Sauti ya dunia Newsweek

16/12/2021

Baraza la Usalama la UN laombwa kujadili Korea Kaskazini.

Baadhi ya wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa ikwemo Japan, wamewaomba wenzao miongoni mwa wanachama 15 kwenye baraza hilo kufanya kikao cha faragha ili kuzungumzia hali inayoendelea ya ukiukaji wa haki za binadamu Korea kaskazini.

Balozi wa Marekani kwenye baraza hilo Linda Thomas Greenfield wakati akizungumza kwa niaba ya Marekani,Uingereza, Estonia, Ufaransa, Ireland, Japan na Norway ambao wote ni wanachama isipokuwa Japan,amesema kwamba ni lazima mwenendo wa Korea kaskazini wa kukiuka haki za binadamu pamoja na matumizi ya silaha nzito upewe kipaumbele na kukomeshwa kwa kuwa unahatarisha usalama wa kimataifa.

Mwaka 2014, ripoti kutoka kwa tume maalum ya uchunguzi iliyobuniwa na baraza hilo ilifichua hali halisi ya ukatili mkubwa dhidi ya binadamu, unaoendelea kutekelezwa Korea kaskazini. Tangu wakati huo , baraza hilo limekuwa likizungumzia hali hiyo kila Decemba licha ya baadhi ya wanachama kusema wamba halifai kushikilia jukumu hilo.

16/12/2021

Bunge la Marekani laidhinisha kikomo cha ongezeko la deni la taifa.

Baraza la Wawakilishi lilipitisha kikomo cha ongezeko la deni, mapema Jumatano kwa kura 221 kwa 209 na kura moja pekee ya Republican iliyounga mkono.

Uidhinishaji wa Seneti ulikuja Jumanne kwa kupitishwa na Wademocrat 50 kwa kura ya “Ndio” huku Warepulikan 49 wakipinga.

Bunge la Marekani limeidhinisha hatua ya kuongeza kiwango cha deni la taifa na kupigia kura ili kuepuka kushindwa kulipa deni. Rais Joe Biden bado anahitaji kutia saini sheria hiyo hatua ya mwisho katika mchakato huo ambao umewagawa waDemocrats na waRepublicans kwa miezi kadhaa.

Baraza la wawakilishi lilipitisha kikomo cha ongezeko la deni, mapema leo jumatano kwa kura 221 kwa 209 na kura moja pekee ya Republican iliyounga mkono. Uidhinishaji wa seneti ulikuja Jumanne kwa waDemocratic 50 kupiga kura ya “Ndio” na waRepuplican 49 wakipinga.

16/12/2021

Biden aahidi msaada kwa watu walioathirwa na dhoruba Kentucky.

Rais wa Marekani Jumatano ametembelea jimbo la Kentucky ili kujionea mwenyewe hasara iliyosababishwa na vimbunga kadhaa vya nguvu sana na kuacha takriban watu 74 wamekufa huku maelfu wengine wakiwa hawana makazi mwishoni mwa juma.

Ijumaa na Jumamosi liyopita, Biden aliarifiwa kuhusu hali ilivyokuwa kuhusu juhudi za uokozi kutoka na dhoruba ambayo ilipiga vibaya jimbo la Kentucky na majimbo jirani. Alitembea kwa helikopta majimbo yaliyokumbwa na dhoruba ambako alishuhudia majengo yalioporomoka pamoja na manusura waliokuwa wakitembea barabarani.

Kiongozi huyo wakati wa ziara ya Jumatano ameahidi msaada kutoka serikali kuu akisema kwamba kutokana na uharibifu uliotokea, baadhi ya miji italazimika kujengwa upya. Gavana wa jimbo la Kentucky Andy Beshear amesema Jumanne kwamba zaidi ya watu 100 hawajulikani walipo jimboni humo na hasa kwenye mji mdogo wa Dawson Springs wenye takriban 3,000.

Msemaji wa ikulu ya Marekani Karine Jean Pierre aliwaambia wanahabari waliokuwa ndani ya ndege ya rais kwamba ujumbe wa rais ulikuwa wa kuwahakikishia watu walioathirika kwamba serikali yake itafanya kila iwezalo kuhakikisha wamerudi kwenye hali ya kawaida ya maisha.

16/12/2021

Serikali ya Israel kuchangia chanjo milioni 1 za virusi vya corona kwa mpango wa COVAX.

Serikali ya Israel siku ya Jumatano imesema itachangia chanjo milioni 1 za virusi vya corona kwa mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wa COVAX.

Serikali ya Israel siku ya Jumatano imesema itachangia chanjo milioni 1 za virusi vya corona kwa mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wa COVAX.

Wizara ya Mambo ya Nje ilisema chanjo za AstraZeneca zitahamishwa katika wiki zijazo, uamuzi ambao ulikuwa sehemu ya kuimarisha uhusiano wa Israeli na nchi za Kiafrika.

Nimefurahi kuwa Israeli inaweza kuchangia na kuwa mshirika katika kutokomeza janga hili ulimwenguni, Waziri wa Mambo ya nje Yair Lapid alisema.

Tangazo hilo lilisema kuwa chanjo hizo zitafikia karibu robo ya nchi za Afrika, ingawa haikutoa orodha. Israel ina uhusiano wa karibu na mataifa kadhaa ya Afrika, yakiwemo Kenya, Uganda na Rwanda. Israel pia ilianzisha uhusiano na Sudan mwaka jana k**a sehemu ya mfululizo wa mapatano yaliyosimamiwa na Marekani.

