Afisi Ya Habari - Hizb Ut Tahrir Tanzania

  • Home
  • Afisi Ya Habari - Hizb Ut Tahrir Tanzania

Afisi Ya Habari - Hizb Ut Tahrir Tanzania Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Afisi Ya Habari - Hizb Ut Tahrir Tanzania, Media/News Company, .
(1)

17/01/2024
16/01/2024

INNA LILLAH WAINNA ILLAYHI RAAJIUN

Tumepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa ya msiba wa ndugu yetu Ust. Abass Hussein wa Zanzibar kufiliwa na mama yake mdogo bi. Saumu Khamis Said kamili ( ndugu khaliswa na mama yake mzazi)

Kifo kimetokea jana tarehe 15 Jànuari 2024 Zanzibar, na maziko yanafanyika leo asubuhi hii saa 4.00.

Maiti itaswaliwa Msikiti wa Mzambarauni (Kwa Mtipura/Kilimahewa bondeni ) na kwenda kuzikwa Jumbi.

Hizb ut Tahrir Tanzania inatoa mkono wa pole kwa Ustadh Abass na familia yake, ndugu jamaa na wafiwa wote kwa msiba huu mkubwa.

Tunamuomba Allah SWT Awalipe wafiwa ujira mkubwa. Pia Tunamuomba Allah Taala kwa Rehma Zake Amsamehe mama yetu na Amuingize katika Pepo ya darja ya juu ya Firdaus. - Amiin

16/01/2024
13/01/2024

FUNGAMANO LETU WAISLAMU

Masjid: Quddus, Kisiwani Kigamboni
Na. Ust. Mkiongwe Mbwana

JANUARI 1492 MWISHO WA UTAWALA WA KIISLAMU HISPANIAUmma wa Kiislamu unakumbuka tukio la kuangushwa kwa ngome ya mwisho y...
12/01/2024

JANUARI 1492 MWISHO WA UTAWALA WA KIISLAMU HISPANIA

Umma wa Kiislamu unakumbuka tukio la kuangushwa kwa ngome ya mwisho ya dola ya Kiislamu katika ardhi ya Hispania ndani ya mji wa Granada zaidi ya 500 iliyopita. Kuanguka huko kukawa ndio kumalizika kwa kijisehemu cha utawala wa Kiislamu katika ardhi hiyo. Sehemu hiyo ya dola iliyokuwa ikiitwa kwa kiarabu Imarat Gharnāṭah/ utawala wa Granada ilianguka mnamo tarehe 2 Januari 1492 milladiya, baada ya kiongozi wa mwisho wa Grenada Muhammad XII kushindwa na kusalimu amri kwa utawala wa Ufalme wa Kikatoliki wa Ferdinand na Isabella("The Catholic Monarchs/ Los Reyes Católicos).

Uislamu uliingia ndani ya ardhi ya Hispania/Andalusia tangu 711 milladiya zama za Khilafah ya Umawiya pale Jemadari wa Kiislamu Tariq ibn Ziyad alipovuka bahari na kikosi cha askari wake kuingia katika rasi ya Iberia. Kuingia kwake ilikuwa baada ya raia wa eneo hilo ambalo kwa sasa linajulikana k**a Hispania kumuomba Khalifa wa Waislamu wa wakati huo awakomboe kutoka kwenye makucha ya utawala dhalimu waliokuwa wakiishi chini yake wa Mfalme Roderick

Utawala wa Kiislamu katika ardhi ya Hispania ulipeleka nuru kwa watu wote wa Ulaya. Vyuo vya fani mbalimbali vilifunguliwa katika ardhi ya Hispania na kuifanya nchi hiyo kushamiri elimu na ustaarabu kiasi cha kusheheni wageni wengi kwa ajili ya kuja kupata maarifa mbalimbali. Uvumbuzi mbalimbali za kisayansi ulifanyika katika vituo vya kisayansi vilivyokuwepo katika ardhi hiyo.

Hispania ilipata maendeleo makubwa chini ya utawala wa Kiislamu. Pia ilirejesha utulivu na amani kwenye eneo lililozeoeleka kwa mauaji kila kukicha. Aidha, iliondoa husuma sugu ya kimadhehebu baina ya wakiristo iliyokuwa imeota mizizi sio tu katika Hispania bali katika bara lote la Ulaya kwa wakati huo. Bila ya kutaja utawala wa Kiislamu ulivyoleta uadilifu wa kijamii baina ya raia wakiwemo mayahudi waliokuwa wanaishi katika khofu na hali ngumu sana chini ya mateso na dhulma kutoka kwa utawala wa kikatoliki.
Historia ya Uislamu ndani ya ardhi ya Hispania ni muhimu kwa Waislamu kuitambua kwa kina, huku wakijifunga na uwajibu wa kuulingania Uislamu ili siku moja inshaAllah ardhi hiyo irudi tena katika milki ya Waislamu chini ya dola ya Kiislamu ya Khilafah Rashidah

Imeandikwa na Kaema Juma

Risala ya Wiki No. 168
30 Jumada al-Thani 1445 Hijria | 12 Januari 2024 Miladi
Afisi Ya Habari - Hizb Ut Tahrir Tanzania

MINASABA YA MWEZI WA RAJAB1.Hijra ya Uhabeshi.Mtume (SAAW) aliwaruhusu  baadhi ya masahaba kuomba hifadhi ndani ya nchi ...
12/01/2024

MINASABA YA MWEZI WA RAJAB

1.Hijra ya Uhabeshi.
Mtume (SAAW) aliwaruhusu baadhi ya masahaba kuomba hifadhi ndani ya nchi ya Uhabeshi/ Ethiopia kufuatia mateso ya Maqureish. Waliondoka Waislamu 16 wanaume, na wanawake 2. Akiwemo Uthman bin Affan Ra. na mkewe Bi Ruqayah bint Rasullulah SAAW.

