Wadau wa Uchaguzi kutoka Taasisi mbalimbali na makundi ya kijamii mkoani Mbeya wametakiwa kushirikiana na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kuhakikisha zoezi la kuboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura linafanikiwa.
Wito huu ulitolewa na Jaji (R) Jacobs C.M. Mwambegele alipozungumza na wadau katika mkutano uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jiji la Mbeya.
Jaji Mwambegele alisisitiza umuhimu wa kutoa elimu sahihi kwa wananchi kuhusu mchakato wa kujiandikisha na kuboresha taarifa zao ili kuimarisha Daftari la Kudumu la Wapigakura.
Aidha, Jaji Mwambegele alikemea vitendo vya udanganyifu, akiwataka wananchi kuepuka kujiandikisha mara mbili, kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kunaweza kuathiri usahihi wa zoezi hilo. Alisisitiza kuwa, ili zoezi hili liwe na ufanisi, ni muhimu kwamba wadau, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, mashirika ya kijamii, na taasisi za serikali na zisizo za kiserikali, wahamasishe umma kuhusu umuhimu wa kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwa wakati.
Mwisho, Jaji Mwambegele aliwahimiza wadau wote kutoa ushirikiano wa karibu na Tume ya Uchaguzi ili kuhakikisha kila raia mwenye haki ya kupiga kura anajiandikisha na kuboresha taarifa zake kwa wakati.
Alieleza kuwa utekelezaji wa zoezi hili kwa ufanisi utahakikisha usalama, uwazi, na haki katika uchaguzi, na kuweka misingi imara ya uchaguzi wa kidemokrasia.
#knews24updates
#tunakutoakichakani
MANGI SHANGALI AHAIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI
Na Linda Akyoo -Hai
Jumla ya Koo 52 kutoka kabila la Wachaga wa Machame wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro,wamempokea kiongozi wao mpya Mangi Gilbert Gileard Shangali aliye simikwa rasmi kuongoza kabila hilo.
Akizungumza mara baada ya kusimikwa na Mangi Marialle Mangi huyo wa Machame amesema kuwa katika utawala wake atashirikiana na serikali ili kusimamia haki zote na kupinga vitendo vya ukatili ili kuchochea maendeleo.
Mangi huyo anatarajiwa kuwa na kazi kubwa ya ya kupambana na mmomonyoko wa maadili pamoja na kusaidia kuweka mkazo katika kudumisha amani na kuondoa migogoro ndani ya jamii.
#knews24updates
#Tunakutoakicha
@tulia.ackson
@tuliatrust_org
TRA KUYAKABILI MAGENDO KWA BOTI YA DORIA
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Mwenda amesema wamejipanga kudhibiti magendo kwa kutumia Boti ya Doria iliyozinduliwa Ziwa Victoria.
Akizungumza jijini Mwanza baada ya uzinduzi wa Boti ya Doria ya TRA, Bw. Mwenda amesema Magendo yanayofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu yamekuwa yakichangia kuharibu Uchumi wa Nchi, kuhujumu Biashara za wengine, kuchochea uhalifu na kuharibu usalama wa Nchi, hivyo Boti ya Doria iliyozinduliwa itakomesha vitendo hivyo.
Amesema kuwa Boti ya Doria iliyozinduliwa itaokoa mapato yaliyokuwa yanapotea kutokana na ukwepaji kodi kupitia bidhaa za magendo.
"Miongoni mwa magendo makubwa yanayoingi kupitia Ziwa Victoria ni vipodozi ambavyo mbali na kukwepa kodi vimekuwa vikiharibu afya za wananchi na kazi yetu siyo tu kudhibiti tu mapato, pia tunaangalia afya za watanzania" Amesema Mwenda.
Kamishna Mkuu Mwenda amesema walipakodi wa Tanzania wanataka kuwepo na usawa katika kodi hivyo kuzinduliwa kwa Boti hiyo kunatekeleza matakwa ya wananchi maana kwa kuzuia magendo kutakuwa na usawa wa biashara kwa kila mtu kulipa kodi.
