11/02/2023
USIKU WA VALENTINE(Mwanzo-Mwisho)
Mwl Joshua
0621723709
Nilitokwa na machozi ya uchungu ,nilijikuta nikamlaumu Mungu kwa kuolewa na mwanaume k**a huyu,Nilijaribu kuwaza na kuwazua kwanini Derick wangu habadiliki miaka nenda miaka rudi ,Ndoa yetu ndio kwanza ilikuwa changa kabisa Bado hata hatujapata mtoto,Kwa mtazamo wangu niliona ni wakati sahihi kwetu sisi kuenjoy maisha mimi pamoja na Derick wangu ,Derick alikuwa na mwonekano wa kuvutia Derick ni kijana mrefu maji ya kunde ,Mungu alimjalia Tabasamu zuri lilikokuwa likivutia kila mtu kumtazama,kwa haraka ukimuona utamfananisha na vijana wanaoonekana kwenye tamthilia mbalimbali zinazorushwa kila siku kwenye televisheni
Ilikuwa tarehe 10 mwezi wa pili siku chache zimesalia kabla ya kufika siku ya wapendanao ,nilimuuliza mume wangu ambaye aliyekuwa ameweka begi mgongoni tayari kwa ajili ya kwenda kwenye mapambano yake ya kila siku
``Baby vipi lakini kuhusu valentine day ,kesho kutwa tutaenda wapi?’’
``Mke wangu naomba mambo haya uachane nayo maisha yapo tu kikubwa jua nakupenda na sina mwingine zaidi yako’’
``Mhhhh Derick awamu hii sitakusamehe’’
``Sawa bhana ‘’
Mume wangu aliondoka ,majirani waliokua kwenye majumba yao walikuwa wakitegea masikio nakusikia yote tuliyokuwa tukiongea ,Ashura jirani yangu aliropoka kwa nguvu
``Halooooooo mwanamke hupendwi wewe acha shobo akufukuzae hakwambii ondoka mwache kaka wa watu’’
Mwingine alidakia
``Haahahah makubwa unajisifia umeolewa na HB bora sie tumeolewa na hawa sura personal lakini wanatutunza mama ,tunadeka na kudekezwa tunapelekwa tunapotaka na kwa taarifa yako kesho kutwa tumekodi hadi gari kwenda kwenye tukio’’
Nilitokwa na machozi ya uchungu kwani nilikuwa natamani sana kuwa na muda na mume wangu ,mashoga zangu walikuwa wakinicheka kila mara ,walikuwa wakiringa sana kwa jinsi wanaume zao wanavyowapenda na kuwatoa out mara kwa mara
Siku hiyo majirani zangu walinichamba sana ,niliamua kujifungia ndani nikimsubiri Derick wangu harudi
Ilipofika saa moja usiku Derick alirudi kutoka kazini ,alipofika kabla hata ya salamu nilianza kumrushia maneno
``Mwanaume gani wewe k**a hunipendi niambie ,najua hujakosa hela ,mbona unaendeleza miradi yako ,umeshindwa kabisa kuninunulia walau zawadi ya valentine kuonyesha walau upendo ‘’
``Mke wangu hiyo ndio pole mbona unakosa heshima namna hii’’
``Hapana Derick nakwambia siwezi kabisa mimi nakuacha k**a hunisikilizi’’
Derick hakujibu chochote alizama bafuni na kuoga kisha alirudi ndani
Nilimsogezea chakula na kumtupia hapo ajipakulie ,derick alipakua chakula huku akiniongelesha maneno ambayo hayakupenya kabisa masikioni mwangu
``Mke wangu sikia ,maisha haya yanakusudi ,siku yoyote usifananishe maisha ya mwenzako na yako wewe ni mtu wa tofauti kabisa na Mungu amekuumba kwa kusudio lake ,nimekuoa umekuja hapa hawa shoga zako huwajui umekutana nao ,usipende kufananisha maisha yako ,sijashindwa kukutoa out ila sitakutoa narudia tena naishi maisha yangu siigizi maisha ya wengine’’
``Sawa kula ulale mwanaume suruali wewe’’
Ilipofika siku ya valentine kelele zilijaa kila mahali wapangaji wenzetu waliamka mapema kabisa ,nyimbo za kimapenzi zilipigwa ,kila mmoja alikuwa akiburudika na alionekana mwenye furaha
Siku hiyo sikuamini kabisa ,Derick alikuwa na roho ngumu aliamka na kuvaa magwanda yake ya kazi kisha alichukua begi na kuondoka zake
