Kihahi Tv

Kihahi Tv Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Kihahi Tv, Media/News Company, Misungwi, Mwanza.

Karibu kwa uhitaji wa Matangazo ya video Kwasasa Tangazo k**a hili unalipata kwa offer ya TSH 50,000/= NA ELFU 75,000/= UNAPATA TANGAZO LA [DK 1 NA SEC. 30] Changamka tajiri nipe maelezo Yako
nikutengenezee Tangazo Zuri lenye kunasa wateja.PIGA 0626248355

 : Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Ester Mahawe amefariki dunia leo Januari 14, 2025 katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya...
14/01/2025

: Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Ester Mahawe amefariki dunia leo Januari 14, 2025 katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya kaskazini -KCMC Mkoani Kilimanjaro alikokuwa anapatiwa Matibabu.

Taarifa ya kifo chake imetangazwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe Mhe. Ester Mahawe. Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ninatoa pole kwa familia, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, wafanyakazi na wananchi wote wa wilaya ya mbozi, ndugu, jamaa na mafariki kwa msiba huu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi' amesema waziri Mchengerwa.


Kwa habari kemkemu Follow page zetu hizi
Follow King Kihahi
Follow Kihahi Tv
fans

11/01/2025

Karibu kwa huduma ya matangazo kwa mfumo wa audio na video bei zetu ni powa kabisa pia tunatengeneza LOGO za aina zote na tunatengeneza poster

Baada ya kazi kukamilika tunakupa ofa ya kutangaza biashara yako bure kabisa siku 2. Kupitia mtandao wetu wa WhatsApp wenye zaidi ya watu elfu 5

Pia matangazo kwa mfumo wa kingereza yapo karibu boss wetu malipo baada ya kazi kukamilika

WhatsApp 0626248355

🤣🤣zingatia neno UREMBO
11/01/2025

🤣🤣zingatia neno UREMBO

🤣🤣🤣🤣
11/01/2025


🤣🤣🤣🤣

Leo ninayo shukrani ya dhati kwasababu nakumbuka siku ya kuzaliwa kwangu. YESU ninakushukuru sana na nina ujasiri wa kuk...
07/01/2025

Leo ninayo shukrani ya dhati kwasababu nakumbuka siku ya kuzaliwa kwangu. YESU ninakushukuru sana na nina ujasiri wa kukushukuru mbele za watu hawa sababu kila zuri linaloonekana kwangu leo ni wewe YESU umelifanya.

Katika Mwaka 2024 umenifundisha vingi na ukanielekeza hata kwa njia ngumu na mwisho wa siku nimejifunza huku nikisherehekea siku yangu ya kuzaliwa nikiwa nimejifunza mapya mengi yaliyonijenga. Uzima, Nguvu, Ushindi, Afya, Furaha, Kibali, Neema na vingine vizuri vyote ni Mali yangu.

Marafiki zangu wote ambao mnanipenda na kuniwazia yaliyo mema na asanteni sana kwa hayo na hata kwa maombi yenu pia.

HAPPY BIRTHDAY TO ME
DR KIHAHI

RAHA YA USHINDI WA CAF UMTWANGE MPEMBA😂😂😂
05/01/2025

RAHA YA USHINDI WA CAF UMTWANGE MPEMBA😂😂😂

UNAITAKIA SIMBA USHINDI UKIWA WAPIKihahi Tv
05/01/2025

UNAITAKIA SIMBA USHINDI UKIWA WAPI
Kihahi Tv

05/01/2025

POLISI WANASWA WAKIPOKEA RUSHWA KWA MADEREVA

🛑 Maafisa wa upelelezi kutoka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini Kenya (EACC) wamewak**ata maafisa tisa wa polisi wa Usalama Barabarani kwa kushawishi ufisadi na kukusanya hongo kutoka kwa madereva wa magari.

🛑 Israel imefanya mashambulizi katika Ukanda wa Gaza na kusababisha vifo vya watu 50 wakiwemo watoto wakati juhudi za kusaka makubaliano ya usitishwaji mapigano zikiendelea.

🛑 Maafisa nchini Korea Kusini wamefanikiwa kuingia katika makazi ya rais mapema leo Ijumaa, wakijaribu kumk**ata kiongozi aliyeondolewa madarakani Yoon Suk Yeol.

Cc Kihahi Tv
King Kihahi

FUNGUKA NA HILIUsisahau kufollow page hiziFollow King KihahiFollow Kihahi Tv
04/01/2025

FUNGUKA NA HILI
Usisahau kufollow page hizi
Follow King Kihahi
Follow Kihahi Tv

China inakumbwa na ongezeko la visa vya virusi vya metapneumovirus (HMPV), hali inayosababisha hofu kwa wananchi k**a wa...
04/01/2025

China inakumbwa na ongezeko la visa vya virusi vya metapneumovirus (HMPV), hali inayosababisha hofu kwa wananchi k**a wakati wa janga la COVID-19.