15/12/2021

Hali ya ukame yaendelea kudorora Somalia.

Ona maoni

Hali ya ukame nchini Somalia inasemekana kudorora licha ya kuwepo kwa mvua katika baadhi ya maeneo kulingana na afisa wa ngazi ya juu kwenye huduma za kibinadamu.

Kulingana na Ian Ridley anayeongoza ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya masuala ya kibinadamu, nchini Somalia, wakati wa mahojiano na VOA amesema mvua za hivi karibuni hazitoshi na kwamba ukame umeendelea kushuhudiwa.

Ridley amekuwa akitembelea maeneo yalioathiriwa zaidi katika wiki za karibuni. Wakati akizungumza kutoka mji mkuu wa Mogadishu, Ridley amesema kwamba visima vilivyoko tayari vimeanza kukauka na kwa hivyo kuongeza hitaji la visima vyenye kina kirefu.

Ameongeza kusema kwamba hali iliyoko imelazimisha watu kuhama makwao, baadhi wakisafiri umbali wa kati ya kilomita 30 na 40 kutoka maeneo ya mashambani hadi kwenye maeneo ya mijini.

Amesema pia kwamba kuna hatari kubwa ya kutokea kwa magonjwa k**a vile kipindupindu huku surua ikisemekana kuongezeka miongoni mwa watu walioko kwenye makambi.

15/12/2021

Utafiti unasema chanjo ya Pfizer-BioNTech inafanyakazi kiasi kuzuia Omicron Afrika Kusini.

logo
Jumatano, Desemba 15, 2021 Local time: 20:13
HABARI
Utafiti unasema chanjo ya Pfizer-BioNTech inafanyakazi kiasi kuzuia Omicron Afrika Kusini
15 Desemba, 2021

Ona maoni

Utafiti mmoja umeonyesha chanjo ya Covid-19 ya Pfizer-BioNTech inafanyakazi kiasi nchini Afrika Kusini katika kuwalinda watu wasipate maambukizi ya virusi nje ya hospitali toka aina mpya ya virusi Omicron kugunduliwa.

Utafiti huo uliofanyika kiuhalisia na matokeo yake kuchapishwa Jumanne, unaonyesha kati ya Novemba 15 mpaka Desemba 7 watu ambao walikuwa wamepata dozi mbili za chanjo walikuwa na asilimia 70 ya kuwawezesha wasilazwe hospitali ikiwa chini ya asilimia 93 kulingana na takwimu za wimbi la maambukizo ya virusi vya Delta.

Inapokuja suala la kujiepusha maambukizo kwa pamoja utafiti uliofanywa na taasisi ya bima binafsi ya Afrika Kusini, Discovery Health, umeonyesha kwamba ulinzi dhidi ya maambukizi ya Covid-19 umeshuka mpaka asilimia 33 kutoka asilimia 80 ya awali.

Takwimu kutokana na uchambuzi uliofanyika kiuhalisia ni za kwanza kuonyesha namna chanjo zinaweza kufanyakazi dhidi ya virusi vipya vya Omicron nje ya tafiti za kimaabara ambazo mpaka sasa zimeonyesha kupungua uwezo katika kukabiliana na virusi.

Matokeo ya utafiti yalitegemea uchambuzi wa taasisi ya Discovery ya utafiti wa kitabibu na timu za wataalamu wakishirikiana na baraza la utafiti wa kitabibu la Afrika Kusini.

Afrika Kusini iliufahamisha ulimwengu mwezi Novemba uwepo wa virusi vipya ya Omicron, na kutoa ishara kwamba vinaweza kusababisha wimbi lingine la maambukizi duniani, na kusabaisha kuwekwa marufuku za kusafiri kwenda kusini mwa Afrika.

Maambukizi ya Afrika Kusini kwa siku yameongezeka mpaka zaidi ya 20,000, huku asilimia 35 ya vipimo vikirejea na maambukizo katika viambatanisho vya Jumanne na zaidi watu ya 600 wakilazwa na vifo vikiwa 24.

15/12/2021

Afrika yalegea katika utoaji wa chanjo za Covid-19.

Shirika la afya duniani WHO Jumanne limesema kwamba huenda Afrika isifikie lengo lake la kutoa chanjo kwa asilimia 70 ya watu wake bilioni 1.3 dhidi ya COVID kufikia nusu ya pili ya 2024, lengo ambalo tayari mataifa mengi tajiri yamefikia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, onyo hilo limetolewa wakati ulimwengu ukikabiliana na aina mpya ya virusi vya omicron. Baadhi ya mataifa tajiri yameidhinisha dozi ya tatu ya booster kwa watu wake, wakati chini ya asilimia 8 ya watu wa Afrika wakiwa wamepokea chanjo kamili.

Flavia Senkubuge ambaye ni mkuu wa chuo cha dawa cha Afrika kusini wakati akizungumza na wanahabari kwenye kikao cha WHO, amesema kwamba tatizo hilo haliwezi kumalizika k**a ulimwengu hautashirikiana pamoja.

