Kanisa Katoliki Tanzania

Kanisa Katoliki Tanzania SALA NA KAZI

MASOMO YA MISA - TAREHE, OKTOBA 13, 2024DOMINIKA YA 28 YA MWAKA (B)  SOMO 1Hek. 7:7-11 Naliomba, nikapewa ufahamu; nalim...
13/10/2024

MASOMO YA MISA - TAREHE, OKTOBA 13, 2024
DOMINIKA YA 28 YA MWAKA (B)


SOMO 1
Hek. 7:7-11

Naliomba, nikapewa ufahamu; nalimwita Mungu, nikajiliwa na roho ya Hekima. Naliichagua kuliko fimbo za enzi na viti vya enzi, wala mali sikuifananisha na kitu cha thamani; mradi dhahabu yote ya nchi ni k**a mchanga kidogo. Naliipenda kupita afya njema na uzuri wa sura, hata Zaidi ya nuru nikataka kuwa nayo, kwa maana mwangaza wake haufifii kamwe. Na pamoja nayo nikajiliwa na mema yote jamii, na mikononi mwake mali isiyoweza kuhesabika.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu


WIMBO WA KATIKATI
Zab. 90:12-17, (K) 14

(K) Utushibishe kwa fadhili zako ili tufurahi.

Utujulishe kuzihesabu siku zetu,
Tujipatie moyo wa hekima.
Ee, Bwana, urudi, hata lini?
Uwahurumie watumishi wako. (K)

Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako,
Nasi, tutashangilia kwa kadiri ya siku ulizotutesa,
K**a miaka ile tuliyoona mabaya. (K)

Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako,
Na adhama yako kwa watoto wao.
Na uzuri wa Bwana, Mungu wetu, uwe juu yetu,
Naam, kazi ya mikono yetu uithibitishe. (K)


SOMO 2
Ebr. 4:12-13

Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu

SHANGILIO
Mdo. 16:14

Aleluya, aleluya!
Fungua mioyo yetu, ee Bwana, ili tuyatunze maneno ya Mwanao,
Aleluya.


INJILI
Mk. 10:17-30

Yesu alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu. Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako. Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu. Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja, Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu! Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu! Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Nao wakashangaa mno, wakimwambia, Ni nani, basi, awezaye kuokoka? Yesu akawakazia macho akasema, Kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maana yote yawezekana kwa Mungu.
Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto na mashamba, pamoja, na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.

Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.

MASOMO YA MISA, OKTOBA 11, 2024IJUMAA, JUMA LA 27 LA MWAKA WA KANISASOMO LA 1 Gal 3:7-14Fahamuni basi, ya kuwa wale wali...
11/10/2024

MASOMO YA MISA, OKTOBA 11, 2024
IJUMAA, JUMA LA 27 LA MWAKA WA KANISA

SOMO LA 1
Gal 3:7-14

Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu. Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa. Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani. Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye. Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani. Na torati haikuja kwa imani, bali, Ayatendaye hayo ataishi katika hayo. Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.

Neno la Bwana………….Tumshukuru Mungu

WIMBO WA KATIKATI
Zab 111:1-6

(K) Alikumbuka agano lake milele.

Aleluya Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote,
Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
Matendo ya Bwana ni makuu,
Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.

Kazi yake ni heshima na adhama,
Na haki yake yakaa milele.
Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu;
Bwana ni mwenye fadhili na rehema.

Amewapa wamchao chakula;
Atalikumbuka agano lake milele.
Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake,
Kwa kuwapa urithi wa mataifa.

Aleluya, aleluya,
Nena, Bwana, kwakuwa mtumishi wako anasikia:
Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
Aleluya.

INJILI
Lk.11:15-26

Wengine wa makutano walisema, Atoa pepo kwa Beelzebuli, mkuu wa pepo. Wengine walimjaribu, wakitaka ishara itokayo mbinguni. Naye akajua mawazo yao, akawaambia. Kila ufalme uliofitinika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa; na nyumba juu ya nyumba huanguka. Basi, ikiwa shetani naye amefitinika juu ya nafsi yake, ufalme wake utasimamaje? Kwa kuwa ninyi mnasema kwamba mimi natoa pepo kwa Beelzebuli. Basi, k**a mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, wana wenu je! Huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo, hao ndio watakaowahukumu. Lakini, ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama; lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang’anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.

Mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu; na mtu aliyekusanya pamoja nami hutawanya.

Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema, Nitarudia nyumba yangu niliyotoka. Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

Historia fupi ya Mtakatifu Fransisco wa Borgia.Fransisko alikuwa kijana mtukufu katika mahak**a ya Mfalme wa Uhispania. ...
10/10/2024

Historia fupi ya Mtakatifu Fransisco wa Borgia.
Fransisko alikuwa kijana mtukufu katika mahak**a ya Mfalme wa Uhispania. Alikua Duke alipokuwa na umri wa miaka thelathini na tatu tu na aliishi maisha ya furaha na amani na mkewe Eleanor na watoto wao wanane. Lakini tofauti na wakuu wengine wengi wenye nguvu, Fransisko alikuwa bwana mkamilifu wa Kikristo, mtu wa kweli wa Mungu na furaha yake kuu ilikuwa kupokea Ushirika Mtakatifu mara kwa mara. Maisha haya ya furaha yaliisha mke wake mpendwa alipokufa. Fransisko alifanya jambo ambalo liliwashangaza wakuu wote wa Hispania; alitoa Dukedom yake kwa mwanawe Charles na kuwa kuhani wa Jesuit. Watu wengi sana walikuja kwenye Misa yake ya kwanza hivi kwamba ilibidi wajenge madhabahu nje, lakini Mkuu wake alimjaribu kwa kumtendea kinyume kabisa alivyokuwa amezoea miaka arobaini na moja ya maisha yake. Yeye ambaye hapo awali alikuwa Duke alilazimika kusaidia mpishi, kubeba kuni kwa moto na kufagia jikoni. Alipowaandalia makasisi na ndugu chakula, ilimbidi apige magoti mbele yao wote na kuwasihi wamsamehe kwa kuwa mzembe sana! Bado hakuwahi hata mara moja kulalamika au kunung'unika. Wakati pekee alikasirika ni pale mtu yeyote alipomtendea kwa heshima kana kwamba bado ni Duke. Wakati mmoja daktari ambaye alipaswa kutunza jeraha la maumivu ambalo Francis alikuwa amepata alimwambia: "Ninaogopa, bwana wangu, kwamba nitaumiza neema yako." Mtakatifu akajibu kwamba hatamuumiza zaidi ya alivyokuwa sawa wakati huo kwa kumwita "bwana wangu" na "neema yako." Muda si muda kasisi huyo mnyenyekevu alitimiza kazi za ajabu kwa utukufu wa Mungu alipokuwa akihubiri kila mahali na kuwashauri watu wengi muhimu. Alieneza Jumuiya ya Yesu kote Uhispania na Ureno. Alipofanywa kuwa Jenerali Mkuu wa Wajesuiti, alituma wamisionari duniani kote. Chini ya uongozi wake, Wajesuti walikua msaada mkubwa sana kwa Kanisa katika nchi nyingi. Kupitia mafanikio hayo yote, Mtakatifu Francis Borgia alibaki mnyenyekevu kabisa. Sikukuu yake ni Oktoba 10.

MASOMO YA MISA, OKTOBA 10, 2024ALHAMISI, JUMA LA 27 LA MWAKASOMO 1Gal. 3:1 – 5Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliy...
10/10/2024

MASOMO YA MISA, OKTOBA 10, 2024
ALHAMISI, JUMA LA 27 LA MWAKA

SOMO 1
Gal. 3:1 – 5

Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na Imani? Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili? Mmepatikana na mateso makubwa namna hii bure? Ikiwa ni bure kweli. Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na Imani?

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WAKATIKATI
Lk. 1:69 – 75 (K) 68

(K) Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake.

Ametusimamishia pembe ya wokovu
Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake.
K**a alivyosema tangu mwanzo
Kinywa cha manabii wake watakatifu. (K)

Tuokolewe na adui zetu
Na mikononi mwao wote wanaotuchukia;
Ili kuwatendea rehema baba zetu,
Na kulikumbu agano lake takatifu. (K)

Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yeu,
Ya kwamba atatujalia sisi,
Tuokoke mikononi mwa adui zetu,
Na kumwabudu pasipo hofu,
Kwa utakatifu na kwa haki
Mbele zake siku zetu zote. (K)

SHANGILIO
1Per. 1:25

Aleluya, aleluya,
Neno la Bwana hudumu hata milele, na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.
Aleluya.