2.Kufariki kwa bwana Abuu Twalib
Ami yake Mtume SAAW aliyekuwa ngome iliyokuwa ikimkinga na kumuhami dhidi ya Maqureish alifariki akiwa na umri wa miaka 82 (Tukio hili ama lilitokea katika Rajab au Ramadhan, mwaka wa 10 wa Utume)

3.Safari ya Israi na Miiraj.
Hii ilikuwa ni safari ambayo Allah Taala alimpeleka Mtume wake SAAW kimiujiza baada ya kuondokewa na watu nyeti na kumpa nguvu kufuatia upinzani wa Maqureishi. Pia ilikuwa ni k**a bishara ya ushindi ambapo mara baada ya kurudi alipewa baayah ya kwanza iliyozaa baaya ya pili iliyopelekea kupata nusra.

4.Kutumwa kikosi cha Nakhlah.
Kikosi hiki kilitumwa chini ya uongozi wa Abdallah bin Jahshi Al-Assad na askari 12 wa Muhajiriina kwenda katika mji wa Nakhlah ili kukusanya habari na kuitisha misafara ya Maqureish. Yalitokea mapigano na kuuwawa Amri bin Hadhram. Tukio hili walilitumia Maqureish kueneza propaganda chafu dhidi ya Uislam. Lakini Allah Taala akavunja uvumi wao. Tukio hili ni miongoni mwa sababu za kutokea Vita vya Badr (Mwaka wa 2AH)

5.Kutumwa Kikosi cha Wadil-Quraa
Zaid bin Harithah aliongoza kikosi cha watu 12 kwenda Wadil-Quraa kukusanya taarifa za kijasusi dhidi ya makafiri. Kikosi hicho kikavamiwa na wakaazi wa mji huo, wakauwawa Waislamu 9 na kusalimika 3 akiwemo Zaid mwenyewe. (Mwaka wa 6AH.)

6. Kutumwa kikosi cha Al-Khabt.
Mtume SAAW alituma kikosi cha watu 300 chini ya Abuu Ubeida Al-Jarrah ili kuwadhoofisha Maqureish kiuchumi.(Mwaka wa 8 AH.)

7.Ghazwatu-Tabuuk.
Mtume SAAW alitoka na jeshi la watu 3000 kwenda Tabuuk kupambana na Warumi na vibaraka wao baada ya vita vya Mutah kutofanikiwa vizuri kulipiza kisasi cha balozi wake Al-Harith bin Umair Al-Azd aliyeuliwa na Shurhabil Al-Ghassan. Khofu na hali ya hewa iliwatisha makafiri na kukimbia. Uongozi wa dola ulikabidhiwa kwa muda kwa Muhammad bin Maslamah Al-Answari au Sibai bin Arfata Al-Ghifariy (kwa masimulizi mengine) ( 9 AH.)

8.Vita vya Yarmouk.
Vita hivi vilitokea katika zama za Khilafah ya Umar bin Khattwab.
9. Kufariki dunia kwa Imam Abu Hanifa (R.A), mmoja katika maimamu wakubwa wa madhehebu ya AhluSunnah (15 Rajab 150 Hijria).

10. Kufariki dunia kwa Imam Shafii (R.A) 14 Rajab 204 Hijria

11.Kufariki dunia kwa Imam Muslim (R.A) mwanachuoni mkubwa wa Hadithi 24 Rajab 261 Hijria.

12.Kufariki dunia kwa Imam Nawawi (R.A), mwanachuoni mkubwa wa madhehebu ya Kishafii. 14 Rajab 677 Hijria

13.Ukombozi wa Al-Quds na Sallahudin Ayoub.
Baada ya Msikiti mtukufu wa Baiutil Muqadas kuwa chini ya Makruseda kwa miaka mingi Waislamu waliweza kuukomboa na kuurejesha tena katika mamlaka yao chini ya k**anda Sallahudin Ayoub (Allah Amrehemu) katika Tarehe 27 Rajab.

14.Kuangushwa kwa Khilafah ya mwisho (Khilafah Uthmania)
Serikali ya mwisho ya Kiislamu ya Khilafah Uthmania iliangushwa na makafiri kwa msaada wa vibaraka wa kituruki na kiarabu. Khalifah wa mwisho wa 101 Abdul Majid II alifungiwa virago vyake pamoja na familia yake na kufukuzwa katika makao makuu Istanbul, Uturuki. Na huu ndio ukawa mwisho wa Khilafah (Tarehe 28 Rajab 1342 AH / Tarehe 3 March 1924 AD)

MAPINDUZI BILA YA MFUMO NI NYUMBA BILA YA MSINGI WALA PAALeo ni tarehe 12 Januari ni siku ya kuadhimisha kinachoitwa Map...
12/01/2024

MAPINDUZI BILA YA MFUMO NI NYUMBA BILA YA MSINGI WALA PAA

Leo ni tarehe 12 Januari ni siku ya kuadhimisha kinachoitwa Mapinduzi ya Zzanzibar yaliyofanyika mwaka 1964.

Katika nchi za Kiislamu pamoja na nchi changa kwa jumla huiyangalia dhana ya mapinduzi kwa mtazamo finyu, potofu na wa kughilibu wananchi. Mapinduzi katika nchi hizi huoneshwa kana kwamba yanalingana na matukio makubwa ya mapinduzi yaliyowahi kutokea duniani k**a vile Mapinduzi ya Ufaransa, Mapinduzi ya Marekani, Mapinduzi ya Urusi nk. Ilhali katika nchi changa wanachoshindwa kuelewa au kujisahaulisha makusudi ni kuwa, matukio ya mapinduzi k**a hayo tuliyoyataja na mengineyo yalikuwa ni mapinduzi ya kimfumo yaliyoleta mabadiliko ya kimsingi na sio mapinduzi kwa jina, nembo na kaulimbiu tu bila ya ajenda pana.