Ni mataifa 20 pekee kati ya 54 barani Afrika ambayo yametoa chanjo kamili kwa takriban asilimia 10 ya watu wake wakati mataifa 10 pekee yakiwa yametoa chanjo chini asilimia 2 kwa watu wake barani humo. Kufikia sasa Afrika imepokea takriban dozi milioni 434 wakati 910,000 zikisemekana kuharibika kwenye mataifa 20.

15/12/2021

Mahak**a kuu ya Afrika kusini imeamuru Rais wa zamani nchini humo Jacob Zuma arudi gerezani baada ya kutengua uamuzi wa kumwachilia kwa msamaha wa kiafya, uamuzi wa mahak**a ulionyeshwa Jumatano.

Jacob Zuma mwenye umri wa miaka 79 alianza msamaha wa matibabu mwezi Septemba na anatumikia kifungo cha miezi 15 kwa kuidharau mahak**a baada ya kupuuza maagizo ya kushiriki katika uchunguzi wa rushwa.

Zuma mwenye umri wa miaka 79 alianza msamaha wa matibabu mwezi Septemba na anatumikia kifungo cha miezi 15 kwa kuidharau mahak**a baada ya kupuuza maagizo ya kushiriki katika uchunguzi wa rushwa. Katika mwezi huo huo mahak**a kuu ya Afrika kusini ilitupilia mbali ombi lake la kutengua hukumu hiyo. Michakato ya kisheria dhidi ya Zuma kwa madai ya rushwa wakati wa utawala wake wa miaka tisa inatazamwa na wengi k**a mtihani wa uwezo wa Afrika kusini baada ya enzi ya ubaguzi kuhusu uwezo wake kuimarisha utawala wa sheria hasa dhidi ya watu wenye madaraka na wenye uhusiano na uongozi.

Zuma alikwenda mwenyewe hapo Julai 7 kuanza kifungo chake na kusababisha ghasia mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini Afrika kusini katika kipindi cha miaka kadhaa huku wafuasi wa Zuma waliokuwa na hasira wakiingia mitaani.

01/08/2021

Baada ya Wanajeshi wa Marekani kutangaza kuondoka Afghanistan baada ya miaka 20 ya vita, kundi la kwanza la Raia wa Afghanistan ambao walifanya kazi na Wanajeshi hao limewasili Washington DC Marekani kuanza maisha mapya baada ya Marekani kuwapatia hifadhi ili kukwepa kuuwawa na Wapiganaji wa Taliban.

Ndege iliyowabeba Raia 221 wa Afghanistan ilitua Alfajiri Washington DC ikijumuisha Watoto zaidi ya 70 ambao wao na familia zao wataanza maisha mapya nchini Marekani chini mpango maalum wa kutoa visa kwa Waafghani waliofanya kazi na vikosi vya Marekani.

Makundi mengine k**a hayo yanatarajiwa kuwasili Marekani katika wiki chache zinazokuja yakijumuisha Watu waliofanya kazi ya ukalimani na shughuli nyingine kuvisaidia vikosi vya Marekani kutimiza jukumu lake Afghanistan.

Chini mpango huo wa visa maalum zaidi ya Waafghani 2,500 pamoja na familia zao huenda watahamia Marekani na kuanza maisha mapya, mpango huu wa visa maalum uliidhinishwa na Bunge la Marekani mwaka 2006 ili kuwapatia hifadhi Raia wa Iraq na Afghanistan ambao wamehatarisha maisha yao kwa kufanya kazi na Serikali ya Marekani.

Kwa jumla Marekani na washirika wake (Nchi nyingine) wanalenga kuwapatia hifadhi Raia 50,000 wa Afghanistan katika juhudi za kuwalinda dhidi ya uwezekano wa kulengwa na kundi la Wanamgambo wa Taliban ambalo liliondolewa madarakani wakati vikosi vya kigeni vilipoingia Afghanistan mwanzoni mwa miaka ya 2000.

01/08/2021

Kwenye list ya habari kubwa za wiki hii imo hii ya Saif al-Islam Mtoto wa aliyekua Rais wa Libya Muammar Muhammad Abu Minyar al-Gaddafi ambapo baada ya miaka 10 ya ukimya, ameibuka na kusema yupo hai na anataka kurudi kuiongoza Libya na kuliunda upya taifa hilo ambalo sasa limepasuka vipandevipande.

Wiki hii New York Times wamemuhoji Islam mwenye umri wa miaka 49 ambae anasema toka kuuwawa kwa Baba yake October 20 2011 Watu wa Libya wamekua wakiishi kwa kuteseka na hakuna chochote bora walichokipata kutoka kwa Watu wanaoiongoza Libya kwa sasa.

Islam ameahidi kurudi tena kufanya siasa kwenye Taifa lake analolipenda na kuongeza kuwa hakuna tena uhasama kati yake na Watu waliowahi kumfunga jela na kumtesa baada ya Baba yake kuuwawa na sasa Watu hao ni Marafiki zake.

Hata hivyo Saif Al Islam ambae ana PhD aliyoipata London School of Economics amekua akitafutwa na Mahak**a ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa tuhuma za uhalifu wa kivita akishutumiwa kuchochea mauaji ya Waandamanaji waliokuwa wakipinga utawala wa baba yake.

