30/04/2024
Kukata Kucha ni miongoni mwa sunnah za lazima za kimaumbile katika Uislamu.
Na Uislamu umeamrisha sana suala la usafi wa kila aina, hasa usafi wa mwili wa Muislamu.
Kukata Kucha ni moja miongoni mwa mambo yaliyoamrishwa na Mtume Muhammad ﷺ katika hadithi mbalimbali.
Amepokea Imam ibnu Hibbaan; kutoka kwa Abii Huraira (R.A) amesema Mtume ﷺ: “Fitra/Maumbile sahihi ni mambo matano: Kukata kucha, kunyoa Sharubu, kunyoa Nywele za kwapani, kunyoa Nywele za sehemu za siri, na kutahiriwa.”
Na muda wa kukata kucha na kujisafisha maeneo hayo ya ndani ya mwili ni k**a ifuatavyo:
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik (R.A) kuwa: “Alituwekea muda Mtume ﷺ wa kukata Kucha, kunyoa Nywele za sehemu za siri, kunyoa Sharubu, na kunyoa Nywele za kwapani kila siku 40 mara moja.”
Mwanamke huyo ikiwa udhu wake umefika sehemu za lazima kufika maji ya udhu, Swala yake itakuwa ni sahihi, lakini atakuwa amefanya jambo la MAKRUUH.
Na kurefucha Kucha ni kuiga mila za waliokuwa sio waislamu.
Allah Aalam !
Namuomba Allah atujaalie kuifuata Muongozo wa Qur’an na Sunnah !!!
Kufaulu ni katika kufuata muongozo wa Qur’an na Sunnah”