04/02/2023
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mhe. Abdulatif Yussuf Alwady (Mb.) na Kamati ya Ardhi, Mawasiliano na Nishati ya Baraza la Wawakilishi – Zanzibar wamefanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Ziara hiyo iliyofanyika Jumamosi tarehe 4 Februari, 2023 imelenga kuwapatia viongozi hao uelewa zaidi wa maendeleo ya usimamizi wa sekta ya Mawasiliano Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari, ameupokea ujumbe huo na kutoa wasilisho kuhusu majukumu ya TCRA na kazi ya usimamizi wa sekta ya Mawasiliano pamoja na utendaji-kazi wa idara na vitengo vya TCRA.