
08/03/2025
"DUNIA"
Hii ni tamthiliya ya kibongo ambayo iko sokoni miezi kadhaa sasa, humu ndani kuna mambo na visa vingi ambavyo vimebebwa na wasanii wenye umahiri. Kati ya kazi bora nyingi nimependezwa nazo kutokea kwenye uzoefu wangu wa kutazama movies na DUNIA iko miongoni mwao.
Kwenye tamthiliya hii nimevutwa mno na kiumbe mmoja anaitwa ALLY MANYANYA.
Humo ndani ni anajua sana huyu broo, namaanisha huyu jamaa ni fundi. Ni mume wa Vailethi na mchepuko wa Matilda.
Je, kuna maajabu gani kwa Manyanya?
Manyanya amebeba haswaaa jukumu la kichwa cha mkewe Vailethi, amekuwa mlinzi, mshauri na mwenye upendo sana kwa mkewe. Ni ile tu sikio la kufa halisikii dawa. Vailethi ni kichwa ngumu hatari.
Manyanya nampenda anavyo ongea, ana hoja sana, pia ana uwezo mkubwa wa kuwasilisha hoja ikaeleweka kwa msikilizaji. Huwezi msikia Manyanya ukaacha kuelewa nia yake uwe umejizima data TU k**a vailethi mkewe😄
Pia kwa uzoefu wangu mdogo tu watu wenye hoja mara chache sana utawaona k**a wana hisia, yaani wao haijalishi unaumia sijui nini wao hawajaligii sanaa. Ila kwa Manyanya ni tofauti kabisa pamoja na kwamba ni smart sana kwenye akili ila linapokuja kwenye suala la kujali bado yumo. Huyu ni people magnet(anavutia watu) nadhani amefanikiwa kumpata Matilda kwa sababu ya huu uwezo wa kushawishi pia hata kwa catherine anavutiwa naye kutokea kwenye huu uwezo.KUPITIA UWEZO WAKE HUO KWA MTU AMBAYE UJIFUNZA KUHUSU KUHUSIANA NA WATU NA UONGOZI KUNA YAKUYAPATA MENGI KUTOKA KWA MANYANYA WA "Dunia"
Mimi ni mtu wa maarifa, ninapenda kujifunza sana. Kuna mambo na uharibifu unaweza ukawa unatokea kwenye ndoa kwa sababu TU hujajua. Hata kiburi(tabia) kinaweza kuwepo kwa sababu hujajua madhara yake, ukijua huwezi kumbatia kiburi ndoani. Kupitia "DUNIA" najua kuna ndoa nyingi ziko zinapona sana Tanzania na nje ya Tanzania.
Nikuombe wewe mwanandoa pia kijana ambae kuna siku utakuja kuingia ndoani ifuatilie tamthiliya hii usaidike.
Bongo movies kuna vitu bora!