INJILI
Lk. 11:5-13

Yesu aliwaambia wafuasi wake: Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu, kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake; na yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe? Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake.

Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nayi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au samaki, badala y asamaki atampa nyoka? Au akimwomba yai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?

Neno la Bwana… sifa kwako Ee Kristo.

MTAKATIFU DENIS,  ASKOFU NA WENZAKE9 OKTOBA         Mtakatifu Denis alizaliwa huko Italia katika karne ya 3. Akapata eli...
09/10/2024

MTAKATIFU DENIS, ASKOFU NA WENZAKE

9 OKTOBA

Mtakatifu Denis alizaliwa huko Italia katika karne ya 3. Akapata elimu na hatimaye Daraja Takatifu la Upadri na kisha akawa Askofu.

Mwaka 250 Mtakatifu Denis na maaskofu 5 ,walitumwa na Papa Clement kwenda Gaul Ufaransa. Mtakatifu Denis, akiambatana na mashemasi 2, Rusticus na Eleutherius, waliweka makazi ya katika mji wa Lutetia Parisorium na sasa Paris. Akawa Askofu wa mji huo.

Kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Askofu Denis na wenzake watu wengi walisikia neno, wakaamini na wakabatizwa.

Jambo hili liliwaghazabisha mno viongozi wa kipagani katika mji huo.Gavana wa mji huo aliyeitwa Fescennius Sisinnius alitoa amri ya kukataza mafundisho ya kikristo katika mji huo.

Kutokana na amri hiyo, Mtakatifu Denis na wenzake walik**atwa na baada ya mateso makali Mtakatifu Denis alikatwa kichwa. Na baadae Rusticus na Eleutherius nao pia wakauwawa.

Mtakatifu Denis na wenzake mashahidi, Watakatifu na Wenyeheri wote mtuombee kwa MUNGU.........

MASOMO YA MISA, OKTOBA 9, 2024JUMATANO, JUMA LA 27 LA MWAKA WA KANISASOMO 1Gal. 2:1 – 2, 7 – 14Baada ya miaka kumi na mi...
09/10/2024

MASOMO YA MISA, OKTOBA 9, 2024
JUMATANO, JUMA LA 27 LA MWAKA WA KANISA

SOMO 1
Gal. 2:1 – 2, 7 – 14

Baada ya miaka kumi na mine, nalipanda tena kwenda Yerusalemu pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito pamoja nami. Nami nalikwenda kwa kuwa nalifunuliwa, nikawaeleza injili ile niihubiriyo katika Mataifa, lakini kwa faragha kwa hao walio wenye sifa, isiwe labda napiga mbio bure, au nalipiga mbio bure. Bali, kinyume cha nayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, k**a vile Petro ya waliotahiriwa. Maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha mimi kwenda kwa mataifa. Tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohane, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara; ila neno moja tu walitutakia, tuwakumbuke maskini; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya.
Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nalishindana naye uso kwa uso, kwa sababu alistahili hukumu. Kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kw Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini walipokuja wao, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa. Na hao Wayahudi wengine wakajigeuza pamoja naye, hata Barnaba pia akachukuliwa na unafiki wao. Walakini, nilipoona ya kuwa njia yao haiendi sawasawa na ile kweli ya Injili, nalimwambia Kefa mbele ya wote, ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za mataifa, wala si za Wayahudi, kwa nini unawashurutisha mataifa kufuata desturi za Wayahudi?

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 117 (K) 16:15

(K) Enendeni ulimwenguni wote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Aleluya.

Enyi mataifa yote, msifuni Bwana,
Enyi watu wote, mhimidini. (K)

Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu,
Na uaminifu wa Bwana ni wa milele. (K)

SHANGILIO
Yak. 1:18

Aleluya, aleluya,
Kwa kupenda kwake mwenyewe, Baba alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe k**a limbuko la viumbe vyake.
Aleluya.

