21/03/2017
"Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala siyo mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho;. ( yeremia 29:11). Mungu anao mpango kwa ajili ya maisha yako; mustakabali ambao aliutengeneza kwa ajili yako ili uutimize. Baadhi ya watu hawalijui hili na matokeo yake wanaishi maisha matupu yasiyo kuwa na maana. Baadhi ya wengine hawaamini kwamba mungu anaweza kuwa na mpango kwa ajili yao; lakini kwanini asiwe nao? Yeye ndiye aliyekuumba! Tafuta kujua mpango wake kwa ajili yako na kisha tembea katika nuru ya mpango wake kwako. Roho wa mungu yu ndani yako, ili kukujenga, kukuimarisha na kukuongoza katika njia za hatma yako ya kiungu.