
23/05/2025
: Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila ametoa wito kukomeshwa kwa kile alichokiita "udikteta" nchini humo siku moja tu baada ya kuondolewa kinga ya kutoshtakiwa.
"Udikteta lazima ukomeshwe, na demokrasia, utawala bora na ustawi wa kijamii lazima urejeshwe," Kabila amesema katika hotuba ya nadra iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye mitandao.