WORLD TV TZ

WORLD TV TZ This pages for news around the world, realistic news and break news like and follow

Jenerali Abdourahmane Tchiani amejitangaza kuwa kiongozi mpya wa Niger baada ya mapinduzi makubwa.Jenerali Abdourahmane ...
28/07/2023

Jenerali Abdourahmane Tchiani amejitangaza kuwa kiongozi mpya wa Niger baada ya mapinduzi makubwa.

Jenerali Abdourahmane ambaye pia anajulikana k**a Omar Tchiani, aliongoza mapinduzi ambayo yalianza Jumatano wakati kitengo cha walinzi wa rais alichoongoza kilimk**ata kiongozi wa nchi hiyo.

Hii inatatiza kipindi cha kwanza cha mpito cha amani na kidemokrasia nchini Niger tangu ijinyakulia uhuru wake mwaka 1960.

Rais Mohamed Bazoum anadhaniwa kuwa katika afya njema, na bado anashikiliwa na walinzi wake.

Good morning Chicago 🇺🇸
21/07/2023

Good morning Chicago 🇺🇸

Singapore, The City of Gardens. 🇸🇬🇸🇬🇸🇬
19/07/2023

Singapore, The City of Gardens. 🇸🇬🇸🇬🇸🇬

Enzi mpya ya magari yanayopaa inakaribia kuanza. Mnamo tarehe 12 Juni 2023, Utawala wa Shirikisho la Usafiri wa Anga (FA...
17/07/2023

Enzi mpya ya magari yanayopaa inakaribia kuanza. Mnamo tarehe 12 Juni 2023, Utawala wa Shirikisho la Usafiri wa Anga (FAA) ulitoa Cheti Maalum cha usafiri wa Anga kwa toleo la gari linalopaa liliyotengenezwa na Aeronautics, na kuruhusu gari hilo kwenda safari za maeneo machache kwa maonyesho, utafiti na maendeleo zaidi.

‘Advanced Air Mobility’ (AAM) ni neno linalotumika kwa ndege za abiria au zinazobeba mizigo ambazo kwa kiasi kikubwa zinajiendesha.

Mara nyingi hujulikana k**a teksi za kwenye anga au ndege za wima za kupaa na kutua, magari haya kwa nadharia hutoa usafiri wa haraka na salama kutoka eneo moja hadi jingine.

Hakuna miundombinu halisi au msongamano wa magari wa ardhini utakaopunguza kasi ya safari zake.

🗣Wakati sisi tunalumbana bandari apewe nani iende isiende, ikae, ivue isivue, wenzetu kwa kuona malumbano yetu wame-jump...
14/07/2023

🗣Wakati sisi tunalumbana bandari apewe nani iende isiende, ikae, ivue isivue, wenzetu kwa kuona malumbano yetu wame-jump wamekwenda kulekule, lile lile jumba lilowekwa bendera ya Tanzania limewekwa bendera ya jirani, sasa Tanzania tumeuza wale jirani wamekimbilia kule kufanya nini?, na siku ambayo bunge letu lilisema ni ruhusa bandari iendeshwe na serikali na sekta binafsi siku ya pili wenzetu wakasema nyinyi moja, sisi zote ziende private sector wakakimbia kule kuwahi nafasi,

🗣Sasa muone jinsi ambavyo fursa zinavyokuja na kukimbia haraka haraka na jinsi wengine wanavyoweza kuzitumia haraka haraka, nilisema nitoe tu mfano huo kuona changamoto na jinsi ya kuzitumia fursa na kuzifanya zisichomoke,"- Rais Samia



🗣Mkisoma kwenye mitandao ya kijamii tunakosolewa sana kushoto kulia mpaka nje ya nchi,  sasa wale mnaohisi wana mchango ...
14/07/2023

🗣Mkisoma kwenye mitandao ya kijamii tunakosolewa sana kushoto kulia mpaka nje ya nchi, sasa wale mnaohisi wana mchango mzuri mnaweza mkawaleta wakawa sehemu ya mipango, wakafikiri pamoja na sisi ili kuondoa lile vuguvugu wanalosema wamepanga nini..

🗣Leteni list yao tuwafanyie veting tuwaweke kwenye Tume ya Mipango tufanye nao kazi". Rais Samia Suluhu Hassan.

🗣Tunataka kuongoza Serikali, na k**a ni upinzani tumechoka kuwa wapinzani, ndio sababu tunakazana kukijenga chama kwa gh...
14/07/2023

🗣Tunataka kuongoza Serikali, na k**a ni upinzani tumechoka kuwa wapinzani, ndio sababu tunakazana kukijenga chama kwa gharama kubwa kwa maumivu makubwa.” –Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha usajili wa beki wa kati Gigy Gift Fred kutoka klabu ya  SC Villa kwa Mkataba wa...
11/07/2023

Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha usajili wa beki wa kati Gigy Gift Fred kutoka klabu ya SC Villa kwa Mkataba wa mwaka mmoja hadi 2024,✅️

Giggy mwenye miaka 24 amejiunga na Yanga SC kwa usajili huru bila malipo baada ya mkataba wake kuisha🚨.

