TIF MEDIA

TIF MEDIA KWA HABARI ZA SIASA MATUKIO JAMII NA MICHEZO KILA WAKATI TEMBELEA UKURASA HUU

Mange Kimambi uso kwa uso na Rais wa Tanzania mama Samia Suluhu Hasan rais wa Tanzania atakwenda kuzungumza na Watanzani...
19/09/2021

Mange Kimambi uso kwa uso na Rais wa Tanzania mama Samia Suluhu Hasan rais wa Tanzania atakwenda kuzungumza na Watanzania wanao ishi Marekani.

14/09/2021

Kwa ufupi Humphrey Polepole akielezea kuhusu serikali za nchi na masuala ya kiuchumi.

Polepole ametoa angalizo kuhusu serikali ya Tanzania kuwa na serikali mbili.

Tizama video.

13/09/2021

Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan awaonya mawaziri wake na sasa ameteua mawaziri wa nne na kumbadilisha mwanasheria mkuu.

"Walichukulia ukimya na utulivu wangu k**a udhaifu, ila nilikuwa nawasoma kwa miezi 6"- Rais Samia

TANZIAMjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba Zacharia Hans Pop amefariki dunia usiku huu.Klabu ya Simba ya jiji...
10/09/2021

TANZIA

Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba Zacharia Hans Pop amefariki dunia usiku huu.

Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imethibitisha kupokea taarifa za msiba wa mwanachama na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi klabu hiyo.

Hii ni taarifa kwa ufupi kutoka klabu hiyo ya Simba SC Tanzania

“Uongozi wa Klabu ya Simba umepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Zacharia HansPope ambaye amefariki dunia usiku huu”

Mungu ailaze mahara pema roho ya marehemu amini.

KWA UFUPI KUHUSU CHANJO YA PROGNOSISHadi Septemba 9, 2021, kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha JohnHopkins, zaidi ya...
10/09/2021

KWA UFUPI KUHUSU CHANJO YA PROGNOSIS

Hadi Septemba 9, 2021, kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha JohnHopkins, zaidi ya dozi bilioni 5.63 za chanjo za covid-19 zimetolewa kwa watu katika nchi 184 duniani sawa na 36.6% ya watu wote duniani. Wastani wa kuchanja kwa siku ni takribani dozi milioni 35.

Marekani imechanja dozi milioni 378 katika wastani wa dozi 784,492 kwa siku.China imechanja dozi bilioni 2.1 sawa na wastani wa dozi 6,879,143 kwa siku. Asilimia 69 ya watu nchini China wamepata dozi kamili ya chanjo.

Katika nchi za Afrika Morocco ni miongoni mwa nchi iliyochanja raia wengi. Takribani dozi milioni 35 zimetolewa sawa na 50% ya watu wote.

Kenya imechanja dozi milioni 2.93
Rwanda dozi milioni 2.57
Uganda dozi milioni 1.48
Tanzania dozi 310,000

Nchi zilizoendelea kiuchumi ndiyo zinaongoza kwa kuchanja raia wake ikilinganishwa na nchi zinazoendelea.
Ushahidi wa kisayansi unaonesha kwamba mpaka sasa chanjo zinao uwezo mkubwa wa kupunguza kasi ya maambukizi, hatari ya kufariki na kupata ugonjwa mkali iwapo mtu ataambukizwa virusi vya ugonjwa wa covid-19

Maambukizi yanayotokea kwa kasi katika baadhi ya nchi yakiambatana na vifo, kwa kiasi kikubwa yanatokea katika kundi la watu ambao hawajapata chanjo.

Imeandikwa na Musa Makongoro.

HIVI PUNDE KUTOKA MAHAKAMANI KESI YA MBOWEFreeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo amekan...
10/09/2021

HIVI PUNDE KUTOKA MAHAKAMANI KESI YA MBOWE

Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo amekana mashtaka yanayo mkabili mbele ya Jaji Mustapher Siyani.