Muammar Gaddafi aliiongoza Libya kwa karibu miaka 40 na Taifa hilo lilitajwa kuwa na utulivu na Wananchi kuishi maisha bora tofauti na wanayoishi sasa baada ya kuuwawa kwake mwaka 2011 na Waasi kuibuka, Watoto 7 wa Gaddafi waliuwawa kwenye machafuko hayo ya mwaka 2011 lakini Islam alifanikiwa kuepuka kifo.

ISRAEL LICHA YA UBABE NA UBISHI ILIONAO ILA KUNA JAMBO LINAWAKOSESHA USINGIZI KIASI CHA KUJIONA BADO HAWAJAKAMILIKA!!!, ...
29/07/2021

ISRAEL LICHA YA UBABE NA UBISHI ILIONAO ILA KUNA JAMBO LINAWAKOSESHA USINGIZI KIASI CHA KUJIONA BADO HAWAJAKAMILIKA!!!, TWENDE PAMOJA TULIJUE JAMBO HILO KIUNDANI NA SABABU ZAKE.

Imeandikwa Na Raphael Mtui.

Waisrael wana changamoto nyingi, k**a vile vita vya mara kwa mara, pamoja na chuki dhidi yao na Utaifa wao (Anti-semitism).

Lakini hayo sio ishu kwa sasa, maana hayo huwa wanayashinda kila mara, na wanaona wana support ya kutosha kutoka mataifa mbalimbali makubwa.

Lakini kuna kikwazo kikubwa na kigumu sana walichonacho, nacho ni KUKOSA HEKALU.

K**a tulivyokwisha kuona katika makala zingine, hekalu halikuwa tu ni swala la jengo, bali lilikuwa ni swala la Uwepo halisi wa Mungu kuwepo katikati ya watu wake.

Kutokuwa na hekalu, mara nyingi humaanisha kuwa Uwepo wa Mungu haupo katikati ya Wana wa Israel.

Ni sawa na Mkristo anayejua Mungu hukaa ndani yetu moyoni, lakini itokee hatuna hiyo mioyo!!

Wakati wa Hekalu, hakukuwa na shaka yoyote kuhusu uwepo wa Mungu ndani ya Hekalu la Yerusalemu, na udhihirisho wa nguvu zake ulikuwa ni dhahiri sana.

Tangu Hekalu la Pili libomolewe mwaka 70AD, hadi leo Hekalu halijajengwa tena hadi leo.

Kwa karibu miaka 2000 ya kuhenyeka bila kuwa na taifa (national home), bado imekuwa vigumu sana sana kujenga Hekalu la Tatu na kurudisha zile ibada zao.

Eneo la kujenga lipo nchini mwao, lipo ndani ya jiji la Yerusalemu, LAKINI HAWATHUBUTU BADO KUJENGA HEKALU!!

Kwa nini? Baba mwenye nyumba anashindwaje kuwasha TV yake tena iliyo sebuleni kwake?

Kuna vikwazo kadhaa very serious ambavyo vinawafanya Waisrael washindwe kujenga Hekalu.

Pamoja na kwamba lazima lijengwe kutimiza mambo ya unabii, lakini swali linajengwaje?

Maswali haya huwanyima usingizi kabisa Wayahudi ama Waisreli wa leo.

Sasa tuone vikwazo vinavyowafanya wasiweze kujenga Hekalu hili:

1) Kikwazo cha kwanza na cha wazi, ni ile misikiti miwili ya kihistoria yenye umri zaidi ya karne 13.

Misikiti hiyo ni Al Shakhrah au maarufu k**a Dome of The Rock na msikiti mwingine ni ule maarufu kwa jina la Al Aqsa.

Misikiti hiyo imejengwa pale pale mlima mtakatifu liliposimama Hekalu.

Eneo hili lilidakwa na Waislamu kwenye miaka ya 600AD, kipindi ambacho Waisrael walikuwa wana miaka k**a mia nne hawaruhusiwi kuishi nchini mwao.

Walipigwa 'pini' hiyo na utawala wa Kirumi.

Hiki ni ndani ya kile kipindi kirefu sana Waisraeli waliishi popote bila kuwa na taifa hadi walipopata uhuru mwaka 1948.

Waislamu walishika mlima huu mtakatifu.

Dini ya Uislamu inapaheshimu sana na panahesabika ni sehemu ya tatu kwa utakatifu duniani baada ya Meka na Medina.

Kitendawili kikubwa sana hapo!!.

Kwa hiyo, jitahada zozote za kuharibu misikiti hiyo, au kupunguza uwezekano wowote wa Waislamu kufika hapo kwa uhuru, au kujenga chochote cha Kiyahudi ndani ya eneo hilo, katikati, chini, pembeni, juu, ni kitu kinachoweza kuleta machafuko mabaya sana ya kimataifa(sio ya kitaifa), ya kimataifa!!

Hicho ndio kikwazo namba moja!!

2) Kingine wanachosubiria kwa miaka mingi sana, ni ng'ombe mke mwekundu (Red Heifer) azaliwe nchini Israel, kwa ajili ya..............!!!!!

ITAENDELEA KWENYE GROUP

WhatsApp Group Invite

29/07/2021

Mamlaka ya udhibiti na kuzuia magonjwa Marekani CDC imetangaza amri mpya kuwa watu wote walio choma chanjo ya kuzuia Corona waanze tena kuvaa barakoa katika mikusanyiko ya ndani.

