29/08/2025
JIFICHE , Jiongezee thamani, usiwe mtu wa “NDIYO” kwa kila jambo,
Kubali,jitenge jipe muda binafsi wa kukua na kujifunza. - Don’t be too much available, sio lazima kila tukio au jambo uwepo, give yourself a time to Grow , pray & meditate.
Tunajifunza hata Mwana wa Mungu mwenyewe hakua na wanafunzi wake kila wakati hata yeye alihitaji muda binafsi wa kua na “ Baba “ kuongea nae , kujifunza kupitia kuomba, Alijitenga na kujificha.
Marko 1:35
“ 35 Hata na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.
36 Simoni na wenziwe wakamfuata;
37 nao walipomwona wakamwambia, Watu wote wanakutafuta. “
Sasa hili lina “gharama zake “ kama kweli unataka kukua kwenye eneo lako na kuonekana “mpya” na wa tofauti kubali kujitenga .
Ukubali kupitwa na fursa za muda mfupi (short-term opportunities).
Unaweza wakati mwingine usieleweke, na sio lazima kila mtu akuelewe kutoonekana kwako, “siku hizi Ndugu hatukuoni mtaani kuna nini nk “
Jipe mda binafsi wa kutosha , jifiche, jifunze,tafakari ,muombe Mungu nae kwa wakati atakuinua na kukupindisha juu tena ukiwa na nguvu mpya!
Daudi akiwa nyikani alipoteza nafasi ya kuonekana haraka hakuonekana kama mtu wa muhimu , alishinda porini akichunga kondoo za baba yake lakini kumbe Mungu alitengeneza mazingira ya kutoonekana kwake ili akue ajifunze, tukio moja la Goliath lilitambulisha upya na kumfanya aonekane kwa viwango vingine .
1 Samweli 16-17 .
Lakini kwa kufanya hivyo, unajiandaa kwa fursa kubwa zaidi na za kudumu.
WEWE NI WA THAMANI SANA MBELE ZA MUNGU HATA AKAKUUMBA KWA MFANO WAKE MWENYEWE - Mwanzo 1:26-27
ANAKUWAZIA MEMA NA KUKUPENDA SANA .
USIKUBALI KUWA WA KAWAIDA , USİWE MNYONGE!
Mpe nafasi , tunamtafute nae atafanya - Jitenge !.
Yeremia 29:12-14.
EK