INJILI
Lk. 11:1 – 4

Yesu alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, k**a vile Yohane alivyowafundisha wanafunzi wake. Akawaambia, Msalipo, semeni: Baba, Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, Utupe siku kwa siku riziki yetu. Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

MASOMO YA MISA JUMANNE, OKTOBA 8, 2024JUMA LA 27 LA MWAKASOMO 1Gal. 1:13 – 24Mmesikia habari za mwenendo wangu zamani ka...
08/10/2024

MASOMO YA MISA
JUMANNE, OKTOBA 8, 2024
JUMA LA 27 LA MWAKA

SOMO 1
Gal. 1:13 – 24

Mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu. Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu. Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu; wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu; bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski. Kisha, baada ya miaka mitatu, nalipanda kwenda Yerusalemu ili nionane na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano. Lakini sikumwona mtume mwingine, ila Yakobo, ndugu yake Bwana. Na hayo ninayowaandikia, angalieni, mbele za Mungu, sisemi uongo. Baadaye nalikwenda pande za Shamu na Kilikia. Lakini sikujulikana uso wangu na makanisa ya Uyahudi yaliyokuwa katika Kristo; ila wamesikia tu ya kwamba huyo aliyetuudhi hapo kwanza, sasa anaihubiri Imani ile aliyoiharibu zamani. Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 139:1 – 3, 13 – 14 (K) 24

(K) Uniongoze, Ee Bwana, katika njia ya milele.

Ee Bwana umenichunguza na kunijua.
Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;
Umelifahamu zazo langu tokea mbali.
Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu,
Umeelewa na njia zangu zote. (K)

Niende wapi nijiepushe na roho yako?
Niende wapi niukimbie uso wako?
K**a ningepanda mbinguni, Wewe uko;
Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko. (K)

Ningezitwaa mbawa za asubuhi,
Na kukaa pande za mwisho za bahari;
Huko nako mkono wako utaniongoza,
Na mkono wako wa kuume utanishika. (K)

Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu,
Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa
Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. (K)

SHANGILIO
Yn. 14:5

Aleluya, aleluya,
Bwana anasema:
mimi ndimi njia,
na ukweli, na uzima;
mtu haji kwa Baba,
ila kwa njia ya mimi.
Aleluya.

INJILI
Lk. 10:38-42

Yesu aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie.
Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

MASOMO YA MISA, OKTOBA 7, 2022JUMATATU, JUMA LA 27 LA MWAKA WA KANISAKUMBUKUMBU YA BIKIRA MARIA WA ROZARISOMO 1Gal. 1:6 ...
07/10/2024

MASOMO YA MISA, OKTOBA 7, 2022
JUMATATU, JUMA LA 27 LA MWAKA WA KANISA

KUMBUKUMBU YA BIKIRA MARIA WA ROZARI

SOMO 1
Gal. 1:6 – 12

Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. K**a tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? K**a ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo. Kwa maana, ndugu zangu, injili hiyo niliyowahubiri, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu. Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 111:1 – 2, 7 – 10 (K) 10

(K) Alikumbuka agano lake milele.

Aleluya.
Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote,
Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
Matendo ya Bwana ni makuu,
Ukawafunulia watoto wachanga. (K)

Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu,
Maagizo yake yote ni amini.
Yamethibitika milele na milele,
Yamefanywa katika kweli na adili. (K)

Amewapelekea watu wake ukombozi,
Ameamuru agano lake liwe la milele.
Jina lake ni takatifu la kuogopwa.
Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima,
Wote wafanyao hayo wana akili njema,
Sifa zake zakaa milele. (K)

SHANGILIO
2Kor. 5:19

Aleluya, aleluya,
Mungu alikuwa ndani ya Kristo,
akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake,
ametia ndani yetu neno la upatanisho.
Aleluya.

INJILI
Lk. 10:25-37

Mwana-sheria mmoja alisimama akamjaribu Yesu, akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zote; na jirani yako k**a nafsi yako. Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.

Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani? Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa. Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipitia kando. Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapitia kando.

Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na lipomwona alimhurumia, akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza. Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na chochote utakachogharimiwa Zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.

Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake, yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi? Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

MASOMO YA MISA JUMAPILI, OKTOBA 6, 2024DOMINIKA YA 27 YA MWAKASOMO 1Mwa 2:18:24Bwana Mungu alisema, Si vema huyo mtu awe...
06/10/2024

MASOMO YA MISA
JUMAPILI, OKTOBA 6, 2024
DOMINIKA YA 27 YA MWAKA

SOMO 1
Mwa 2:18:24

Bwana Mungu alisema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanya msaidizi wa kufanana naye. Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ilia one atawaitaje; kila kiumbe hai, jna alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake. Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye. Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huyo ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume, atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 128

(K) Bwana atubariki siku zote za maisha yetu.