Na tunapozungumzia suala la mapinduzi ya kimfumo ni kule mapinduzi kuwa juu ya fikra msingi inayoongoza muelekeo mzima na kuzaliwa kutokana na fikra hiyo masuluhisho mbalimbali kutatuwa matatizo ya dola husika.

Sasa utaona kwamba Mapinduzi ya Ufaransa ya mwaka 1789 na ya Marekani ndani ya mwaka 1765 yalibeba mfumo wa kidemokrasia/kibepari chini ya fikra yao ya kutenganisha dini na maisha/ kisekula kuwa muongozo wao baada ya migongano iliyoibuka baina ya wanafalsafa na wasomi kwa upande mmoja dhidi ya makasisi na watawala mabwanyenye. Amma mapinduzi ya Urusi (Bolshevik Revolution 1917) yalibeba fikra ya kukana uungu kwa kuona kwamba kila kitu ni kutokana na mabadiliko ya mada na hakuna zaidi ya mada.

Hapana shaka fikra zote mbili za mapinduzi tuliyoyataja ni fikra batil zilizozaa mifumo hiyo miwili batil. Yaani ubepari na ukomunisti. Lakini kwa kuwa kwa udhati wake ni mifumo iliweza kuyafanya madola yao kuwa na malengo na ajenda pana katika kuyaendea waliyokusudia japo kwa muda, halafu madola hayo kuanguka. Na hilo ni jambo lenye kutarajiwa kwa kuwa si mifumo ya haki.
Lakini ukweli unabakia kuwa madola hayo yalikuwa huru yanayojitegemea, yalikuwa au yana malengo ya mbali kinyume na nchi zetu zisizokuwa na mfumo zaidi ya kufuata fuata tu.

Katika hali k**a hiyo utaona sasa takriban yote yanayoitwa mapinduzi katika nchi zetu changa kimsingi huwa sio mapinduzi kwa maana ya kupatikana mabadiliko ya kimfumo k**a tulivyotaja sifa za mfumo. Bali huwa amma ni matukio ya mauwaji, dhulma, chuki za kibaguzi kufuatia kuchanganyikiwa raia, au yalikuwa ni mbinu ya kumakinisha zaidi athari za madola makubwa ya kibepari kwa kuwagonganisha vichwa raia wa kundi moja dhidi ya wengine. Na hii ndio hali halisi ya yaliojiri ndani ya Zanzibar ndani ya mwaka 1964.

Ndani ya Afrika Mashariki wakati ule dola ya Uingereza ilikabiliwa na changamoto kadhaa. Kwanza, ilitaka kujizatiti zaidi kwa sura nyengine baada ya kufanya kazi na utawala wa Sultan. Kwa kuwa kufuatia kampeni kali dhidi ya ukoloni mkongwe, dunia ilikuwa haikubali tena dhana ya Usultani. Kwa hivyo, Uingereza ilibidi ibadilishe mbinu kwa kujizatiti kutoa uhuru wa bendera kwa kuweka vibaraka watakaolinda maslahi yake. Kwa bahati mbaya katika muktadha wa Zanzibar vyama vilivyofanikiwa baada ya uchaguzi kunyakuwa uhuru wa bendera wa mwaka 1963, japo kwamba havikuwa vyama vya Kiislamu, lakini Uingereza haikukinai kwamba vitaweza kulinda vyema maslahi yake.

Kwa hivyo, Uingereza haikuwa na namna ila kuleta machafuko kwa jina la mapinduzi ili kumakinisha chama ilichokikinani zaidi cha Afro-Shirazi.

Pili, Uingereza ilibidi ije na mkakati wa yanayoitwa mapinduzi ili isije kuporwa ushawishi wake na dola la Marekani ambalo lilikuwa na shauku kubwa kuzichukuwa ngome zake hususan baada ya Marekani kuuchukuwa uongozi wa kilimwengu mara baada ya Vita vya Pili.

Umma wa Kiislamu una wajibu wa kumuangalia kiongozi wetu Mtume SAAW namna alivyoleta mapinduzi ya kimsingi ya kimfumo kwa kubeba fikra thabiti ya Kiislamu kuwa ndio dira yake. Fikra hiyo ikiwa fikra huru kutoka kwa Muumba ambayo ilizalisha dola huru yenye masuluhisho ya matatizo yote ya mwanadamu.

INNA LILLAH WAINA ILLAH RAJIUNTumepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa ya msiba wa ndugu yetu Ust. Abass Husse...
03/01/2024

INNA LILLAH WAINA ILLAH RAJIUN

Tumepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa ya msiba wa ndugu yetu Ust. Abass Hussein wa Zanzibar kufiliwa na mama watoto wake Ummu Kawthar (aliyekuwa mkewe) ambae kazaa nae watoto kadhaa.

Msiba umetokea jana jijini Dar es Salaam, na mwili wa marehemu tayari umesafirishwa asubuhi ya leo asubuhi tarehe 03 Januari 2024 kuelekea Zanzibar kwa maziko.

Msiba kwa Zanzibar upo Magogoni, nyumbani kwao marehemu (jirani na zahanati ya Huruma (karibu na Msikiti wa Msumbiji), na maiti itaondokea hapo kwenda kuzikwa kijiji cha Hanyegwa Mchana leo leo Jumatano 03 Januari 2024 wakati wa adhuhuri.

