Juma Issihaka

  • Home
  • Juma Issihaka

Juma Issihaka -Ukurasa rasmi wa Jukwa la Habari chanya za Tanzania
-Habari mbalimbali (Siasa, Uchumi, Burudani & Michezo)
-Ukweli, Uwazi, Uhakika

AJALI YA NDEGE COMORO BADO KITENDAWILIBALOZI wa Tanzania nchini Comoro, Pereira Ame Silima, amethibitisha kutokea kwa aj...
27/02/2022

AJALI YA NDEGE COMORO BADO KITENDAWILI

BALOZI wa Tanzania nchini Comoro, Pereira Ame Silima, amethibitisha kutokea kwa ajali ya Ndege ya Fly Zanzibar na kusema juhudi za kuwatafuta abiria wa ndege hiyo na marubani wake wawili ambao ni raia wa Zanzibar zinaendelea.

Amesema vikosi vya uokozi kutwa nzima vimekuwa vikiendelea kuwatufata abiria hao waliokuwemo katika ndege hiyo huku yakionekana baadhi ya mabaki yakiwemo matairi.

Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Usafirishaji na Uchukuzi, Amour Hamil Bakari, amesema wamepokea taarifa za tukio hilo na wanafuatilia kwa karibu kujua taarifa kamili kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Comoro.

''Ndege imesajiliwa Zanzibar lakini imekuwa ikifanya kazi zake za kutoa huduma za usafiri wa abiria katika visiwa vya Comoro baada ya kukodiwa, " amesema

Aidha, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui, amesema kijana wake aliyekuwa rubani wa pili katika ndege hiyo hajulikani alipo baada ya ajali hiyo.

''Familia tumekutana hapa huku tukitegemea zaidi kupata taarifa kutoka katika ubalozi wa Tanzania uliopo Comoro kuhusu ajali ambayo imehusisha mjukuu wetu'' amesema.

(Picha kwa hisani ya Millard Ayo)

Kinachoendelea kuhusu vita ya Urusi dhidi ya Ukraine Waziri Mkuu wa Uingereza, Borris Johnson, amesema tayari ameuma vik...
27/02/2022

Kinachoendelea kuhusu vita ya Urusi dhidi ya Ukraine

Waziri Mkuu wa Uingereza, Borris Johnson, amesema tayari ameuma vikosi vya Jeshi lake kuasidia ulinzi nchini Ukraine.

Barris anachukua uamuzi huo ikiwa ni siku kadhaa tangu Urusi ilivamie taifa hilo la pili kwa ukubwa barani Ulaya.

Waziri Mkuu huyo amesisitiza kwamba sambamba na kutuma jeshi, pia ataendelea kuiunga mkono Jumuiya ya Kujihami (NATO).

Hadi sasa inadaiwa zaidi ya wakazi 100,000 wa Ukraine wameyahama makazi yao kukimbilia maeneo yenye usalama zaidi, huku Rais wa taifa hilo, akigomea mazungumzo na Urusi yaliyopangwa kufanyika Belarus.

Wakati huo huo, serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje, imeeleza mpango wake wa kuandaa utaratibu wa kuwarudiaha nchini wananchi wanaoishi Ukraine.

MABADILIKO YA TABIANCHI HUGHARIMU 5% MAPATO YA NCHI ZA AFRIKA KWA MWAKA Mataifa ya Afrika yanalazimika kutumia asilimia ...
27/02/2022

MABADILIKO YA TABIANCHI HUGHARIMU 5% MAPATO YA NCHI ZA AFRIKA KWA MWAKA

Mataifa ya Afrika yanalazimika kutumia asilimia tano (5) ya mapato yao ya kiuchumi kwa mwaka, kujikinga na athari za mabadiliko ya tabianchi, ingawa huchangia kiwango kidogo cha uchafuzi cha gesi chafu duniani.

Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti uliofanywa na Shirika la Power Shift Africa la Nairobi nchini Kenya, kiwago hicho cha mapato hutumika ikiwa ni gharama za kuzuia athari za mabadiliko ya tabianchi.

Shirika hilo linabainisha kwamba gharama hizo hutumika kuimarisha miundombinu ya usafiri, mawasiliano, kujenga kinga za mafuriko na hatua nyingine za kudhibiti athari hizo.

Mkuu wa shirika hilo, Mohamed Adow, amesema ripoti hiyo inaonesha dhuluma kubwa kwa mataifa ya Afrika.

Ameongeza, "Haikubaliki kwamba gharama hizo zinawaangukia watu walioathirika zaidi wakati mchango wao ni mdogo katika mabadiliko ya tabianchi".

English version

African nations are obliged to spend 5% of their economic revenues annually, to protect themselves from the effects of climate change, despite the low levels of greenhouse gas emissions they contribute.

According to a research report by the Power Shift Africa Agency of Nairobi in Kenya, the revenue scale is used as a cost to mitigate the effects of climate change.

The agency notes that the costs are used to improve transportation, communications, flood protection and other measures to control the effects.

The head of the organization, Mohamed Adow, said the report showed serious injustice to African nations.

He added, "It is unacceptable that these costs fall on the most affected people when their contribution is limited to climate change."

Forumcc

Address


Telephone

+255693799413

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Juma Issihaka posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Juma Issihaka:

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share