CG FM Radio

CG FM Radio This is CG Fm Radio's official page,unakaribishwa kuweza kuchangia mada na kupata habari mb Owned by C.G.

Traders, the C.G fm Radio Station started broadcasting services in Tabora municipality in 2004 after being registered by the Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) on September 1, 2004. Throughout its existence it has never been involved in any legal wrangle. The Radio Station has built a good working relations at high level of integrity with many residents of Tabora region and other

audiences in the neighbouring regions of Singida, Shinyanga and Kigoma regions. On top of that it has good working relations with government leaders, policy makers, religious leaders, Civic Organisations, Community Based Organisations (CBOs), Faith Based Organisations (FBOs), Small and Medium Enterprises (SMEs) and other actors in the media arena

The Radio Station has ample potentials for growth and expansion of services in the forthcoming years, because is well prepared in terms of coping with the the latest transmission technology in Tanzania.

Mkuu wa mkoa Kijana Paul Chacha atashiriki katika kuchagua kiongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa November 27.Wew...
26/11/2024

Mkuu wa mkoa Kijana Paul Chacha atashiriki katika kuchagua kiongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa November 27.

Wewe kijana, mwanamke na mtu mwenye ulemavu umeshiriki vipi katika uchaguzi wa mwaka huu.

Sikiliza CG MORNING POWER Kwa taarifa zaidi za uchaguzi.

MWANAMKE AUWAWA KWA MAPANGA, AKATWA T**I NA SEHEMU ZA SIRI- TABORAMwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Mahene wilaya ya Nz...
14/11/2024

MWANAMKE AUWAWA KWA MAPANGA, AKATWA T**I NA SEHEMU ZA SIRI- TABORA

Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Mahene wilaya ya Nzega mkoani Tabora aliyefahamika kwa jina la Sagali Masanja (62) ameuwawa kwa kukatwa katwa na panga kisha wauaji hao kumkata t**i moja na sehemu za siri na kuondoka nazo.

K**anda wa polisi mkoa wa Tabora kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea November 14 huku chanzo kikitajwa kuwa imani za kishirikina.

K**anda Abwao amesema watuhumiwa wawili wa mauaji hayo walik**atwa na wananchi katika kijiji cha Seki wilaya ya Nzega wakiwa kwenye nyumba ya mganga wa kienyeji aliyekua anawazindika kwa dawa ili wasik**atwe wakiwa na vidhibiti ikiwa ni pamoja na t**i moja na sehemu za siri.

Abwao amesema wananchi wenye hasira wakawashambulia wauaji hao pamoja na mganga wa kienyeji wakawaua na kuwachoma moto wote watatu.

Waliok**atwa na kuuwawa ni Masumbuko Ngasa (33) mkazi wa Segese wilaya ya Kahama, Silinde Kaseko (30), mkazi wa kijiji cha Seki wilaya ya Nzega na watatu ni mganga wa kienyeji Sana Maganga (66) mkazi wa kijiji cha Seki ambaye ni mama mzazi wa mtuhumiwa wa pili.

Inadaiwa kwamba uchunguzi wa jeshi la polisi ulibaini watu watatu waliowatuma watutumiwa wawili kwenda kufanya mauaji.

K**anda Abwao amesema watuhumiwa hao Lucia Mabula (36), mume wake Makenzi Mabula na Ramadhan
K***a (38) waliwalipa wauaji hao shilingi laki mbili ili wakafanye mauaji hayo wakimtihumu marehemu kwa uchawi kwamba alimroga mtoto wao mwaka 2023 aliyefariki kwa kutumbukia ndani ya kisima.

Zaidi ya wasaidizi wa kisheria 225 na wanasheria 26 kutoka halmashauri zote za wilaya na miji nchini wamejengewa uwezo w...
12/11/2024

Zaidi ya wasaidizi wa kisheria 225 na wanasheria 26 kutoka halmashauri zote za wilaya na miji nchini wamejengewa uwezo wa kutoa elimu ya mpiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa ,sambamba na kukabiliana na vitendo vya ukatili.

Akifungua mafunzo yaliyofanyika siku mbili kwa wanahabari 120 kutoka mikoa mbalimbali nchini Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Mtandao wa mashirika yanayotoa msaada wa kesheria nchini- TANLAP Christina Ruhinda amesema lengo la kutoa elimu hiyo kwa wadau hao ni kuwawezesha kuwa mabalozi.