Dubai, Emiratos árabes unidos 🇦🇪.
11/07/2023

Dubai, Emiratos árabes unidos 🇦🇪.

ATHUMANI Yengayenga (35), mkazi wa Shanwe Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amewashangaza watu wengi kwa kuamua kufunga ...
10/07/2023

ATHUMANI Yengayenga (35), mkazi wa Shanwe Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amewashangaza watu wengi kwa kuamua kufunga ndoa na wanawake watatu kwa siku moja huku akidai kuwa lengo lake lilikua ni kufunga ndoa na wanawake wanne kwa siku hiyo,
Athuuman amesema aliamua kuoa wanawake wanne baada ya kupata hasira kwa aliekuwa mke wake kumuacha, ndio ikapelekea kuoa wanawake wengi ili ikitokea tena mke mwingine kumuacha basi atabaki na hao wengine, ameongeza kuwa haikuwa kazi rahisi lakin alifanikiwa kuwapata na ilichukua mda mrefu kuwashawishi mpaka wakamkubalia kwa pamoja.

Calgary Canada 🇨🇦
10/07/2023

Calgary Canada 🇨🇦

Rais mpya wa Latvia Katika hotuba yake ya kwanza k**a rais, Edgars Rinkevics alisema "mapambano dhidi ya rushwa, uhalifu...
08/07/2023

Rais mpya wa Latvia Katika hotuba yake ya kwanza k**a rais, Edgars Rinkevics alisema "mapambano dhidi ya rushwa, uhalifu na makampuni ya biashara lazima yawe kipaumbele cha kitaifa"

Waziri wa mambo ya nje wa muda mrefu wa Latvia Edgars Rinkevics amekuwa kiongozi wa kwanza wa taifa la Umoja wa Ulaya kuwa mpenzi wa jinsia moja wa aliye wazi.

Bw Rinkevics, ambaye alihudumu k**a waziri wa mambo ya nje tangu 2011, ameapishwa k**a rais wa Latvia Jumamosi katika mjini Riga Ingawa kwa kawaida cheo chake ni cha hadhi, Rais wa Latvia anaweza kupinga sheria na kuitisha kura za maoni.
Muungano wa Ulaya (EU) umewahi kuwa na wakuu wa serikali wapenzi wa jinsia moja hapo awali, lakini haujawahi kuwa na mkuu wa serikali wapenzi wa jinsia moja.

Katika nchi nyingi, wakuu wa nchi na wakuu wa serikali ni watu tofauti - kwa mfano rais na waziri mkuu. Waziri Mkuu wa zamani wa Ubelgiji Elio di Rupo alikuwa kiongozi wa kwanza wa serikali ya Umoja wa Ulaya ambaye anashiriki mapenzi ya jinsia moja.
Bw Rinkevics, 49, alijitokeza kwa mara ya kwanza mwaka wa 2014 kutangaza kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja na amekuwa bingwa wa haki za LGBT tangu wakati huo.

Ndoa za wapenzi wa jinsia moja ni kinyume cha sheria nchini Latvia, ingawa mahak**a ya kikatiba ya nchi hiyo ilitambua ndoa za jinsia moja mwaka jana.

Hivi ndivyo vilabu 10 Bora barani Afrika kwa sasa kwa mujibu wa CAF.1. Al Ahly —  🇪🇬 2. Wydad —  🇲🇦 3. ES Tunis — 🇹🇳 4.R...
08/07/2023

Hivi ndivyo vilabu 10 Bora barani Afrika kwa sasa kwa mujibu wa CAF.

1. Al Ahly — 🇪🇬
2. Wydad — 🇲🇦
3. ES Tunis — 🇹🇳
4.Raja CA — 🇲🇦
5.Sundowns — 🇿🇦
6.CR Belouizdad — 🇩🇿
7.Simba — 🇹🇿
8.Petro De Luanda -🇦🇴
9. Pyramids —🇪🇬
10.Zamalek — 🇪🇬

Mwanasiasa mkuu wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko siku ya Alhamisi alionya kuhusu "machafuko yasiyoelezeka" ikiwa...
07/07/2023

Mwanasiasa mkuu wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko siku ya Alhamisi alionya kuhusu "machafuko yasiyoelezeka" ikiwa hataweza kugombea uchaguzi wa Februari, katika maoni yake ya kwanza tangu Rais Macky Sall athibitishe kuwa hatatafuta mamlaka nyingine.

Twitter inakusudia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Meta kuhusu programu yake pinzani inayokua kwa kasi ya Threads.Th...
07/07/2023

Twitter inakusudia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Meta kuhusu programu yake pinzani inayokua kwa kasi ya Threads.
Threads, ambayo ilizinduliwa kwa usajiri wa mamilioni ya watu siku ya Jumatano, ni sawa na Twitter na imeanzishwa na wakuu wa Meta k**a programu mbadala "rafiki".

