Musoma Tv

Musoma Tv Musoma Tv is a Digital Multmedia Storytelling for Local News with the Public Interest.

MCHENGERWA: MIRADI YOTE NGAZI YA MSINGI ITANGAZWE KUPITIA NeSTWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ...
06/02/2025

MCHENGERWA: MIRADI YOTE NGAZI YA MSINGI ITANGAZWE KUPITIA NeST

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na wakuu wa vitengo vya manunuzi kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa kwenye ngazi ya msingi inatangazwa kupitia mfumo wa Nest.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati akizungumza na Wabunge,Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala Wasaidizi Miundombinu na wakuu wa vitengo vya manunuzi kutoka kwenye Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi kuhusu mfumo wa Nest kilichofanyika kwenye ukumbi wa wa Mabeyo jijini Dodoma leo tarehe 04.02.2024.

Amesema baada kupata mafunzo haya leo hii nendeni mkabadilike, fuateni Sheria ya Manunuzi, onyesheni mabadiliko hayo kwenye utekelezaji wa miradi na kuanzia sasa miradi yote itangazwe kupitia mfumo wa Nest na si vinginevyo alisisitiza.

Miradi hiyo ikishatangazwa kupitia Nest hakikisheni mnaisimamia kwa Weledi wa hali ya juu na kwa uaminifu ili itekelezwe kwa viwango vinavyotakiwa na thamani ya fedha iweze kuonekana’ amesema!

Aidha Mhe. Mchengerwa aliwataka PPRA kuhakikisha inawajengewa uwezo watumiaji wa mfumo wa Nest katika ngazi za msingi ili kupunguza changamoto zinazojitokeza wakati wa kuomba zabuni mbalimbali.
Chanzo:OR-Tamisemi

MAHAKAMA KUU KANDA YA BUKOBA YAFANIKIWA KUTOA ELIMU YA SHERIA KWA WANANCHI ZAIDI YA MILIONI 15  WA NDANI NA NJE YA NCHIA...
04/02/2025

MAHAKAMA KUU KANDA YA BUKOBA YAFANIKIWA KUTOA ELIMU YA SHERIA KWA WANANCHI ZAIDI YA MILIONI 15 WA NDANI NA NJE YA NCHI

Angela Sebastian-Bukoba,

Jaji mfawithi wa mahak**a kuu kanda ya Bukoba Immaculata Banzi amesema mahak**a hiyo imefanikiwa kutoa elimu ya sheria kwa wananchi ml.15.9 wa ndani na nje ya mipaka ya nchi hii juu ya sheria mbalimbali ikiwemo ya ubakaji na ukiukwaji wa maadili .

Amesema idadi hiyo ya wananchi inatokana na kupitia vyombo mbalimbali vya habari vilivyotoa elimu hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria nchini.

Pia amesema kwa mwaka huu mahak**a hiyo imepanua wigo ambapo katika wiki hiyo mahak**a kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walifanya zoezi la utoaji elimu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo, katika viwanja vya mahak**a kuu kanda ya Bukoba,shule za msingi 25,shule za Sekondari 17, vyuo vitano,magereza na viwandani.

Pengine ni vituo vya magari yaendayo ndani na nje ya mkoa,magulio,masoko mialo iliyopo kandokando ya ziwa victoria,Bodaboda na kuchangia damu katika hospitali ya rufaa Bukoba.

"Pamoja na hayo yote tumetoa elimu kupitia vyombo 41 vya habari vya ndani na nje ya mkoa ambazo ni radio,TV,mitandao ya kijamii na magazeti hivyo,kupitia vyombo hivyo tumeweza kufikia makadilio ya wananchi mil.15.9 ambayo ni idadi kubwa katika utoaji elimu na mafanikio makubwa kwetu sisi tunamshukuru sana waandishi wa habari"ameeleza Jaji Banzi.

Akielezea juu ya dira ya Taifa ya maendeleo anasema dira ya Taifa ni andiko maalum linaloainisha mipango iliyowekwa,mikakati inayotekelezwa na raslimali zitakazotumika ili kufikia mipango ya mendeleo hivyo, hutafsiliwa katika mipango midogo ya maendeleo ambapo uandaaji wake ushirikisha wananchi na wadau wa maendeleo .

"Dira inayoelekea mwishoni kuisha ya miaka 25 imeleta mafanikio ya kuridhsha hususani kuboresha maisha,ukuaji wa uchumi na utawala hivyo uandikishaji wa dira mpya 2050 ina malengo mbalimbali ikiwemo , Tanzania ni nchi yenye kipato cha kati cha ngazi ya juu yenye uchumi mseto ,ustaimilivu,imala na jumuishi,kutokomeza aina zote za umasikini hususani kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu"anaeleza

Anasema mwaka 2050 kutakuwepo ongezeko la vijana mjini ambapo inasababisha ongezeko kubwa la mashauri Mahak**ani kwakuwa vijana ndiyo wenye nguvu kazi na pilikapilika nyingi pia, kuongezeka kwa shuguli za kilimo,madini,utalii na uzalishaji viwandani uashiria ongezeko la mashauri Mahak**ani na ukuaji wa teknolojia.

