14/12/2023
๐จ ๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐-๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐
M'bungoni United ndio mabingwa wa mchuano wa KENGA WEHU SUPER CUP wadi ya Kambe-Ribe, baada ya kuwarambisha mchanga City Boys goli moja komboa ufe.
Goli la pekee la Abdallah Mdeka lilitosha kwa vijana hao kutia kibindoni kitita cha shilingi 70,000/- pesa taslim.
United pia iliweza kutoa mchezaji Bora pamoja na mfungaji Bora wa mchuano huo ambao ni MWABANZA GEORGE{Dubai} na DICKSON JEWA mtawalia.
Kwa sasa wanawinda kombe la Rabai kwenye mchuano hiyo ya Kenga Wehu Super Cup itakapoingia Sub-County level ambapo watachuana na wana Orlando Fc kwenye awamu ya muondowano{Round of 16} ambao pia wako kwenye fomu nzuri baada ya kuwabwaga vigogo Usintate Fc, Stopper Fc na Red Stars Fc.
Hongera sana team M'bungoni United{Nyuki}
๐ท Cc/