Christina amesema kutokana na baadhi ya wananchi kutoelewa sheria na kanuni zinazoongoza mchakato wa uchaguzi,wanasheria watatoa elimu hiyo kupitia vyombo vya habari ili kukabiliana na vitendo vya ukatili katika kipindi hiki.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari kutoka ofisi ya Msemaji Mkuu wa serikali Zamarad Kawawa amesema lengo la elimu hiyo kwa wadau na wahabari ni kuwaelimisha umma kufanya maamuzi sahihi tarehe 27 mwezi huu.

Kwa upande wake Meneja wa huduma za utangazaji kutoka mamlaka ya mawasiliano nchini-TCRA amewataka wadau hasa wanahabari kuweka usawawa vyama vya siasa wakati wa kuripoti habari zao.

Baadhi ya wadau walionufaika na mafunzo hayo wakiwemo wanahabari wamesema watahakikisha wanazingatia sheria,kanuni na miongozo katika kuandika na kuripoti habari za uchaguzi.

TANLAP inatekeleza mradi wa miaka mitatu kuanzia mwaka huu 2024-2026 unaoitwa WANANCHI TUAMUE ambao unalenga kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika michakato yote ya uchaguzi.

"TUMIENI MVUA ZA MWANZO KUPANDA"- BODI YA TUMBAKUBodi ya Tumbaku Tanzania, imewataka wakulima wa tumbaku nchini kutumia ...
08/11/2024

"TUMIENI MVUA ZA MWANZO KUPANDA"- BODI YA TUMBAKU

Bodi ya Tumbaku Tanzania, imewataka wakulima wa tumbaku nchini kutumia mvua za masika zilizoanza kunyesha kupanda miti na tumbaku kwa wakati k**a inavyoelekezwa na maafisa ugani ili kuleta tija katika kilimo hicho.

Akizungumza na CG FM mkurugenzi mkuu wa bodi ya tumbaku nchini Stanley Mnozya amewataka wakulima kuzitumia taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinazotolewa na mamlaka hizo ili kuwa na uhakika wa tija ya uzalishaji.

Aidha Mnozya amesema anafahamu kuwa kuna baadhi ya wakulima wachache ambao bado hawajalipwa fedha zao za msimu ulioisha na kwamba bodi inaendelea kufuatilia kuhakikisha wakulima hao wanalipwa fedha hizo.

Amesema katika msimu wa kilimo 2023/2024 wakulima waliuza tumbaku yenye thamani ya dola za kinarekani zaidi ya milioni 269 na kwamba malipo yaliyokwisha kulipwa kwa wakulima ni dola milioni 267 sawa na asilimia 99.13 ya pesa yote na kiasi kilichobaki ni sawa na asilimia 0.87.

Amewataka wakulima kuendelea na maandalizi ya kilimo wakati suala la fedha likiendelea kufuatiliwa kwa kina na Bodi ya tumbaku.

BODI YA TUMBAKU YATAKA MPANGO KAZI WA UJENZI WA MABANI KABLA YA NOBEMBER 6‎‎Bodi ya tumbaku nchini imeziagiza kampun zot...
31/10/2024

BODI YA TUMBAKU YATAKA MPANGO KAZI WA UJENZI WA MABANI KABLA YA NOBEMBER 6

‎Bodi ya tumbaku nchini imeziagiza kampun zote za ununuzi wa tumbaku nchini kuwasilisha tathmini ya upungufu wa mabani kwa kila chama na mpango wa kujenga mabani hayo kabla ya November 6 mwaka huu.

‎Akizungumza katika mkutano wa wakulima wa Tumbaku mkoa wa Mara Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Stanley Mnozya amesema ni maelekezo ya serikali ya awamu ya sita kupitia Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kwamba kampuni ziingie mikataba ya miaka 3 ili kusaidia kujenga mabani kwa mikopo himilivu ya miaka mitatu.

‎Mnozya amesema ameshtushwa na takwimu za uwepo wa mabani kwa asilimia 5 tu katika eneo hilo huku zao hilo likiwa limestawi vizuri shambani.

‎Amewaeleza wakulima hao kuwa tumbaku ni maban hivyo kutokuwepo mabani maana yake hakuna tumbaku. na kuitaka kampuni inayonunua tumbaku hizo kufikia ijumaa wiki hii iwe imewasilisha takwimu za mabani yaliyopo na yasiyokuwepo na mpango wa kunusuru hali hiyo.