Anaserma kutokana na hayo kuna haja ya kuangalia nafasi ya taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya Taifa ya maendeleo ili kukabiliana na kwendana na mazingira hayo ya Tanzania ya 2050 hivyo, kuna umuhimu wa mahak**a na wadau wake na wanamaendeleo wote kutoa maoni ya kuboresha rasimu hiyo atimaye kuweza kupata dira ya Taifa ya 2050 inayokidhi malengo ya dira hiyo na watanzania wote katika elimu na haki madai.

Kwa upande wake wakili wa Serikali wa mkoa wa Kagera Richard Nkaina amesema siku ya sheria nchini inayo malengo makuu matatu kuashilia kuanza kwa mwaka wa shuguli za mahak**a,kutathimini dhana ya utoaji haki na mchango wa kila taasisi ya utoaji haki na kuwaombea viongozi wa mahak**a ambapo ,kauli mbiu ya wiki ya sheria mwaka huu ni Tanzania ya 2050,nafasi ya taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya Taifa ya maendeleo .

Nkaina amesema kaulimbiu hiyo inawataka waeleze namna ambavyo taasisi zinazosimamia haki madai zinavyotekeleza au zinavyojipanga kutekeleza malengo ya dira ya Taifa ya maendeleo ya 2050 pia, malengo makuu ya dira hiyo yanaweza kufikiwa ikiwa kila raia atapata haki yake bila vikwazo vya aina yoyote kutoka katika taasisi zinazosimamia haki madai

"Kutakuwa na mifumo imara ya kisheria na kitaasisi itakayowezesha haki kufikia kwa haraka,kwa ufanisi na kila taasisi inayosimia haki madai itafanya tathimini ya mipango na mikakati yake ili kuona k**a inaendana na kasi ya viwango,ubora,ufanisi na tija inayolengwa "mesema Nkaina

Amesema imeshuhudiwa kwa miaka hivi karibuni jinsi mahak**a kuu ya Tanzania inavyopiga hatua katika utoaji haki kwa kusogeza huduma kwa wananchi kwa kujenga vituo jumuishi vya utoaji haki,kujikita katika matumizi ya tehama katika kutoa haki na kupunguza hatua za kusikiliza mashauri kutoka hatua 38 hadi 21.

Anasema hiyo ni mchango mkubwa katika kutekeleza dira ya Taifa ya maendeleo ijayo kwasababu inachangia kuvutia biashara na uwekezaji.

Wakati huo huo kaimu mkuu.wa mkoa ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima akisoma hotuba ya mkuu wa mkoa wa Kagera hajat Fatma Mwassa amewahimiza wananchi katika mkoa humo kutoa maoni kwenye rasmu ya dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2050 yatakayochangia kutokomeza matukio yaliyokithiri katika mkoa huo ya ukatili wa kijinsia, ubakaji na mauaji ya kikatili ambayo yanahatarisha hali ya amani.

Tunasema Asante sanaAngela Batuli
03/02/2025

Tunasema Asante sana
Angela Batuli

BILISHANGA ATAJA SABABU ZA KUONGEZEKA MATUKIO YA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA MKOA WA KAGERANa Angela Sebastian-Bukob...
30/01/2025

BILISHANGA ATAJA SABABU ZA KUONGEZEKA MATUKIO YA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA MKOA WA KAGERA

Na Angela Sebastian-Bukoba

Mwendesha mash*taka wa mkoa wa Kagera Ajuaye Bilishanga ametaja visababishi vinavyopelekea kuwepo kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo,mbali na kwamba jamii inatambua uwepo wa adhabu kubwa kwa wahusika wa vitendo hivyo.

Bilishanga alisema hayo leo wakati akitoa elimu kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali juu ya mada inayozungumzia sheria ya ubakaji na ukiukwaji wa maadili katika ukumbi wa mikutano wa mahak**a kuu kanda ya Bukoba ambapo zinaendelea shughuli za maadhimisho ya wiki ya sheria nchi.

"Matukio ya ukatili wa kijinsia kwa ujumla wake kwa mkoa wa Kagera ni mengi kwa richa ya kwamba kumekuwa kunatolewa adhabu kali na kubwa lakini bado watu wanaendelea kufanya vitendo hivyo kwa kasi, ila tumebaini zipo sababu mbalimbali zinazochangia uwepo wa vitendo hivyo kubwa ikiwa ni ufahamu mdogo kwa jamii"ameeleza Bilishanga

Alisema wanajamii ambao ni wahanga wa matukio hayo pamoja na walezi au wazazi wao wanaingia katika makubaliano na familia ya mtenda kosa au na mkosaji mwenyewe wanakwenda pembeni nje ya mahak**a wanamalizana hivyo inakuwa ngumu kwa wanaosimamia haki kuthibitisha bila kuacha shaka yoyote ili mkosaji aweze kuadhibiwa.

Alizitaja nyingine kuwa ni imani za kishirikina ambapo watu wanaambiwa wawabake watoto wao,mama zao,kuingilia wengine kinyume na maumbile na watu wenye magonjwa ya akili kuingiliwa kinyume na maumbile eti mtu apate utajiri.

