Michezo

Michezo Habari, uchambuzi na matukio ya kimichezo kitaifa na kimataifa - www.michezoleo.com One Team, One Spirit, One Win

Rashford mshambuliaji hatari Ulaya. Meneja wa Barcelona Xavi Hernandez amemwagia sifa mshambuliaji wa Manchester United ...
16/02/2023

Rashford mshambuliaji hatari Ulaya.

Meneja wa Barcelona Xavi Hernandez amemwagia sifa mshambuliaji wa Manchester United Rashford kuwa ni miongoni mwa wafunga magoli hatari kwa sasa Ulaya.

Pia Xavi amempongeza Erik ten Hag kwa kuiboresha na kuimalisha klabu ya Manchester United huku akimfanya Marcus Rashford kurudi kwenye ubora wake.

Kwa sasa Rashford amefunga mabao 13 katika mechi 15 tangu kombe la dunia lilivyomalizika. Idadi hiyo ya magoli inamfanya Rashford kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi bara la ulaya kwa kipindi hicho.

Kocha huyo wa Barcelona ameongeza kuwa wanatahadhari kwa wachezaji wote United na hasa mshambuliaji Rashford aliyepo kwenye kiwango cha juu kwa sasa.

Barcelona inawaalika Man united usiku wa leo Alhamis kwenye michuano ya Europa League ngazi ya mtuano.

Arsenal Kuchunguza mashabiki wake.Arsenal imeanzisha uchunguzi baada ya kiungo mshambuliaji wa Man City, Kevin De Bruyne...
16/02/2023

Arsenal Kuchunguza mashabiki wake.

Arsenal imeanzisha uchunguzi baada ya kiungo mshambuliaji wa Man City, Kevin De Bruyne kushambuliwa kwa kurushiwa vitu mbalimbali ikiwemo chupa za maji kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa Arsenal.

Tukio hilo lilitokea baada ya kufanyiwa mabadiliko dakika ya 87 kumpisha mchezaji mwingine Kalvin Phillips hivyo kumlazimisha kupita pembeni mwa uwanja walipokuwa mashabiki wa Arsenal.

De Bruyne ni miongo mwa wachezaji waliofunga mabao na kutengeneza nafasi ya bao moja dhidi ya Arsenal katika ushindi wa 3-1 katika uwanja wa nyumbani wa Arsenal, Emirates.

Taarifa iliyotolewa na Arsenal ni ya kulaani vitendo hivyo ambavyo sio vya kiuanamichezo na kuhatarisha usalama wa wachezaji. Hivyo Arsenal itachunguza na kuchukua hatua kali kwa wote waliohusika na vitendo hivyo.

Chama cha soka nchini Uingereza FA nacho kimethema wanachunguza kuelewa nini kilitokea kupitia kamera za uwanjani.

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Michezo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share