#Michuzitv_updates
"Prof. Janabi nimekuteua kuwa mshauri wangu wa masuala ya afya lakini bado nataka utupe jicho lako Muhimbili, na jingine nitatoa siri hapa hapa tumeangalia CV nyingi zilikuwepo zae wenzako kama watano tukaona yako tunaweza kuipeleka kwenye ushindani wa WHO Kwa hiyo tunakuandaa kwenda huko wakati ukifika tutapeleka CV yako na kukuingiza kwenye ushindani jiandae Kwa hilo."- RAIS Samia
Rais Samia ameyazungumza hayo Leo Ikulu ndogo Zanzibar wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni.
#Michuzitv_updatea
Kampeni ya msaada wa kisheria ( Mama Samia Legal Campaign #MSLAC ) inatarajiwa kuendelea kutekelezwa, katika Mikoa minne ya Tanzania.
Kampeni hiyo itafanyika kwa siku 10 mfululizo katika kila Mkoa, ambapo Mkoani Iringa itazinduliwa tarehe 10, Desemba, 2024, Mara tarehe 11 Desemba, 2024, Songwe tarehe 12 Desemba 2024, kisha itaendelea Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ester Msambazi, amesema kuwa lengo kuu la kampeni hiyo ni kuhakikisha kuwa msaada wa kisheria unafika kwa wananchi katika katika kila eneo, na kwamba kampeni hiyo itakuwa endelevu ili kufikia mikoa yote 26 ya Tanzania katika mwaka huu wa fedha 2024/25.
Ester Msambazi ameongeza kuwa kampeni hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha haki za wananchi zinaheshimiwa na kuwawezesha kupata msaada wa kisheria bila kikwazo.
#MSLAC
#Michuzitv_updates
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amewataka wakazi wa Arusha kuhakikisha kuwa mara zote wanamuhusisha Mwenyenzi Mungu kwenye maisha yao ili awanusuru na madhila mbalimbali ikiwemo ajali, vifo vya ghafla na kudumaa katika ustawi.
RC Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Disemba 09, 2024 akiwa kwenye Mnara wa Saa Jijini Arusha wakati wa matembezi ya sala maalum ya kuombea Mkoa wa Arusha yaliyojumuisha viongozi wa Dini zite mkoani Arusha, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania bara.
Katika hatua nyingine ametoa rai kwa wakazi wa Arusha kuwa makini na watu wanaowapa nafasi za Uongozi, kwa kuhakikisha Viongozi wanaowachagua ama kuwateua wanatokana na madhabahu ya Mungu kwa kuzishika amri na maelekezo ya Mungu.
#Michuzitv_updates
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, leo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, kampasi ya Buyu, iliyopo takribani kilomita 13 kusini mwa Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Dkt. Kikwete ameonyesha kuridhishwa na hatua zilizopigwa katika mradi huo wa ujenzi, ambao ni sehemu ya miradi inayofadhiliwa na Mradi wa Elimu ya Juu kwa Maendeleo ya Kiuchumi (HEET) chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, kuoanisha programu za mafunzo na mahitaji ya soko la ajira, pamoja na kuboresha usimamizi wa mfumo wa elimu ya juu nchini Tanzania.
Katika kampasi ya Buyu, ujenzi huo unahusisha vyumba vya mihadhara vyenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 216, maabara zitakazoweza kuhudumia wanafunzi 125, chumba cha mikutano chenye uwezo wa watu 150, pamoja na bweni litakalohifadhi wanafunzi 40.
Kukamilika kwa mradi huo kutaiwezesha Taasisi kuanzisha Diploma ya Utalii wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani, Shahada ya Kwanza ya Uchumi wa Buluu, na pia kuanzisha Kituo cha Umahiri cha Uchumi wa Buluu.
#Michuzitv_updates
Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu, ubunifu, juhudi, maarifa na upendo ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu), Dkt. Khatibu Kazungu wakati akifungua Baraza la Tano la Wafanyakazi wa REA leo tarehe 7 Disemba, 2024 katika ukumbi wa Ledger Plaza, Bahari Beach Hotel jijini Dar es Salaam.
Dkt. Kazungu amewataka watumishi REA kuwahudumia Watanzania kwa maarifa na upendo hususan katika kufikia malengo ya Serikali yanayotarajiwa katika Sekta ya Nishati.
"Niwasisitize wajumbe wa mkutano huu kusikiliza kwa umakini, kufuatilia na kutoa maoni na ushauri utakaokuwa chachu ya kufikia malengo ya Serikali ya kutoa huduma bora ya nishati kwa wananchi," amesisitiza Dkt. Kazungu.
Naye, Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Bw. Heri Mkunda ameipongeza Menejimenti ya REA kwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa wafanyakazi na kusisitiza na kuomba ushirikiano huo uimarishwe ili kuongeza ufanisi na weledi katika kutekeleza majukumu yao.
Awali Mkurugezi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy ameeleza kuwa uhusiano wa Menejimenti na Wafanyakazi umeimarishwa katika nyanja zote na kuahidi kuendelea kuahirikiana na TUGHE ili kuongeza ufanisi wa wafanyakazi katika utendaji kazi.