Pia nyingine ni ulevi, umaskini,utandawazi na watoto wengine wanajifunza kutoka shuleni kwa watoto wenzao ambapo hii yote inatokana na staiili za maisha watu wanayoishi mfano mzazi anapowaacha watoto kuanzia asubuhi hadi jioni wakijilea wenyewe au kulelewa na wasichana wa kazi.

Aliwashauri wazazi na jamii wanapogundua uwepo na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dora na mahak**a wanapoitwa kutoa ushahidi wasiogope kwasababu mahak**ani ni sehemu salama na kuna usiri pia ni kwa manufaa yao wenyewe,jamii na Taifa ili kuondokana na tatizo la ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wa hakimu mkazi mwandamizi mahak**a ya hakimu mkazi Bukoba Yona Wilson alisema makosa ya kubaka yanatoa adhabu kwa mazingira tofauti mfano mtu aliyembaka mwanamke mtu mzima na mahak**a ikialidhika na ushahidi adhabu ni miaka 30.

"Yule atakayepatikana na hatia amembaka mtoto wa k**e chini ya miaka 10 adhabu yake ni kifungo maisha,ubakaji wa kundi (genge la watu zaidi ya mmoja) adhabu ni kifungo kisichopungua miaka 30,kosa la kupoka au kuteka msichana kwa ajili ya kumuoa bila ridhaa yake adhabu ya kifungo miaka saba na kosa la kumshikashika mtu bila ridhaa yake kwa maslahi binafsi ni kifungo cha miaka mitano"Wilson

Pia makosa ya ulawiti inapobainika mtu kafanyiwa mapenzi kinyume na maumbile au katoa ridhaa kufanyiwa hivyo adhabu ni miaka 30 na pale akifanyiwa mtoto chini ya miaka 10 kifungo maisha jera.

Alisema hizo ndizo adhabu zinazotolewa na sheria ambayo wanaitumia kwa mara nyingi kwa makosa hayo ni sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022 na kuna adhabu nyingine ambazo wakosaji unakuta ni watoto kwa makosa hayohayo sheria inayotumika ni ya watoto .

Kwa upande wa wakili wa kujitegemea ambaye pia ni ni makamu mwenyekiti wa chama cha wanasheria mkoa wa Kagera (TLS) Sethi Niyikiza alizungumzia sheria inayotumika kudhibiti virusi vya Ukimwi sheria namba nane ya mwaka 2008 inazungumzia kipengele moja wapo cha mtu kumsababishia mtu kuathirika na virusi vya Ukimwi wakati mtu akijua kuwa ameathirika.

"Kifungu cha 46 cha sheria hiyo kimetaja kosa la mtu anayeambukiza mtu virusi huku akijua kuwa ameathurika na kuna njia za kujizuia kutomwambukiza mtu mwingine sheria imeweka wazi adhabu atakayoipata ili jamii kuhakikisha hawafanyi mambo ambayo yataathiri maisha ya wengine "alieleza Niyikiza

MHE. MOLLEL AWATAKA WANANCHI KAGERA KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MARBURG.Na Angela Sebastian-Bi...
29/01/2025

MHE. MOLLEL AWATAKA WANANCHI KAGERA KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MARBURG.

Na Angela Sebastian-Biharamulo.

Watu wawili wa familia moja wamefariki dunia huku Wahisiwa 44 wakiendelea kuwekwa chini ya ungalizi wa wataalam wa Afya wakiwa majumbani kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa marburg uliotokeaWilayani Biharamulo mkoani Kagera.

Watu 281 walihisiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya marburg ambapo 145 kati ya hao waliwekwa chini ya uangalizi katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma baada ya kusambaa kwa ugonjwa huo.

Kutokana na taarifa ya Wizara ya Afya watu hao 145 waliokuwa chini ya uangalizi kwasasa wameruhusiwa kuungana na familia zao baada ya wataalam wa afya kujiridhisha kuwa hawana maambikizi ya virusi hivyo.

Naibu waziri wizara ya Afya Dk.Godwini Mollel amefanya ziara ya kutembelea Kambi za wahisiwa wa virusi vya Marburg katika Wilaya ya Biharamulo na kupata taarifa juu ya mwenendo wa ugonjwa huo kwasasa kutoka kwa Mkurugenzi wa huduma za kinga wizara ya Afya Ntuli Kapologwe.

Amesema wahisiwa 92 wanaendelea na uangalizi katika kambi mbalinbali za kutolea huduma za Afya kwa kufanya uchunguzi mbalimbali na kujua hali zao zinaendeleaje ndani ya siku ya siku 21.

Amesema mpaka sasa kwa kushirikiana na Mashirika ya kimataifa na Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii tayari Kaya 10,892 wamepatiwa Elimu ya kujikinga huku vitu o vya ukaguzi wa abiria wanaotoka nchi mbalimbali vikiongezeka kutoka vituo 8 Hadi 11 ambapo kwa siku abria 8,000 hadi 10,000 wanapimwa hali zao.

Mollel ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa kufuata Sheria zinazotolewa na Wizara ya Afya ili kuendelea kukinga afya zao bila kuathiri uchumi wao.

