Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Lindi, wameungana na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, na kutoa tamko la pamoja la kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa mgombea pekee wa urais 2025 kupitia Chama hicho.
Sherehe hizo zimefanyika Leo Katika viwanja vya makao Mkuu ya CCM, wilayani Lindi, mkoani humo.
Katika sherehe hizo mbunge wa Jimbo la Mchinga Mama Salma Kikwete akasoma tamko kwa niaba ya Jumuiya amewapongeza wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika huko jijini Dodoma kwa maamuzi yao ya kumpitisha Rais Samia kwa kuwa amestahili kuendelea kuwa katika nafasi hiyo.
Imeandaliwa na Hadija Omary-Lindi
#jukumuletukukuhabarisha
#kusiniyetuupdates
Hayo ni kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX)Godfrey Malekano, wakati akizungumza katika kikao cha wadau wa kilimo Mkoani Shinyanga.
Malekano ameeleza kuwa soko la bidhaa Tanzania TMX limesaidia kuleta uwazi kupitia minada ya kielektroniki ambayo imekuwa likiiendesha katika mauzo ya mazao na bidhaa mbalimbali nchini.
"soko la bidhaa Tanzania limeleta transparency na kurahisisha ununuzi na uuzaji kwani hakihitaji kusafari kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa anayeuza au kununua" amesema Malekano
#jukumuletukukuhabarisha
#kusiniyetuupdates
Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwaka huu Naibu Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM bara Bwn. John Mongella amewataka mabalozi nchini kudumisha mshikamano ili kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi kwenye uchaguzi huo.
Mongella ametoa wito huo alipokuwa anazungumza Katika mkutano maalumu wa mabalozi wa Jimbo la Mchinga uliofanyika huko tarafa ya Mchinga kijiji cha Mchinga moja Manispaa ya Lindi Mkoani humo.
Amesema ili kuweza kupata ushindi katika Uchaguzi huo na chaguzi zinazoendelea ni muhimu kuwa na mshikamano kweny kupanga mikakati ya ushindi kwa pamoja.
Imeandaliwa na Hadija Omary-Lindi
KAMPENI YA SAMIA LEGAL AID YAENDELEA KUWAFIKIA WANANCHI MTWARA.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Samia Legal Aid imeendelea kuwafikia wananchi mbalimbali katika Mkoa wa Mtwara ikiwa leo tarehe 25 Januari 2025 imeingia katika siku yake ya pili mkoani humo.
Wananchi wameendelea kujitokeza na kupata huduma za msaada wa Kisheria katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, huku wengi wao wakikiru kunufaika na Kampeni hiyo.
#jukumuletukukuhabarisha
#kusiniyetuupdates
#jukumuletukukuhabarisha
#kusiniyetuupdates
Waratibu 100 wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid campaign) kutoka halmashauri tisa za mkoa wa Mtwara wamepatiwa mafunzo ya utekelezaji wa kampeni hiyo kuelekea kuanza kwa utoaji huduma ya kisheria kwa wakazi wa mkoa huo ambayo yataanza Januari 24 hadi Februari 2, mwaka huu.
#jukumuletukukuhabarisha
#kusiniyetuupdates
Viongozi wa AMCOS ya Namapwia wilayani Nachingwea, mkoani Lindi wamekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi kufuatia uchunguzi uliofanywa kuhusu ubadhirifu wa fedha za wakulima na upotevu wa mazao.
Uchunguzi huo ulifanywa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wanachama wa chama hicho, na ripoti ya ukaguzi kubaini kwamba viongozi hao walihusika katika ufisadi wa mazao na malipo yasiyostahili kwa wakulima.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo alitoa agizo la kuchukuliwa kwa hatua za kisheria dhidi ya wahusika na kusema kuwa wote watapelekwa polisi kwa mahojiano zaidi.
Agizo hilo lilitolewa wakati wa ziara yake kata ya Namapwia ambapo alikabidhiwa ripoti ya ukaguzi iliyofanywa na timu ya ukaguzi iliyoongozwa na Afisa Ushirika Wilaya ya Ruangwa, Patrobas.
Ripoti ya ukaguzi iliyofanywa kati ya tarehe 15 hadi 22 Oktoba 2024 ilibaini upotevu wa tani 21 za mazao, pamoja na ulipaji wa fedha kwa wakulima ambao hawajauza mazao yao kupitia AMCOS hiyo.
Vilevile, ilibainika malipo ya zaidi ya milioni tatu msimu wa ufuta ambazo hazikuingizwa kwenye akaunti rasmi ya AMCOS, huku baadhi ya malipo hayo hayakuwa yameidhinishwa na kamati ya chama hicho,upotevu wa fedha shilingi milioni 60 ambazo walizilipa kwa kugawana wajumbe wote.
#jukumuletukukuhabarisha
#kusiniyetuupdates
Rais Samia Suluhu Hassan amemtaka Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe kusimamia milipuko ya magonjwa ambayo imekuwa ikitokea nchini, ili kuiepusha nchi kuwekewa alama za tahadhari na kuingizwa kwenye changamoto za usafiri kutokana na milipuko hiyo ya magoniwa.
Dkt. Samia ametoa maelekezo hayo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, alipokuwa akiwaapisha Majaji wa Mahakama ya Rufani pamoja na viongozi wengine aliwawateua hivi karibuni.
