Ni kabila gani wanakula nyama mbichi?
Barabara ya Morogoro eneo la jangwani imefungwa kutokana na maji kujaa barabarani
WAWEKEZAJI KUNUFAISHA WANASHERIA WA TANZANIA: Serikali imesema wakati wawekezaji kutoka nje wakimiminika kuja kuwekeza hapa nchini, ni wakati wa taasisi za kifedha na sekta ya sheria kuhakikisha wanatumia fursa hizo kikamilifu na sio kuwaachia wanataaluma kama zao kutoka nje kunufaika na uwekezaji unaokuja kufanywa hapa nchini.
Waziri wa katiba na sheria Balozi Pindi Chana ameyasema hayo kwa wanasheria wakati wa mkutano na taasisi za Sheria na wanasheria binafsi kutoka mkoa wa dar es salaam, mkutano uliandaliwa na benki ya NMB huku lengo likiwa kufahamiana nao kwa karibu lakini pia kuwashukuru kwa kazi kubwa wanayofanya ndani ya taaluma yao ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika uwekezaji unaendelea kufanyika nchini kuwa wa utulivu na mafanikio makubwa.
Balozi Chana amesema serikali imeweka utaratibu ambao unawalinda wanasheria wa hapa nchini katika kuhakikisha kuwa wananufaika na wawekezaji wanaokuja kuwekeza toka nje ya nchi, na kwa takwimu alizonazo hadi sasa nchi inazaidi ya mawakili elfu kumi na moja. #sometimes #nmbtanzania #gudiengai

ISHU YA FEI TOTO NA YANGA, Rais Samia ataka imalizwe...
AJALI YA MOTO KIWANDA CHA PLASTIKI JAMBO...
Moto mkubwa umezuka katika Kiwanda cha plastiki, JAMBO kilichopo Vigunguti, jijini Dar es Salaam, bado chanzo cha moto hakijafahamika. Jeshi la uokoaji wamewasili kusaidia uzimaji. #sometimestz
AJALI TANGA : Watu 17 wameripotiwa kufariki katika ajali iliyohusisha magari mawili, Ajali imetokea usiku wa tarehe 03/02/2023 Majira ya Saa 4.30 Usiku Eneo la Magila Gereza Kata ya Magila Gereza Tarafa ya Mombo Wilayani Korogwe, Barabara Kuu ya Segera - Buiko..
Kumeripotiwa majeruhi 12, 10 kati yao hali zao ni mbaya kulingana na mkuu wa mkoa wa Tanga Bw. Mgumba T.Omary...
Magari yaliyohusika na Ajali hiyo ni gari na T.673 CUC aina Mitsubish Fuso, lililogongana uso kwa uso na gari T.863 DXN aina ya Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 kutoka Dar es Salaam kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa mazishi...
Kulingana na Raya Kipingu mwandishi wa Channel TEN mkoani humo, zoezi la utambulizi wa miili limeratibiwa huko Korogwe, ambapo miili 14 ni ya familia moja wakiwemo watoto wawili wa Marehemu aliyekuwa akisafirishwa kwaajili ya kwenda kuzikwa Moshi... #sometimes #ajaliTanga #channelten
Kwa wasikilizaji ambao mko Mwanza na mlinikosa hewani kitambo, sasa unaweza kunisikiliza kupitia 101.7 MAGIC FM
Saa Moja usiku hii leo tuungane nawe katika DURU ZA AFRIKA...
KUKU WENYE MIGUU MIKUBWA : Nyama yake ni ghali sana, huliwa na familia za kishua sanaa... Wanajulikana kwa jina la Dong Tao chicken ama kwa Vietnam gà Đông Tảo; kwa jina lingine ni Dragon Chicken...
Hii aina ya kuku ndra kabisa kuwapo, na wanapatikana sana nchini Vietnam, katika kijiji cha Đông Tảo katika wilaya ua Khoái Châu karibu na Hanoi...
Kuku hawa inaelezea kuwa na nyama tamu sana, na ya hadhi ya juu kabisa nchini Vietnam, na zamani walikuwa maalumu kwa familia za kifalme na watu wa hadhi ya juu...
Suala la kutotoa vifaranga kwao ni changamoto, hasa na kutokana na ukubwa miguu yao ambayo huyavunja mayai kirahisi sana, hivyo utotoaji hutegemea mashine maalumu 'incubator'
Kuku hawa 'dragon chicken' wanaathiriwa sana na mabadiliko ya hali ya joto, na huchukua hadi mwaka mmoja kuwa tayari kufanywa kitoweo, ambapo wakati huo huwa wamefikia uzito wa hadi kilo sita.
Kulingana na mtandao wa Wikipedia, Nyama yake huuzwa laki tatu hadi nne fedha za Vietnam, kwa kilo moja...
Nakukumbusha fedha ya kiVietnam mfano hii 400,000/- VND ni sawa na shilingi za kitanzania 37,552.38 (elfu thelathini na saba) #sometimes