mnazungumza kuhusu wpaenzi wenu na hata kuvaliana au kuazimana vitu kwenu ilikua k**a kawaida, mlikua k**a mapacha.

Umeolewa unataka kuendeleza urafiki wa namna hiyo, hapana shoga yako si sehemu ya ndoa yako tena. Si sehemu ya maisha yako mapya, hutakiwi tena kumuambia kila kitu na anapaswa kuwa na mipaka na nyumba yako, hakuna tena kuazimana vitu na mambo k**a hayo. Labda nifafanue kidogo ndiyo mtanielewe, sisemi umchukie shoga yako hapana, bali kuwe na mipaka.

Kabla ya ndoa ulikua unamuambia shoga yako kila kitu kuhusu wewe, yalikua ni maisha yako, lakini sasa umeolewa, maisha yako hayawi yako, siri zako haziwi zako, matatizo yako hayawi yako bali ni yako na mume wako. Kwa maana hiyo unapomuambia shoga yako siri zako humuambii zako tu unamuambia na siri za mume wako bila idhini yake.

Wakati hujaolewa ulikua unamuazimisha nguo na vitu vingine, zilikua nguo zako vitu vyako. Lakini sasa umeolewa, si nguo zako tena, si vitu vyako tena, ni vitu vyako na mume wako, hata k**a hajakununulia yeye lakini ulinunua wewe yeye akanunua chakula, ni vyenu, nguo zako si zako ni zenu, sasa iweje nguo ambayo anakuvua mumeo umpe na rafiki yako naye avae?

Kabla ya ndoa alikua huru kuingia chumbani kwako, akakaa na khanga moja na kupiga stori lakini umeolewa, si chumbani kwako tena ni chumbani kwenu, hana uhuru huo kwani ukishampa uhuru huo basi unamnyima uhuru mume wako wa kujidai chumbani. Nilazima kuwe na mipaka, shoga yako aishie sebuleni hata jikoni haruhusiwi.

Narudia haya mambo ya shoga yako anakuja kwako mnaingia jikoni kupika yaache huko huko katika uchumba, ushakua mke wa mtu si jikoni kwako tena ni jikoni kwenu. Sijui k**a mmenipata, ni mambo ya kawaida lakini yanavunja ndoa, tena katika hili kuwa makini sana kwani nirahisi shoga yako kukugeuka na kukuchukulia mume.

K**a unavyojua sisi wanaume kuchukuliwa nako si kazi sana, unapomambia shoga yako kila tatizo la ndoa yako unakua unampa silaha, unamuambia kwa huna furaha una matatizo hivyo mumeo nirahisi kuibika, anajua udhaifu wa mume wako hivyo unampa vitu vya namna ya kumteka, trust me shoga yako anamtaka na mumeo hatajivunga akitakwa.

Lakini unapomuambia kila furaha, kila kudekezwa na starehe basi ni k**a unampa wivu, unamuambia vitu ambavyo yeye anavitamani lakini havipati hivyo unamlazimisha kufanya juu chini ilia avipate na si kwa kufanya kingine bali kwa kumtafuta huyo huyo mume wako.

Sijui k**a mmenipata Dada zangu, hembu jifunze kutenganisha urafiki na ndoa, shoga yako ni rafiki yako lakini si rafiki wa ndoa yako. Usiruhusu awe sehemu ya ndoa yako na hata k**a ikilazimika kuongea basi hakikisha unayemuambia anaweza kukusaidia, usiruhusu akajua kila kitu katika ndoa yako kwani wewe hujui kila kitu katika maisha yake.

Address

Mombasa
Mombasa
80400

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when WILD ROCKY TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category