Hizb ut Tahrir Tanzania inatoa mkono wa pole kwa Ustadh Abass na familia yake, ndugu jamaa na wafiwa wote kwa msiba huu mkubwa.
Tunamuomba Allah SWT Awalipe wafiwa ujira mkubwa. Pia Tunamuomba Allah Taala kwa Rehma Zake Amsamehe maiti wetu na Amuingize katika Pepo ya darja ya juu ya Firdaus. - Amiin

01/01/2024

MATUKIO YA MWEZI JAMADUL AKHIRI

Na Ust. Msafiri Ndiyembuke

‘UWENDAWAZIMU’ KATIKA SHEREHE ZA MWAKA MPYAوَمَا كَانَ صَلاَتُهُمْ عِنْدَ الْبَيْتِ إِلاَّ مُكَاءً وَتَصْدِيَةً فَذُوقُو...
01/01/2024

‘UWENDAWAZIMU’ KATIKA SHEREHE ZA MWAKA MPYA

وَمَا كَانَ صَلاَتُهُمْ عِنْدَ الْبَيْتِ إِلاَّ مُكَاءً وَتَصْدِيَةً فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ

‘Na haikuwa ibada yao kwenye hiyo nyumba (kaaba) ila ni kupiga miunzi na makofi(kelele). Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyokuwa mkikufuru’ (TMQ 8:35)

Miongoni mwa ibada za Maqureishi katika zama za jahilliya ilikuwa ni kupiga makelele, makofi, kutufu uchi, na kila aina ya uovu katika masiku ya Hijja. Na shetani aliwapambia uovu wao huo kwa kujiona wanatenda wema. Uislamu ukaja ukawakomboa na matendo hayo ya ‘uwendawazimu’ na ukuwapangia ibada inayowafikiana na maumbile yao kukidhi ghariza/hisia ya kuabudu. Aidha, Uislamu uliwakuta na sikukuu na sherehe mbalimbali walizojiwekea, ukaziondoa na kuwawekea sikukuu maalum na namna maalum ya kusherehekea, kwa vipimo vya ‘halali’ na ‘haramu’ na kwa namna ya kuzishukuru neema za Allah Ta’ala mara baada ya kumalizika ibada tukufu ya Hijja na kumalizika saumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Leo chini ya mfumo wa kidemokrasia ‘uwendawazimu’ wa kupiga makelele na kufanya vitendo vya fujo na ufuska katika ‘ibada ya sherehe za mwaka mpya’ vinaendelea kupamba moto kila mahali hususan katika nchi za Magharibi zinazoitwa zimeendelea na kustaarabika, na pia katika nchi zetu changa zinazoburuzwa na thaqafa/mila chafu na potofu za za kimagharibi. Na kwa hakika uovu wa leo ni mkubwa na hatari zaidi kwa ustawi wa wanaadamu hata kuliko ule wa waarabu katika zama za kiza na ujahillia. Uovu huu wa kufanya vitendo vya uwendawazimu ati kwa kusherehekea kuingia mwaka mpya uliosh*tadi zaidi katika mataifa ya Magharibi unatokana na mambo mawili makubwa:

Kwanza, hii ni katika athari ya kuziba uwazi mkubwa (vacuum) uliopo wa hitajio la kiibada ndani ya nafsi za raia wa nchi hizo, ambao wengi wao k**a si wote hawana namna ya kuliziba pengo hilo kutokana na mfumo wao wa kidemokrasia kuwaonesha dini ni kitu duni. Kwa sababu mwanaadamu ana hisia ya ndani ya kimaumbile inayomsukuma kuhitajia ibada fulani kwa ajili ya kumtukuza Muumba wake (ghariza ya kuabudu). Kwa hivyo, anapokosa mwanaadamu ibada sahihi kukidhi kiu yake hiyo ya kimaumbile, hujibunia ibada yake mwenyewe au hubuniwa na wengine ili kukidhi kiu yake hiyo ya kimaumbile. Ukiangalia kwa makini, namna ya sherehe hizi zinavyofanywa katika nchi za Magharibi, kimsingi japo kwamba kidhahiri utaona ni sherehe lakini kwa umbali wake zimefanywa kuwa ‘ibada ya kuingia mwaka mpya’. Aidha, ukiangalia namna watu wa magharibi wanavyowatukuza, kuwaenzi na kuwanyenyekea watu wao maarufu (celebrities) k**a wanamuziki, wacheza filamu, wacheza mpira nk. Unyenyekevu ambao huwezi kuamini kwa mwanaadamu kudiriki kumfanyia mwanaadamu mwenzake anaekula, kwenda haja, kuumwa na hatimae kufariki. Lakini kwa umbali, jambo hili huwa ni kutokana na msukumo wa ghariza hii ya ibada. Kwa kuwa asili Mwenye haki ya kutukuzwa, kunyenyekewa na kuenziwa katika kiwango hicho ni Muumba pekee. Na kwa kuwa watu hawa wamekwenda kombo na njia ya haki, na kuikosa ibada sahihi, ilhali ghariza ya ibada kimaumbile inatokota nafsini mwao, hapana shaka ghariza hiyo hutafuta njia ya kutokea. Na badala yake watu hawa badala ya kumnyenyekea Muumba wa haki, humalizikia kunyenyekea, kutukuza, kuwaenzi watu maarufu (celebrities). Kiasi cha kutokea matukio ya ajabu! k**a vile mashabiki (wafanya ibada) kuwahi kukesha nje ya vipenu vya hoteli aliyofikia Michel Jackson alipofanya ziara ndani ya jiji la London, huku maskini! mashabiki (wafanya ibada)wakiandamwa na baridi kali isiyomithilika.