‎Aidha ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutoa ruzuku kwa wakulima wa tumbaku na kuwataka wakulima wazingatie kuwasilisha jina la mkulima chama chake, mifuko na akaunti yake k**a alivyoelekeza Mhe Waziri wa Kilimo.

‎Mkurugenzi Mkuu pia amekagia kilimo cha tumbaku katika eneo jipya la kilimo wilaya ya Tarime, ambapo amesema serikali ya awamu ya sita imeona umuhimu wa wakulima hao kulima tumbaku ili kujipatia kipato.

  WA CG ASHINDA TUZO,AWEKA REKODI.Mwandishi wa Habari wa kituo cha CG FM ya mkoani Tabora,Adam Hhando ameweka rekodi ya ...
29/10/2024

WA CG ASHINDA TUZO,AWEKA REKODI.

Mwandishi wa Habari wa kituo cha CG FM ya mkoani Tabora,Adam Hhando ameweka rekodi ya kuwa miongoni mwa waandishi wa habari wa kwanza kutwaa tuzo ya Mwandishi bora wa taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania-TMA kwa waandishi wanaotoka nje ya mkoa wa Dar es salaam.

Hhando ameshinda tuzo ya mwandishi bora wa mikoani na ametunukiwa tuzo na mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA,Jaji Mshibe Ali Bakari Katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Usafirishaji-NIT,Dar es salaam Oktoba 28,2024.

Jaji Mshibe amesema katika kuhakikisha tuzo hizi zinaendelea kuwa bora zaidi, mwaka huu Mamlaka imeboresha maeneo kadhaa ikiwemo kuongeza vipengele viwili vya waandishi kutoka nje ya Dar es Salaam na Zanzibar pamoja na kuboresha zawadi za washindi.

Hhando pamoja mshindi wa Zanzibar Othman Juma wa Alnoor FM ni washindi pekee walioshinda kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Orodha Kamili ya washindi wote ni Mshindi wa Runinga na Redio John Mathias kutoka TBC1, mshindi wa Zanzibar ni Othman Ali Juma kutoka Alnoor FM,mshindi wa mikoani ni Adam Hhando kutoka CG FM-Tabora, mshindi wa magazetini ni Superious Ernest kutoka gazeti la Uhuru na kwa mitandao ya kijamii ni Zaituni Mkwama kutoka Dailynews Digital TSN.

16/10/2024


Hatimaye Tuzo Za BET Hiphop 2024 Zimetangaza List Ya Washindi Wa Tuzo Hizo Usiku Wa Kuamkia Leo, Ambapo Rapa Wa Marekani Ndiye Aliyeongoza Kuondoka Na Tuzo Nyingi Zaidi Akiondoka Na Jumla Ya Tuzo 8;

Kendrick Lamar Ameshinda Tuzo Hizi Katika Vipengele Vya 👇

- Song Of The Year (Not Like Us)
- HipHop Artist Of The Year
- Best HipHop Video Of The Year (Not Like Us)
- Lyricist Of The Year
- Best Collaboration (Like That)
- Best Featured Verse
- Video Director Of The Year (W/ Dave Free)
- Impact Track

Mastaa Wengine Walioibuka Washindi Katika Tuzo Hizi Ni K**a Vile !!

- IAM HIPHOP 🏆

- HIPHOP ALBUM OF THE YEAR (PF2) 🏆

- BREAKTHROUGH HIPHOP ARTIST 🏆

& - BEST DUO GROUP 🏆

- BEST LIVE PERFORMER 🏆

- PRODUCER OF THE YEAR 🏆
- DJ OF THE YEAR 🏆

- HUSTLER OF THE YEAR 🏆

✍️: ( )


  YA EJATAdam Hhando wa CG FM ya Tabora ndiye aliyeibuka mshindi wa kwanza katika Tuzo za umahiri wa Uandishi wa Habari ...
09/10/2024

YA EJAT

Adam Hhando wa CG FM ya Tabora ndiye aliyeibuka mshindi wa kwanza katika Tuzo za umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania-EJAT kundi la wazi kwa upande wa Radio.

Hafla ya utoaji tuzo ilifanyika jijini Dar es salaam Septemba 28,2024.