Nililia kwa uchungu sana ,sina namna ya kueleza uchungu niliokuwa nao,maneno niliyomjibu mume wangu usiku yalimchukiza hivyo alivyoamka alibeba begi na kuondoka zake bila hata salamu cha zaidi aliweka fedha ya matumizi mezani na kuondoka
Shoga zangu walitoka nje wakiwa wamevaa tisheti zilizoandikwa
``You are my king’’ tisheti nyeupe zenye maandishi mekundu wale wenye watoto waliwavalisha vitisheti vidogo vimeandikwa princess na prince ,nilipowatazama marafiki zangu moyo uliniuma sana ,nilijiona k**a sina thamani ,machozi yalinimwagika k**a mvua
Mwajuma shoga angu aliniambia kwa sauti
``Wewe mbwa wa kufugwa kaa hapo ndani mwanamke wewe ,kwanza hupendwi huna thamani yoyote una mwaka hapa hata out moja haloooo kidimbwi wewe bora uondoke utaozea hapa kwanza umefubaa cheki komwe hiloo’’
``haloooooooooo mpambe’’
Walicheka sana ,ndani ya dakika kumi gari aina ya noah lilifika ,wote waliingia wakiwa na waume zao pamoja na watoto ,walipojazana kwenye gari dereva aliwasha gari
Ashura aliropoka
``Wewe kuku wa kufugwa tulindie mji’’
Wote walicheka
Nililia sana sikuwa na cha kufanya zaidi ya hicho ,nilishika simu na kumwandika Mume wangu kwa hasira
``NAJUTA KUOLEWA NA WEWE DERICK’’
Nilisubiri jibu atakalonipa Derick
Baada ya masaa mawili meseji iliingia
``SAWA MKE WANGU’’
Ilikuwa ni siku ya uzuni sana
Upande wa pili Ashura ,Mwajuma na familia zao waliingia ukumbi mkubwa uitwao MAUA PUB walienjoy walipiga picha nyingi kwa haraka walizituma zote kwangu ,nikiwa nimeketi nilisikia meseji ya whatsapp ,nilipofungua nilikutana na mvua za picha jambo lililoongeza maumivu zaidi kwangu
Ilipofika majira ya saa mbili usiku Bwana wangu alirudi akiwa na Apple na zawadi kidogo amebeba mkononi
Alinikabidhi ,kwa hasira nilizitupa chini na kumsonya
Derick wala hakujali aliziokota na kuziweka mezani
Upande wa pili Ilipofika saa nne za usiku ,ashura ,mwajuma na familia zao walikuwa wamelewa chakari ,safari ya kurejea ilianza ,dereva aliwasha gari na kusonga mbele
Dereva alikuwa amelewa sana ,alikimbiza gari bila kujali ,Ashura na Mwajuma walikuwa wakiropoka
``Suka chochea moto unaanya au washa motooo’’
Wakiwa katika kona moja karibu na nyumbani ,gari yao ilivaana uso kwa uso na lori la mizigo
Gari lao lilipindinduka na kupasuka vipande vipande
Huwezi amini hauna kilichosalia pale walifia pale wote
Tukiwa nyumbani na mume wangu ,majirani wa mtaa wa tatu walikuja na kusema
``Derick mbona mpo ndani hamjui majirani wenzenu wamepata ajali na hakuna aliyepona ‘’
Ilikuwa taharuki nilitamani kulia nikashindwa nilirejea whatsapp sikuamini k**a wamepoteza maisha muda si mrefu walinitumia picha za bata whatsapp huku wakinitukana na kunidhalilisha
Nilimwegemea Mume wangu kifuani huku nikilia kwa uchungu
``Nashukuru Mume wangu sasa nayaelewa maneno yako ,kamwe sitokaa niigize maisha ya watu ,kweli sisi ni mavumbi walinidharau sana walinibeza sina kinyongo nao lakini adhabu hii ni kubwa sana kwanini Mungu hakuwapunguzia ,Mwaju na Ashura shoga zangu siamini k**a hatupo nao tena ,Mungu wanguuu’’
``Mke wangu sikuzote usidharau mtu ishi maisha yako ,na Mungu akikupa uwezo wa kufanya jambo lolote usidharau kwani katika furaha yako muda wowote linaweza tokea baya la kukusikitisha au kuchukua maisha ‘’
``Kweli Mume wangu’’
Tulikumbatiana na Mume wangu katikati ya giza tororo huku machozi yakitutoka
MWISHOOOOOOOO
Usiache kutoa maoni yako,Share kwa bidii kabisa ujumbe ufike kwa wengine
ZIPO HADITHI NYINGI ZA KUELIMISHA
Wasiliana nami kwa namba hii
0621723709