"Usawa wa biashara unakosekana maana unakuta mtu aliyeingiza bidhaa za magendo anaziuza kwa bei ya chini kuliko wenzake maana hajazilipia kodi, sasa tutahakikisha wote wanalipa kodi" Bw. Mwenda
Kamishna Mkuu Mwenda amesema Magendo yanayofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu yamekuwa yakichangia kuharibu Uchumi wa Nchi, kuhujumu Biashara za wengine, kuchochea uhalifu na kuharibu usalama wa Nchi, hivyo Boti ya Doria iliyozinduliwa leo mkoani Mwanza itakomesha vitendo hivyo.
Ameeleza kuwa TRA itatoa motisha kwa mwananchi yeyote atakayefichua watu wanaojihusisha na magendo au wanaokwepa kodi na kuwa suala la kotisha lipo kisheria.
#knews24updates
#tunakutoakichakani
#knews24updates
#tunakutoakichakani
MFUMO WA TEHAMA KUTUMIKA KUDHIBITI MAGENDO MIPAKANI
Akiwa kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia uliopo Tunduma Mkoani Songwe Dkt Ashura, amesema bidhaa zinazopotishwa kwa njia zisizo rasmi nizile ambazo hazijakidhi vigezo vya kutumika hapa nchini, zikiwemo za vipodozi vyenye viambata vya sumu ambavyo hupelekea madhara kwa watumiaji wakati wengine ni wale wanaokwepa kulipa Kodi pale wanapo pitisha kwenye njia rasmi za mipaka ya Tanzania na Nchi mbalimbali.
Nae Mkurugenzi mkuu wa shirika la viwango Tanzania TBS Dkt Ashura Katunzi, amesema kutokana na changamoto kubwa ya kupitisha bidhaa kweye njia zisizo rasmi za mipaka mbalimbali hapa Nchini, shirika limeweka mikakati ya kukabiliana na shida hiyo kwa njia ya TEHAMA kwa kutoa utambulisho wa bidhaa zinazo ingizwa hapa Nchini nazile zinazozalishwa ndani ya Nchi.
#knews24updates
#tunakutoakichakani
#knews24updates
#tunakutoakichakani
Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha katika kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mkoani humo wametoa mitaji kwa warahibu wa dawa za kulevya ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru.
Akiongea wakati wa kukabidhi mitaji hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa huo, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Georgina Matagi amebainisha kuwa baada ya serikali kutoa huduma ya tiba kwa warahibu hao, wameona ni vyema kuunga juhudi hizo kwa kutoa mitaji ya biashara ili iweze kuwaingizia kipato, kuwakwamua kiuchumi na pia kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.
Aidha SSP Georgina ametaja baadhi ya misaada waliyoitoa kwa vikundi vya warahibu hao ni vifaa vya saluni ya kike na kodi ya pango ya saluni hiyo kwa muda wa miezi sita ambapo jumla imegharimu Tshs 4,580,000/=, mtaji wa Tshs 500,000/= kwa ajili ya biashara ya matunda na mbogamboga, Tshs 500,000/= kwa ajili ya utengenezaji wa sabuni, na Tshs 500,000/= kwa ajili ya biashara ya mtumba.Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Afya ya akili katika Hospitali hiyo ya Rufaa Dkt. Salum Seif amesema kituo hicho kilianza na jumla ya warahibu 12 ambapo mpaka sasa kinahudumia warahibu 746 ambapo wameona ni vyema kupitia siku 16 za kupinga ukatili kuwashirikisha wadau ikiwemo Jeshi la Polisi ili kulifikia kundi hilo ambalo ni wahanga wa ukatili wakisaikolojia na uchumi.
#knews24updates
#tunakutoakichakani
#knews24updates
#tunakutoakichakani
#knews24updates
#tunakutoakichakani
#knews24updates
#tunakutoakichakani
#knews24updates
#tunakutoakichakani