Amri hii inakuja miezi kadhaa tangu mamlaka hiyo ilipotoa ruksa kwa wote walio chanjwa kuto vaa barakoa.

Maamuzi ya CDC kutaka waliochanjwa kuvaa barakoa yametokana na kuongezeka kwa watu wenye maambukizi ya Corona katika miji kadhaa nchini humo ikiwemo Florida na Missouri vilevile kutokana na kuongezeka kwa ripoti ya maambukizi ya virusi hatari zaidi aina ya Delta kwa watu ambao wamekwisha pata chanjo zote mbili.

Mamlaka hiyo imeongeza kuwa kila mtu anapaswa kuvaa barakoa na kuweka msisitizo kwa Walimu, wafanyakazi, wanafunzi na wageni katika shule zote bila kujali wamechanjwa au bado.

23/07/2021

Kampuni moja ya magari kwenye Mji wa Munich Ujerumani imevumbua gari linalotumia miale ya umeme wa jua, umeme unaotokea kwenye betri zilizo kwenye paa na milango pekee unatosha kabisa kuliendesha gari hili kwa kilometa 30 kwa siku.

Iwapo Mtu atataka kulitumia kwa safari ndefu bado kuna betri nyingine, Wataalamu walioliunda wanasema wamelishughulikia kwa miaka mitano mpaka kufika walipofikia. via DW Kiswahili.

03/07/2021

Imezoeleka kwa baadhi ya Watu Tanzania kutumia page zao za mitandao ya kijamii 'kuchamba' Watu waliowazingua au waliowaudhi, sasa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dr. Faustine Ndugulile amewakumbusha Watu kuacha kufanya hivyo kwani kisheria ni kosa 'kuchamba' Mtu mtandaoni.

Dr. Ndugulile akiwa kwenye uzinduzi wa mpango mkakati wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na tovuti ya Wizara hiyo alisema moja ya vitu Watanzania wanapaswa kufahamu ni kwamba Mtu akitumia mfano Instagram kumsema Mtu vibaya (kumchamba), ni kosa kisheria au kumkashifu Mtu mtandaoni pia ni kosa hata k**a account iliyotumiwa kufanya kosa hilo inatumia jina feki Mtu ilimradi account hiyo imefanya uhalifu Mmiliki wake atatafutwa na kuchukuliwa hatua.

03/07/2021

Mchekeshaji wa Marekani Bill Cosby aliyesote gerezani kwa zaidi ya miaka miwili ya kifungo alichopewa cha kati ya miaka mitatu hadi miaka kumi jela, ameachiwa huru na Mahak**a kuu ya Pennsylvania.

Mwaka 2018, Cosby alihukumiwa hadi miaka 10 jela baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu ya unyanyasaji wa kingono kwa kumlewesha na kumnyanyasa kingono Mwanamke aitwae Andrea Constand mwaka 2004.

Mahak**a kuu ya jimbo la Pennsylvania leo Jumatano imetengua hukumu yake na kumfutia mash*taka yake na hivyo kuachiwa huru.

21/02/2021

Serikali haijazuia barakoa lakini tuwe waangalifu katika kuchagua barakoa ipi ninavaa, tutaangamia, msifikiri tumapendwa mno vita ya kiuchumi ni mbaya, namuona mama pale amevaa ya kitenge, hongera sana mama, hizi tunazozinunua madukani tunajiua wenyewe''.
''Ni lazima niliseme, watatukana lakini nina wajibu wa kusema ukweli. Tutaje ni nchi gani ambayo hawajafa watu kwa corona, maelfu wanakufa, kuna nchi iliwahi kupoteza watu elfu tatu kwa siku moja na wanavaa barakoa, saa nyingine wanavaa mbilimbili. Rais John Pombe Magufuli leo kanisani Das es Salaam.

06/02/2021

Idadi ya nchi za Afrika ambazo watu wake hawataruhusiwa kuingia Uingereza imefikia 17, kuanzia februari 15. Raia wa Uingereza na wale wenye ukaazi wanaowasili toka nchi hizo watatakiwa kujitenga kwa lazima kwa siku 10, watakaa kwenye hoteli zilizochaguliwa na serikali na kujilipia pound 73 kwa siku. Jumla ya nchi zilizowekwa kwenye orotha hiyo ya Uingereza ni 33 ambapo 17 ni za Africa ikiwemo afrika yakusini, botswana, zambia, msumbiji, malawi, angola, congo DRC, Rwanda, Tanzania, Burundi, cape verde, Eswatini, lesotho, Mauritius, Namibia na Ushelisheli. Uingereza ni miongoni mwa nchi zenye vifo vingi vinavyotokana na Uingereza ambapo mpaka sasa watu zaidi ya laki moja na elfu kumi na moja wamefariki, wagonjwa wakifikia milioni tatu laki tisa huku dunia nzima ikiwa na wagonjwa zaidi ya milioni 105, vifo milioni 2.3 na waliopona ni milioni Idadi ya nchi za Afrika ambazo watu wake hawataruhusiwa kuingia Uingereza imefikia 17, kuanzia februari 15. Raia wa Uingereza na wale wenye ukaazi wanaowasili toka nchi hizo watatakiwa kujitenga kwa lazima kwa siku 10, watakaa kwenye hoteli zilizochaguliwa na serikali na kujilipia pound 73 kwa siku. Jumla ya nchi zilizowekwa kwenye orotha hiyo ya Uingereza ni 33 ambapo 17 ni za Africa ikiwemo afrika yakusini, botswana, zambia, msumbiji, malawi, angola, congo DRC, Rwanda, Tanzania, Burundi, cape verde, Eswatini, lesotho, Mauritius, Namibia na Ushelisheli. Uingereza ni miongoni mwa nchi zenye vifo vingi vinavyotokana na Uingereza ambapo mpaka sasa watu zaidi ya laki moja na elfu kumi na moja wamefariki, wagonjwa wakifikia milioni tatu laki tisa huku dunia nzima ikiwa na wagonjwa zaidi ya milioni 105, vifo milioni 2.3 na waliopona ni milioni 58.6