Pili ni msukumo wa fikra zao potofu za kikafiri za ‘uhuru binafsi’ (personal freedom) zinazotok**ana na nidhamu yao ya kikafiri ya kidemokrasia. Kwa kuingia mwaka mpya wao huona ni muda muwafaka wa kufanya kila aina ya uchafu k**a kulewa, kuzini, kufanya liwati, kufanya vitendo vya usagaji, kupiga makelele kwa honi za magari inapoingia saa sita na dakika moja usiku, makelele ya magoma, mikusanyiko ya mchanganyiko ya wanawake na wanaume, kwenda utupu wa mnyama nk. Yote hayo kwa kisingizio cha kuutumia ‘uhuru wao’ wa kibinafsi kwa kusherehekea usiku wa kuingia mwaka mpya. Kwa bahati mbaya na hata baadhi ya Waislamu kimakosa hujiingiza katika aina hii ya ujahilia katika kusherehekea kuingia mwaka mpya wa kalenda ya miladia na kujiingiza katika vitendo vichafu vya haramu. Tunawanasihi kwa ikhlasi waache mara moja.

Kalenda ya miladia iliasisiwa tangu zama za utawala wa Himaya ya waroma chini ya mtawala Julius Caesar miaka ya 150 BC. Na katika mwaka 1582, Pope Gregory xiii aliimakinisha zaidi kalenda hiyo na kuitia sura rasmi, na ndio maana baadhi wameipa jina kalenda hii kwamba ni ‘kalenda ya Gregory’ (Gregorian calendar) Zama zote hizo sherehe mbalimbali zilikuwa zikifanywa kuukaribisha mwaka mpya, zilizoambatana na vionjo vya kidini na mila za kipagani. Na ubepari/uarasilmali ulipopata nguvu ndani ya Ulaya na Marekani waliendelea kuitumia kalenda hiyo na pia kuendelea kufanya sherehe maalum za kuingia mwaka mpya. Hata hivyo, sherehe hizi za mwaka mpya zilianza kupata nguvu zaidi katika karne ya 19 wakati raia wa Marekani walipokuwa wakikusanyika kusherehekea katika viwanja vya miji mikuu k**a New York, Philadelphia, Baltimore nk. Na mtindo huo kuanza kuenea katika miji mikuu mbali mbali ndani ya Ulaya na nje ya Ulaya.

Kwa hivyo, imekuwa ni ada ya wanademokrasia kutokana na fikra zao chafu kufanya kila aina ya ufuska katika kusherehekea kuingia mwaka mpya. Na uchafu huo hutendwa mbele ya macho ya serikali zao, na raia wao kukusanyika katika viwanja vikubwa kwa ajili ya sherehe hizo. Serikali zao huwaachia huru, kwa kuwa kwanza hunufaika kiuchumi, kwa kuwa siku hii imekuzwa sana k**a ni siku tukufu kiasi cha kufanywa ni siku ya mapumziko (public holiday) katika nchi nyingi. Na raia wao hujiingiza gharama zisizokuwa za lazima kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya. Lakini pia serikali zao zinaifanya sherehe hii miongoni mwa mbinu ya kuwapumbaza raia wao ili wapunguze joto la kubanwa na mfumo wao muovu wa kibepari. Na kubwa zaidi, wanademokrasia hudai kwamba kazi ya serikali za kidemokrasia ni kulinda na kudhamini uhuru wa mtu binafsi.

Uislamu umekuja kumuwekea mwanaadamu ibada maalum ili kukidhi na kukinaisha hisia zake za kimaumbile. Aidha, umeweka sherehe maalum zinazoambatana na vipimo vya ‘halali’ na ‘haramu’ katika kusherehekea sherehe hizo. Kamwe Uislamu hauwaachii wanaadamu kuwa k**a wanyama mbugani kufanya wanayotaka kwa kisingizio cha ‘uhuru’. Fikra chafu zinazomuangamiza binaadamu leo. Kadhalika Uislamu ukaichukulia neema ya umri/wakati miongoni mwa neema kubwa ambayo kamwe si ya kubezwa wala kutumiwa kwa vitendo vya fujo na ufuska. Bali unamtaka mwanaadamu kujifunga katika umri wake wote kumcha Allah Ta’ala. Mtume SAAW alimuusia sahaba Abudhar al- Ghifari na umma mzima kwa kusema:

“Ewe Abu dhar ,nufaika na vinne kabla ya vinne: ujana wako kabla ya uzee wako, na siha yako kabla ya maradhi yako, na wasaa wako kabla ya ufukara wako, na uhai wako kabla ya mauti yako.”

SHEREHE ZA ‘MWAKA MPYA’ MBINU YA KUSAHAULISHA MALENGO YA UMRIMwaka 325 AD Kanisa Katoliki lilifanya Mkutano Mkuu wa Kwan...
01/01/2024

SHEREHE ZA ‘MWAKA MPYA’ MBINU YA KUSAHAULISHA MALENGO YA UMRI

Mwaka 325 AD Kanisa Katoliki lilifanya Mkutano Mkuu wa Kwanza huko Nicea. Mkutano huu uliitishwa na Mfalme Constantine (mpagani) ili kutuliza hali ya machafuko iliyosababishwa na wakristo waliokuwa wakipinga falsafa ya uungu iliyoasisiwa mwanzoni na Justin Martx, (Yusto). Huu pia ndio mkutano ulioanzisha misingi ya aqeeda ya ukristo wa leo iliyohusisha ‘utatu mtakatifu’, ‘dhambi ya asili’, kufufuka kwa Yesu nk.

