03/03/2024
Chama cha ACT kimetangaza kuwepo kwa mdahalo wa wagombea wa nafasi ya uenyikiti ndani ya chama hicho, mdahalo huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 4 mwezi Marchi 2024 utakuwa kati ya Juma Duni Haji ambaye anatetea nafasi yake na Othuman masudi ambaye ni makamu wa kwanza wa rasi wa serikali mapinduzi Zanzibar.
Hatua hiyo imepongezwa na wadau mbalimbali wa siasa nchini ambapo wamesema uwepo wa midahalo katika vyama vya siasa ni nyenzo ya kuimarisha demokrasia na uwazi na wameshauri vyama vingine viige kitendo hicho kwani ni njia ya kutengeneza Imani kwa wanachama juu ya uwezo wa wagombea katika chaguzi za nafasi za juu katika chama.