03/02/2021

Utawala wa rais wa Marekani Joe Biden umesema unafikiria kuzuia Trump asipewe taarifa za siri nzito za nchi hiyo ambazo kwa kawaida marais wastaafu huwa wanapewa, msemaji wa ikulu Marekani Jen Psaki amesema kitendo cha Trump kuwashawishi wafuasi wake kuvamia bunge ni miongoni mwa mambo ambayo bado yanawapa wasiwasi kuhusu kumuamini Trump. Sababu nyingine ambazo zinatajwa k**a chanzo cha Trump kutaka kuzuiliwa kupewa siri nzito za serikali ya Marekani ni madai ya kwamba alivujisha taarifa kuhusu ISS kwa warusi na aliwahi kupost kwenye mtandao wa Twitter picha za satellite za kituo cha nyuklia cha Iran ambazo zilikuwa za siri.

31/01/2021

Wabunge nchini Ureno wamepitisha muswada unaohalalisha mgonjwa ambaye ameteseka kwa muda mrefu akiugua, kupewa dawa au kuchomwa sindano itakayomuua kabisa kwa kile kinachoaminika njia nzuri ya kumpunguzia mateso ya dunia. Wabunge 136 wamepitisha muswada huo, huku wabunge 78 wakisema hapana na wanne hawakuwepo bungeni, sasa yamebaki maamuzi ya rais Marcelo Rebelo de Sousa kuusaini muswada na kuufanya uwe sheria rasmi. K**a rais atasaini na muswada kuanza kutumika, Ureno itakuwa nchi ya nne ulaya kuwa na sheria hiyo, nchi za Ubelgiji, Netherlands na Luxembourg tayari sheria hiyo inafanya kazi.

30/01/2021

Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza madaktari waliohama hospitali hiyo ya serikali na kuhamia hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe. "Madaktari wanapata mkopo 100% wakiwa chuoni, halafu tunawapa ajira serikali wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendo" -JPM. "Mtafuteni huyo daktari aliyekimbia hospitali ya serikali na hiyo hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia daktari, tunaifungia na hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawa" -JPM.

07/01/2021

Mdemokrat Jon Ossof amepata ushindi katika duru ya pili ya uchaguzi jimbo la Georgia jumatano, na kuwapa wademokrat udhibiti wa baraza la seneti la Marekani. Mchungaji Raphael Warnock alitangazwa mshindi wa uchaguzi wapili wa seneti katika jimbo la Georgia jumanne jioni. Warnock pia amekuwa ni mdemokrat mweusi wa kwanza kushinda nafasi ya seneti katika jimbo la warepublikan. Kiyang'anyiro kati ya Ossoff na seneta mrepublikan David Perdue ulikuwa na ushindani wa karibu kabla ya kutangazwa kwa siku nzima. Ossoff, msaidizi wa zamani wa bungeni na mtengenezaji wa makala ya televisheni, alijitangazia ushindi mapema jumatano lakini wakati huo kura zilikuwa zimekaribiana kwa yeyote kutangaza ushindi. Ushindi huo unawapa wademokrat udhibiti kamili wa bunge, na kuongeza uwezekano kwa rais mteule Joe Biden na wabunge wademokrat wataweza kwa urahisi kutunga sheria za kuzipitisha kwa mujibu wa ajenda Mdemokrat Jon Ossof amepata ushindi katika duru ya pili ya uchaguzi jimbo la Georgia jumatano, na kuwapa wademokrat udhibiti wa baraza la seneti la Marekani. Mchungaji Raphael Warnock alitangazwa mshindi wa uchaguzi wapili wa seneti katika jimbo la Georgia jumanne jioni. Warnock pia amekuwa ni mdemokrat mweusi wa kwanza kushinda nafasi ya seneti katika jimbo la warepublikan. Kiyang'anyiro kati ya Ossoff na seneta mrepublikan David Perdue ulikuwa na ushindani wa karibu kabla ya kutangazwa kwa siku nzima. Ossoff, msaidizi wa zamani wa bungeni na mtengenezaji wa makala ya televisheni, alijitangazia ushindi mapema jumatano lakini wakati huo kura zilikuwa zimekaribiana kwa yeyote kutangaza ushindi. Ushindi huo unawapa wademokrat udhibiti kamili wa bunge, na kuongeza uwezekano kwa rais mteule Joe Biden na wabunge wademokrat wataweza kwa urahisi kutunga sheria za kuzipitisha kwa mujibu wa ajenda zao.

