14/01/2025
*S H A I R I* *
*SOMA MWANANGU.*
1.
Nimekuja pasi hodi,ila sinuze maswali,
Si ambari si ye udi, ninao wote wawili,
Mzazi sinayo budi,nikushauri mawili,
*SOMA WEWE MWANA SOMA,ELIMU NI UFUNGUO.*
*2* .
Nayasema ya wahenga,elimu ni ufunguo,
Si wa nyumba ulojenga,maisha yavishe nguo,
Ya hadhi ila so kanga,mvuvi hachi ufuo *,
*SOMA* *WEWE MWANA** *SOMA,ELIMU NI UFUN*
*GUO*
*3* .
Kalamu ishike titi,andika yote ya sawa,
Ukaapo kwa dawati,mafunzo na yawe dawa,
Katu usiwe na ati,paa njiwa una mbawa,
*SOMA WEWE MWANA SOMA,ELIMU NI UFUNGUO.*
*4* .
Aku sipende mkia,hauna kamwe minofu,
Bora kichwa mara mia,sitelekeze udufu,
Namba moja pambania,waweza sinayo hofu,
*SOMA WEWE MWANA SOMA,ELIMU NI UFUNGUO.*
*5* .
Nidhamu iwe msingi,siendekeze vituko,
Linda utu kwa vigingi,heshimu walimu wako,
Wa kesho ni wewe dingi,iboreshe kesho yako,
*SOMA WEWE MWANA SOMA,ELIMU NI UFUNGUO.*
*6* .
Huwezi kudijitika k**a hunayo elimu,
Analogi tulitoka,hakunao umuhimu,
Bila ya cheti hakika,huwezi chonga sanamu,
*SOMA WEWE MWANA SOMA,ELIMU NI UFUNGUO.*
*7* .
Nalikunja jamvi langu,ila sitoenda nalo,
Libaki hapa mwanangu,talirudia tumolo,
Huno ushauri wangu,uthibiti zake kilo,
*SOMA WEWE MWANA SOMA,ELIMU NI UFUNGUO.*
*S H U K R A N I.!!!*
゚viralシ