Ripoti na machapisho kwenye mitandao ya kijamii yanaonyesha hospitali zikiwa zimefurika, huku ikidaiwa uwepo wa virusi mbalimbali k**a HMPV, mafua A, Mycoplasma pneumoniae na hata COVID-19.

HMPV ni virusi vinavyosababisha maambukizi ya mfumo wa kupumua, hasa mafua, Virusi hivi vinawaathiri sana watoto wadogo, wazee na wale wenye kinga dhaifu lakini watu wa rika zote wapo kwenye uwezekano wa kupata.

Dalili za HMPV ni sawa na zile za mafua na maambukizi mengine ya kupumua, zikiwemo Kikohozi, Homa, Mafua na kupumua kwa shida.

Virusi vya HMPV huenea kupitia matone ya kikohozi au chafya, kugusana na mtu aliyeambukizwa na kugusa vitu vilivyochafuliwa na kisha kugusa uso, pua au macho.

Ili kujikinga na HMPV unatakiwa kuosha mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji, kuepuka kugusa uso bila kunawa mikono, kujitenga na watu wenye dalili za maambukizi.

Swali: Je, Kuna Tiba au Chanjo?

Jibu: Kwa sasa, hakuna tiba maalum au chanjo dhidi ya HMPV.

Follow page hizi
Kihahi Tv
King Kihahi

04/01/2025

Rais William Ruto amesema anapenda jina jipya la utani la 'Kasongo' ambalo Wakenya wamempa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza leo Januari 3, 2025 katika Kaunti ya Bungoma wakati wa mazishi ya mama wa Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetangula, Maayi Nanyama, Rais ametania kuhusu majina ya 'Kasongo' na 'Zakayo,' akiyataja kuwa mazuri.

Amesema anatambua wimbo maarufu wa ‘Kasongo’ ambao umekuwa ukivuma kote nchini na ambao umesababisha jina hilo la utani, akisema hana tatizo nalo.

“Kuna watu mitandaoni hawapendi tusimame na kusema kuna kazi inaendelea Kenya, wanabaki na fitina, hadithi... mara Kasongo, mara Zakayo,” amesema.

“Hiyo Kasongo ni sawa, ni wimbo mzuri ambao ulikuwa unaendelea, kwa hivyo tuendelee nao. Na hiyo ya Zakayo pia si mbaya kwa sababu tunakusanya ushuru kupeleka Kenya mbele. Hiyo ni sawa.”

Rais Ruto pia amefananisha jina la Zakayo na mhusika wa Kibiblia wa jina hilo, akiwahimiza watu wawe k**a Zakayo ili waweze kutumiwa na kutembelewa na Mungu.

“Na kwanza Zakayo ndio Mungu alimtembelea; sasa wewe hujakuwa Zakayo utatembelewa na Mungu namna gani?” ameuliza.

Jina 'Kasongo' linatokana na wimbo wa Rhumba wa bendi maarufu ya Super Mazembe, ambao unahusu mwanamke anayemsihi mume wake, Kasongo, kurejea katika ndoa yao.

K**a ilivyokuwa kwa 'Zakayo,' ambalo Rais alilikubali mwaka wa 2024, Wakenya wamebadilisha wimbo wa 'Kasongo' na kuutumia kumfananisha Rais Ruto kwa taswira zinazohusiana na baadhi ya sera ambazo wengine wanaziona kuwa zisizopendwa. Taswira hizi zimepata umaarufu mkubwa mitandaoni.

Awali, Rais alikuwa kimya kuhusu jina hilo na wimbo, lakini alijitokeza wakati wa Mkesha wa Mwaka Mpya katika Kaunti ya Kisii, akicheza wimbo wa Kasongo pamoja na viongozi wenzake.

Kihahi Tv
King Kihahi

😂😂😂😂😂
28/12/2024

😂😂😂😂😂

Kiongozi wa zamani na aliyekuwa mfanyabiashara wa kampuni ya Suzuki Motor ya nchini Japan, Osamu Suzuki, amefariki dunia...
28/12/2024

Kiongozi wa zamani na aliyekuwa mfanyabiashara wa kampuni ya Suzuki Motor ya nchini Japan, Osamu Suzuki, amefariki dunia Desemba 25, 2024 akiwa na umri wa miaka 94 baada ya kuugua ugonjwa wa saratani.

Baada ya kuwa Rais wa nne wa kampuni hiyo mnamo mwaka 1979 alizindua gari dogo la bei nafuu ambalo lilipata mafanikio makubwa na kuuzwa katika masoko ya kimataifa.

Alijipa jina la 'mzee wa kampuni ndogo hadi ya kati' hiyo ni kutokana na ucheshi wake.