Mbowe na wenzake watatu wamekana tuhuma hizo za ugaidi na sasa washtakiwa wanasomewa hoja za awali (PH) na wakili wa serikali Tulimanywa Majigo.

“Najua TAMISEMI ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi na hiyo kazi itafuata hivi karibuni (Uteuzi ...
06/04/2021

“Najua TAMISEMI ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi na hiyo kazi itafuata hivi karibuni (Uteuzi na Utenguzi), ili safu itimie na kazi iende ikafanywe....Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Kazi Iendelee)"

Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi wapya Ikulu Dar es salaam leo

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu amewasili Zanzibar tayari Kwa ajili ya Karume Day
06/04/2021

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu amewasili Zanzibar tayari Kwa ajili ya Karume Day

  Nafasi iliyo kuwa ya mkurugenzi wa  mawasiliano nchini Eng. James Kibala sasa imechukuliwa na Dkt. Kabir Bakari Kuwe u...
05/04/2021

Nafasi iliyo kuwa ya mkurugenzi wa mawasiliano nchini Eng. James Kibala sasa imechukuliwa na Dkt. Kabir Bakari Kuwe uteuzi huu ulifanyika jana na rais Samia Suluhu.

Dr. Kuwe amewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA)

  TCRA ambayo imepewa mamlaka kikatiba kwenye masuala mazima ya kimawasiliano hivi karibuni iliwataka makampuni husika y...
04/04/2021

TCRA ambayo imepewa mamlaka kikatiba kwenye masuala mazima ya kimawasiliano hivi karibuni iliwataka makampuni husika ya simu kutoa punguzo kwenye vifurushi Kwa wateja wake.

Mabadiliko hayo yamekuwa yakilalamikiwa na watumiaji wengi wa simu ambapo TCRA sasa imesitisha bei hii mpya.

Na sasa ndani ya siku nne vifurushi vitarudi kwenye bei ya zamani.

  Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu amewatakia Watanzania wakristo wote heri ya Pasaka salamu hiz...
04/04/2021

Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu amewatakia Watanzania wakristo wote heri ya Pasaka salamu hizo amezitoa kupitia mtandao wa kijamii Twitter.

  Hospitali ya White Plains iliyopo jiji la New York nchini Marekani juzi ijumaa ilimpokea rapa mahiri Earl Simon (DMX) ...
04/04/2021

Hospitali ya White Plains iliyopo jiji la New York nchini Marekani juzi ijumaa ilimpokea rapa mahiri Earl Simon (DMX) akiwa mahututi Baada ya kuzidisha kiwango cha matumizi ya dawa za kulevya.

Kufikia Jana jumamoso rapa huyo aliondolewa Mashine ya kupumulia na sasa hatumii na anaendelea vizuri.

  Ushindi wa Leo dhidi ya As Vita unaifanya timu ya Simba FC kufuzu robo fainali ya Mabingwa Afrika Baada ya ushindi wa ...
03/04/2021

Ushindi wa Leo dhidi ya As Vita unaifanya timu ya Simba FC kufuzu robo fainali ya Mabingwa Afrika Baada ya ushindi wa goli 4 dhidi ya As Vita.

Simba inatinga hatua hiyo ikiwa na alama 13, huku ikiwa bado na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Al Ahly ya Misri ikumbukwe Simba ilikuwa ukihitaji point moja pekee ushindi huu unaifanya Simba kuwa na alama 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye kundi lake.

FT: Simba SC 4-1 AS Vita Club

82 Simba SC 4-1 AS VitaMiquissone 30’ Chama 45+1’ Dk 82Bwalya 67’Soze 32’
03/04/2021

82 Simba SC 4-1 AS Vita

Miquissone 30’
Chama 45+1’ Dk 82
Bwalya 67’
Soze 32’

Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu akitoka nje ya uwanja wa ndege Mwl Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea Dodom...
03/04/2021

Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu akitoka nje ya uwanja wa ndege Mwl Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea Dodoma.

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TIF MEDIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to TIF MEDIA:

Videos

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Videos
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share