Heri kila mtu amchaye Bwana,
Aendaye katika njia yake.
Taabu ya mikono yako hakika utaila,
Utakuwa mwenye heri na baraka tele. (K)

Mke wako atakuwa k**a mzabibu uzaao,
Vyumbani mwa nyumba yako.
Wanao k**a miche ya mizeituni,
Wakizunguka meza yako. (K)

Hakika, atabarikiwa hivyo,
Yule amchaye Bwana.
Bwana akubariki toka Sayuni,
Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;
Naam, ukawaone wana wa wanao.
Amani ikae na Israeli. (K)

SOMO 2
Ebr 2:9-11

Ndugu, twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevitwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu. Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso. Maana yeye atakassaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO
Yn 14:23

Aleluya, aleluya!
Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake.
Aleluya.

INJILI
Mk 10:2-16

Mafarisayo walimwendea Yesu, wakamwuliza, Je, ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu. Naye akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini? Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha. Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii. Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja, hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo. Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake; na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine azini. Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea. Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto k**a hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni, Yeyote asiyeukubali ufalme wa Mungu k**a mtoto mdogo hatauingia kabisa. Akawakumbatia, akaweka mikono juu yao, akawabarikia.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

MASOMO YA MISA JUMAMOSI, OKTOBA 05, 2024JUMA LA 26 LA MWAKASOMO 1Ayu. 42:1 – 3, 5 – 6, 12 – 17Ayubu alimjibu Bwana na ku...
05/10/2024

MASOMO YA MISA
JUMAMOSI, OKTOBA 05, 2024
JUMA LA 26 LA MWAKA

SOMO 1
Ayu. 42:1 – 3, 5 – 6, 12 – 17

Ayubu alimjibu Bwana na kusema, najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, nay a kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika. Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, mambo ya ajabu, ya kunishinda mimi, nisiyoyajua. Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; bali sasa jicho langu linakuona. Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu katika mavumbi na majivu.

Basi hivyo Bwana akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo kumi nan ne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng’ombe elfu, na punda wake elfu. Tena laikuwa na wana waume saba, nab inti watatu. Akamwita huyo wa kwanza jina lake Yemima; na wa pili akamwita jina lake Kesia; na wa tatu akamwita jina lake Keren-hapuhu. Katika nchi hiyo yote hawakuwapo wanawake waliokuwa wazuri k**a hao wana wa Ayubu; na baba yao akawapa urithi kati ya ndugu zao wana waume. Kisha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia na arobaini, naye akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hata vizazi vine. Basi Ayubu akafa, mzee sana mwenye kujawa na siku.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 119:66, 71, 75, 91, 125, 130 (K) 135

(K) Umwangazie mtumishi wako uso wako, Ee Bwana.

Unifundishe akili na maarifa,
Maana nimeyaamini maagizo yako.
Ilikuwa vema kwangu kuwa naliteswa,
Nipate kujifunza mari zako. (K)

Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki,
Ee Bwana, na kwa uaminifu umenitesa.
Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo,
Maana vitu vyote ni watumishi wako. (K)

Mimi ni mtumishi wako, unifahamishe,
Nipate kuzijua shuhuda zako.
Kufananisha maneno yako kwatia nuru,
Na kumfahamisha mjinga. (K)

SHANGILIO
Yn. 15:15

Aleluya, aleluya,
Bwana anasema: Siwaiti tena watumwa, lakini ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu, nimewaarifu.
Aleluya.

INJILI
Lk. 10:17-24

Wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni k**a umeme. Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.

Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza. Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.