07/01/2021

Polisi wa jengo la bunge wameamisha, kufungwa kwa jengo lote, wakieleza sababu za kuwepo na kitisho kikubwa, pale maelfu ya waandamanaji wafuasi wa rais Trump, kuvamia jengo hilo jumatano jioni kulalamika dhidi ya utaratibu wa kuidhinisha ushindi wa Joe Biden. Baraza la seneta lililazimika kuahirisha kikao chake wakati kilipokua kinaendelea na utaratibu wa kuidhinishwa kura za wajumbe wa uchaguzi kwa ajili ya Biden. Makamu rais Mike Pence, aliyekua anaongoza kikao hicho aliondolewa mara moja na walinzi wa usalama wa rais kupitia njia ya chini kwa chini za jengo la bunge. Picha za video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya Marekani, zinaonesha wafuasi wa Trump wakivuka kwa nguvu uzio wa polisi nje ya njengo la Bunge kuingia ndani na wengine wakizunguka kwenye uwanja wa jengo hilo. Utaratibu wa kuidhinisha matokeo ya uchaguzi wa rais kawaida ni sherehe inayofanyika ndani ya bunge k**a hatua ya mwisho ya kuidhinisha rasmi matokeo ya wajumbe wa uchaguzi watompatia ushindi BidePolisi wa jengo la bunge wameamisha, kufungwa kwa jengo lote, wakieleza sababu za kuwepo na kitisho kikubwa, pale maelfu ya waandamanaji wafuasi wa rais Trump, kuvamia jengo hilo jumatano jioni kulalamika dhidi ya utaratibu wa kuidhinisha ushindi wa Joe Biden. Baraza la seneta lililazimika kuahirisha kikao chake wakati kilipokua kinaendelea na utaratibu wa kuidhinishwa kura za wajumbe wa uchaguzi kwa ajili ya Biden. Makamu rais Mike Pence, aliyekua anaongoza kikao hicho aliondolewa mara moja na walinzi wa usalama wa rais kupitia njia ya chini kwa chini za jengo la bunge. Picha za video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya Marekani, zinaonesha wafuasi wa Trump wakivuka kwa nguvu uzio wa polisi nje ya njengo la Bunge kuingia ndani na wengine wakizunguka kwenye uwanja wa jengo hilo. Utaratibu wa kuidhinisha matokeo ya uchaguzi wa rais kawaida ni sherehe inayofanyika ndani ya bunge k**a hatua ya mwisho ya kuidhinisha rasmi matokeo ya wajumbe wa uchaguzi watompatia ushindi Biden.

03/01/2021

Papa Francis jumapili amewakosoa watu walio safiri nje ya nchi kwa ajili ya sikukuu na kukiuka amri ya masharti dhidi ya virusi vya corona, akisema walitakiwa kuonyesha uelewa zaidi juu ya taabu wanazopata watu wengine kutokana covid-19. Akiongea baada ya maombi yake ya mchana ya kila wiki, Francis amesema alikuwa amesoma ripoti za magazeti juu ya watu kusafiri kwa ndege ili kukimbia katazo la serikali na kwenda kustarehe sehemu nyingine, shirika la habari la Reuters linaripoti. Wao hawakuwafikiria wale waliokaa majumbani, kutokana na matatizo ya kiuchumi yanayo wakabili watu wengi walioathiriwa na amri ya kutotoka nje, na wagonjwa (walijifikiria wao wenyewe) tu na kwenda mapumzikoni na kufurahi, "Papa alieleza". Hili kwa hakika lilinisikitisha sana, alisema katika hotuba yake iliyorekodiwa katika video kutoka kwenye maktaba ya apostolic palace mjini Vatican. Utamaduni wa maombi ya kuitakia dunia baraka kwa kawaida hufanyika wakati Papa akiwa kwenye roshati mkabala na uwanja wa mtakatifu PetePapa Francis jumapili amewakosoa watu walio safiri nje ya nchi kwa ajili ya sikukuu na kukiuka amri ya masharti dhidi ya virusi vya corona, akisema walitakiwa kuonyesha uelewa zaidi juu ya taabu wanazopata watu wengine kutokana covid-19. Akiongea baada ya maombi yake ya mchana ya kila wiki, Francis amesema alikuwa amesoma ripoti za magazeti juu ya watu kusafiri kwa ndege ili kukimbia katazo la serikali na kwenda kustarehe sehemu nyingine, shirika la habari la Reuters linaripoti. Wao hawakuwafikiria wale waliokaa majumbani, kutokana na matatizo ya kiuchumi yanayo wakabili watu wengi walioathiriwa na amri ya kutotoka nje, na wagonjwa (walijifikiria wao wenyewe) tu na kwenda mapumzikoni na kufurahi, "Papa alieleza". Hili kwa hakika lilinisikitisha sana, alisema katika hotuba yake iliyorekodiwa katika video kutoka kwenye maktaba ya apostolic palace mjini Vatican. Utamaduni wa maombi ya kuitakia dunia baraka kwa kawaida hufanyika wakati Papa akiwa kwenye roshati mkabala na uwanja wa mtakatifu Peter.