Mmiliki wa Twitter Elon Musk na Kampuni yake walisema 🗣ushindani ni sawa, kudanganya sio" - lakini Meta ilikanusha madai katika barua ya kisheria kwamba wafanyakazi wa zamani wa Twitter walisaidia kuunda programu ya Threads.
Zaidi ya watu milioni 30 wamejisajiri kwenye programu hiyo mpya, kulingana na Meta.

Mwonekano na hisia za Threads ni sawa na zile za Twitter, mwandishi wa masuala ya teknolojia wa BBC James Clayton alibainisha, Alisema upashaji wa habari na utumaji upya ni wa kawaida sana.
Katika hatua iliyoripotiwa kwanza na chombo cha habari cha Semafor, wakili wa Twitter Alex Spiro alituma barua kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Meta Mark Zuckerberg Jumatano akiishutumu Meta kwa "utumiaji mbaya wa kimfumo, wa makusudi, na usio halali wa siri za biashara za Twitter na mali nyingine za kiakili"- katika kuunda Threads.
Bw Spiro hasa alidai kuwa Meta ilikuwa imeajiri wafanyakazi kadhaa wa zamani wa Twitter ambao "walikuwa na wanaendelea kupata siri za kibiashara za Twitter na taarifa nyingine za siri sana" ambazo hatimaye ziliisaidia Meta kuunda kile alichokiita programu ya "kunakili" Threads.
"Twitter inakusudia kutekeleza kwa dhati haki zake za uvumbuzi, na inaitaka Meta kuchukua hatua za haraka kuacha kutumia siri zozote za biashara za Twitter au habari nyingine za siri," barua hiyo inasema.
BBC, imeona nakala ya barua hiyo, ambayo imewasiliana na Meta na Twitter kwa maoni.
Bw Musk alisema kuwa "ushindani ni sawa, kudanganya sio" akijibu chapisho kwenye Twitter ambalo lilirejelea barua ya kisheria.

Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema maswali mengi juu ya mchezaji atakayevaa jezi namba sita kwenye timu hiyo s...
06/07/2023

Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema maswali mengi juu ya mchezaji atakayevaa jezi namba sita kwenye timu hiyo sasa yamepata majibu baada ya kuwa na uhakika wa mchezaji huyo.

Akizungumza katika mahojiano wakati wa mchezo dhidi ya Nyasa Big Bullets, Kamwe amesema kesho anawasili kocha mkuu na kutangazwa kwa benchi la ufundi na kuanza kutangaza wachezaji wapya wa timu hiyo.

Kamwe ameongeza kuwa tayari timu hiyo imefunga usajili na kilichobaki sasa ni kuanza kutambulisha wachezaji wapya na kumalizia kuwaaga ambao wameachana nao.

🗣Niwambie tu mashabiki wa Yanga kuwa mchezaji atakaye vaa jezi namba sita yupo Dar es Salaam na tutaanza kuvitambulisha vyuma vipya na kuaga ambao hatutaendelea nao,” amesisitiza Kamwe

Yanga SC ipo nchini Malawi kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo ambapo mchezo wa leo ulikuwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 59 ya uhuru wa Taifa hilo.

Kikosi cha Azam FC kimeanza kujifua katika viunga vya Azam Complex, Chamazi katika kujiandaa kuelekea msimu mpya wa 2023...
06/07/2023

Kikosi cha Azam FC kimeanza kujifua katika viunga vya Azam Complex, Chamazi katika kujiandaa kuelekea msimu mpya wa 2023/24.

Kikosi hicho kitakwenda kuweka kambi katika mji wa Sousse nchini Tunisia kuanzia Julai 9-30, 2023.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Mary Chatanda amesema bandari ya Dar es Salaam haijauzwa k**a wanav...
06/07/2023

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Mary Chatanda amesema bandari ya Dar es Salaam haijauzwa k**a wanavyosema baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema na Taifa.

🗣Naomba kuwahakikishia suala hili lipo vizuri wala bandari haijauzwa k**a wanavyosema baadhi kuwa bandari imeuzwa, Hayo ni maneno ya wapotoshaji na kipindi hiki mtasikia mengi, Rais Samia hawezi kuuza Bandari na wala hajaingia mkataba wa huo wanaosema wa miaka 100, bado wapo kwenye mazungumzo". Amesema Chatanda

🗣Hata shukurani hakuna, mikataba ya huko nyuma ilikuwa inasainiwa tu juu kwa juu lakini Rais Samia muwazi ameamua kupeleka mkataba mbele ya Bunge ujadiliwe, imekuwa nongwa?".

🗣Bandari hii walipewa Wawekezaji na mapato yalikuwa yanaingia ni kidogo, Sasa tuendelee na mtu anatupa Trilioni 7? K**a tumepata mwekezaji anataka kutupa Trilioni 26 bora.

Amesema Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa, Mary Chatanda

Address

Mwanza

Telephone

+255757602572

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when WORLD TV TZ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to WORLD TV TZ:

Videos

Share