Katika kipindi cha CG MORNING POWER Jumatano Oktoba 09,2024 tutakuwa na Profesa Philipo Sanga, Naibu Mkuu wa Taasisi ya ...
08/10/2024

Katika kipindi cha CG MORNING POWER Jumatano Oktoba 09,2024 tutakuwa na Profesa Philipo Sanga, Naibu Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu wazima. (Taaluma, Utafiti na Ushauri)

Mada:Elimu ya Watu Wazima kwa Maendeleo Endelevu.

Yanga SC yapangwa kundi A-CAF Champions League.Klabu ya soka ya Yanga ya Tanzania imepangwa kundi A katika mashindano ya...
07/10/2024

Yanga SC yapangwa kundi A-CAF Champions League.
Klabu ya soka ya Yanga ya Tanzania imepangwa kundi A katika mashindano ya ligi ya mabingwa Afrika msimu wa 2024-25 sambamba na timu za TP Mazembe ya DRC,Al Hilal ya Sudan na MC Alger ya Algeria.

Hatua ya makundi itaanza mwishoni mwa mwezi wa Novemba mwaka huu hadi January mwakani.
𝐆𝐫𝐨𝐮𝐩 𝐀:
▶️TP Mazembe 🇨🇩
▶️Yanga 🇹🇿
▶️Al Hilal 🇸🇩
▶️MC Alger 🇩🇿

𝐆𝐫𝐨𝐮𝐩 𝐁:
▶️Mamelodi Sundowns 🇿🇦
▶️Raja Club Athletic 🇲🇦
▶️AS FAR 🇲🇦
▶️AS Maniema 🇨🇩

𝐆𝐫𝐨𝐮𝐩 𝐂:
▶️Al Ahly SC 🇪🇬
▶️CR Belouizdad 🇩🇿
▶️Orlando Pirates 🇿🇦
▶️Stade d’Abidjan 🇨🇮

𝐆𝐫𝐨𝐮𝐩 𝐃:
▶️ES Tunis 🇹🇳
▶️Pyramids FC 🇪🇬
▶️GD Segrada Esperance 🇦🇴
▶️Djoliba AC

RATIBA YA MECHI ZA YANGA SC

26/27.11.24 : Young Africans v Al Hilal

6/7.12.24 : MC Alger v Young Africans

13/14.12.24 : TP Mazembe v Young Africans

3/4.01.25 : Young Africans v TP Mazembe

10/11.01.25 : Al Hilal v Young Africans

17/18.01.25 : Young Africans v MC Alger

Simba SC yapangwa kundi A mashindano ya Shirikisho barani Afrika 2024-25.Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya  S...
07/10/2024

Simba SC yapangwa kundi A mashindano ya Shirikisho barani Afrika 2024-25.

Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Shirikisho barani Afrika(CAF Confederation Cup),Timu ya soka ya SIMBA imepangwa kundi A samba na timu za CS SFAXIEN ya Tunisia,CS CONSTANTINE ya Algeria na FC Bravos ya Angola.

Hatua ya makundi itaanza mwishoni mwa mwezi wa Novemba mwaka huu hadi January mwakani.
𝐆𝐫𝐨𝐮𝐩 𝐀:
▶️Simba SC 🇹🇿
▶️CS Sfaxien 🇹🇳
▶️CS Constantine 🇩🇿
▶️FC Bravos do Maquis 🇦🇴

𝐆𝐫𝐨𝐮𝐩 𝐁:
▶️RS Berkane 🇲🇦
▶️Stade Malien 🇲🇱
▶️Stellenbosch 🇿🇦
▶️CD Luanda 🇦🇴

𝐆𝐫𝐨𝐮𝐩 𝐂:
▶️USM Alger 🇩🇿
▶️ASEC Mimosas 🇨🇮
▶️ASC Jaraaf 🇸🇳
▶️Orapa United 🇧🇼

𝐆𝐫𝐨𝐮𝐩 𝐃:
▶️Zamalek SC 🇪🇬
▶️Al Masry 🇪🇬
▶️Enyimba FC 🇳🇬
▶️Black Bulls

𝐑𝐀𝐓𝐈𝐁𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐄𝐂𝐇𝐈 𝐙𝐀 SIMBA SC 𝐂𝐀𝐅 𝐂𝐎𝐍𝐅𝐄𝐃𝐄𝐑𝐀𝐓𝐈𝐎𝐍 𝐂𝐔𝐏

28.11.24 : Simba SC 🆚 Bravos Do Maquis

08.12.24 : CS Constantine 🆚 Simba SC

15.12.24 : Simba SC 🆚 CS Sfaxien

05.01.25 : CS Sfaxien 🆚 Simba SC

12.01.25 : Bravos Do Maquis 🆚 Simba SC

19.01.25 : Simba SC 🆚 CS Constantine

Usikose kusikiliza kipindi cha Cg Morning Power kesho-Septemba 24 2024 kuanzia saa 3:00  hadi saa 4:00 Asubuhi Atasikika...
23/09/2024