Aidha, Baraza hilo la Nicea ndio lililoweka msingi wa kalenda iliyokuja kuitwa Kalenda ya Greogarian kwa kulazimisha wakiristo wote washerehekee Pasaka siku moja. Misimamo ya Baraza la Nicea ulipingwa vikali na baadhi ya wakristo ikabidi kanisa kuomba msaada kwa serikali (ya kipagani) isaidie kurejesha amani na utulivu. Katika upinzani huu waliteswa maelfu k**a si malaki ya wakristo na wengi kuuwawa. Mabaki ya vifaa vya kutesea bado vinapatikana katika jumba la makumbusho huko Rhine, Ujerumani.

Kuanzishwa kwa kalenda ya Miladi ya Papa Gregory XIII lilikuwa ni jaribio la kufanya marekebisho kalenda ya Julian (iliyoanza mwaka 45BC) iliyokuwa ikitumiwa awali. Papa Gregory alisimamia mabadiliko haya, na rasmi katika tarehe 24 Februari 1582 akasaini waraka maalumu unaojulikana kwa jina la “Papal bull’ ili kuimakinisha kalenda hii : http://en.wikipedia.org/wiki/Gregorian_calendar.

Wakatoliki waliikubali kalenda hii kwa kuwa waliamini kwamba dhamira ya Mkutano wa Baraza la Nicea ulioanzisha muundo mpya wa siku ya Pasaka ilikuwa pia kuanzisha kalenda mpya. Japo kwamba lengo la Mkutano lilikuwa ni kupata tarehe maalumu ya kusherehekea Pasaka kwa Wakristo wote kwa pamoja. Kabla ya hapo Pasaka ilikuwa ikisherehekewa mwezi wa habib (unavyojulikana katika Bibilia) uliokuwa ukiisabiwa kwa kalenda ya mwezi. Lakini kwa kuwa muandamo wa mwezi hubadilika badilika ndipo Kanisa Katoliki likafanya mabadiliko makubwa ndani ya mwaka 325. Mabadiliko ambayo yalitoa viashiria vya kubadilisha muundo mzima wa kalenda ambao baadae ulikuja kumakinishwa na Papa Greogry wa kumi na tatu.

Hata hivyo, baadhi ya makanisa yasiyokubaliana na upapa wa Kikatoliki yalikataa kalenda hii. Miongoni mwao ni Waporestanti na Kanisa la Orthodox. Mataifa mengine yalianza kuikubali kalenda hii kidogo kidogo, hata Khilafah Uthmaniya ilikubali kuitumia kalenda hii katika miaka ya 1890 wakati wa zama zake za uzorotefu, na kuibakisha kalenda ya Hijiria katika mambo ya kiroho na ibadat tu. K**a vile katika hesabu ya Ramadhani na Hijja.

Hii ni baada ya kudorora kwa kiasi kikubwa kwa dola ya Kiislamu, kiasi cha baadhi ya Waislamu hususan wasomi walioathiriwa na fikra za kimagharibi k**a vile mhasibu Morali Othman (Msomi wa Kiislamu aliyeathiriwa na umagharibi) kupendekeza kutupilia mbali kalenda ya Hijiria kwa kudai ina usumbufu katika masuala ya hesabu za kifedha.

Suala la kalenda au kuhesabu siku ni jambo tu la kumuwezesha mwanaadamu kuweka kumbukumbu na malengo yake ya kiutendaji na haliingii katika masuala la kiutawala. Ndio maana, japo kuwa kalenda hii asili ni ya Kanisa katoliki, lakini inafuatwa/adopted na sehemu kubwa ya dunia k**a si yote. Pamoja na ukweli kwamba si Ukatoliki unaotawala dunia leo. Na badala yake dunia inatawaliwa na mfumo wa kibepari/kidemokrasia. Kwa kuwa ukristo kamwe sio mfumo wa kimaisha wenye sifa na uwezo wa kumtawalia mwanaadamu na wala hauna masuluhisho ya mambo ya kimaisha. Bali ni kijidini kinachojumuisha baadhi ya fikra za masuala ya kiroho tu.

Mfumo wa kibepari unazitumia sherehe za mwaka mpya kukuza na kuimarisha fikra zake za ‘uhuru’ kwa kiasi kikubwa na masoko ya kibiashara. Huhamasisha kusherehekea kwa namna tofauti k**a kulewa, kuzini, kucheza miziki, k**ari, kuleta vurugu nk. Aidha, wanaipotosha na kuidogosha hazina muhimu na yenye thamani ya umri wa mwanaadamu na kupongezana kwa kumaliza mwaka salama usalimini bila ya kuwaonesha watu dira na malengo ya umri huo.

Uislamu ni kinyume na Ubepari/Udemokrasia ambao huwafanya watu kutokujua lengo la kuwepo duniani. Wao huona kila kitu kinaishia hapahapa na hakuna hisabu ya matendo kwa Muumba. Na ndio maana itikadi ya Ubepari/Udemokrasia wao huona kwamba k**a Muumba yupo basi baada ya kuumba na kumpa mtu akili amemuachia ajipangie mfumo wake anaoutaka maishani kwa faida na hasara ya mwanaadamu mwenyewe. Wala Muumba hana tena nafasi ya kumhisabu mtu huyu. Aidha, Uislamu kamwe haudandii sherehe zisizokuwa za Kiislamu kwa kuwa tayari una sherehe zake zilizowekwa na sheria.

Badala yake Uislamu umeweka wazi lengo la mwanaadamu katika maisha haya kwamba ni kumtumikia Muumba. Na kila dakika mtu ajihesabu kabla ya kuhesabiwa, sio kwa faida ya kimada bali katika kushik**ana na maamrisho ya Muumba. Tathmini hiyo sio baada ya kumalizika mwaka. Bali ni kila dakika na kila siku. Yaani Muislamu ajihesabu kabla ya kuhesabiwa.