01/01/2021

Rais wa jamhuri ya kinemokrasia ya congo Felix Tshisekedi ameomba maseneta waliokaribu naye kuunda kundi la maseneta na wabunge wanaoweza kumsaidia kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri linalotawaliwa na watu wanaomuunga mkono aliyekuwa rais wa nchi hiyo Joseph Kabila. Tshisekedi alivunja mkataba wa kugawana madaraka na kabila mnamo mwezi Desemba. Kabila aliondoka madarakani januari mwaka 2019 baada ya kutawala jamhuri ya kidemokrasia ya congo kwa mda wa miaka 18 lakini watu walio karibu naye bado wanadhibiti bunge. Rais Tshisekedi amesema kwamba mgawanyiko katika muungano wake na kabila umekwamisha juhudi zake za kumaliza mashambulizi ya makundi ya waasi mashariki mwa Congo, kulipo na utajiri mkubwa wa madini, kufanya mabadiliko katika mfumo wa mahak**a, pamoja na kupata ufadhili kutoka shirika la fedha duniani IMF pamoja na benki kuu ya dunia. Tshisekedi amemteua seneta Modeste Bahati kusimamia shughuli ya kuhakikisha kwamba muungano wa seneta wanaomuunga mkono una una wafuasi wenRais wa jamhuri ya kinemokrasia ya congo Felix Tshisekedi ameomba maseneta waliokaribu naye kuunda kundi la maseneta na wabunge wanaoweza kumsaidia kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri linalotawaliwa na watu wanaomuunga mkono aliyekuwa rais wa nchi hiyo Joseph Kabila. Tshisekedi alivunja mkataba wa kugawana madaraka na kabila mnamo mwezi Desemba. Kabila aliondoka madarakani januari mwaka 2019 baada ya kutawala jamhuri ya kidemokrasia ya congo kwa mda wa miaka 18 lakini watu walio karibu naye bado wanadhibiti bunge. Rais Tshisekedi amesema kwamba mgawanyiko katika muungano wake na kabila umekwamisha juhudi zake za kumaliza mashambulizi ya makundi ya waasi mashariki mwa Congo, kulipo na utajiri mkubwa wa madini, kufanya mabadiliko katika mfumo wa mahak**a, pamoja na kupata ufadhili kutoka shirika la fedha duniani IMF pamoja na benki kuu ya dunia. Tshisekedi amemteua seneta Modeste Bahati kusimamia shughuli ya kuhakikisha kwamba muungano wa seneta wanaomuunga mkono una una wafuasi wengi.

31/12/2020

Karibu watu 13 wameuawa katika milipuko miwili inayo ripotiwa kuutikisa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aden, kusini mwa Yemen, jumatono muda mfupi tu baada ya kuwasili ndege iliyokuwa ina wasafirisha wajumbe wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa. Ingawa hakuna kati ya maafisa hao wa serikali waliojeruhiwa lakini ina ripotiwa kuna zaidi ya watu 50 waliojeruhiwa na huenda idadi ya vifo ikaongezeka. Haijafahamika mara moja kilicho sababisha milipuko hiyo lakini milio ya bunduki ya hapa na pale ilisikika karibu na uwanja huo. Serikali ya Yemen inayotambulika kimataifa na wapiganaji wanaotaka kujitenga huko kusini wameunda serikali mpya ya pamoja kushirikiana madaraka hapo disemba 18 na waliwasili katika mji huo wa kusini wa Aden jumatano baada ya kuapishwa nchini Saudi Arabia. Serikali hiyo ya wajumbe 24 iliundwa nchini ya usimamizi wa serikali ya Riyadh ambayo inaongoza muungano wa nchi za kiarabu unaopambana na wathouthi wanaoungwa mkono na Iran wanaoshikilia mji mkuu wa Sanaa tangu 2014Karibu watu 13 wameuawa katika milipuko miwili inayo ripotiwa kuutikisa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aden, kusini mwa Yemen, jumatono muda mfupi tu baada ya kuwasili ndege iliyokuwa ina wasafirisha wajumbe wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa. Ingawa hakuna kati ya maafisa hao wa serikali waliojeruhiwa lakini ina ripotiwa kuna zaidi ya watu 50 waliojeruhiwa na huenda idadi ya vifo ikaongezeka. Haijafahamika mara moja kilicho sababisha milipuko hiyo lakini milio ya bunduki ya hapa na pale ilisikika karibu na uwanja huo. Serikali ya Yemen inayotambulika kimataifa na wapiganaji wanaotaka kujitenga huko kusini wameunda serikali mpya ya pamoja kushirikiana madaraka hapo disemba 18 na waliwasili katika mji huo wa kusini wa Aden jumatano baada ya kuapishwa nchini Saudi Arabia. Serikali hiyo ya wajumbe 24 iliundwa nchini ya usimamizi wa serikali ya Riyadh ambayo inaongoza muungano wa nchi za kiarabu unaopambana na wathouthi wanaoungwa mkono na Iran wanaoshikilia mji mkuu wa Sanaa tangu 2014.

Adresse

Muhungu
Bukavu

Téléphone

+243970863452

Site Web

Notifications

Soyez le premier à savoir et laissez-nous vous envoyer un courriel lorsque Sauti ya dunia publie des nouvelles et des promotions. Votre adresse e-mail ne sera pas utilisée à d'autres fins, et vous pouvez vous désabonner à tout moment.

Contacter L'entreprise

Envoyer un message à Sauti ya dunia:

Partager

Type


Autres Média à Bukavu

Voir Toutes

Tu pourrais aussi aimer