15/05/2024
WAMEKUJA KUTEMBEA NA KUJIFUNZA PIA
Msafara wa Viongozi wa TP Mazembe ukiongozwa na CEO wao Frederic Kitengie, siku ya jana wamefika Makao Makuu ya Klabu ya Yanga na kupokelewa na Mtendaji Mkuu wa Yanga SC Andre Mtine.
Mtendaji Mkuu (CEO) wa TP Mazembe Frederic Kitengie amesema kuwa kwao ni Furaha na heshima kubwa na wamefurahia mapokezi mazuri waliyoyapata.
“Tunafuraha kubwa kufika hapa, ni heshima kubwa kwetu na tumefurahi kwa mapokezi mazuri mliyotupatia, tumekuja hapa kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Yanga na kutengeneza urafiki mzuri utakaoweza kuvisaidia vilabu vyetu hivi viwili bora Afrika Mashariki na kati hivi sasa" amesema Frederic.
Akizungumzia msafara huo Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga SC Simon Patrick amesema kuwa TP Mazembe wamevutiwa na namna Yanga SC inavyojiendesha na kuamua kuja kujifunza mambo mbalimbali.
Ameongeza kuwa kutakuwa na makubaliano Ya ushirika wa kirafiki baina Ya klabu hizo mbili.
“Tumepokea ugeni mzito kutoka moja ya Klabu kubwa Barani Afrika, TP Mazembe ya DR Congo ambao wamevutiwa na namna Klabu yetu ya Yanga inavyoendeshwa hivyo wamekuja hapa Tanzania kujifunza mambo mbalimbali kwenye Mfumo wetu wa Mabadiliko ya Uendeshaj.
“Pia tutakuwa na makubaliano rasmi ya urafiki wa kushirikiana kati ya Klabu yetu ya Yanga na TP Mazembe ili kuweza kubadilisha ujuzi wa mambo mbalimbali ya kimpira yatakayoweza kuisaidia Klabu yetu" amesema Simon.
Afisa Habari wa Yanga SC Ali Kamwe naye ameongeza kuwa TP Mazembe wametoka DR Congo kuja kujifunza ila kuna watu wapo jirani hapa wanapiga kelele kuwa hawana cha kujifunza.
“Klabu kubwa k**a TP Mazembe imesafiri kutoka DR Congo kuja hapa Jangwani kujifunza kwa kichwa chetu, Rais wetu Eng. Hersi Said halafu kuna watu wako nyumba ya 16 tu jirani hapo, wanapiga kelele kuwa hawana cha kujifunza kwa Yanga. Niwaambie tu, tutabeba Makombe hadi kila Mwanachama atakuwa anabeba la kuweka nyumbani kwake.” amesema Kamwe.