Waislamu lazima tukumbuke katika umri huu tuna jukumu la kuongoza ulimwengu:

وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا

‘Na vivo hivyo tumekufanyeni muwe Umma bora, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu……’’ (TMQ 2:143)

Kwa bahati mbaya leo tunaishi chini ya mfumo wa kikafiri wa kibepari ulimwenguni kote, licha ya kuwa ni faradhi kwetu kuishi chini ya dola ya Kiislamu ya Khilafah, na ni dhambi kubwa kuishi zaidi ya siku tatu nje ya dola hiyo.

Leo kwa kalenda ya miladia ni miaka 100 tangu iangushwe Khilafah, tukiwa bado chini ya utwaghuti wa kirasilimali na demokrasia ilhali baadhi hata hawajatanabahi wala kuamka. Kila siku inayopita inachukua sehemu ya umri wetu, tunasonga hatua mbele kuelekea mauti na kuhisabiwa na Allah Taala na hatua moja nyuma ya muda wa kutekeleza majukumu tuliyofaradhishiwa na Allah SW.

Basi jee wakati haujafika wa sisi Waislamu kuamka na kujizatiti katika majukumu yetu?

Hamza S. Sheshe

Risala ya Wiki No. 168
18 Jumada al-Thani 1445 Hijria | 31 Disemba 2023 Miladi
Afisi Ya Habari - Hizb Ut Tahrir Tanzania

BAADHI YA MINASABA NDANI YA JANUARI1 /01- Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Miladi1/01 1801 – Kuasisiwa rasmi Muungano baina ...
01/01/2024

BAADHI YA MINASABA NDANI YA JANUARI

1 /01- Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Miladi
1/01 1801 – Kuasisiwa rasmi Muungano baina ya Ufalme wa Uingereza na Ireland.
1/01 1999 - Kuasisiwa rasmi kwa sarafu ya Euro. Awali ilianza na nchi 11 wanachama wa nchi za Jumuiya ya Ulaya.
1/01 1956 – Uingereza yaitenga Sudan kutoka Misri kwa kishingizio cha ati kuipatia uhuru wake.
2/01 1492 - Kuangamizwa ngome ya mwisho ya utawala wa Waislamu wa Andalucia/Spain ndani ya Visiwa vya Grenada (Reconquista of the Emirate of Granada).
2 /01 1642 – Kuzaliwa kwa Khalifah wa Kiuthmani Mehmed IV. Alifariki mnamo mwaka 1693.
2/01 au 3/01 1699 – Kuzaliwa kwa Khalifah Osman III. Alitawala kuanzia mwaka 1754 mpaka alipofariki mwaka 1757.
4/01 2010 - Ufunguzi rasmi wa Ghorofa ya ‘Burj Khalifa’ nchini Dubai. Hii ndio ghorofa ndefu duniani. Ujenzi wake ulianza mnamo Januari 2004 na kumalizika Oktoba 2009.
6/01 1993 – Majeshi ya mipakani ya India yauwa Waislamu 55 wa Kashmiri katika miji ya Sapore na Jammu Kashmir.
8/01 1867 – Wamarekani wenye asili ya kiafrika kwa mara ya kwanza wapata haki ya kupiga kura ndani ya mji wa Washington, D.C.
12/01 1964- Mauwaji ya halaiki ya Waislamu Zanzibar kwa jina la Mapinduzi. Mauwaji hayo yaliambatana na vitendo vya ubakaji, mateso na kupora mali za raia na kuchochea fikra za kibaguzi.
19/01/820 Kufariki dunia Imam Abdillah Muhammad ibn Idriss Al- Shafii, mmoja katika mujtahid wakubwa na gwiji la Usul, pia ni imamu wa moja ya madhehebu ya Sunni.
27/01 Siku ya Umoja wa Mataifa ya Kumbukumbu kwa kinachoitwa Mauaji ya Halaiki kwa Mayahudi yaliyotendwa na Manazi.
(International Holocaust Remembrance Day). Siku hiyo iliteuliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa chini ya Azimio No. 60/7 Mnamo Novemba 2005.

MATUKIO YA TARIIKH NDANI YA JUMADA AL-THANIY1. Mtume SAAW kuanza kulelewa na kunyonyeshwa na Bi. Halima Al-Saadiya2. Dor...
29/12/2023

MATUKIO YA TARIIKH NDANI YA JUMADA AL-THANIY

1. Mtume SAAW kuanza kulelewa na kunyonyeshwa na Bi. Halima Al-Saadiya
2. Doria ya Zaid bin Harithah
Kikosi hiki cha askari 100 kilitumwa kuwadhoofisha makureish na kuandaa mazingira ya vita. Kilifanikiwa sana kuwatia hasara makureish na kuchangia kutokea vita vya Uhud (3AH Hijri)

3.Kutumwa kwa Kikosi eneo la A-taraf
Kikosi hiki kilitumwa ama A-taraf au Al- twaraq kikiwa chini wa uongozi wa Zaid bin Harithah na askari 15 kupambana na Bani Tha’alabah ambao walikimbia, waislamu wakapata ngawira ya ngamia 20 waliowawacha.(Mwaka wa 6AH)

4. Kutoka kwa msafara wa Waislamu kuelekea katika Vita dhidi ya mayahudi wa Khaybar 7 Hijria

5. Kutumwa kwa kikosi cha Dhatu-Salasili
Kikosi cha askari 300 chini ya Amr ibn Al-Ass kilitumwa kupambana na makabila ya kiarabu mashariki ya Shaam kwa kuwaunga mkono kwao Warumi dhidi ya waislamu katika vita vya Mutah. Askari 200 waliongezwa nguvu akiwemo Umar na Abu Bakar chini ya uongozi wa Abu Ubaida ibn Jarrah. (Mwaka wa 8AH)

