29/12/2024
Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua amewataka Gen Z na Milenia kuendelea kuiwajibisha serikali kwenye mitandao ya kijamii, Akizungumza mjini Kakamega hii leo alipohudhuria mtanange wa Cleo Malalah SuperCup, Gachagua amesema kuna haja ya wao kuendelea kufichua maovu katika jamii.
Gachagua anasema kizazi cha vijana ni matumaini ambayo nchi inayo katika njia ya uadilifu, akisema kwamba watasuluhisha matatizo ya kisiasa ya nchi hii mara moja na kwa wote, amewarai vijana kupiga hatua zaidi na kuwa wapiga kura waliosajiliwa ili kubadilisha uongozi wa nchi.
Amesisitiza wito wake kwa vijana kukamilisha kikamilifu uharakati wao kwenye mitandao ya kijamii kwa kuleta mabadiliko na kuyafanya kuwa kweli kupitia kura ya 2027, Vijana hao wamekuwa wakitumia nafasi ya X na Tiktok kutoa wito wa uwajibikaji kutoka kwa uongozi wa nchi, tangu kabla ya maandamano ya kupinga serikali ya Juni 2024, Uwepo wao kwenye mitandao ya kijamii ulimlazimu Rais William Ruto kufanya mkutano wa anga wa X, ili kujadili mwelekeo wa nchi na vijana.
Vuguvugu la Gen Z pia liliona mabadiliko ya baraza la mawaziri, kuahirishwa kwa Mswada wa Fedha wa 2024, kuundwa kwa serikali pana na mkutano na Rais wa zamani Uhuru Kenyatta.