Aidha, Rais Samia amesisitiza umakini kwa Mganga Mkuu huyo wa Serikali Dkt. Grace Magembe wakati wa kuifanya kazi hiyo.
#jukumuletukukuhabarisha
#kusiniyetuupdates
Maafisa ugani walioajiriwa na Bodi ya Korosho Tanzania kupitia program ya BBT Korosho waliopo Mtwara - Makao Makuu ikiwa ni moja kati ya vituo tisa vinavyotoa mafunzo, wamehitimu mafunzo ya nadharia na vitendo yaliyoanza Januari 13, 2025.
Mafunzo hayo yanahusisha ufahamu wa mbinu bora za kilimo cha korosho ikiwa ni pamoja na udhibiti wa magonjwa na wadudu waharibifu kupitia matumizi sahihi na salama ya viuatilifu ili kuongeza uzalishaji wa korosho nchini.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo leo Januari 17, 2026, Dkt. Benedicto Ngaiza Mganga mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambae alimwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara amesema serikali na bodi ya korosho imewaamini na inayo mategemeo makubwa kwamba watakuwa na mchango mkubwa katika kusimamia shughuli za kilimo pamoja na usambazaji wa pembejeo na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya pembejeo
Kwa upande wa maafisa ugani hao wameahidi kwenda kufanya kazi bora zitazoowasaidia kuhamasisha wakulima kwa kuwasiliana nao kwa ufanisi ili kuboresha zao la korosho.
#jukumuletukukuhabarisha
#kusiniyetuupdates
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imefanya mkutano na wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoani Mtwara.
Mkutano huu umefanyika leo, Januari 16, 2025, kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) tawi la Mtwara.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya uchaguzi, Mhe. Jaji Jacob Mwambegele, amewahasa wananchi kujiepusha na kosa la kujiandikisha zaidi ya mara moja ili kuepuka uvunjaji wa sheria.
Jaji Mwambegele amewakumbusha viongozi wa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kuzingatia sheria ya uchaguzi, kanuni za uboreshaji, na maelekezo ya tume pamoja na kusimamia miiko na mipaka ya uendeshaji wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Kwa upande wa wawakilishi wa asasi za kiraia mkoani hapa, wameelezea furaha yao kwa kushirikishwa katika mkutano huku wakiahidi kuwa mabalozi wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
#jukumuletukukuhabarisha
#kusiniyetuupdates
Benki ya Biashara ya Walimu ijulikanayo kama ‘Mwalimu Commercial Bank’ imeendelea kuboresha huduma zake ili kuhakikisha kuwa inawafikia walengwa waliopo katika maeneo mbalimbali nchini.
Uanzishwaji wa Benki hiyo ambayo imekuwa ikifanya huduma zote za Kibenki ikiwepo utoaji wa Mikopo, ulikuwa na Lengo la kuwasogezea karibu waalimu huduma za kifedha katika maeneo yao.
Martha Alfred Gambosi ambaye ni Meneja wa Mtandao wa Matawi kutoka Kitengo Cha biashara cha Benki hiyo, ambaye amesema muitikio wa waalimu kutumia benki hiyo umekuwa mkubwa.
#jukumuletukukuhabarisha
#kusiniyetuupdates
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew ametembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28 Kilwa Masoko wilayani Kilwa mkoani Lindi unaojengwa kwa kutumia chanzo cha mto Mavuji unaogharimu dola za Marekeni zaidi ya Milioni 18 sawa na Bilioni 44.
Mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Afcons Infrastructure Ltd na Vijeta Projects and Infrastructure Ltd JV chini ya usimamizi wa mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya M/S WAPCOS Ltd za nchini India.
Akizungumza mara baada ya kukagua Mradi huo naibu Waziri Kundo amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo kukamilisha kwa wakati ili kuwawezesha wananchi kupata huduma.
Naibu Waziri Kundo amesema makubaliano yanaonyesha mradi huo unatakiwa kukamilika mnamo mwezi septemba, hivyo wakandarasi wafanye kazi usiku na mchana sambamba na kuongeza nguvu kazi ili ukamilike kwa wakati.
Akitoa taarifa,Mratibu wa Mradi huo wa maji wa miji 28 kwa upande wa Kilwa Masoko Bwn. Birune Simon Kawonga kutoka Wizara ya maji ameeleza kwamba, awali mradi ulipangwa kutekelezwa kwa miezi 20 kuanzia Aprili 11,2023 hadi Disemba 10,2024 lakini Mkandarasi ameongezewa muda wa utekelezaji wa miezi 8 kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika usanifu na ujenzi licha ya mpaka sasa kufikia asilimia 68.42 ya utekelezaji.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Omary Nyundo ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Dkt.Samia kwa mradi huo ambao unatarajiwa kunufaisha watu zaidi ya 59,983 katika Miji ya Kilwa Masoko na Kilwa Kivinje pamoja na vijiji viwili ambavyo ni Mavuji na Mchakama.
Ujenzi wa mradi wa maji wa Miji 28 kwa Wilaya ya Kilwa utakapokamilika utaongeza hali ya upatikanaji wa maji kutokai wastani wa asilimia 56 kwa miji ya Kilwa Masoko na Kilwa Kivinje hadi kufikia asilimia 96.
Imeandaliwa na Hadija Omary-Lindi
#jukumuletukukuhabarisha
#kusiniyetuupdates