"Nawapongeza wataalam wetu kwa kuchukua hatua za haraka mlizofanya na mnaendelea kutoa huduma katika jamii , ugonjwa huu ni hatari na wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari , kwa kuwa hatua za kujikinga ziko wazi basi wanaweza kuendelea na shughuli zao huku wakijikinga"alisema

Kwa upande wa mkurugenzi wa kinga toka Wizara ya Afya Dk.Ntuli Kapologwe aliyataja mashirika ya kimataifa yanayoendelea kutoa huduma kwa huko Biharamulo kuwa ni WHO,UNICEF na CDC ambao wanaendelea kisaidia Serikali katika mapambano ya ugonjwa huo mpaka sasa.

RC FATMA MWASSA AWAHASA WANANCHI KAGERA KUEPUKANA NA IMANI POTOFU KUHUSU UGONJWA WA MARBURGNa Angela Sebastian Mkuu wa m...
28/01/2025

RC FATMA MWASSA AWAHASA WANANCHI KAGERA KUEPUKANA NA IMANI POTOFU KUHUSU UGONJWA WA MARBURG

Na Angela Sebastian

Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amewataka wananchi wa mkoa huo kuepukana na imani potofu na za kishirikiana ili kuwezesha kudhibiti kwa kiasi kikubwa mlipuko wa ugonjwa wa marburg ambao ni hatari na haujapata tiba ya moja kwa moja na kunusuru kuenea kwa kiwango kikubwa.

Mwassa ameeleza hayo leo wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari zaidi ya 100 wa vyombo mbalimbali ili wapate elimu juu ya kuandika habari sahii,wapate wapi taarifa sahii zisizozua taaruki katika jamii juu ya mlipuko wa ugonjwa wa marburg yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya na wadau mbalimbali.

"Wananchi wengi hawaamini na wanapuuza kila kinachosemwa na wataalam,Watanzania tuna hulka ya kutoamini jambo hasa pale tunaposikia aliyeambukizwa ni mmoja au kufa ni mmoja yaani sisi kuamini kwetu ni mpaka wawe wamekufa wengi hii ni fikra potofu tena wengine wanafananisha na imani za kishirikiana tuache tufuate maelekezo yanayotolewa na wataalam"Rc Mwassa

Amesema busara ni kukinga na siyo kusubiri kutibu, siyo kusubiri watu watu wadondoke bali kuwaelimisha watu wajikinge kabla hivyo akawataka waandishi kuhakikisha wanatoa elimu kwa ĵamii kupitia vyombo vyao vya habari jinsi ya kuchukua tahadhari na kujikinga na ugonjwa huu, hatari ambapo ametoa mfano kuwa wakiugua watu 10 tisa kati yao hufari.

Amesema hivyo tunahitaji nguvu kubwa katika kufanya kampeni juu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko k**a huu wa marburg pindi yanapotokea.

Amesema kuwa Marburg ilitangazwa rasmi na Rais Dk Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 20 mwezi huu na kusema kuwa kipo kisa cha mtu mmoja ambacho kimetokea wilayani Biharamulo hari ambayo imesababisha timu ya Serikali kupitia idara ya Afya na wadau mbalimbali kufika Wilayani humo na kuanza kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha ugonjwa huo hausambai na kuleta visa vipya.

Naye Mkurugenzi wa kinga toka Wizara ya Afya Dk. Ntuli Kapologwe
ametaja dalili za ugonjwa huo kuwa ni homa,maumivu ya kuchwa,maumivu ya misuli,kuharisha,mwili kuishiwa nguvu,vidonda vya koo,vipelele vya ngozi,maumivu ya tumbo,kutapika ,kutokwa damu sehemu mbalimbali za wazi mfano puani,kutapika damu na kuharisha damu.

Naye dk.Norman Jonas ni mratibu wa huduma za Afya ngazi ya jamii kutoka Wizara ya Afya alimesema ugonjwa wa marburg unasababishwa na virusi vya marburg na unaambukizwa kwa haraka kwa njia mbili ambazo ni kutoka kwa wanayama na kwa binadamu na binadamu kwenda kwa binadamu.

Jonasi amesema unaenea kwa njia zifuatazo kugusa majimaji ya mwili k**a vile kinyesi,matapishi,jasho,,mkojo na damu pia vyombo,magodoro na nguo,kula au kugusa mizoga au wanayama walioambukizwa mfano popo,nyani,tumbuli na sokwe.

Naye mwakilishi kutoka Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani(UNICEF) Dkt. Edna Moturi ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na wadau katika mapambano ya ugonjwa wa Marburg kwa jamii hivyo kwa kushirikiana na Serikali wataendeleza Mafunzo kwa makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, Waganga wa Tiba Asili, Bodaboda na makundi mengine.

MHE. KIKWETE: SERIKALI ITAENDELEA KUSIMAMIA TARATIBU KWA WATANZANIA  WANAOTAFUTA AJIRA NJE YA NCHI. Na Ghati Msamba,SERI...
28/01/2025

MHE. KIKWETE: SERIKALI ITAENDELEA KUSIMAMIA TARATIBU KWA WATANZANIA WANAOTAFUTA AJIRA NJE YA NCHI.

Na Ghati Msamba,

SERIKALI ya Tanzania imekemea vikali tabia ya baadhi ya Watanzania kwenda kufanya kazi nje ya nchi bila kufuata utaratibu wa kisheria, ikieleza kuwa hatua hiyo inachangia kutokuwa na taarifa sahihi kuhusu mahali walipo na shughuli wanazozifanya.

