Uongozi wa Kiroho

  • Home
  • Uongozi wa Kiroho

Uongozi wa Kiroho A Swahili podcast for spiritual leaders in East Africa and around the world

Heri ya Mwaka Mpya! Siku za kwanza za mwaka mpya ni wakati mzuri wa kutathmini juu ya maisha yetu, huduma yetu, na hali ...
01/01/2021

Heri ya Mwaka Mpya! Siku za kwanza za mwaka mpya ni wakati mzuri wa kutathmini juu ya maisha yetu, huduma yetu, na hali yetu ya kiroho k**a viongozi. Podcast hii ni ujumbe maalum nilioandaa kwa ajili yako tunapoanza mwaka 2021. K**a umeanza kuchoka, kushuka moyo, au kukosa maono katika huduma, naomba usikilize podcast hii na kutiwa moyo. Tutaangalia mfano wa watu wa Mungu waliochoka na kupoteza furaha katika huduma, lakini kupitia ujumbe wa nabii wa Mungu walisaidiwa sana na hatimaye kuona mafanikio, ridhaa, na furaha katika huduma yao mbele za Bwana. https://uongoziwakiroho.podbean.com/e/tafakari-njia-yako/

10/12/2020
05/12/2020
05/12/2020

FAMILIA YA KIONGOZI WA KIROHO
Pasipo familia yenye ushuhuda mzuri na sifa njema, kiongozi atakosa nguvu na msaada unaotakiwa katika huduma yake. Mchungaji Onesimus Kibera anashiriki nasi katika podcast hizi mbili akieleza umuhimu wa familia katika maisha na huduma ya kiongozi wa kiroho, na kwa njia gani tunaweza kuongoza familia zetu vema. Kusikiliza podcast, nenda kwenye tovuti: www.UongoziwaKiroho.com au utume WhatsApp na kuomba kuwekwa kwenye orodha ya viongozi wanaopokea podcast mara kwa mara.

27/11/2020

NIDHAMU ZA KIROHO (Sehemu ya 2)
Adui wetu hufurahi sana akiona kiongozi anayeacha nidhamu za msingi za kiroho na kuanza kujitegemea nguvu zake na hekima yake. Katika podcast hii tunaendelea na maongezi yetu na Mzee Vernon Smith juu ya maisha ya kiroho ya kiongozi. Mgeni wetu anatupa mashauri mazuri juu ya utunzaji wa hali yetu ya kiroho na umuhimu wa kutembea na Yesu kwa karibu siku zote. Kuona podcast zote zilizopatikana, fungua tovuti: www.uongoziwakiroho.com. Ukitaka kuwekwa kwenye orodha ya viongozi wanaopokea podcast kwa njia ya WhatsApp, tuma email kwenye [email protected].

27/11/2020

NIDHAMU ZA KIROHO (Sehemu ya 1)
Mzee Vernon Smith yuko nasi katika podcast hii, akijibu maswali yangu juu ya Nidhamu za Kiroho katika maisha ya kiongozi. Katika podcast hii ya kwanza anatoa ushauri wake juu ya mambo ya lazima yaliyopaswa kuwemo katika maisha ya kiongozi wa kiroho ili adumu katika huduma na awe na ushuhuda mwema k**a mtu wa Mungu. Ili kusikiliza podcast, fungua www.uongoziwakiroho.com au kupokea podcast kwa njia ya WhatsApp uandike email kwenye [email protected] na kuomba kuwekwa kwenye orodha.

24/11/2020

Lengo la podcast hii ni kutoa ushauri wa kiutendaji na mafundisho ya kibiblia ili kusaidia kukidhi mahitaji ya Viongozi wa Kiroho. Hauko peke yako katika uongozi. Msaada upo! Ombi langu ni kwamba Bwana atumie podcast hii ili kukutia moyo, kukujenga, na kukupa mawazo mapya na ushauri wa kibiblia kwa ajili ya uongozi wako!

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Uongozi wa Kiroho posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Uongozi wa Kiroho:

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share