22/06/2024
aictkambarageinfo's profile picture
TAFAKARI YA KICHUNGAJI :
WAZO KUU : UTOAJI WA SADAKA KWA KUZINGATIA MFUMO WA KI BIBLIA
1- Kutoka 25:1 - 9.
2- 2Wakor.9:7 - 8
UTANGULIZI:
Kuna ukweli kwamba,mali zote tulizonazo ni mali za Mungu,amempatia kila mtu kwa kadrii ya mapenzi yake, ili zisaidie mahitaji katika Nyumba ya Mungu,mahitaji ya mtu mwenyewe na kuwasidia wahitaji.Pia kuna ukweli kwamba ni wakristo wachache sana wanaomtumikia Mungu kwa kumtolea sadaka zao kwa kuzingatia mfumo wa Ki-maandiko,kutokana na makosa ya Ki-mfumo wa utoaji.Basi tutajifunza mambo hayo kwa kupitia hatua mbili:
I: UTOAJI NJE YA MFUMO ULIVYO:
* Umejengwa katika mafundisho potofu, yasiyo na maarifa ya Kristo,yakujipatia mali kinyume kwa mapunjo na udanganyifu,wenye kuleta hofu na hukumu kwa Mwalimu na Mwanafunzi.
* Utoaji usio huru.
II: UTOAJI UNAOZINGATIA MFUMO ULIVYO:
* Unaofuata na kutii maelekezo ya Mungu kupitia Neno,wakutoa kwa kuzingatia uwezo,upendo na furaha. Unaozingatia wakati,uzito wa jambo.
* Unaitwa utoaji huru na baraka,Unaobariki moyo wa MUNGU na kuleta mafanikio.
* Wito kwa Kanisa:
Imeandaliwa na Mchungaji : Charles Petro Lugembe,Mch.msaidizi Askofu,SHD.
Tembelea kurasa zetu kupitia mitandao ya kijamii ili kupata matangazo na mahubiri yetu kwa Link zifuatazo :
https://www.youtube.com/
https://audiomack.com/aictkambarageinfo
https://www.instagram.com/aictkambarageinfo
https://www.facebook.com/aictkambarageinfo