Hali hii inahatarisha usalama wao na pia inakuwa kikwazo kwa juhudi za serikali kuhakikisha usalama wa raia wake.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, wakati akizindua rasmi utekelezaji wa makubaliano ya kuwezesha na kuratibu ajira za Watanzania nchini Saudi Arabia, hafla iliyofanyika jana, Januari 27, 2024, katika jiji kuu la Dar es Salaam.

Akizungumza katika tukio hilo, Mheshimiwa Kikwete amesema kuwa uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Saudi Arabia unatoa fursa kubwa kwa Watanzania kufanya kazi katika taifa hilo la Kiarabu, lakini ni muhimu kuwa na utaratibu ulio wazi na wa kisheria ili kuepuka matatizo yanayoweza kutokea kwa watu wanaosafiri bila kujali sheria zilizowekwa.

“Tunaamini kwamba, kwa kushirikiana na Saudi Arabia, tutahakikisha kuwa kila Mtanzania anayekwenda kufanya kazi huko atakuwa akifuatilia taratibu zote za kisheria na kufanya kazi kwa usalama na ustawi wake,” alisema Mheshimiwa Kikwete.

Aidha, Waziri Kikwete aliendelea kusema kuwa serikali haitaruhusu wala kuvumilia Watanzania kufanya kazi au kusafiri kwenda Saudi Arabia au nchi nyingine yoyote bila kupitia kwa mawakala waliotambulika na serikali ya Tanzania pamoja na ile ya Saudi Arabia. Hii ni hatua muhimu ili kuhakikisha kwamba wanapokwenda, wanapata huduma bora na wanajua haki zao na wajibu wao.

Miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa katika ushirikiano huu ni pamoja na kuwepo kwa utaratibu wa kisasa utakaowezesha Watanzania kusafiri kwenda kufanya kazi Saudi Arabia kwa njia sahihi. Aidha, utaratibu huu utaambatana na upimaji wa afya kwa waombaji wa ajira, ambapo wote watapewa fursa ya kufanya kazi katika mazingira bora na salama, wakipata mishahara yenye staha na fursa za kujikwamua kiuchumi.

Waziri Kikwete amesisitiza kuwa serikali inatambua mchango mkubwa wa ajira za kigeni katika kuboresha maisha ya Watanzania na kuchangia maendeleo ya taifa. Alisema kwamba, kupitia makubaliano haya, Tanzania itakuwa na mfumo bora wa kuratibu ajira za nje na hivyo kuepuka matatizo ambayo yamekuwa yakijitokeza kutokana na watu kufanya kazi kwenye nchi za nje bila kufuata taratibu.

Hivyo basi, serikali imejizatiti kuunda mazingira bora kwa Watanzania wanaotaka kufanya kazi nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na kuboresha ushirikiano na nchi k**a Saudi Arabia ili kuhakikisha ajira hizi zina manufaa kwa pande zote mbili.

RAIS DKT. SAMIA AMEGEUZA CHANGAMOTO ZA WAKAZI WA BUKOBA VIJIJINI KUWA FURSA- MHE KUNDO METHEWNa Angela Sebastian Naibu w...
24/01/2025

RAIS DKT. SAMIA AMEGEUZA CHANGAMOTO ZA WAKAZI WA BUKOBA VIJIJINI KUWA FURSA- MHE KUNDO METHEW

Na Angela Sebastian

Naibu waziri wa maji Mhandisi Kundo Mathew amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan amebadilisha changamoto za wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bakoba vijijini mkoani Kagera na kuwa fursa .

Methew amesema fursa hiyo inakuja baada ya Dk.
Samia kutoa kiasi cha shilingi bilioni 15.8 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji wa Kemondo-Maruku unaotarajiwa kunufaisha wananchi zaidi ya laki moja wa kata sita ili kuondokana na kero ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Methew ametoa kauli hiyo leo baada ya kutembelea na kukagua hatua ya ujenzi iliyofikiwa kwa sasa kisha kuongea na wananchi na watumishi wa wakala wa maji Vijijini (RUWASA) na mamlaka ya maji safi na maji taka (BUWASA) ,katika maeneo ya Kemondo kinapojengwa chanzo cha mradi huo na Kanazi lilipojengwa tanki.

"Rais Dk Samia anapoleta mradi wa maji anabadilisha kero,changamoto na shida za maji kwa wanachi wake hususani nyie wa Bukoba vijijini kuwa fursa ambazo ni kupata ajira,biashara na ongezeko la mapato katika halmashauri zetu, kutokana na ajira au biashara kwani watu watalipa kodi hivyo, changamoto ya maji katika nchi yetu Dk.Samia anaitatua na kuitimisha kwa kubadilisha kuwa fursa kwetu"ameeleza Methew

Amesema zaidi ya shilingi bilioni tisa zimekwishalipwa kwa mkandarasi ndiyo maana inashuhudiwa mradi huo kufika katika hatua hiyo ambapo kuanzia kwenye chanzo (kidakio )mpaka kwenye tanki ni kilomita nne mpaka sasa kilomita 3.7 maji tiyali yamefikishwa huku mita 300 ikiwa katika hatua za mwisho za kukamilika.

