27/12/2023
KUSUDI
Maana ya kusudi.
Part 1.
Meaning of purpose.
Maana ya kusudi.
Kusudi ni dhumuni au kiini cha uwepo wako duniani yaani ni sababu ya wewe kuumbwa na kutimiza KAZI Fulani ambayo Mungu aliiweka ndani yako kwa ajili ya utukufu wake.
Mwanadamu aliyeumbwa kwa Mfano wa Mungu hawezi kujibunia utaratibu wake wa kuishi hapa duniani pasipo kupata instruction yaani maelekezo kutoka kwa Mungu, 'kabla sijakuumba nalikujua, Mungu alitujua kabla hajatuumba hivyo hii inamaanisha kwamba kuna sababu iliyosababisha mpaka Mungu kukuumba yaani kifupi ni kwamba dhumuni la kuumbwa wewe lilitangulia kabla ya wewe kuja ndipo wewe ufuate ili kukamilisha ule mpango wa Mungu au KAZI aliyokusudia uje kuifanya hapa duniani.
Mambo ya kuzingatia kuhusu kusudi.
1. Kusudi ni wazo la Mungu aliloliweka ndani ya MTU kwa ajili ya utukufu wake.
2. Kusudi lilitangulia kabla ya MTU mwenyewe, mfano simu haikutengenezwa mpaka ulipoonekana UMUHIMU wake au UHITAJI wake katika kufanya suala la mawasiliano kuwa rahisi au kufikisha Taarifa mapema na kusave time.
Hivyo matumizi ya simu anayajua vizuri aliyetengeza simu kuliko mtumiaji wa simu, hivyo kusudi la Kila mwanadamu aliyeumbwa na Mungu analijua Mungu kuliko mwanadamu mwenyewe, hivyo ni muhimu kumuuliza Mungu juu ya kusudi lako ili aweze kukwambia ndipo uweze kuishi maisha ya maana na kugundua thamani yako na kutumika kikamilifu katika eneo ambalo MUNGU ALIKUUMBIA KWALO KULIFANYA HAPA DUNIANI.
YOHANA 4:34
hapa Yesu anaeleza juu ya KAZI ambayo anatakiwa kuimaliza hapa duniani hivyo hata na wewe unayokazi Maalum UNAYOTAKIWA KUIKAMILISHA KWA UFANISI NA UFASAHA NDIPO UWEZE KUWA SATISFIED.
3.Kuna njia mbili tuu za kugundua kusudi lako njia ya kwanza ni kufunuliwa na Mungu yaani kwa njia ya UFUNUO. Na njia ya pili ni kwa kukisia sasa wengi huwa wanakisia ndio maana watu wengi wanaishi nje ya kusudi lao ila ukilenga kusudi lako utaishi maisha yenye maana na mafanikio kwa kiasi kikubwa.
ANGALIZO SIO KILA MTU ALIYEFANIKIWA SANA ANAISHI KWENYE KUSUDI LA MUNGU.