RND news

RND news Nyumbani kwa habari

20/04/2021

hi my followers leo Niko na zawadi unacho hitajikufanya ni kutuma ujumbe wa kuonyesha uliko kisha utulie usubiri airtime.

05/04/2021

COVID19 NI HATARI.
Kutoka RND NEWS tunakuomba popote ulipo kuendea kufuata masharti yaliowekuwa ili kukabiliana na covid19.Osha mikono,zingatia umbali pamoja na kuvalia barakoa.

04/04/2021

MADHILA YA COVID19
Pasaka ya mwaka huu na uliopita imekuwa tofauti Sana hii ni baada ya covid19 kuasili humu nchini,kulingana na masharti aliyo yatoa rais katika hotuba yake kwa nchi maeneo ya kuabudu katika eneo hili la marachi central hii leo yameshuhudia watu wachache mno ikilinganganishwa na miaka miaka mingine iliyopita ambapo masharti yaliyo tolewa yanasema waumini thuluthi tatu tu ndio wanaohitajika kanisani. Wengi wa waumini wamesalia manyumbani huku wakifatilia ibaada kupitia redio au televisheni.

02/04/2021

USALAMA UMEZOROTA BUKHALALIRE.
Wizi umekithiri katika soko ya kale ya bukhalalire kwani usiku wa kuamkia leo duka limeripotiwa kuvunjwa na wezi na kuibwa Mali ya thamani isiyo julikana,hayo yametokea wiki chache baada ya mwizi kuwawa na wakaazi na wengine aliokuwa nao kutoroka,wakaazi wanasema ni utepetevi wa maafisa wa wapolisi walio katika kituo cha Bukhalalire ndio umesababisha hayo kwani hawashiki Doria nyakati za usiku na huku wakiitwa wanawasili k**a wamechelewa, wanaomba maafisa hao wahamishiwe kwingine kwani huenda wanashirikiana na wahalifu hao ,wakaazi wanawaonya wanaotenda uhalifu huo kuwa arubaini zao zitafika

01/04/2021

watu wangu plz like and follow hii page kwa habari za marachi central.

01/04/2021

HOSIPITALI YA KHUNYAGU KUIMARISHWA.
Naibu wa gavana kaunti ya busia amesema hosipitali ya khunyangu inaenda kuekewa mashine ya upasuaji pamoja na ile ya 'exray' ili kuwasaidia wakaazi wa wadi zilizo karibu sambamba na kupunguza msongamano wa wanaotafuta matibabu hayo katika hosipitali ya rufaa ya busia pia amesema makafani itawekwa katika hosipitali hio,amesema pia hosipitali ya Bumala B itapandishwa na kuwa ya kaunti ndogo(sub county),pia amedokeza kuwa wahudumu wa afya wa kujitolea watalipwa marupurupu yao,asema hayo akiwa katika shule ya msingi ya Dadira.

01/04/2021

TUKO TAYARI KUKABILIANA NA COVID19.
Gavana wa busia alisema ako tayari kukabiliana na mgonjwa wa covid 19 atakayehitaji hewa ya oksigeni kwani mitungi ya kutosha imewekwa katika hosipitali ya rufaa ya busia,alisema hayo mnamo jumanne katika mahojiano na redio moja humu nchini,alitumia fursa hio kuwaomba wakaazi wake wanaohitajika kupata chanjo ya covid19 kufika katika hosipitali za kaunti ndogo (sub county)ili kupata chanjo hio.

31/03/2021

KIU KIMEMALIZWA
Ni afueni kwa wachuuzi katika soko la murumba katika wadi ya marachi central hii ni baada mfadhili kujitokeza na kuwachimbia maji katika soko hilo,wanasema kuwa wamekuwa wakigaramika sana ili kupata bidhaa hio muhimu,mfadhili huyo ni Mozartbet ambaye ni mmoja wa mashirika ya k**ari nchini.

20/03/2021

kutakwa na vipindi tutakavyokuwa tukikulea hapa kwenye rnd news ikiwemo taarifa zinazochipuka huku busia ,makala ya tembea busia na kadhalika.

20/03/2021

karibu kwa habari zaidi hapa kwenye rnd news

Address

Busia

Telephone

+254762345758

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when RND news posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category


Other Media in Busia

Show All

You may also like