"Hapa tulipofikia zaidi ya shilingi bilioni tisa zimekwishalipwa ndiyo maana tunashuhudia mradi huu kufika katika hatua hii ambapo kuanzia kwenye chanzo (kidakio )mpaka kwenye tanki ni kilomita nne mpaka sasa kilomita 3.7 maji tiyali yamefikishwa huku mita 300 ikiwa katika hatua za mwisho kukamilika"amesema Methew

Alisema kuwa changamoto za maji zimefiki ukingoni kutokana na wataalam walioko chini ya Wizara hiyo kufanya kazi usiku na mchana hivyo, muda mfupi ujao maji yataingia kwenye tanki na kazi hiyo nzuri iliyofanywa na Wizara hiyo inakwenda kukamilika kabla ya mwezi Oktoba mwaka.

Pia amesema maelekezo ya Dk.Samia ni kwamba maji hayo yawe na gharama nafuu hivyo hakuna mtu wa kudhubutu kukiuka maagizo hayo kwasababu ni sheria hivyo tunatii shetia bila shuruti.

Amesema wizara hiyo itaendelea kutekeleza maelekezo yanayotolewa na chama cha Mapinduzi (CCM) nankuwa wasikivu wakati wote.

Naye katibu wa CCM wa Wilaya ya Bukoba Vijijini Jesca Ndyamuk**a amepongeza uongozi wa Dk.Samia na Wizara ya maji kwa kazi kubwa na mipango mikubwa anayoendelea kufanya hususani utekelezaji wa miradi ya maji nchi nzima kuni hari hiyo inaleta matumaini kwa wananchi .

Kaa upande wa diwani wa kata ya Kemondo Hatwibu M***a amesema mradi huo ulianza mwak 2021 ambapo hapo katika ulianza kusuasua na kusababisha maneno mengi kutoka kwa wananchi hivyo kwaasasa tunayo matumaini na tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan mwenyezi Mungu aendelee kumtinza ili athletes maendeleo zaidi.

Mradi huo wa Kemondo- Maruku ambao ulianza utekelezaji wake katika bajeti ya 2021/2022 unaotarajiwa kunufaisha wananchi wapatao laki moja kutoka katika kata sita unaelekea hatu ya mwisho ya utekelezaji ambapo kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu utakuwa umekamilika na wananchi kupata maji safi na salama.

BASHUNGWA AITAKA UHAMIAJI KUTOWAZUNGUSHA WANANCHI, MCHAKATO WA KUPATA KITAMBULISHO CHA TAIFA.Waziri wa Mambo ya Ndani ya...
23/01/2025

BASHUNGWA AITAKA UHAMIAJI KUTOWAZUNGUSHA WANANCHI, MCHAKATO WA KUPATA KITAMBULISHO CHA TAIFA.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameiagiza Idara ya Uhamiaji kuboresha ushirikiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kuondoa urasimu wa kuwazungusha Wananchi wakati wanapokuwa katika mchakato wa kutafuta Kitambulisho cha Taifa.

Bashungwa ameelekeza hayo leo tarehe 23 Januari 2025 wakati alipofanya ziara Makao Makuu ya dara ya Uhamiaji, Dodoma ambapo ameitaka Idara hiyo kuendelea kuboresha utoaji huduma kwa Wananchi.

Bashungwa amemtaka Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji CGI, Dkt. Anna Makakala kuhakikisha kila Ofisi ya Wilaya ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa inakuwa na Afisa wa Uhamiaji ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa Wananchi.

“Nitakapokuwa naenda kwenye Wilaya, nikifika ofisi za NIDA nikute kuna Afisa wa NIDA lakini awepo Afisa wa Uhamiaji ambao wanashirikiana kuwahudumia Wanzania ili kuepuka upumbufu kwa Wananchi na Malalamiko yasiyokuwa na tija” amesisitiza Bashungwa

Aidha, Bashungwa ameiagiza Idara ya Uhamiaji kuendelea na Operesheni, misako na doria za kuk**ata wahamiaji haramu na kuhakikisha wageni wote wanaoingia ndani ya nchi, wanafuata tararibu na sheria za kuingia nchini.

Kadhalika, Bashungwa ametoa onyo kwa baadhi ya Maafisa wa Idara ya Uhamiaji ambao sio waaminifu, wanaowaonea Wananchi wakati wa Operesheni na misako inapofanyika

Awali, Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji CGI, Dkt. Anna Makakala ameeleza kuwa Idara ya Uhamiaji inaendelea na misako, doria na kaguzi mbalimbali kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa.

“Katika mwaka 2024 tumefanya Oparesheni, mikasako na doria nchi nzima, jumla ya Wahamiaji wa makosa mbalimbali 14,368 walik**atwa na kuchukuliwa hatua ” ameeleza CGI, Dkt. Makakala

Nimeelekeza Idara ya Uhamiaji na NIDA kushirikiana ngazi za wilaya maafisa wote wa NIDA na Uhamiaji wawepo ofisi moja wakati wanahudumia wananchi ili kuondoa usumbufu wa wananchi kutoka ofisi moja kwenda nyingine na wakati taasisi zote 2 zipo ndani ya Wizara moja na wilaya moja. Nitakapokuwa napita huko kwenye wilaya tutasimamia ipasavyo utekelezaji wa hili jambo kupitia mrejesho wa wananchi.