Hata hivyo, katika miaka ya 2000 ya uongozi wake, mauzo ya kampuni hiyo yaliongezeka zaidi ya mara kumi na kufikia yen trilioni 3 ($19 bilioni).

King Kihahi

Watu sita wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Kijiji cha Lumalu Kata ya Upolo kwenda Kilosa wil...
28/12/2024

Watu sita wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Kijiji cha Lumalu Kata ya Upolo kwenda Kilosa wilayani Nyasa kuanguka na kuwaka moto katika eneo la chunya mpakani mwa wilaya ya Nyasa na mbinga mkoani Ruvuma.

Waliofariki kati yao ni walimu wanne wa shule ya msingi Lumaru, mfamasia mmoja na Dereva wa gari hilo.

Akiwa katika eneo la ajali hiyo Bw. Salumu Mohamedi Ismail Katibu Tawala Wilaya ya Nyasa aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Nyasa Mhe Peres Magiri ,amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema kuwa watu Sita wamefariki na miili imehifadhiwa katika hospital ya Mbinga na amewaomba ndugu wa marehemu kwenda hospitalini hapo kwaajili ya utambuzi.

Chanzo Cha ajali Bado hakijafahamika, Endelea Kufuatilia kurasa Zetu kwa Taarifa zaidi


Follow Kihahi Tv

Watu Tisa wamefariki dunia papo kufuatia ajali mbaya iliyotokea mapema leo Tarakea wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro ik...
27/12/2024

Watu Tisa wamefariki dunia papo kufuatia ajali mbaya iliyotokea mapema leo Tarakea wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro ikihusisha basi la abiria la kampuni ya Ngassero lililogongana uso kwa uso na gari dogo la abiria aina ya Toyota Noah .

Kwa mujibu wa taarifa za mashuhuda kutoka eneo la ajali wameleza kuwa Basi la kampuni ya Ngassero linalofanya safari zake kati ya Tarakea na Dodoma lilikuwa likielekea Tarakea na gari dogo la abiria lilikua likitoka Tarakea kuelekea Moshi Mjini.

Mkuu wa wilaya ya Rombo Raymond Mangwala amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Karume iliyopo wilayani huku dereva wa basi la Ngassero akitajwa kukimbia.

“Ni kweli kumetokea ajali mbaya iliyosababisha vifo vya abiria tisa pamoja na dereva waliokuwa kwenye gari dogo, inaonekana dereva wa gari dogo alikua akiovertake gari jingine ndipo likakutana na basi na Ngassero “ Alisema Mangwala .

Na King Kihahi

HIII NI KWA WANAUME TUUFollow Kihahi Tv
27/12/2024

HIII NI KWA WANAUME TUU
Follow Kihahi Tv

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara, limemuonya shabiki na mwanachama wa Yanga Sc, Haji Mana...
23/12/2024

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara, limemuonya shabiki na mwanachama wa Yanga Sc, Haji Manara kwa kauli isiyo ya kiungwana aliyoitoa baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa jana kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Dimba la KMC kati ya Yanga na Tanzania Prisons.

“Baada ya kumalizika kwa mchezo, Haji Manara alianza kuongea na Vyombo vya Habari akiwa ameegesha gari lake mbele ya gari la Jeshi la Magereza.

“Kwa kuwa alikuwa amezuia gari la Jeshi kuondoka, aliombwa atoe nafasi kwa kusogeza gari lake kuruhusu gari alilokuwa amelizuia liweze kupita na yeye aendelee na mahojiano yake.

“Hata hivyo, pamoja na kuombwa alikataa kwa dharau na kuanza kutoa maneno yasiyo ya kiungwana, yenye viashiria vya kutweza utu na yenye mwelekeo wa kulifedhehesha Jeshi la Magereza.

“Uongozi wa Jeshi unatoa onyo na kuwataka wananchi kuacha kutoa kauli zenye mwelekeo wa kubeza, kutweza, kudharau mamlaka yake au kulifedhehesha na kwamba halitasita kuchukuwa hatua kali kwa yeyote atakayehusika,” Taarifa ya Jeshi la Magereza.

Watu wa wawili wa familia moja; aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kwenye Ofisi ya Msajili na Hazina, Am...
23/12/2024

Watu wa wawili wa familia moja; aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kwenye Ofisi ya Msajili na Hazina, Amos Nnko na binti yake wa kwanza, Maureen Nnko wamefariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea wilayani Same, mkoani Kilimanjaro.

Taarifa ya Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu imeeleza kuwa katika ajali hiyo iliyotokea jana mchana, mke wa marehemu na watoto wengine wawili na mwanafamilia mmoja wamejeruhiwa na wanapatiwa matibabu katika hospitali za KCMC na Mawenzi Mkoani Kilimanjaro.

Follow King Kihahi

Address

Misungwi
Mwanza

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kihahi Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share