06/01/2026
AAH! SHEMEJI... ACHA!
SEHEMU YA 01
Aisha alijiona k**a mtu mwenye bahati ya mtende kwa kutongozwa na shemeji yake. Nafsi yake ilikuwa njia panda; aliwaza amkubalie au amkatalie kwa kigezo cha undugu wa shemeji. Hata hivyo, akili yake iligubikwa na taswira ya utajiri wa shemeji yake huku akilinganisha na hali duni aliyokuwa nayo.
“Endapo nikikubali na dada akigundua, itakuwaje?” alijiuliza moyoni. “Aah! Lakini si amenitongoza mwenyewe? Siwezi kupiga teke fuko la pesa... Potelea mbali.”
Siku iliyofuata, Aisha alikutana na shoga yake kipenzi, Anita. Bila kusita, Aisha alimsimulia Anita kuhusu yaliyojiri kati yake na shemeji yake.
“Shoga yangu, basi ngoja nikupe mkanda kamili.”
Anita alichekelea kwa hamu. “Hapo ndipo ninapokupendea! Tukikutana barazani huchangamka kwa stori. Haya shoga, hebu nipe huo ubuyu.”
Aisha akaanza kuelezea, “Jana usiku wakati tunakula, dada aliwahi kushiba akaenda zake kulala. Sebuleni tukabaki mimi na shemeji tukipata chakula cha usiku. Basi shoga yangu, shemeji si ndio akaanza... ‘Ooh Aisha unajua wewe ni mzuri sana kuliko hata dada yako.’ Mimi nikabaki kucheka tu.
Dakika chache zikapita mara akaanza tena, ‘Aisha, najua wewe ni mtu mzima na unaweza kutunza siri. Mimi nataka uwe mpenzi wangu lakini dada yako asijue.’”
Aisha alivuta pumzi kidogo kisha akaendelea, “Shoga, nilishtuka! Kwani sikutegemea hata siku moja k**a shemeji atakuja kunitamkia maneno k**a yale, ukizingatia jinsi ninavyomheshimu.”
“Shuu! Atabeba mimba huyo!” Anita alidakia kwa mshangao uliochanganyika na furaha ya umbea. “Heshima hiyo weka pembeni, kwani yule ni baba yako mzazi?” Wote kwa pamoja waliangua vicheko vya umbea.
Anita akaendelea kumpa darasa, “Sasa sikiliza shoga yangu nikwambie; maisha ndiyo hayo yanaanza kukunyookea. Ukizingatia shemeji yako alivyo na utajiri, kumuacha ni sawa na kukataa kuolewa na mfalme ili uje kuwa malkia.”
📣🔈🔉SIMULIZI HII HAIJAFIKA MWISHO