WENYEVITI NA WAJUMBE WA SERIKALI YA MTAA NSHAMBYA WATAKIWA KUTOA HUDUMA BURE KWA WANANCHI.Na Angela Sebastian-BukobaWENY...
22/01/2025

WENYEVITI NA WAJUMBE WA SERIKALI YA MTAA NSHAMBYA WATAKIWA KUTOA HUDUMA BURE KWA WANANCHI.

Na Angela Sebastian-Bukoba

WENYEVITI na wajumbe wa Serikali za mitaa katika kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wametakiwa kutowatoza wananchi kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya kulipia huduma pale wanapofika katika ofisi za Serikali ya mitaa na kata bali fedha hiyo iwe inatambulika kisheria.

Wito huo umetolewa na Meya wa Manispaa hiyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Nshambya Godsoni Gibsoni wakati akiongea katika mafunzo aliyoyaanda yeye ya kuwajengea uwezo na kuwapa vitendea kazi viongozi wa mitaa katika kukuza maendeleo ya wananchi na kuwapongeza kwa kuchaguliwa.

Gibson amesema baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa wanatozwa ela kiasi cha shilingi 5,000 wanapokwenda kupata huduma kwa wenyeviti,wajumbe na watendaji kwa ajili ya kupata huduma hivyo ndipo akaamua kutoa vitendea kazi ikiwemo karatasi kwasababu wapo wananchi ambao hawana ela hiyo.

"Inawezekana inatolewa hiyo ela wasababu ya ulipaji wa ada kwa ajili ya kununua karatasi,uchapaji wa barua,kwenda kuangalia tukio kunahitajika gharama hivyo mimi k**a diwani wa Kata Nshabya nimeamua kufadhili ofisi zetu za mitaa mitatu kutoa vifaa ambavyo ni karatasi limu tisa,stamp pad kwa ajili ya kugonga mhuri,karamu na mahitaji mengine na hili litakuwa endelevu pale wanapoishiwa wanijulishe niwapatie vifaa hivyo"ameeleza Gibson

Anasema nia yake ni kuhakikisha mwananchi yoyote wa kata ya Nshambya asitozwe hata shilingi moja ili kupata huduma inawezeka wengine wakachukia lakini, nia hii ni kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha wananchi wanapata haki zao k**a inavyostahili.

Amesema viongozi hao wamejifunza mada sita zinazohusu wajumbe na wenyeviti wa Serikali za mitaaa ili watambue majukumu yao ambazo zimetolewa baada ya kumaliza uchaguzi wa Serikali za mitaa lengo kubwa waweze kupeleka huduma bora kwa wananchi na kutambua majukumu yao.

Maye Katibu tawala wa wilaya ya Bukoba Proscovia Mwambi akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Sima amewataka viongozo hao kuyafanyie kazi mafunzo hayo kwakua wazalendo na waadilifu katika kuwahudumia wananchi na kutotumika tofauti na malengo ya Serikali kwani wao ni kiungo muhimu kwa wananchi na Serikali.

Mjumbe wa mtaa Bunkango kata Nshabya Anna Mshumbuzi akaiongea kwa niaba ya viongozi wa mtaa ambao wamepatiwa mafunzo na vitendea kazi akaeleza kwa namna gani maafunzo hayo yatakavyo enda kuwasaidia katika utendaji kazi wao
ambapo amesema wametakiwa kuwafichua wazazi ambao mpaka sasa hawajawapeleka watoto shule ili wachukuliwa hatua

Semina hiyo ambayo imefanyika katika chuo cha King Rumanyika Manispaa ya Bukoba imejumuisha wenyeviti wa serikali za mitaa,wajumbe na watumishi kutoka kata ya Nshabya mkoani humo.

FURSA ZA UWEKEZAJI WA KILIMO CHA VIUNGO(SPICES) NA VIWANDA VYA THAMANI MOROGOROMkoa wa Morogoro, ni wenye ardhi yenye ru...
21/01/2025

FURSA ZA UWEKEZAJI WA KILIMO CHA VIUNGO(SPICES) NA VIWANDA VYA THAMANI MOROGORO

Mkoa wa Morogoro, ni wenye ardhi yenye rutuba na hali nzuri ya hewa kwa kilimo, umeibuka kuwa kitovu cha fursa za uwekezaji, hasa katika sekta ya kilimo cha viungo na viwanda vya kuongeza thamani ya mazao.

Katika ziara maalum katika miradi ya uwekezaji mkoa wa Morogoro iliyofanyika tarehe 13 Januari 2025, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kwa kushirikiana na viongozi wa mkoa, ilitoa wito kwa wawekezaji wa ndani na wa kimataifa kuchangamkia fursa hizi adimu.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, M***a Ali Musa, alieleza kuwa mkoa huo, licha ya mafanikio katika kilimo cha mpunga, bado una nafasi kubwa ya kuendeleza kilimo cha viungo(spices) k**a karafuu, tangawizi, mdalasini, na mazao mengine ya thamani kubwa.