6. Kutumwa kikosi cha kupambana na majambazi
Kikosi hiki chini ya sahaba Alqama bin Majaziz Al Mudlaj kikiwa na askari 300 kwenda kupambana na majambazi katika mwambao wa Jeddah (Mwaka wa 9AH)

7. Kifo cha bi. Fatma bint wa Mtume SAAW - 03 Jumada al-Thaniyah, 11 Hijria

8. Kifo cha Khalifah wa mwanzo Saydna Abubakar ra. - 22 Jumada al-Thaniyah, 13 Hijria

9. Ushindi wa Khalifa wanne Imam Ali bin Abu Twalib katika mapigano ya Bassora, Vita vya Jamal - 10 Jumada al-Thaniyah.

10. Kifo cha Khalifah wa 5 wa Abassiya, Haroun Rashid - 03 Jumada al-Thaniyah 193 Hijri

11. Jemadari Salahudiin Ayoub kuwa Amiri wa Misri - 25 Jumada al-Thaniyah 564 Hijria

KUINGIA MWAKA MPYA TUKIO LISILOZINGATIWA IPASAVYOAllah Taala kwa Rehma Zake licha ya kuleta Mitume As. kuwaongoza wanada...
29/12/2023

KUINGIA MWAKA MPYA TUKIO LISILOZINGATIWA IPASAVYO

Allah Taala kwa Rehma Zake licha ya kuleta Mitume As. kuwaongoza wanadamu namna ya kumuabudu Mola wao na kuwapa sharia Zake kusimamia maisha yao, pia akawabakishia ndani ya maumbile ya nafsi zao hisia ya utambuzi wa kimaumbile ambao lau watatanabahi huwawezesha kujua uwepo kwa Muumba huyo.

Utambuzi huo ndio huitwa fitra. Maana ya fitra ni ile hisia ya utambuzi wa ndani isiyopingika kwenye nafsi ya kila mwanadamu kuhisi kusiko na shaka kuwepo anayemtenza nguvu mwanadamu bila ya ridhaa yake. Mwenye nguvu huyo hutenda ayatakayo kwa mwanadamu bila ya mwanadamu kuweza kudhibiti maaumuzi hayo. Huyo ndio Mola, Muumba wa mwanadamu na kila kilichomzunguka. Hisia hii ya kuwepo Muumba anayo kila mwanadamu akipenda asipende, kilichobakia ni kwa mwanadamu kukiri hadharani utambuzi huo na kujisalimisha, au kujisahaulisha mpaka arudi kwa Mola wake na kustahiki adhabu.

Ukiangalia kwa makini maisha yote ya mwanadamu tangu kuzaliwa kwake, kuishi kwake duniani na kumalizika umri wake kwa kufariki ni miongoni mwa mambo ambayo kwa kila mwenye fikra iliyosalimika bila ya chuki, taasub wala kasumba humpelekea kwenye utambuzi wa kuwepo Mola wake, yaani fitra.

Mwanadamu hakujua lini atakuja duniani. Aidha, hajui ataondoka lini. Pia kuondoka kwa walioondoka kabla si kutokana na uzembe. Kwa sababu k**a sababu ya kufariki kwa waliotangulia ni uzembe, wapo wazembe wengi ambao bado wanaendelea kuishi. Na lau k**a sababu ya wanaoishi duniani leo ni kwa kuwa mahodari, wajanja au kuwa na afya njema, basi walikuwepo mahodari wengi, wajanja na waliokuwa na afya njema lakini leo hawapo wameshafariki.

Hili kwa ufupi ni dhihirisho la kuwa mwanadamu hana khiyari katika kuwa na umri mrefu au mfupi, na wala hana athari katika kuendelea kuishi katika maisha haya au kufariki.

Kwa msingi huo, kuingia kwa mwaka mpya, uwe wa kalenda ya Kiislamu au nyengineyo yoyote kinachodhihirika ni kusonga mbele kwa umri wa mwanadamu, kuongezeka maisha yake na pia kurefuka muda wa waliotutangulia makaburini.
Jambo hilo kamwe mwanadamu hawezi kabisa kuliingilia wala kujipangia kwa namna yoyote. Kwa hivyo, kwa kuingia mwaka mpya na kwa kuwa mwanadamu hawezi kuliingilia suala hilo, ilitarajiwa mwanadamu atanabahi kwa utambuzi wa kuwepo Muumba wake na kujinyenyekeza kwake na sio kufanya vitendo vya fujo, vurumai na ufuska kwa kisingizio cha ati sherehe za mwaka mpya.

Katika mfumo wa kidemokrasia jambo la kufanya vurugu kwa kuingia mwaka mpya ni lenye kutarajiwa. Kwa kuwa ni mfumo wa fujo na ujanja wa kukimbilia kwenye matawi/mitagaa badala ya chanzo.

Ilikuwa mfumo huu umuoneshe mwanadamu ikiwa umri wake umeongezeka, jee amechangia chochote katika kuongezeka huko? Na kwa kuwa hana mchango katika hilo hana budi amkiri Muumba ambae ndie Mpangaji wa hayo na mengineyo. Na kilichobakia ni kumnyenyekea yeye peke yake. Hii ndilo suala la msingi ambalo hupaswa kulikabili kila makini na mwenye fikra angafu.

Masoud Msellem

Risala ya Wiki No. 167
15 Jumada al-thani 1445 Hijria | 28 Disemba 2023 Miladi
Afisi Ya Habari - Hizb Ut Tahrir Tanzania

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afisi Ya Habari - Hizb Ut Tahrir Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Videos
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share