Michenzani
Hivi ndivyo Hali Ilivyokuwa Baada Ya Jumba Namba 8 Michenzani Kushika Moto.
Tume ya Utangazaji
Taarifa Kutoka Tume Ya Utangazaji Zanzibar Kwa Vyombo Vya Habari
Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akielezea kuhusu Ugonjwa wa Covid 19 na Mtazamo wake kuhusu Ugonjwa huo na hatua ambazo Serikali inapaswa kuzichukua ili kuzuia Maambukizi zaidi.
Ajali
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Amon Kakwale ambaye ni kamanda wa polisi Temeke jijini Dar es Salaam, amethibitisha kutokea kwa ajali Mbaya iliyohusisha daladala na lori katika maeneo ya Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Magufuli mnazi mmoja
"Ukimsikia Mtu anasema Muungano hauna faida wakati Serikali ya Muungano imekopa Tsh. Trilion 2.3 kwa ajili ya Zanzibar pekee yake ujue huyo Mtu amepungikiwa kichwani, naomba tudumishe Muungano,pia Unguja na Pemba Mgawanyiko unatakiwa upotee, sisi ni Taifa moja”- JPM akiwa Zanzibar
“Nimejitokeza kugombea ili niutetee, kuulinda na kuudumisha Muungano, kwasababu kwenye Uchaguzi huu wamejitokeza Watu ambao kwa maneno yao, vitendo na hata sura zao na muonekano wao wanaonesha dhahiri kwamba hawapendi na hawautaki Muungano huu” -JPM
“Nitayalinda Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, changamoto ndogondogo za Muungano tutazimaliza, hata mgogoro wa ZECO na TANESCO , ZECO ilikuwa inadaiwa zaidi ya Bilioni 22.9 nikalifuta Deni, kwasababu Zanzibar ni Tanzania na Tanzania ni Zanzibar”-JPM.
Dk Mruma wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF akielezea muhimu na faida wa mfuko huo utakapokuwa mwanachama.
Dk Mruma kutoka Mfuko wa Bima ya Afya
Muhunzi
Shabani Muhunzi Mhasibu wa Mfuko wa Bima Ya Afya NHIF akifafanua jinsi ya kujiunga na kifurushi cha "Total Afya Kadi" ambayo inakuwa kwa wale walio na Umri chini ya miaka 18.
Kangeta
Ismail Kangeta NHIF Akifafanua nini Bima ya Afya na Vituo walivyonavyo ambavyo vinaweza kuwahudumia wananchi waliojiunga na Mfuko huo.
Magufuli akiwa Dumila
Rais John Magufuli amewaahidi wananchi wa eneo la Dumila mkoani Morogoro kuwa Serikali itatoa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vibanda vya wafanyabiashara na kumuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Morogoro kufanya upanuzi katika eneo hilo.
Ahadi hiyo ameitoa wakati akiwa njiani akitokea jijini Dar es Salaam akielekea Dodoma ambapo alisimama na kuwasalimu wananchi wa eneo hilo ambao wengi wao ni wafanyabiashara ndogo ndogo za kuuza mahindi, nyanya na mbogamboga ambao walimuomba Rais Magufuli kuwasaidia uwezekano wa kupanuliwa kwa barabara ili wajenge vibanda vya biashara katika eneo hilo.
Rais Magufuli amekubali ombi hilo la kupanuliwa kwa barabara hiyo na kujengwa kwa vibanda vya biashara kutokana na mazingira yaliyopo kwa sasa kuwa ni finyu na hatarishi kutokana na msongamano katika barabara kuu.
Rais Magufuli ameshawasili jijini Dodoma salama.
Rais Shein
Wafanyabiashara wameaswa kutotumia vibaya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kupandisha bei za vyakula hasa vile ambavyo hutumika kwa ftari
Taarifa kwa Umma
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imetangaza rasmi kusitisha shughuli zote za Kuftarishana,Darsa za pamoja za Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,Kusitisha shughuli za Baraza la Eid pamoja na shughuli zote zinazoambatana na mikusanyiko katika sherehe za Eid.