Wilaya za Gairo, Mvomero, na Kilosa zimeainishwa kuwa na ardhi yenye rutuba inayofaa kwa uzalishaji wa mazao haya, huku zikilenga kuwa kitovu cha uzalishaji kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi.
Chanzo:TIC

WAZIRI RIDHIWANI KIKWETE AWASILISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA KAZI BUNGENIWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ...
17/01/2025

WAZIRI RIDHIWANI KIKWETE AWASILISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA KAZI BUNGENI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, amewasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Kazi (The Labour Laws (Amendments) (No. 13) Bill, 2024) bungeni mjini Dodoma.

Kikao cha uwasilishwaji wa muswada huo kilifanyika tarehe 24 Januari, 2025, na kilihusisha wadau mbalimbali, ikiwemo wajumbe wa k**ati ya Bunge.

Aidha, Waziri Kikwete alieleza jitihada zinazofanywa na serikali kutatua changamoto zinazowakabili watumishi nchini, ikiwemo utatuzi wa changamoto za ajira kwa wanawake wanaojifungua watoto njiti na migogoro ya ajira nchini.

WATANZANIA 250 KUNUFAIKA NA KIWANDA CHA KUCHAKATA MCHELE (WILMAR RICE TANZANIA LTD)Januari 13, 2025, Kituo cha Uwekezaji...
17/01/2025

WATANZANIA 250 KUNUFAIKA NA KIWANDA CHA KUCHAKATA MCHELE (WILMAR RICE TANZANIA LTD)

Januari 13, 2025, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kilifanya ziara katika kiwanda cha kuchakata mpunga cha Wilmar Rice Tanzania Ltd, kilichopo Morogoro. Lengo la ziara hiyo lilikuwa kujionea maendeleo ya mradi huo na kujadili mchango wake katika sekta ya kilimo na viwanda nchini.

Kwa taarifa iliyotolewa na mwekezaji wa kiwanda hicho, Vinod Godara, Watanzania 250 wamepata ajira katika kiwanda hicho, ikiwa ni pamoja na ajira za kudumu na zisizo za kudumu. Hivyo, kiwanda hicho kinachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mkoa wa Morogoro.

Mwekezaji huyo aliipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kutatua changamoto mbalimbali za uwekezaji, ikiwemo kuboresha miundombinu, umeme, na maji—vitu ambavyo ni muhimu kwa mafanikio ya uzalishaji.

KIKWETE: SERIKALI ITAENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA UMMA NCHINI.Na Hamida Ramadhan -DodomaWAZIRI wa Nchi Ofi...
16/01/2025

KIKWETE: SERIKALI ITAENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA UMMA NCHINI.

Na Hamida Ramadhan -Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kusimamia mapato na malimbikizo ya madai kwa watumishi wa umma.

Katika ufunguzi wa kikao cha 30 cha Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) jijini Dodoma, Kikwete alisisitiza kuwa Serikali haitakubali waajiri wanaoshindwa kutekeleza matakwa ya kisheria kuhusu ushirikishaji wa mabaraza ya wafanyakazi.

“Ni muhimu kwa waajiri kufuata sheria na kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki zao na Serikali itachukua hatua stahiki dhidi ya waajiri watakaoshindwa kutekeleza wajibu wao,” amesema Kikwete.

Waziri Kikwete alikiri kwamba Serikali inatambua changamoto hizi na iko tayari kushirikiana na TALGWU kutafuta suluhisho la kudumu.

"Tutaendelea kufanya kazi pamoja na vyama vya wafanyakazi ili kuhakikisha tunatatua matatizo yanayowakabili watumishi wa umma. Ufanisi wetu unatokana na ushirikiano na uwazi katika usimamizi wa fedha,” alisema Kikwete.

Katibu wa TALGWU, Rashid Mtima, ameeleza changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya umma, ikiwa ni pamoja na malipo ya fedha za likizo kutolipwa kwa wakati, matatizo katika malipo ya leseni kwa kada ya afya, na ucheleweshaji wa fedha za uhamisho.

"Tunahitaji mfumo thabiti ambao utaweza kutatua changamoto hizi mara moja, ili watumishi wetu waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kwa moyo mmoja,” alisisitiza Mtima.

Aliongeza kuwa mfumo wa PEPMIS umekuwa na dosari zinazohitaji marekebisho ili kuboresha utendaji wa watumishi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Mitaa Tanzania TALGWU Tumaini Nyamhokya ilipongeza juhudi za Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.

Amesema Samia Suluhu Hassan, akitaja hatua k**a vile kupandisha madaraja ya watumishi, kuboresha mifumo ya kikokotoo cha mafao, na kuimarisha miundombinu ya usafiri, ikiwemo mradi wa treni ya umeme (SGR).

"Tunafarijika kuona juhudi za Serikali katika kuboresha mazingira ya kazi, lakini bado tunahitaji kuhakikisha haki za wafanyakazi zinafikiwa kwa wakati,” alihimiza .

Kikao hicho kililenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na vyama vya wafanyakazi, na kujadili mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizopo ili kuhakikisha watumishi wa umma wanapata haki zao na mazingira bora ya kazi.

Address

Musoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Musoma Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Musoma Tv:

Videos

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Videos
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share