Usikose kusikiliza kipindi cha Cg Morning Power kesho-Septemba 24 2024 kuanzia saa 3:00 hadi saa 4:00 Asubuhi

Atasikika Meneja wa TCRA Kanda ya Kati Mhandisi ASAJILE JOHN.

MADA | Usalama Mdandaoni: Matumizi sahihi na salama ya mtandaoni.

  WANAFUZU MAKUNDI CAF CC.Klabu ya Simba SC  imefuzu hatua ya makundi michuano ya kombe la shirikisho Afrika kwa ushindi...
22/09/2024

WANAFUZU MAKUNDI CAF CC.

Klabu ya Simba SC imefuzu hatua ya makundi michuano ya kombe la shirikisho Afrika kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya mchezo uliochezwa uwanja wa Mkapa,Dar es salaam muda mfupi uliopita.

Inafuzu kwa jumla ya 3-1 baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza kutoka suluhu.

FT Simba-Tanzania 3-1 Al Ahli Tripoli-Libya.
Agg 3-1
⚽️ Kibu
⚽️ Ateba
⚽️Balua
⚽️Mabululu.

  HATUA YA MAKUNDI.Klabu ya Yanga imefuzu hatua ya makundi michuano ya klabu bingwa Afrika kwa kuifunga CBE ya Ethiopia ...
21/09/2024

HATUA YA MAKUNDI.

Klabu ya Yanga imefuzu hatua ya makundi michuano ya klabu bingwa Afrika kwa kuifunga CBE ya Ethiopia magoli 6-0 katika uwanja wa New Aman Complex-Zanzibar.

Jumla CBE wanafungwa 7-0
⚽️ Clatous Chama
⚽️ Clement Mzize
⚽️ ⚽️Ki Aziz
⚽️ Mudathir Yahaya
⚽️ Duke Abuya.

  72 KUWANIA TUZO ZA EJAT.Waandishi wa habari 72 nchini akiwemo ADAM HHANDO wa CG FM wameteuliwa kuwania tuzo za umahiri...
19/09/2024

72 KUWANIA TUZO ZA EJAT.

Waandishi wa habari 72 nchini akiwemo ADAM HHANDO wa CG FM wameteuliwa kuwania tuzo za umahiri wa uandishi wa habari TANZANIA-EJAT 2023 baada ya kukidhi vigezo vinavyotakiwa.

Taarifa iliyotolewa Leo Septemba 19,2024 na Mwenyekiti wa k**ati ya maandalizi ya EJAT ERNEST SUNGURA imeeleza kuwa miongoni mwa waandishi hao ni wanaume 45 na wanawake 27.

Wateule hao wamekidhi vigezo vya ubora katika habari ikiwemo ukweli,usahihi,haki,kina,utafiti,uadilifu,uwasilishaji na ufichuaji maovu.

Katika tuzo za Mwaka 2022,Hhando alishinda tuzo mbili katika vipèngele vya Habari za Elimu na Sensa ya watu na makazi.

Tuzo hizo zitatolewa mwishoni mwa mwezi huu jijini DAR ES SALAAM ambapo mgeni rasmi atakuwa spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Daktari TULIA ACKSON.

FT CAF CCAL Ahly Tripoli-Libya 0-0 Simba SC-Tanzania.
15/09/2024

FT CAF CC
AL Ahly Tripoli-Libya 0-0 Simba SC-Tanzania.

Matokeo ya NBC PLSeptemba 14,2024.Azam FC 0-0 Pamba Jiji
14/09/2024

Matokeo ya NBC PL
Septemba 14,2024.

Azam FC 0-0 Pamba Jiji

Address

PO Box 2207 TABORA
Tabora

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when CG FM Radio posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to CG FM Radio:

Videos

Share