#Michuzitv_updates
Kamanda wa Jeshi la polisi kanda maaulum ya Dar es Salaam Murilo Jumanne amesema Jeshi hilo linawaonya vikali na halitovumilia watu ambao wanataka kujenga tabia ya kuwashambulia watumishi wa Serikali wakati wakitekeleza majukumu yao kisheria licha ya kuwa wanafuata taratibu za kiutendaji lakini bado kuna tabia inataka kujengeka ya watu kutaka kuwashambulia watumishi wa serikali lwa sababu mbali mbali ambazo hazikubaliki”
"Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar Es Salaam halitasita kuchukua hatua kali za kisheria na za haraka dhidi ya wahusika ikiwa ni pamoja na kuwahoji na kuwakamata na kuwapeleka kwenye mamlaka nyingine za kutenda haki”
Kamanda Murilo ameyazungumza hayo Leo jijini humo wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
// #Imeandaliwa na @janeeeraphael
#michuzitv_updates
Makamu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Prof. Lughano Kusiluka, ameyazungumza hayo wakati asoma hotuba yake katika Mahafali ya 15 ya mwaka huu chuoni hapo yaliyofanyika ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma
#Michuzitv_updates
Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa amekemea utaratibu wa uwekaji wa Vizuizi na vituo vya ukaguzi barabarani bila kuzingazia tahadhari ya usalama kwa watumiaji wengine wa barabara.
Waziri Mkuu amekemea utaratibu unaofanywa na baadhi ya Halmashauri kuweka vizuizi na vituo vya ukaguzi kwa kuziba barabara bila ya kuzingatia matumizi sahihi ya barabara na hivyo kusababisha ajali.
Ameeleza hayo, jijini Arusha wakati akifungua Kongamano la Kimataifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), na kusisitiza kuwa mwenye dhamana kutoa kibali cha kuweka vizuizi na vituo vya ukaguzi ni Jeshi la Polisi.
“Jeshi la Polisi kaeni na Halmashauri, vizuizi vyao barabarani vinasababisha ajali, hakuna sababu ya Halmashauri kuweka kizuizi cha kuzuia magari, mwenye kibali hicho ni Jeshi la Polisi peke yake kwa ajili ya ukaguzi wa usalama”, amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.
#MichuziTvUpdatesSport
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akishiriki UDS Marathon iliyoandaliwa kwa ajili ya kuboresha mazingira ya Wanafunzi chuoni hapo.
Kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya nne na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Jakaya Kikwete, Kulia ni Makamu
Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye, Jijini Dar es Salaam.
#Michuzitv_updates
Jaji Mkuu Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Mustapher Mohamed Siyani ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kujiendeleza kielimu ili kuchangia maendeleo ya taifa kwa kutumia taaluma wanazopata katika vyuo vya elimu.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa Mahafali ya Kumi na Tano ya kutunuku Shahada. Stashada na Astashahada ya Chuo Kikuu cha Dodoma yaliyofanyika Chimwaga Jijini Dodoma.
#Michuzitv_updates
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa awataka wahandisi wote nchini wazingatie miiko na maadili ya taalum hiyo ikiwemo kuitekeleza miradi ya ujenzi kwa ubora unaoendana na thamani ya fedha halisi iliyotolewa.
“Sote tunatambua kwamba wapo wachache katika taaluma yenu ya uhandisi ambao wanaichafua kwa kufanya matendo ambayo ni kinyume na taaluma lakini pia ni kinyume na maadili.”
“Matendo hayo ni pamoja na rushwa, ubadhilifu, na ukosefu wa weledi. Hii si tu kwamba inachafua taaluma ya uhandisi, bali pia inaharibu taswira ya nchi”.
Ameyasena hayo leo (Desemba 06, 2024) kwenye Kongamano la Kimataifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza Bodi ya usajili wa Wahandisi isimamie maadili ya kihandisi na makampuni ya kihandisi kwa mujibu wa sheria ili kulinda hadhi ya uhandisi nchini.
#Michuzitv_updates
Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz, ametoa wito wa kuanzishwa kwa semina mikoani kwa ajili ya kuwaelimisha wafanyabiashara wadogo namna ya kufanya biashara kwa mafanikio, kupata mikopo, na kupanua shughuli zao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika kikao cha “Roundtable” cha wafanyabiashara na wawekezaji wa Kitanzania, Rostam alisisitiza umuhimu wa kutoa elimu ya uzoefu wa kibiashara kwa wafanyabiashara wadogo. Alieleza kuwa hakuna tofauti kubwa kati ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo, akibainisha kuwa yeye mwenyewe alikulia katika mazingira ya kawaida wilayani Nzega, mkoani Tabora, na alianza kuvaa viatu akiwa na umri wa miaka tisa.
“Nimetoka shule ya kijijini. Kama mimi nimeweza, Watanzania wengi wanaweza. Inatakiwa tuwasaidie, maana huwezi kuachia Serikali peke yake. Serikali inatunga sera nzuri, lakini nasi tunapaswa kushiriki kuwaongoza Watanzania wenzetu kufanikisha biashara zao,” alisema.
Aidha, Rostam alihimiza wafanyabiashara wakubwa kuwashirikisha wenzao wa Kitanzania katika fursa mbalimbali za kibiashara na kuhakikisha kuwa wanapata mafunzo ya kujiepusha na kufilisika.
Kauli ya Rostam imeibua mjadala wa umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na Serikali katika kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kukuza uchumi wa nchi.