07/09/2022
Mchungaji Siva Moodley kutoka Gauteng, nchini Afrika Kusini ambaye alifariki dunia Agosti, 2021 bado yupo mochwari hadi leo akisubiriwa kufufuka k**a alivyoahidi.
Mchungaji huyo maarufu nchini Afrika Kusini, alikuwa na wafuasi wengi na alikuwa anaheshimika kwa sababu ya ‘miujiza’ aliyoifanya wakati wa mahubiri yake pale alipokuwa hai.
Mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa tangu kifo chake karibia siku 400 zilizopita, Mchungaji Moodley amehifadhiwa katika mochwari ya Martins Funeral Home ambapo wamiliki wa mochwari hiyo wamemelipwa ili kumweka kiongozi huyo wa imani katika uangalizi wao lakini hata mtiririko wa pesa wa karibia R60 000 (Tsh. 8,137,595) uliotolewa k**a bima ili kuhifadhi mwili huo unaanza kupungua.
Martin du Toit anayeendesha nyumba hiyo ya kuhifadhia maiti, hivi karibuni alisema anaomba idhini kutoka kwa Mahak**a ili kuchoma mwili huo, huku ikionekana kuwa hata Wafusi wake wamekata tamaa juu ya ufufuo wake kwasababu mwili wake haujatembelewa na Mtu yeyote kwa zaidi ya miezi 12 sasa.