Akawageukia wanafunzi wake, akasema nao kwa faragha, Heri macho yaonayo mnayoyaona ninyi. Kwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

MASOMO YA MISA OKTOBA 4, 2024 IJUMAA, JUMA LA 26 LA MWAKASOMO 1Ayu. 38:1, 12 – 21, 40:3 – 5Ndipo Bwana alimjibu Ayubu ka...
04/10/2024

MASOMO YA MISA OKTOBA 4, 2024
IJUMAA, JUMA LA 26 LA MWAKA

SOMO 1
Ayu. 38:1, 12 – 21, 40:3 – 5

Ndipo Bwana alimjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake? Yapate kuishika miisho ya nchi, waovu wakung’utwe wakawe mbali nayo? Hubadilika mfano wa udongo chini ya muhuri, vitu vyote vinatokea k**a mavazi. Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie, na mkono ulioinuka huvunjika. Je! Umeziingia chemchemi za bahari, au umetembea mahali pa siri pa vilindi? Je! Umeziingia chemchemi za bahari, au umetembea mahali pa siri pa vilindi? Umeyafahamu mapana ya dunia? Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote. Iko wapo njia ya kuyafikia mako ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi? Upate kuipeleka hata mpaka wake, upate kuelewa na mapito ya kuiendea nyumba yake? Hukosi unajua, maana ulizaliwa wakati huo, na hesabu ya siku za ni kubwa! Ndipo Ayubu akamjibu Mungu, na kusema, Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini? Naweka mkono wangu kinywani pangu. Nimenena mara moja, nami sitajibu; naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 139:1 – 3, 7 – 10, 13 – 14 (K) 24

(K) Uniongoze Bwana, katika njia ya milele.

Ee Bwana umenichunguza na kunijua.
Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu:
Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu,
Umeelewa na njia zangu zote. (K)

Niende wapi nijiepushe na roho yako?
Niende wapi niukimbie uso wako?
K**a ningepanda mbinguni, Wewe uko;
Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko. (K)

Ningezitwaa mbawa za asubuhi,
Na kukaa pande za mwisho za bahari;
Huko nako mkono wako utaniongoza,
Na mkono wako wa kuume utanishika. (K)

Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu,
Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa
Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. (K)

SHANGILIO
Yn. 14:5

Aleluya, aleluya,
Bwana anasema: mimi ndimi njia, na ukweli, na uzima, mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Aleluya.

INJILI
Lk. 10:13 – 16

Yesu aliwaambia wafuasi wake: Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa k**a miujiza hiyo iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu tangu hapo, huku wakiketi katika nguo za kigunia na majivu. Lakini, siku ya hukumu itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zake kuliko ninyi. Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu. Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

MAOMBI KWA MAMA MARIA TUKIMWOMBA ATUOMBEE KWA MWANAE YESU KRISTO.(ONGEZA PIA MAOMBI YAKO BINAFSI)Ee Mama Bikira Maria, M...
03/10/2024

MAOMBI KWA MAMA MARIA TUKIMWOMBA ATUOMBEE KWA MWANAE YESU KRISTO.
(ONGEZA PIA MAOMBI YAKO BINAFSI)

Ee Mama Bikira Maria, Mama wa Neema,
Ninakuja mbele zako kwa unyoofu wa moyo,
nikiwa na ombi la imani na matumaini.

Nakuombea Kanisa lako,
Kanisa lililoongozwa na Roho Mtakatifu,
ili liweze kutekeleza mpango wako wa wokovu.
Ujazi viongozi wetu wa Kanisa,
wapate hekima na ujasiri katika huduma yao,
ili waweze kuwa chombo cha upendo na umoja.

Ee Mama, tunaomba ulinzi wako kwa familia zetu,
uweze kuziimarisha katika upendo na mshik**ano.
Ujaze nyumba zetu kwa furaha na amani,
na uondoe kila dhara na mgawanyiko.
Tuwe na uwezo wa kushirikiana na kusaidiana
katika nyakati za furaha na majaribu.

Tunaomba pia kwa ajili ya amani duniani,
ukaweze kuingilia kati katika mizozo na mafarakano.
Tuonyeshe mwanga wa matumaini,
ili watu wote waweze kuishi kwa upendo na huruma.
Wewe ambayo ni Nyota ya Baharini,
sisi tunakutafuta kwa imani yetu,
utuongoze kwenye njia ya Amani.

Sote kwa pamoja,
tunakushukuru kwa neema zako zote,
na kuungana na wakristo wote katika dunia,
tukiomba kwa ajili ya umoja na upendo.

Mama yetu, katika mikono yako,
tunaweka maombi yetu yote.
Utuombee sisi na ulimwengu kwa jumla,
ili tuweze kufikia pengo la wokovu
katika Yesu Kristo, Mwana wako.

Amina.

Address

Moshi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kanisa Katoliki Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share


Other Moshi media companies

Show All